Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa mtaalamu kutoka
kampuni ya Symbion iliyopewa kazi ya kujenga miundombinu ya umeme katika kijiji cha Nyamikoma kilichopo
wilayani Busega Bw. Steve Thomson
(kushoto)
Meneja wa Tanesco- Kanda
ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma, akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo na wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega
(hawapo pichani)
Mkazi wa kata ya
Ijitu iliyopo wilayani Busega
ambaye jina lake halikupatikana mara moja akitoa hoja yake
mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka
kushoto waliosimama mbele) mara Waziri
alipofanya ziara katika kijiji hicho na kusikiliza kero za wananchi
Diwani wa Kata ya
Ijitu iliyopo wilayani Busega Vumi Magoti akielezea kero za umeme katika kata yake mbele
ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka
kushoto), viongozi na wananchi (hawapo
pichani).
Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya
Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo
anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu,
Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.