MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeanza kusikiliza kesi inayomkabili msanii wa filamu, Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili, huku upande wa mashtaka ukiiomba mahakama hiyo kubadili hati ya mashtaka.
Akiwasilisha hoja hiyo juzi mbele ya Hakimu Thomas Simba, Mawakili upande wa jamhuri, Constantine Kakula na Paulina Fungameza, walianza kuwasomea upya mashtaka washtakiwa hao ambao ni Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili, Angelina Msigwa na Matrida Abas.
Alidai shtaka la kwanza linalowakabili watuhumiwa hao ni pamoja na kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya ambapo mnamo Februari 4, mwaka huu katika maeneo ya Kunduchi Ununio, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kukutwa na msokoto mmoja na vipisi vya dawa za kulevya aina ya bangi yenye gramu 1.08.