Wanajeshi wa Kenya walisaidia Somalia kufurusha wapiganaji wa Al shabaab kutoka Mogadishu
Kufichuliwa
kimakosa kwa barua ya siri ya kidiplomasia kumefichua mgawanyiko mkubwa
kati ya serikali ya Somalia inayoungwa mkono na mataifa ya Magharibi na
nchi za kiafrika pamoja na kikosi cha kulinda amani cha Kenya
kinachohudumu Somalia.
Katika
barua hiyo,iliyoonekana na BBC, Somalia inakishutumu kikosi cha Kenya
kwa kushindwa kufanya kazi na kusababisha mapigano ya hivi karibuni kati
ya makundi tofauti yaliyosababisha vifo vya watu 65.
Taarifa zinazohusiana
Kenya ina kikosi Kusini mwa Somalia karibu na mpaka wake kama sehemu ya kikosi cha Umoja wa Afrika cha kulinda amani.
Somalia
imekuwa katika vita kwa miongo kadhaa sasa lakini matumaini yalikuwa
kwamba kikosi cha Umoja wa Afrika wakiwemo wanajeshi wa Kenya wataleta
tofauti kubwa katika nchi hiyo.
Lakini
barua hii kutoka wizara ya mashauri ya kigeni kwa Umoja huo wa Afrika
inawashutumu walinda amani wa Kenya kuegemea upande mmoja katika eneo
hilo la kusini mwa Somalia.
Barua
hiyo inasema kikosi cha Kenya kinapendelea kundi moja dhidi ya makundi
mengine na kilimkamata afisa mmoja mkuu wa jeshi la Somalia na kilitumia
silaha nzito katika maeneo yalio na raia.
Watu 65 waliuawa huku wengine 155 wakijeruhiwa.
Barua
hii ya kidiplomasia imefichuliwa tu lakini Kenya haijatamka chochote
kuihusu. Lakini Jeshi la Kenya awali lilisitiza kwamba haliegemei upande
wowote na jukumu lake Somalia ni kuleta amani.
Tuhuma
hizo za serikali ya Somalia huenda zikathibitisha wasiwasi katika eneo
hilo kwamba wakati kenya ni sehemu ya kikosi cha Umoja wa Afrika cha
kulinda amani lakini pia kina ajenda yake.
Wanadiplomasia
katika eneo hilo wanasema inajaribu kuunda jimbo ndani ya Somalia
linaloendeshwa na wanasiasa wa Somalia ambao inaweza kuwadhibiti.
No comments:
Post a Comment