Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib
Bilal atakuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Miradi ya
Maendeleo inayotekelezwa na Wizara ya Ujenzi kuanzia tarehe 04/03/2013
mkoani Mara.
Pamoja
na shughuli nyingine, siku ya Jumatatu tarehe 04 Machi 2013 akiwa
mkoani humo, Mhe. Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya
ukarabati wa barabara ya kutoka mpakani mwa Mkoa wa Simiyu na Mara hadi
Musoma yenye urefu wa kilomita 85.5. Barabara ambayo ujenzi wake
utawekewa jiwe la msingi ni sehemu ya Barabara ya Mwanza – Nyanguge –
Makutano – Musoma ambayo ni kiungo muhimu na nchi jirani za Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi. Hivyo kukamilika kwake ni fursa nyingine
nzuri ya kuibua uchumi wa nchi yetu na ukanda huu.
Jumanne
ya tarehe 5 Machi 2013 asubuhi Mhe. Makamu wa Rais atazindua Kivuko cha
Musoma kinachotoa huduma kati ya Musoma na Kinesi. Siku hiyo hiyo
mchana Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa
Nyumba za Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) zilizoko eneo la Old Customs
katika barabara ya Lake Side, Musoma.
Uzinduzi
wa miradi hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya nne ya
kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri na makazi kwa wananchi wake.
Aidha, uzinduzi wa Kivuko cha Musoma (MV Musoma) kinachotoa huduma kati
ya Manispaa ya Musoma na Kinesi Wilayani Rorya ni utekelezaji wa ahadi
za Mheshimiwa Rais baada ya kupokea ombi la Kivuko kutoka kwa wakazi wa
Musoma na vitongoji vyake.
No comments:
Post a Comment