![]() |
| Siku za hivi karibuni mwigizaji anayefanya vizuri kwasasa katika filamu
nchini Niva Zubery amekuwa akiweka status zikimhusu mwigizaji mwenzake
Wema Sepetu na baadhi ya mashabiki wa mastaa hao na wasomaji wa
Swahiliworldplanet kutaka kuupata ukweli kama mastaa hao ni wapenzi kwa
siri au lah. "nyie swp hembu muulizeni Niva kama mtu wake kwasasa ni
Wema coz status zake ni za kuchombeza kwa bibieee then kama wako close
sana siku hizi, maskini kaka wa watu kaoza kwa wema tayariii !" alisema
shabiki mmoja wa kike aliyekataa kutajwa jina lake. Status za Niva
zinaonekana kama kuchombeza kitu flani kwa Wema kwa mujibu wa wasomaji
walioitonya SWP. Baadhi ya status hizo za Niva katika facebook yake ni
hizi hapa "Baaabaa eti wewe upo na wemaa?
(Apana mwanangu) huku akiwa ameweka picha yake mwenyewe na ya mtoto
anayedaiwa kuwa wake", nyingine iko hivi "Niva hanipokerei cm jamaani mwambieni basi kama nampigiaa mwambieeni nawaomba tafazalii" huku akiwa amepost picha ya Wema Sepetu akiwa ameweka simu sikioni".
Status nyingine akiwa ameweka picha hiyo hapo chini wakiwa pamoja na Wema ilisomeka hivi "Etiiiiiii kama tunamuaa kuwa nanihiii na nanihiii itakuwa poa? basi nipe maoni yako ili nijue simmeshajua nilicho maanisha so nataka jibu ili nijue". Baadhi ya wachangiaji walimwambia Niva kuwa wakiwa wapenzi yeye na Wema watapendeza huku wengine wakimwambia kuwa Wema sio hadhi yake, wengine walimwambia ajaribu bahati yake kama tayari ameshamzimikia mrembo huyo. Ili kuupata ukweli kutoka kwa Niva mwenyewe kama baadhi ya wasomaji walivyotutumia ujumbe mwanzoni ilibidi kumtafuta Niva jana na kumueleza kila kitu na yeye alikataa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema na alipoulizwa kama kweli sio wapenzi status zake zikionekana kwa mtu wa Wema si zinaweza kuzua tafrani? Niva alijibu kwa ufupi kwa kusema "hakuna kitu kama hicho kaka" Niva na Wema |
Sunday, July 28, 2013
SKENDO KUHUSU KUHUSU NIVA NA WEMA SEPETU KUWA WAPENZI HIKI NDICHO ALICHOKISEMA NIVA.
GADNA AFUNGUA MILANGO KWA WASANII

MTANGAZAJI aliyejizolea umaarufu kupitia kipindi chake cha Maskani kinachorushwa katika kituo cha redio Times, Gadna G. Habashi ameweka mikakati ya kutoa nafasi ya kucheza muziki wa kizazi kipya ndani ya kipindi hicho bila ya kuchagua.
Gadna ambaye anaamini kuwa kipindi cha redio kinapendezeshwa kwa kupiga muziki, hivyo kwa upande wake anaamini kipindi chake kinaboreshwa na muziki hususani wa bongo fleva.
Mtangazaji huyo aliweka wazi juu ya mikakati hiyo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi, ambapo alisema njia hiyo ni moja ya mikakati yake ya kutoa fursa kwa wanamuziki wa hapa nchini, ambayo inaonekana wengine wanakosa kwenye redio nyingine.
"Unajua mimi nisipopiga muziki kipindi hakipendezi, hivyo nikipiga muziki huo kwanza ni njia ya kuutangaza muziki pamoja na msanii mwenyewe bila ya kubagua muziki huu ni wa nani?" alisema Gadna.
Alisema kwenye kipindi chake hachagui ni mwanamuziki gani apige nyimbo zake, bali anachokifanya ni kuangalia jamii inahitaji burudani ya aina gani.
Gadna ni mtangazaji anayeamini kuwa neno la kutoa fursa linaendana na vitendo, hivyo moja ya kitendo anachokiamini kinachowasaidia wasanii nyumbani ni kupiga nyimbo zao kwenye redio, ili kumuwezesha msanii afahamike na aweze kupata shoo.
Saturday, July 27, 2013
WATANZANIA WENGINE WAWILI WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA HONG KONG....!!!
Mtu mmoja jana alisema sasa hivi wasafiri watokao Tanzania wanakaguliwa kwa makini zaidi ya ilivyokuwa hapo awali kutokana na matukio ya kukamatwa na dawa za kulevya! Hii ni sifa mbaya mno kwa raia na Taifa zima!
Iliyopachikwa hapo chini ni taarifa kutoka kwenye tovuti ya Serikali ya Hong Kong ya Julai 26, 2013
Hong Kong Customs yesterday (July 25) detected three drug trafficking cases, with seizures totally valued at $4.78 million, in the department's escalated anti-narcotics efforts to combat drugs.
BAADA YA NEY WA MITEGO, KALA JEREMIAH NAYE ATANGAZA NIA YAKE YA KUMPIGIA KAMPENI LOWASSA....!!!

Msanii wa Hip Hop na mshindi wa tuzo 3 za KTMA 2013, Kala Jeremiah amefunguka kwa kuandika waraka mrefu kuelezea jinsi anavyomkubali waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kwamba anafaa kuiongoza nchini.
Usome waraka wake huo wote;
Mimi Kala Jeremiah nilikuwa msanii wa kwanza Tanzania kumsema mheshimiwa Edward Lowassa kupitia wimbo wangu uitwao wimbo wa taifa baada ya mheshimiwa kukumbwa na kashfa ya ufisadi wa Richmond.
Kwa kipindi kile kila mmoja wetu alihamaki sana na kuona kweli mzee wa watu ni fisadi.Kwenye wimbo huo kuna mistari nilisema, ‘mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowassa.
Kwa kuwa mimi ni mzuri sana kwenye kufanya uchunguzi binafsi nilitumia muda mwingi sana kulichunguza swala hili la kashfa hii na baadae niligundua kuwa ni swala la kisiasa, na yalikuwa ni mapito ambayo mwanadamu yoyote hupewa muda wa kupitia magumu ili kupimwa imani yake kwa Mungu.
Baada ya kugundua hayo mwaka jana nilitengeneza wimbo unaoitwa ‘Azimio la Arusha’ ambao upo kwenye album yangu ya Pasaka ambayo iko sokoni tokea mwaka jana.
RAY C ATANGAZA KURUDI KWENYE GAME KWA KISHINDO.... APANIA KUFANYA MAMBO MAKUBWA AGOSTI MWAKA HUU...!!!
![]() |
| Mabibi na mabwana mko tayari kwa ujio mwingine wa Ray- C. Malkia wa
kiuno bila mfupa Rehema Chalamila aka Ray-C ametangaza ujio wake rasmi
baada ya kuwa chimbo kwa kipindi kirefu toka apate matatizo miezi kadhaa
iliyopita. Ni baada ya siku chache kupita toka Ray-C atamke kuwa anapenda sauti ya ‘dogo lake’ Recho na kuwa atakuja kufanya naye kazi, leo amethibitisha kuwa mwezi Agosti ndio anarudi rasmi kutoka chimboni. |
AZAM TV YALIPA BILLIONI 6.5 ILI KUONYESHA MECHI ZA LIGI KUU YA TANZANIA BARA
Badhi
ya viongozi wa TFF wakisaini mikataba na Meneja Mkuu wa Kampuni ya
Azam, Said Mohammed (wa kwanza kulia) leo kwenye Ofisi za TFF zilizopo
Karume jijini Dar es Salaam.
Televisheni
ya Azam inayojulikana kama Azam TV imeingia mkataba wa miaka mitatu wa
kuonesha michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) ambapo mkataba huo umetajwa kuwa na thamani ya Tsh
bilioni 6.5
Aidha
Televisheni hiyo itakuwa na majukumu ya kuonesha mechi za moja kwa moja
(LIVE) zisizopungua 60 za Ligi hiyo huku nyingine 180 zikiwa
zimerekodiwa.
SOURCE: GLOBAL PUBLISHER
WAZIRI MKUU WA ZAMANI ATAKIWA KURUDISHA MAGARI YA SERIKALI MARA MOJA...!!!
Former Prime Minister Raila Odinga. Through the spokesman Muthui Kariuki, the government also accused the former premier of putting a siren on one of the cars and using it to manoeuvre through traffic in the city.
In Summary
- The spokesman was, however, dismissed last evening by Cord deputy minority leader Jakoyo Midiwo, who said two former presidents who had the same status as the former PM, had not returned anything to the government.
Through the spokesman Muthui Kariuki, the government also accused the former premier of putting a siren on one of the cars and using it to manoeuvre through traffic in the city.
“He is forever mourning that the government is not giving him recognition, yet he has refused to return six government vehicles and has gone on and bought an illegal siren and is forever driving all over town using the wrong lanes,” the spokesman said yesterday.
STARS WAKIWA MAZOEZI KUPAMBANA NA CRANE LEO

Wachezaji
mbalimbali wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Satrs' ambao wanasakata
kabumbu ndani ya nchi wakijifua katika Uwanja wa Taifa wa Mandela uliopo
Nambole nchini Uganda. Stars ipo nchini Uganda na leo inataraji
kushuka katika dimba la uwanja huo kumenyana vikalina The Crenes ya
Uganda kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa
Ndani CHAN.

Moja
ya mikakati ya Taifa Stars kwenye mechi ya leo (Julai 27 mwaka huu)
dhidi ya Uganda kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Tatu za Afrika kwa
Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini
ni kushambulia kwa muda mwingi wa mchezo.
POLISI AZUA BALAA MKUTANO WA CHADEMA NUSURA APIGWE

Na Bryceson Mathias, Kikombo
ASKARI
Polisi wa Kata ya Kikombo aliyejulikana kwa jina Moja la Sivanus
(pichani), Jana alizua Tafrani kwenye Mkutano wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), baada ya Kumnyanganya Kipaza Sauti (Mike) Katibu
wa Wilaya wa Dodoma Mjini, Jella Mambo.
Silvanus
alizua hayo Julai 26, ambapo alinusurika Kipigo cha Wananchi waliokuwa
na hasira kwa kufanya tukio hilo, ambapo walidai hata kungekuwa na
makosa ya Matamko au kitu kingine chaochote, hakustahili kuingia jukwani
na kumnyang’anya Kipaza sauti Katibu huyo.
Askari
Silvanus aliyeonekana kulewa na kuwaacha wenzie kwenye gari, alichukuwa
hatua hiyo, Mambo alipomtambulisha aliyekuwa Mgombea wa Chadema Kata
hiyo, Yona Kusaja, kwamba, uchaguzi uliopita Kusaja hakushindwa ila
Chama Tawala (CCM) kilichakachua kura zake na kutoa vitisho kwa wapiga
kura.
Friday, July 26, 2013
HUYU NDO MSANII ALIYETANGAZA KUMPORA MUME WA AUNT EZEKIEL... !!!
![]() |
Vai wa Ukweli bila ya kupindisha maneno amedai kuwa hapati usingizi kutokana na kumzimia Sunday Demonte ambaye ni mume wa Aunt.
Akizungumza na mwandishi wetu, Vai alisema ili kuonesha kuwa anachokisema kinatoka moyoni mwake, amekata vipande vya picha za Dimonte na kuvibandika chumbani kwake.
“Kusema ukweli nampenda sana Sunday na sijaanza kumpenda leo wala jana kwani namfahamu tangu zamani alipokuwa Kariakoo,” alisema Vai.
Msanii huyo chipukizi alisema anamuonea wivu Aunt kwa kuamini kuwa anafaidi sana kwa kuwa na mwanaume huyo.
Kwa upande wake Aunt alishangazwa na taarifa hizo na akaomba atafutwe baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili ajue cha kufanya.
FABREGAS AFUNGUKA, ATAMANI KUJIUNGA NA MOYES, VAN PERSIE OLD TRAFFORD
Haijulikani hatima yake: Cesc Fabregas anaweza kujiunga na Manchester United
Lakini
ukweli ni kwamba Fabregas amewaambia maswahiba wake wa England kuwa
anataka kuondoka Camp Nou, na hii inawapa moyo zaidi kumnasa.
Inafahamika
kuwa Fabregas amevutiwa na ahadi nzuri ya kucheza muda wote katika
kikosi cha United na anapenda kujiunga na nyota mwenzake wa zamani wa
Asernal, “Hakunaga” Robin Van Persie ambaye kwa sasa ndio roho ya
ushambuliaji ya pale Old Trafford.
MZEE SMALL ANAENDELEA VIZURI KIASI,LAKINI BADO ANAHITAJI MSAADA WETU WADAU

Taarifa ya Mrejesho : Hali ya Msanii nguli wa maigizo hapa nchini Tanzania, Ndg
Said Bin Wangamba almaarufu kama Mzee Small inaendelea vizuri, na
ANASHUKURU sana kwa wale wote wanaomkumbuka katika kipindi hiki kigumu
cha maradhi. Kwa sasa anaweza kujikongoja taratibu mwenyewe.,
Anaendelea na mazoezi ya kila siku, na kubwa ni dozi ya dawa kwa ajili
ya kumsaidia kuondoa uvimbe uliogundulika miezi kadhaa iliyopita,
kichwani mwake ambapo dozi moja tu inagharimu takribani 30,000TZS pamoja
na mahitaji mengine ya lazima ya kila siku,
Kwa
yeyote atakaeguswa tafadhali unaweza kuwasiliana na Mzee wetu kupitia,
M-PESA kwa kutumia namba ya Said Ngamba (Mzee Small) 0754647265 na
TIGO PESA kwa kutumia namba ya mkewe 0658111311,
Changamoto: Ni Wakati MUAFAKA Sanaa kuwa Ajira Rasmi na yenye MAPATO STAHIKI, Alituchekesha na kutuondolea uchovu kwa kipaji chake, nasi tumkumbuke na kumuenzi,
Matukio-Amani OleAfrika Aranyande M Chuma
MAJANGA MADANGURO YA MAKAHABA YAZIDI KUFUMULIWA....!!!

Hili ni sakata la
kikongwe
mmoja anayedaiwa kumiliki idadi kubwa ya madanguro katika uwanja wake na
kuwapangisha makahaba katika eneo maarufu kwa jina la Kijiji cha
Makahaba.
Mwandishi wetu alipokea ujumbe mfupi ulioelezea ufuska unaofanywa na mabinti ambao hupewa eneo na kujenga vibanda kisha kujiuza kwa bei chee katika kijiji hicho maeneo ya Kigamboni jijini Dar.
Bada ya simu hiyo, uchunguzi wetu ulibaini kwamba, eneo hilo linalofanyiwa
ufuska huo linamilikiwa na kikongwe aliyejitambulisha kwa jina la mzee
Matutu akidaiwa kuendesha maisha kwa biashara hiyo ya madanguro.
Baada ya kujiridhisha na uchunguzi kuwa ni kweli jambo hilo linafanyika eneo hilo,waandishi walivamia eneo la tukio wakiwa na mjumbe wa mtaa huo aliyefahamika kwa jina la Abbas na kujionea madanguro yaliyojengwa kwa mstari ambapo milango yake iliachwa wazi huku ndani wakionekana mabinti wakiwa wamejilaza kihasarahasara wakiwatega wateja wanaopita katika mtaa huo.
Mwandishi wetu alipokea ujumbe mfupi ulioelezea ufuska unaofanywa na mabinti ambao hupewa eneo na kujenga vibanda kisha kujiuza kwa bei chee katika kijiji hicho maeneo ya Kigamboni jijini Dar.
Baada ya kujiridhisha na uchunguzi kuwa ni kweli jambo hilo linafanyika eneo hilo,waandishi walivamia eneo la tukio wakiwa na mjumbe wa mtaa huo aliyefahamika kwa jina la Abbas na kujionea madanguro yaliyojengwa kwa mstari ambapo milango yake iliachwa wazi huku ndani wakionekana mabinti wakiwa wamejilaza kihasarahasara wakiwatega wateja wanaopita katika mtaa huo.
MAAJABU: BINTI ALIYEZALIWA BILA MACHO WALA PUA ATAKIWA KUTOA UBAVU WAKE ILI AFANYIWE UPASUAJI...!!!

Brave anategemewa kufanyiwa upasuaji huo (July 31) mwaka huu ambapo inategemewa sehemu ya mfupa utaondolewa katika ubavu wake kwaajili ya kutumika kutengeneza paji la uso wake, mfupa huo utasaidia kama kiunganishi cha pua mpya atakayowekewa.
IRENE UWOYA AREJEA NCHINI KUTOKA KWA MSWATI - AMEAIDIWA MAMBO MAKUBWA
Mwigizaji Irene Uwoya amerejea nchini toka nchini Swaziland alipokuwa kwa takribani wiki tatu.
Irene Uwoya aliyerejea nchini leo hii amerejea na salamu toka nchini Swaziland alizoziandika kupitia ukrasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii alisema…
Irene Uwoya aliyerejea nchini leo hii amerejea na salamu toka nchini Swaziland alizoziandika kupitia ukrasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii alisema…
“Mswat anawasalinmu sana! Nahiv karibun atatinga hapa nakanipa kibali chakufanyya move na ful suport...I wl prove u wrong...try me”
Akimaanisha, amerejea nchini na Mswati amnawasalimia sana na amesema atakuja nchini hivi karibuni na amenipa kibali cha kufanya Filamu na atanisaidia kwa kila kitu. Nijaribu nitakuthibitishia kuwa umekosea (Kwa Kiswahili fasaha).
Bado tunamtafuta Irene amabye namba yake ya simu haipatikani kujua kama kauli hii ni ya kweli au anawatania tuu mashabiki wake.
Thursday, July 25, 2013
ALEX SONG SAYS CESC FABREGAS "WILL NOT BE LEAVING BARCELONA"
Alex Song: With Cesc Fabregas at Barcelona last season
Alex Song is convinced Cesc Fabregas will still be a Barcelona player at the start of the new season.
Song,
the former Arsenal midfielder who spent six years at the Emirates
before moving to Spain in 2012, says his team-mate has no intention of
quitting Camp Nou. Fabregas, also a former Gunner, has been the subject of two bids from
Manchester United already this summer, and David Moyes said this week
he will give the transfer "every opportunity to materialise".
But
after featuring in Barca's friendly defeat at Bayern Munich Song
told Sky Sports News he is "100%" sure Fabregas is going nowhere. He
said: "I did not speak with him but I know Cesc is 100 per cent here.
"He loves Barcelona, he loves the club. He will stay here next season
and give 100 per cent because I know him very well and he'll want to
fight. He's focused on the club.
"He wants just to give his best for Barcelona. He's from Barcelona,
he loves Barcelona and he'll want to start the season to show what he
can do.
"People are talking and talking, but we know he is focused here and ready to start the season."He's enjoying a holiday with his family and I'm sure he wants just to come back here. "It's my own opinion but I know he will stay here, 100 per cent."
MAAJABU:- MTOTO WA MWAKA MMOJA APATA UJAUZITO...!!!
Madaktari wa nchini China walishangazwa kuona mtoto wa mwaka mmoja ana ujauzito.
Mtoto Kang Mengru wa nchini China alipelekwa hospitali baada ya wazazi wake kushtushwa na hali ya tumbo lake kuzidi kuwa kubwa siku hadi siku.
Baada ya mtoto huyo kufanyiwa ultrasound, madaktari waligundua kuwa mtoto huyo wa kike alikuwa amebeba kitoto kichanga kwenye tumbo lake ambacho kilikuwa kikiendelea kukua.
Madaktari wanaamini kuwa mama wa mtoto huyo alikuwa na mimba ya watoto wawili mapacha na pacha mmoja alijitokeza ndani ya tumbo la pacha mwenzake.
Hali kama hiyo ya kichanga kuzaliwa ndani ya kichanga kingine ni nadra sana kutokea na humtokea mwanamke mmoja katika wanawake 500,000.
Mtoto Kang atafanyiwa upasuaji kukiondoa kichanga hicho tumboni mwake.
Wednesday, July 24, 2013
HATIMAE KITUKUU CHA MALKIA ELIZABETH CHAPEWA JINA....!!!
Prince William akiwa na familia yake saa24 baada ya mtoto George Alexander Louis kuzaliwa.
Prince William alipokuwa amezaliwa akiwa amebebwa na baba yake Prince Charles na mama yake Princess Diana mwaka 1982.
RAIS KIKWETE AWASILI BUKOBA, AKUTANA NA TAIFA STARS MWANZA, AWATAKIA USHINDI DHIDI YA UGANDA

Jakaya Mrisho Kikwete akifungua jengo la Kagera Coperative Union leo Julai 24, 2013
mjini Bukoba.
mjini Bukoba.

Picha ya Pamoja
MBONA MAJANGAAAAA: ALIKIBA NAE ATIWA MBARONI NJE YA NCHI... KISA ........!!!
Meneja wake Guru akiongea na mama yake Ally Kiba nyumbani kwao Kariakoo amesema bwana mdogo alikuwa uwanja wa ndege wa Amsterdam akisubiri ndege za American Airlines ili aelekee jijini Oklahoma City USA akiwa na mwanamama maarufu mwenye mvuto hapa bongo ndipo alipokamatwa.
Haijajulikana sababu za kukamatwa kwake na mpaka leo familia wapo kimya hawajafunguka na wanailinda habari isivuje japo baadhi ya wadau washazinasa. Haijajulikana sababu za kukamatwa ila mpaka kesho media zitatuambia sababu. Sina hakika kama kisa cha kukamatwa bwana Singleboy ni kitu cha Sembe au laaaaa!!! TUSUBIRI
HII NDIO PARTY TWO YA BIFU LA IRENE UWOYA NA LUCY KOMBA...!!!
NYOTA wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Mama Krrish’ ametoa kali ya mwaka baada ya kudai kwamba amemshika ugoni msanii mwenzake, Lucy Komba mara baada ya kuziona picha za msanii huyo akiwa na mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ wakiigiza filamu. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutokea nchini Swaziland, Uwoya amepinga vikali utetezi unaosemwa kwamba Lucy na Kataut walikuwa wakishuti filamu na anaamini kuwa msanii huyo ameamua kumzunguka na kutaka kuibomoa ndoa yake. “Lazima kuna kitu kinaendelea kwani katika dunia hii sijawahi kuona filamu inayochezwa na watu wawili tu mwanzo mpaka mwisho, ninachotaka kusema ni kwamba Lucy ana mpango wa kuiharibu ndoa yangu,” alisema Uwoya kwa hasira.
Uwoya amehoji usiri wa filamu hiyo na kila alipokuwa akimpigia simu mumewe alikuwa akimjibu kwamba yuko Rwanda kumbe alikuwa Bongo akiigiza filamu na Lucy. “Kwanza Lucy ashukuru niko mbali, laiti ningekuwa karibu angenieleza vizuri kwa sababu hata yeye angeweza kunipigia simu na kunifahamisha ushiriki wa mume wangu kwenye filamu hiyo kwa kuwa namba zangu anazo, ilikuwaje hakufanya hivyo?” alihoji.
Kuonesha kwamba amechukizwa na kitendo hicho, Uwoya alisema kwamba akitua Bongo atamtafuta Lucy ili aweze kumshughulikia vizuri na ikiwezekana amuoneshe hiyo filamu waliyoigiza watu wawili tu. “Nitatua Bongo siku si nyingi na cha kwanza ni kumtafuta Lucy, anieleze vizuri kuhusu filamu hiyo waliyocheza na mume wangu,” alisema Uwoya. Filamu hiyo ambayo imekuwa maumivu makubwa kwa Uwoya, imechezwa na Lucy na Ndikumana tu mwanzo hadi mwisho na imepewa jina la Kwa Nini Nisikuoe
STARS YAMALIZA KAMBI YAKE JIJINI MWANZA KUONDOKA KESHO KUELEKEA UGANDA, KASEJA BADO CHAGUO BORA.
![]() |
Kocha
mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen (kulia) akizungumza na wandishi wa
habari (hawako pichani) ikiwa ni siku moja kabla ya kuondoka jijini
Mwanza mara baada ya kumaliza kambi, kushoto ni Afisa habari wa TFF
Michael Wambura.
|
NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
Ni
takribani majuma mawili sasa Taifa Stars imekuwa jijini Mwanza ikiweka
Kambi kuelekea kipute cha marudiano na 'The Cranes', katika mchezo
unaotarajiwa kuchezwa jumamosi hii ya tarehe 27 mwezi wa 7mwaka 2013
mjini Kampala.
Sasa kambi
imefikia tamati, yamesalia masaa kadhaa ambapo kesho mchana majira ya
saa 7 na dakika 25, wawakilishi hao wa taifa la Tanzania, Taifa Stars
wataondoka kwa ndege ya Shirika la Precission Air kuelekea nchini Uganda
kuisaka tiketi ya CHAN.
Msikilize hapo chini
.
Msikilize hapo chini
.
KWA UFUPI:
Kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen amezungumzia mapengo yaliyopo
kwenye kikosi chake kuanzia kutokuwepo kwa Kapombe kwenye idara ya
ulinzi na sasa Mwinyi Kazimoto katika idara ya kiungo, bila shaka kikosi
kitakuwa na utofauti ambao anaona ni sehemu ya marekebisho na
anamaboresho.
WASHINDI WA TIGO ‘MILIKI BIASHARA YAKO’ WAKABIDHIWA BAJAJI ZAO

Meneja
Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga (kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi
wa pili wa promosheni ya ‘Miliki Biashara Yako’, Bw. Riziki
Lucas Kisemo (36) mfanyakazi wa viwandani, mkazi wa Makabe, Dar es Salaam. Tigo
tayari imelipia leseni ya barabani (Road license) na bima kwa ajili ya Bajaji
hizo. Anachotakiwa mteja sasa, ni kuanza biashara yake bila shida mara moja.

Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga
(kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi wa kwanza wa promosheni ya
‘Miliki Biashara Yako’, Bw. Mohamed Ramadhani Mnjori (39) muuza nguo za
mitumba, mkazi wa Ilala – Dar es Salaam kwenye halfla ya makabidhiano
iliyofanyika eneo la Soko Kuu la Kariakoo, Dar es Salaam.
SHILOLE MATATANI WIZI SIMU ZA DIAMOND...!!!
Stori:Shakoor Jongo na Musa Mateja
STAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ..........
ameingia matatani akidaiwa kuingia mitini na simu tatu za mkononi alizoaminiwa nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kufanya shoo.
Msanii huyo alikumbwa na kasheshe hilo Julai 19, 2013 nyumbani kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sinza Mori, Dar. Siku hiyo Diamond alikuwa akifuturisha na aliwaalika watu mbalimbali wakiwemo mastaa lakini nusura futuru iingie doa kufuatia zogo hilo.
Tuesday, July 23, 2013
MASELA WAUWANA KWA MARUNGU KISA DEMU WA KISUMKUMA...!!!

Mnamo tarehe 21/07/2012 majira ya saa 23:30hrs huko kijiji cha Nkwangu wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya, Seni s/o Sandu, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu aliuawa kwa kupigwa fimbo kichwani na Tolo s/o Seko, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu.
Chanzo ni ugomvi wa kumgombania msichana aitwaye Holo d/o Kulwa, miaka 16, Msukuma mkulima na mkazi wa Nkwangu.
Mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaandaliwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anatoa wito kwa jamii kutojichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na kudhibiti hasira zao kwa kuyatatua matatizo ya kimapenzi kwa njia ya mazungumzo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Signed by, [Diwani Athumani – ACP] kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya.
Source: Watemi
Subscribe to:
Comments (Atom)











