Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa akiwahutubia wakazi wa Kigamboni.
******
Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa amewaomba wanachama
wa CCM kushawishi suala la elimu bure na bora liwe ajenda ya kwanza
katika Ilani ijayo ya uchaguzi ya Chama hicho.
Akiwahutubia
wananchi wa kata ya Kigamboni ambako alikuwa mgeni rasmi katika sherehe
ya kukabidhiwa madawati shule za msingi za kata hiyo, Mh Lowassa
amesema kwa maoni yake anapendekeza suala hilo liwe ajenda ya kwanza
katika Ilani ya uchaguzi ya ccm.
"Wana CCM wenzangu naomba tushawishi suala la elimu bure kwa wanafunzi wote wa shule tena elimu bora liwe la kwanza katika ilani ijayo ya uchaguzi" alisema Lowassa na kushangaliwa na mamia ya wananchi wa kata hiyo.
Alisema kuwa ana ndoto hiyo kuwa siku moja elimu itakuwa bure tena elimu iliyo bora, kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kujenga usawa wa matabaka kwa taifa letu.
Lowassa ambaye ni miongoni mwa wana CCMinakosemekana yuko katika mbio za kuwania urais uchaguzi ujayo, alisema kuwa kutokana na hali nzuri ya uchumi hivi sasa suala hilo linawezekana.
"Wakati Mzee Mkapa anaingia alikuta madeni mengi sana Serikali yake ikafanya juhudi kulipa na kuanza kukopesheka, Rais Kikwete yeye ameunyanyua uchumi kwa kuimarisha miundo mbinu na sasa hali ni nzuri kabisa, hebu sasa tuelekeze nguvu katika elimu"alisema na kuongeza iwe kipaumbele cha sasa.