Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba amewaagiza UNHCR kuwaondoa wakimbizi 32,000 ambao wameomba kwa hiari yao kurudi katika nchi yao ya Burundi haraka tofauti na wanavyofanya sasa.
Waziri Dr Mwigulu ameyasema hayo wilayani Ngara alipotembelea kituo cha mapokezi ya wakimbizi cha Lumasi kujionea shughuli zinazoendela katika vituo vya mapokezi ya wakimbizi ambavyo serikaki ikishaagiza vifungwe mala moja.
Dr Mwigulu amesema shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia UNHCR wao wanafanya kazi masaa 24 katika kuwapokea wakimbizi kuingia nchini lakini wanakuwa wazito pale wakimbizi wenyewe wanapotaka kwa hiari yao kurudi kwao baada ya kujiridhisha kuwa kuna amani nchini kwao.
“Tunaanza kupata wasiwasi kuwa mnafaidika na hawa wakimbizi kubaki hapa nchini wakati wao wanaitaji kurudi makwao, naagiza muwaandikie barua leo hii kuwa hao wakimbizi ambao wapo katika kambi za Nduta, Nyarugusu na mtendeli waondolewe haraka sababu hatuwezi kaa na watu ambao wanaitaji kurudi kwao wakajilete maendeleo,” alisema Dkt. Mwigulu
Waziri Nchemba aliongeza kuwa hatakaa kikao cha pande tatu kujadili kuhusu kuondoka kwa wakimbizi hao kwani wamesha kaa mwaka jana wakakubaliana jinsi ya kuondoka kwa wakimbizi hao nchini kwani mda huu ndii mda wa kilimo na kuwapeleka mwezi wa nne huko nikiwafanya wakaishi maishi magumu zaidi.
Naye mratibu wa wakimbizi kanda ya Kigoma Tonny Laizer amesema kutokana na hali ya usalama nchini burundi pamoja na utekelezaji wa maagizo ya serikali ya kutopokea waomba hifadhi, kituo cha Lumasi kinafungwa na serikali ya wilaya itakabidhiwa na UNHCR kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
No comments:
Post a Comment