Thursday, May 09, 2013

RATIBA YA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA HII HAPA.


KLABU ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambayo inajivunia washambuliaji wawili wa Kitanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu itamenyana na Liga Maculmana ya Msumbiji kuwania tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Hiyo inafuatia upangwaji wa droo ya hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo, inayodhaminiwa na Orange mjini Cairo, Misri leo. Katika droo hiyo, AS FAR Rabat ya Morocco iliyoitoa Azam FC katika Kombe la Shirikisho imepangwa kukutana na wapinzani wao, FUS Rabat. Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani aliongoza droo hiyo kwa pamoja na wawakilishi wa baadhi ya klabu zinazoshiriki michuano hiyo.



Klabu nane zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa, St George, CA Bizerte, TP Mazembe, Enugu Rangers, JSM Bejaia, FUS Rabat, Stade Malien na Entente Setif zimeingia kwenye mbio za kuwania kurithi taji la AC Leopards ya Kongo, mabingwa wa Kombe la Shirikisho na mechi za kwanza zitachezwa kati ya Mei 17, 18 na 19 mwaka huu wakati marudiano yatakuwa kati ya Mei 31 , Juni 1 na 2. Mazembe ambao ni mabingwa mara nne Afrika, walitolewa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika Raundi ya Tatu ya Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 3-2, wakifungwa 3-1 Afrika Kusini na kushinda 1-0 nyumbani.

DROO KAMILI YA 16 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO:
Stade Malien (Mali) vs Lydia (Burundi)
Enugu Rangers ( Nigeria) vs C.S.S (Tunisia)
FUS Rabat ( Morocco) vs ASFAR (Morocco)
CAB (Tunisia) vs Ismailia (Misri)
E.S Setif ( Algeria) vs US Bitam (Gabon)
JSM Bejaia ( Algeria) vs E.S.S (Tunisia)
TP Mazembe (DRC) vs Liga Maculmana (Msumbiji)
St George (Ethiopia) vs ENPPI (Misri)  

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...