Onyo hilo limetolewa asubuhi hii na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, wakati akieleza Polisi ilivyojiandaa kuhakikisha uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, unafanyika kwa amani na utulivu, Jumapili hii, ya Marchi 16, 2014.
Kamanda Mungi amesema, Intelijensia ya jeshi hilo, imeshawabaini watu ambao wameletwa na baadhi ya vyama vinavyoshiriki kwenye uchaguzi huo, wakitokea mikoa mbalimbali kwa lengo la kufanya vurugu au kutisha wananchi wakati wa kupiga kura na kwamba ikiwa watathubutu kufanya vurugu watakiona cha moto.
“Tunafahamu na tunawajua watu walioletwa na baadhi ya vyama kwa lengo la kufanya vujo hapa Kalenga. Nawatahadharisha watu hao wajue kwamba wakijaribu kufanya vurugu, waliowaleta wataondoka halafu sisi tutabaki nao hapa Iringa kuhakikisha wanakiona cha moto”, alisema kamanda wa Polisi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz