Monday, August 18, 2014

MeTL GROUP YAPATA MKOPO WA BILIONI 300/- KUTOKA RMB...!!!

signing deal
Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane (wa pili kulia) wakitiliana saini ya mkopo huo wa bilioni 300 za kitanzania. Kushoto ni Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipul Kakad na kulia ni Gregory Havermahl wa RMB wakishuhudia tukio hilo la utiliaji saini wa mkopo baina ya RMB na MeTL Group.

 Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imetiliana saini mkataba na benki ya Rand Merchant (RMB) ya Afrika Kusini utakaoiwezesha kupata mkopo wa zaidi ya sh bilioni 300. Mkataba huo umetiwa saini nchini Afrika Kusini na Ofisa Mtendaji Mkuu MeTL GROUP, Mohammed Dewji.

Akizungumza kabla ya kutiwa saini kwa mkataba huo,Dewji alisema kwamba mkataba huo wa kihistoria unatokana na RMB kuiamini kampuni yake ya MeTL tangu walipoanza mahusiano ya kibiashara mwaka 2007.

“MeTL na RMB tulianza mahusiano yetu mwaka 2007, wakati RMB ilipotukopesha dola za Marekani milioni 7.5million. Wakati huo MeTLilikuwa na bidhaa mbili tu,ngano na sukari! Toka wakati huo, MeTL imekuwa ikikua na kuongeza bidhaa zaidi.” Alisema Dewji na kuongeza kuwa mwaka jana 2013, uwezo wa MeTL wa kukopa sasa umefikia dola milioni 100. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAN U TAYARI KUMTOA ‘KAFARA’ LUIS NANI ILI KUINASA SAINI YA MARCOS ROJO

1408305526734_wps_2_MANCHESTER_ENGLAND_AUGUST
United wapo tayari kumruhusu Nani (kulia) kujiunga na Sporting Lisbon kama sehemu ya kubadilishana na beki Marcos Rojo.
MANCHESTER United imefanya mazungumzo na Sporting Lisbon ili kumjumuisha Luis Nani kama sehemu ya jaribio la kutaka kumsajili beki wake, raia wa Argentina, Marcos Rojo.
Baada ya mazungumzo baina ya wakala wa Rojo na Sporting mapema wiki hii, United wanajiandaa kumjumuisha Nani kwa mkopo.
Hata hivyo winga huyo mwenye miaka 27 anaonekana kuweka ngumu kurudi katika klabu yake hiyo ya zamani ya nchini Ureno.
Sporting wao wanahitaji kumuuza Rojo kwa paundi milioni 24, lakini wiki hii Man United waliweka mezani dau la paundi milioni 16.
Rojo, 24, aliwaomba radhi mashabiki wa Sporting katika mahojiano maalumu na TV ya klabu jumapili usiku baada ya kujaribu kulazimisha kuondoka.
Apology: Rojo said sorry to the Sporting Lisbon fans on Sunday night for attempting to force through a move

ANGALIA PICHA ZA WASANII WALIOPITIA MORO KUMFARIJI AFANDE SELE KWA MSIBA WA MAMA TUNDA...!!!

Baadhi ya Wasanii waliokuwa kwenye onesho la Kilimanjaro Music Tour lililofanyika mkoani Dodoma jana, leo walipitia nyumbani kwa Mfalme wa Rhymes a.k.a Simba Mzee a.k.a Afande Sele kumpa mkono wa pole na kumfariji kufuatia kifo cha Mzazi mwenzake Mama Tunda kilichotokea mwisho mwa wiki mjini Morogoro. Pichani ni Msanii wa Muziki wa Bongofleva atambulikae kwa jina la Shilole akimfariji Afande Sele.

Malkia wa Taarab hapa nchini, Bi Khadija Kopa akimfariji Afande Sele,pichani nyuma ya Afande Sele ni guli wa muziki wa Reggae hapa nchini, Innocent Nganyagwa.
Afande Sele akifarijiwa na mkali wa Hip Hop katika anga ya muziki wa Bongofleva, Joh Makini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

LIPUMBA: MOYO WETU UKAWA NI WAJUMBE 14

Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa gazeti hili.

Wakati mchakato wa Katiba mpya unaendelea mjini Dodoma na suala la theluthi mbili likisumbua vichwa vya wengi, mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameeleza kuwa kura za wajumbe 14 kutoka Zanzibar ndizo zitauokoa au kuukwamisha mchakato huo.
Profesa Lipumba alikuwa kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi nyumbani kwake, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kuhusu mustakabali wa mchakato wa Katiba baada ya kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia kuhudhuria vikao.
Kundi hilo lilisusia vikao Aprili 16 kwa madai kuwa Bunge lilipoteza mwelekeo kwa kuacha kujadili Rasimu ya Katiba, hasa katika suala la muundo wa serikali ya Muungano na kwamba chama tawala, CCM kiliingiza suala la serikali mbili ambalo halimo kwenye rasimu hiyo badala ya serikali tatu.
Kutokana na uamuzi wa Ukawa, ambayo inaundwa na wajumbe kutoka CUF, Chadema, NCCR Mageuzi na baadhi wa kundi la 201 kutoka taasisi mbalimbali za kijamii, kuna shaka kwamba mchakato huo huenda usifanikiwe kutokana na ukweli kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inataka uamuzi upitishwe na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Bara na idadi kama hiyo kutoka Zanzibar. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 18, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

PHIRI AONGEZA DOZI MSIMBAZI, HANS POPPE ASAKA VIFAA KIGALI, YANGA, COASTAL WATIMKIA PEMBA

DSC_0007
WEKUNDU wa Msimbazi Simba wanaendelea vyema na maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kushika kasi septemba 30 mwaka huu.
Simba wamepiga kambi visiwani Zanzibar (Unguja) chini ya kocha mkuu mpya, Mzambia, Patrick Phiri akisaidiwa na kocha msaidizi, kiungo wa zamani wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Suleiman Abdallah Matola ‘Veron’ na kocha wa makipa, Idd Pazzi ‘Father’.
Simba ilianza programu ya mazoezi mara moja kwa siku hapo jana katika fukwe za bahari ya Hindi, lakini Phiri ameamua kuongeza dozi ambapo leo atafanya mazoezi mara mbili, (asubuhi na jioni).
Lengo la Phiri ni kupata muda wa kutosha wa kusuka kikosi chake akijua wazi kuwa msimu ujao atakumbana na changamoto kubwa ya kusaka ubingwa wa Tanzania bara.
Pia kocha huyo alisisitiza suala la mechi za kirafiki ili kukiona kikosi chake kwa mara ya kwanza na kujua nini cha kufanya zaidi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ROBO FAINALI KOMBE LA KAGAME: WANYARWANDA WAANZA KUTIFUANA LEO, AZAM, EL MERREIKH KESHO

AZAM FC
MICHUANO ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati, Kombe la Kagame, imefikia patamu mjini Kigali, Rwanda ambapo hatua ya robo fainali inaanza kutimua vumbi leo hii.
Mechi ya kwanza itaanza majira ya 9:00 alasiri kwa kuwakutanisha Polisi dhidi ya Atletico, zote za Rwanda.
Robo fainali ya pili itaanza majira ya saa 11:00 jioni ambapo timu mbili pinzani nchini Rwanda, Rayon Sport na wanajeshi wa APR wataoneshana kazi.
Kibarua kingine kitaendelea kesho ambapo mechi iliyotabiriwa kuwa ngumu zaidi katika hatua hii ya kombe la Kagame itawakutanisha mabingwa wa Tanzania, Azam fc dhidi ya El Merreikh ya Sudan.
Kutokana na historia nzuri ya El Merreikh katika soka la Afrika mashariki na kati, hakika Azam wametumbukia katika daraja zito, lakini kama watajipanga vizuri wanaweza kuibuka na ushindi.
Meneja wa Azam fc, Jemedari Said alisema wamejiandaa vizuri na wanafurahia kuchuana na timu ngumu ambayo itawapa kipimo kizuri  cha kujua maendeleo ya kikosi chao.
“Sio pambano jepesi, El Merreik ni timu yenye historia kubwa. Sisi kama Azam hatuwaogopi, tunawaheshimu, tutapambana kupata ushindi ili kutinga nusu fainali na hatimaye fainali na kutwaa ubingwa”. Alisema Jemedari.
Jemedari alisema katika mazoezi ya jana jioni, wachezaji wote waliokuwa majeruhi, Waziri Salum ambaye hajacheza mechi yoyote, Saint Prex Lionel, Shomari Salum  Kapombe wote walifanya mazoezi, na kwa mara ya kwanza kikosi kizima kilikuwa uwanjani kujiandaa na mchezo huo.
Mechi nyingine ya kesho jumatano itawakutanisha KCC ya Uganda dhidi ya Altabara ya Sudan Kusini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na Baraka Mpenja

'MCHAWI' AKATALIWA KUINGIA DUBAI

Rolf Bushholz
Mwanamume wa Ujerumani ambaye anaongoza rikodi ya dunia kuwa na mwili uliotogwa mara nyingi kabisa ameketaliwa ruhusa ya kuingia Dubai, baada ya kwenda huko kutokeza katika klabu ya starehe.
Rolf Buchholz, ametogwa mwahala 453 kwenye mwili na uso wake na ana pembe mbili kwenye kipaji.
Ameeleza kwenye mitandao ya kijamii kuwa alikataliwa na maafisa wa uwanja wa ndege kuingia nchini kwa sababu, kama alivosema, alikuwa "mchawi".
Bwana Buchholz ameapa kuwa hatarudi tena Falme za Kiarabu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

WALIOTOROKA ZAHANATI YA EBOLA WATAFUTWA

Ebola  Liberia
Kituo kilichotengwa na kuwekewa karantini kwa sababu ya ebola, kimeshambuliwa na zana kuporwa katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia. Watu kama 20 hadi 30 waliowekwa hapo kuangaliwa kama wana dalili za ebola walitoroka baada ya kituo hicho kuporwa Jumamosi usiku..
Kituo kiko kwenye mtaa wa West Point, wenye wakaazi wengi. Washambuliaji walipora magodoro na vitu vyengine. Mwandishi wa BBC katika kanda hiyo anasema pengine washambuliaji walikerwa kuwa kituo hicho kimewekwa katika mtaa wao.

Wakuu wa Liberia wanajaribu kuwatafuta wagonjwa waliotoroka ili kuwarejesha tena kwenye kituo hicho.
Watu zaidi ya 400 wamekufa kwa sababu ya ebola nchini Liberia kati ya zaidi ya 1,000 katika kanda ya Afrika Magharibi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

Thursday, August 14, 2014

UKAWA WAOMBWA KURUDI BUNGENI


UKAWA waombwa kukubali maoni ya watanzania walio wengi ya kuheshimu pesa za walipa kodi kwa kurudi bungeni na kupingana kwa hoja kwani hoja zao zikiwa za huakika hazitapingwa bali kanuni na taratibu zinazoendesha bunge zitafuatwa badala ya kuendelea kulalamika katika majukwaa ya kisiasa.

Kauli hiyo imetolewa na balozi wa amani Tanzania Risasi Mwaulanga alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo leo jijijni Dar es Salaam.

"Nawaomba UKAWA warudi bungeni ili tuweze kupata katiba mpya itayoyokidhi changamoto za watanzania wote na sio masuala ya vyama vya kisiasa na maslahi binafsi kwani vyama hiyvo vinaweza kutoweka wakati wowote na nchi ikabaki palepale".Alisema Mwaulanga.

Aidha Mwaulanga anaiomba iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya jaji Warioba, viongozi wa dini, na asasi za kiraia kuendelea na jitihada za kuitaka UKAWA kurejea Bungeni ili kurahisisisha upatikanaji wa Katiba mpya yenye maslahi mapana kwa ummma kuliko ya kisiasa.

Balozi huyo wa amani amesema kuwa kauli za vitisho na uvunjifu wa amani unapaswa kupigiwa kelele na kulaniwa na kila mwanademokrasia duniani katika kipindi hiki cha kuandaa Katiba mpya ili wajumbe waweze kuwa huru wakati wa kutoa maoni.

Tanzania ni nchi ya amani,umoja, upendo na maelewano na siyo nchi ya vita,chuki na mafarakano hivyo watanzania tunapaswa kutambua ni Katiba gani tunayoitaka na kuwa na mtazamo sahihi na maamuzi bora. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
 
 Na Rose Masaka-MAELEZO

ASKOFU ATUPWA JELA MIAKA 32 KWA UJAMBAZI BENKI...!!!




Benki ya NBC tawi la Moshi. Picha ya Maktaba

Askofu wa Kanisa la Christian Fellowship Assemblies of God la Arusha, Jumanne Kilongola amehukumiwa kifungo cha miaka 32 jela baada ya kupatikana na hatia ya kupora Sh5.3 bilioni ndani ya Benki ya NBC, Tawi la Moshi Mei 21, 2004.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kilimanjaro, Simon Kobelo, askofu huyo amehukumiwa kifungo hicho pamoja na raia watano wa Kenya baada ya kupatikana na hatia ya kufanya wizi huo kwa mtutu wa bunduki.

Kati ya fedha hizo, Sh126.2 milioni zilikuwa mali ya Benki ya NBC wakati Sh5.1 bilioni ni mali ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo ilikuwa ikitumia NBC Moshi kama kituo chake kidogo.

Ilielezwa mahakamani hapo wakati wa ushahidi kuwa Askofu Kilongola ndiye aliyekodi gari aina ya Toyota Landcruiser lililotumiwa kubeba fedha hizo kwa Sh320,000 na alimweleza mmiliki wake kuwa alikuwa anakwenda kubeba wanakwaya wake.

Raia wa Kenya waliohukumiwa kifungo hicho cha miaka 32 ni Wilfred Onyango Nganyi, Patrick Muthee Murithi, Gabriel Kungu Kariuki, Jimmy Maina Njoroge na Simon Ndungu Kiambuthi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KENYA HATArINI KUPATA EBOLA...!!!

Afisa wa shirika la afya duniani aeleza kuhusu janga la Ebola Duniani
Shirika la afya duniani, limetahadharisha kuwa Kenya inaweza kuwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa Ebola, kutokana na kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.
Hatari hii inatokana na Kenya kuwa kitovu cha usafiri wa ndege huku wasafiri wengi wanaokwenda Afrika Magharibi wakipitia nchini humo.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa onyo ya afisaa mkuu wa shirika la afya duniani WHO.(Martha Magessa)
Hili ndilo onyo kali zaidi kuhusiana na ugonjwa wa Ebola kutolewa na shirika la WHO kwamba Ebola huenda ikaenea katika kanda ya Afrika Mashariki.
Wataalamu wa afya wanasema kwamba wanajitahidi kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo Afrika Magharibi, ambako zaidi ya watu 1,000 wamefariki. Canada imesema kwamba itatoa mchango wa dozi 1000 za chanjo ya majaribio ya Ebola kusaidia watu kutoambaukizwa ugonjwa huo.
Kisa cha kwanza cha Ebola,kiliripotiwa nchini Guinea mwezi Februari kabla ya kuenea hadi nchini Sierra Leone na Liberia. Nigeria ni nchi yenye idadi kuwba ya watu barani Afrika na ndio ya hivi karibuni kuripoti kuwa na thuluthi moja ya vifo kutokana na Ebola.
Kisa cha tatu kiliripotiwa siku ya Jumanne.
Mkurugenzi wa shirika la afya duniani tawi la Kenya, Custodia Mandlhate, amesema kuwa nchi hiyo iko katikahatari kubwa ya kupata Ebola.
Hatua za kuzuia maambukizi na kuweza kutambua wagonjwa zimeshika kasi mjini Nairobi katika siku za hivi karibuni.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Serikali hata bhivyo imesema kuwa haitasitisha safari za ndege kutoka katika nchi nne zilizokumbwa na ugonjwa huo Afrika Magharibi.
"Hatushauri, safari za ndege kusitishwa kwa sababu ya mipaka yetu ambayo watu wanaingia na kutoka pasipo vikwazo vingi, '' alisema waziri wa afya James Macharia.
Kenya hupokea zaidi bya safari 70 za ndegekuoka Afrika Magharibi.
Shirika la kikanda la Ecowas, limesema kuwa mmoja wa maafisa wake Jatto Asihu Abdulqudir, mwenye umri wa miaka 36, alifariki kutokana na Ebola nchini Nigeria.
BBC

SOMA HAPA UPATE ELIMU KUHUSU KUJIKINGA NA UGONJWA HATARI WA EBOLA

Hivi karibuni tumesikia Mlipuko wa Ugonjwa Hatari wa Ebola ambapo tayari umesharipotiwa kuua zaidi ya watu 1000 huko Guinea, Siera Lione, Liberia ...Na Juzi umeripotiwa Kuingia Nigeria......na Mpaka Sasa watu takribani 1750 wameripotiwa kuathirika na Ugonjwa huu.
SASA TUJIFUNZE KIDOGO

Ebola Ni Nini?

Ebola ni ugonjwa wa Mlipuko ambao virusi vyake hushambulia mfumo wa Damu wa Binadamu. Kwa Lugha ya Kisayansi Ebola huitwa haemorraghic fever, Ugonjwa huu hupelekea Muathirika kuvuja damu sehemu karibu sehemu yoyote ile ya mwili wake na hatimaye kusababisha kifo kutokana na muathirika huyo kupoteza damu nyingi. Na Kuvuja Damu huko kunaweza kuwa ni ndani ya Mwili au Nje ya Mwili.

Dalili za Ugonjwa Wa Ebola huanza kuonekana siku mbili hadi wiki tatu mara baada ya mtu kuambukizwa virusi hivyo na Kupelekea Homa, Muscle kuuma pamoja na Kichwa Kuuma huku dalili zingine zikiwa ni Kutapika, kuharisha kukifuatiwa sambasamba na Kupungua kwa ufanyaji kazi wa Ini na Figo katika Mwili wa Binadamu.

Virusi Vya Ebola vinaweza kupatikana kwa kugusa damu au majimaji kwenye mizoga ya Wanyama hususani Nyani na Popo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI YA MIVUMONI ILIYOPO KWENYE MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI YATEKETEA KWA MOTO

 Moto Mkubwa ukiendelea kuwaka katika eneo la juu la Jengo la Shule ya Sekondari ya Kiislam ya Mivumoni (Mivumoni Islamic Seminary) iliyopo ndani ya Msikiti wa Mtambani,Kinondoni B Jijini Dar es Salaam leo.

 Moto mkubwa ukiendelea kuwaka kwenye eneo hilo.
 Ulinzi mkali wa Polisi ulitawala katika eneo la Msikiti huo wa Mtambani kuhakikisha Usalama unakuwepo kwenye eneo hilo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BIASHARA MPYA, KONDOM ZAAGIZWA KWA SIMU, ZINALETWA MAHALI ULIPO, SIKILIZA HII...!!!

Huenda uliwahi kupata huduma ya taxi au kuletewa chakula popote ulipo kwa kupiga tu simu, lakini je utanyanyua simu kwa kutaka huduma ya condom?
Kundi la wafamasia nchini Uganda wameibuka na ubunifu wa kipekee wa kupata huduma ya condomu kwa kupiga tu simu.
Huduma hiyo inaitwa DIAL A CONDOM...yaani unapiga simu tu na kuaguza Condom.
Na hutoa nambari za simu ambazo wateja huweza kupiga, kwa ahadi kuwa watapelekewa aina yoyote ya condom katika kipindi cha dakika 15 au chini ya hapo.
Muliro Telewa anaelezea zaidi kuhusu huduma hiyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...