Like page yetu ya facebook ya Jambo Tz tu-follow instagram @jambotz. YouTube channel @jambotz.
Sunday, February 18, 2018
WAZIRI NCHEMBA AAGIZA WAKIMBIZI WA BURUNDI 32,000 KURUDISHWA KWAO
Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba amewaagiza UNHCR kuwaondoa wakimbizi 32,000 ambao wameomba kwa hiari yao kurudi katika nchi yao ya Burundi haraka tofauti na wanavyofanya sasa.
Waziri Dr Mwigulu ameyasema hayo wilayani Ngara alipotembelea kituo cha mapokezi ya wakimbizi cha Lumasi kujionea shughuli zinazoendela katika vituo vya mapokezi ya wakimbizi ambavyo serikaki ikishaagiza vifungwe mala moja.
Dr Mwigulu amesema shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia UNHCR wao wanafanya kazi masaa 24 katika kuwapokea wakimbizi kuingia nchini lakini wanakuwa wazito pale wakimbizi wenyewe wanapotaka kwa hiari yao kurudi kwao baada ya kujiridhisha kuwa kuna amani nchini kwao.
Friday, February 16, 2018
HII HAPA LYRICS YA WIMBO MPYA WA PAPII KOCHA
Like page yetu ya facebook ya Jambo Tz tu-follow instagram @jambotz. YouTube channel @jambotz.
NIGERIA WAZINDUA NDEGE ISIYO NA RUBANI
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amezindua ndege inayojiendesha yenyewe bila ya rubani ambayo ni ya kwanza kutengenezwa nchini humo.
Kifaa hicho kilichotengenezwa na Taasisi ya Teknolojia ya jeshi la anga la Nigeria, kitatumika kupambana na wapiganaji pamoja na majambazi.
Mipango ya jeshi la nchi hiyo ni kutengeneza vifaa hivyo kwa wingi na pia uwezekano wa kuvisafirisha katika nchi nyingine.
Nigeria imekuwa ikikabiliwa na kitisho cha usalama, ikiwemo wapiganaji wa kiislamu walioko kaskazini mwa nchi hiyo, wapiganaji walioko katika eneo lenye utajiri wa mafuta, kusini mwa nchi na mapigano kati ya wafugaji na wakulima katika jimbo la kati mwa nchi hiyo
Thursday, February 15, 2018
RAIS WA AFRIKA KUSINI AJIUZULU...!!!
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amejiuzulu baada ya shinikizo nyingi kutoka kwa chama chake.
Kapitia hotuba yake iliyopeperushwa kwa njia ya televisheni alisema anajiuzulu mara moja lakini akaongeza kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC.
Chama cha ANC kilikuwa kimemuambia aondoke madarakani au akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.
ZARI AMMWAGA DIAMOND SIKU YA WAPENDANAO
Katika siku ya wapendanao, jana Februari 14, 2018, Mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari the Boss Lady ametangaza kuvunja rasmi mahusiano yake ya kimapenzi na Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Kupitia ukurasa wake wa Instagaram, Zari amefunguka kuwa kilichompelekea kufanya hivyo ni kutokana na Diamond kutokuwa mwaminifu kwenye mahusiano yao huku akibainisha kuwa kuachana katika mahusiano ya kimapenzi hakutaathiri uhusiano wao kama wazazi.
Diamond ambaye alianza mahusiano na Zari takribani miaka mitano iliyopita baada ya kuachana na staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu, amezaa na Zari watoto wawili ambao ni Tiffah na Nilan huku pia akitajwa kuchepuka jambo ambalo limepelekea akazaa mtoto mwingine na mwanamitindo Hamissa Mobeto.
Mbali na Mobeto, Diamond amekuwa akihusishwa kurudiana na Wema ambapo hivi karibuni walionekana kugandana kwenye hafla ya kutambulishwa kwa msanii Mbosso kwenye lebo ya WCB Wasafi.
Bado haijathibitika moja kwa moja iwapo kweli wameachana ama ni kiki kama ambavyo wasanii wengine wamekuwa wakifanya.
KIONGOZI MKUU WA UPINZANI ZIMBABWE AFARIKI DUNIA
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika kusini.
Kwa mujibu wa kiongozi Mwandamizi wa chama cha MDC, Tsvangirai mwenye umri wa 65, na aliyewahi kushika nafasi ya Uwaziri mkuu nchini Zimbabwe ameripotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya utumbo.
Makamu Rais wa chama chama cha MDC Elias Mudzuri ameliambia Shirika la Habari la Uingereza Reuters kwamba marehemu alifariki jioni ya Februar 14.
Monday, February 12, 2018
MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEBRUARY 12, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS
Subscribe YouTube Channel @jambotz
ZUMA KUNG'OLEWA LEO...?!!
Kiongozi wa Chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa chama kitafanya uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya Rais Jacob Zuma.
Akizungumza kaika mkutano wa hadhara mjini Cape Town, Ramaphosa amedokeza kuwa Rais Zuma atatakiwa kujiuzulu.
Amesisitiza kuwa wala rushwa wote wanatakiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria, kitu ambacho anasema Nelson Mandela, baba wa taifa hilo angekitaka.
AGONGWA NA TRENI NA KUFARIKI AKIJIPIGA SELFIE...!!!
Picha haihusiani na tukio hili.
Mwanamke mmoja amefariki akipiga picha aina ya Selfie na rafikiye katika barabara ya treni nchini Thailand.
Rafiki yake alisema kuwa walikuwa wamekunywa pombe na kuamua kujipiga picha hiyo na treni lakini hawakuona treni nyengine iliyokuwa ikija kutoka barabara nyengine ya treni, kwa mujibu wa polisi.
Miguu yake ilikatika na kufariki hospitalini ambako alikuwa amepelekwa kwa matibabu zaidi.
Rafiki huyo wa kiume alipata majeraha mabaya. Idadi ya watu wanaofariki wakipiga selfie katika maeneo hatari inaongezeka.
Wednesday, February 07, 2018
MKUTANO WA KUMJADILI RAIS ZUMA WAAHIRISHWA
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimeahirisha mkutano wa viongozi wa juu wa chama hicho ulio tarajiwa kujadili hatima ya rais Zuma.
Hata hivyo badala yake taarifa iliyotolewa na chama hicho imeeleza kuwa wamekuwa na mazungumzo yenye ufanisi mkubwa na rais Zuma.
Rais Zuma yupo katika wakati mgumu kufuatia shinikizo la kumtaka aachie madaraka ambalo linatoka ndani ya chama chake,halikadhalika upinzani.
Siku ya jumanne bunge la taifa hilo liliahirisha hotuba ya kitaifa iliyotarajiwa kutolewa na rais Zuma.
Hata hivyo baadhi ya mitandao nchini humo imekaririwa ikisema kuwa rais Zuma anajiandaa kuachia madaraka iwapo makubaliano katiika mambo kadhaa yatafikiwa.
Mkutano wa kamati kuu ya chama hicho NEC unatarajiwa kufanyika siku ya februari 17 na 18 kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na kiongozi wa chama hicho cha ANC Cyril Ramaphosa.
Upande wa upinzani wenyewe unashinikiza Zuma kupigiwa kura ya kutokuwa na Imani, huku kikao cha kamati kuu kikidaiwa kuwa na nguvu ya kuweza kumuondoa Zuma madarakani hata bila hiari yake.
Friday, February 02, 2018
MZEE KINGUNGE AFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO
Mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia alfajiri ya leo..
Mzee Kingunge enzi za uhai wake amelitumikia Taifa la Tanzania mpaka ngazi za juu kabisa kama vile kuwa Mkuu wa Mkoa, Mbunge na hata Waziri.
Ni mmojawapo wa vijana wa TANU enzi zao hizo, walioshiriki harakati za kuutafuta uhuru mpaka ukapatikana. Yeye kingunge ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kuzigawa kadi mia za kwanza kabisa za wana TANU baada ya TANU kuanzishwa ambapo, Bwana Sykes ndiye aliyezichapisha kwa pesa za kutoka mfukoni mwake.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Animal.
Tuesday, January 30, 2018
NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NA QT 2017
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) 2017 yametangazwa. Bofya hapo chini
Tuesday, January 09, 2018
Tuesday, January 02, 2018
TAZAMA PICHA 9 ZA BABU SEYA NA FAMILIA YAKE WAKIWA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Disemba 09, 2017 kwenye sherehe za Muungano wa Tanzania, Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 8,158 ikiwemo familia ya Nguza Viking.
Subscribe to:
Posts (Atom)