MNAMO
TAREHE 12.09.2013 MAJIRA YA SAA 19:30HRS
HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KIBUMBE
KATA YA KIWIRA
– TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA, RAPHAEL S/O FRANK, MIAKA 42,
KYUSA, MKULIMA NA MKE WAKE SUZANA W/O
FRANK, MIAKA 38, KYUSA, MKULIMA WOTE
WAKAZI WA KIBUMBE KIWIRA – TUKUYU WAKIWA NYUMBANI KWAO WALIGUNDUA KUTOWEKA
KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA KWA
MTOTO WAO AGNES D/O RAPHAEL, MIAKA
18, KYUSA, MWANAFUNZI KIDATO CHA NNE
SHULE YA SEKONDARI KIWIRA HIVYO JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZILIANZA MARA MOJA USIKU KUCHA BILA MAFANIKIO.
§ MNAMO TAREHE 13.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:00HRS WAZAZI HAO BAADA YA KUONA MTOTO WAO HAKULALA NDANI KAMA ILIVYO
KAWAIDA WALIAMUA KWENDA KATIKA KITUO CHA POLISI KIWIRA NA KUTOA TAARIFA YA KUPOTELEWA NA MTOTO. HATA HIVYO MAJIRA YA SAA
09:00HRS MTOTO WAO AGNES D/O RAPHAEL
ALIRUDI NYUMBANI NA WAZAZI WAKE WALIPOMHOJI JUU YA MAHALI
ALIPOKUWA ALIWAJIBU KUWA ALIKUWA NA
MHE DIWANI WA KATA YA KIWIRA [CHADEMA] LAURENT S/O MWAKALIBULE, MIAKA 28, KYUSA, MKAZI
WA KIWIRA – KATI NA KWAMBA WALILALA KATIKA NYUMBA YA MDOGO WAKE NA DIWANI HUYO AMBAYE JINA LAKE
BADO KUFAHAMIKA NA KUWA KABLA YA
KUKUTANA WALIWASILIANA KWA NJIA YA
SIMU YA KIGANJANI.
§
MTUHUMIWA
AMEKAMATWA, UPELELEZI WA SHAURI HILI UNAENDELEA .
§
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII HASA WANAFUNZI KUJIEPUSHA NA MADHARA YA KUFANYA MAPENZI [NGONO] KWANI NI HATARI
KWA AFYA ZAO NA PIA KWA MAISHA YAO
YA BAADAE BADALA YAKE WAZINGATIE ZAIDI MASOMO KWA FAIDA YAO , VIZAZI VYAO NA TAIFA
KWA UJUMLA..
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment