Saturday, December 31, 2016

SERIKALI NA UPINZANI WAAFIKIA MWAFAKA DRC

Wapatanishi wanaojaribu kutatua mzozo wa kisiasa huko Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo wamesema serikali ya nchi hiyo na vilevile washirika kutoka makundi ya upinzani sasa wameafikia mwafaka.

Maaskofu kutoka kanisa katoliki waliokuwa wakiendesha kikao hicho cha majadiliano wanasema makubaliano ni kwamba rais Joseph Kabila anaweza kusalia madarakani kwa mda wa mwaka mmoja, lakini ni sharti uchaguzi ufanyike ndani ya kipindi cha miezi 12.

Sharti jingeni ni kuwa rais Kabila asiwanie tena kiti cha urais katika uchaguzi huo.
Mwafaka huo unatarajiwa kutiwa saini hii leo. 

Mda wa utawala wa rais Kabila umemalizika mwezi huu lakini kutong'atuka kwake kumesababisha maandamano yaliyokumbwa na ghasia ambapo watu zaidi ya 40 wamefariki.

TRUMP AMONGEZA PUTIN KWA KUTOLIPIZA KISASI

 
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amempongeza mwenzake wa Urusi Vladmir Putin kwa kutowafukuza wanadiplomasia wa Marekani ,licha ya Marekani kufanya hivyo kujibu madai ya kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Bwana Trump alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter: Hatua nzuri ya kusubiri, nilijua kwamba yeye ni mwerevu sana!.

Moscow imekana madai yoyote ya kuingilia uchaguzi wa Marekani kupitia udukuzi.
Lakini katika hatua moja ya mwisho ya uongozi wa rais Obama ,Marekani iliagiza kuondoka kwa wanadiplomasia 35 wa Urusi kufikia siku ya Jumapili mchana. Lakini Putin alikataa kulipiza kisasi.

Mvutano huo unafuatia madai kwamba Urusi ilidukua kampeni ya chama cha Democrat na mgombea wake Hillary Clinton na kutoa habari kupitia mtandao wa Wikileaks ili kumsaidia Bwana Trump kushinda uchaguzi .

Mashirika kadhaa ya Marekani ikiwemo lile la FBI na CIA yamesema hayo yalitendeka ,lakini Trump amekuwa akipuuzilia mbali madai hayo akisema ni ya ''ujinga''. Hatahivyo amesema kuwa atakutana na maafisa wa ujasusi nchini Marekani ili kuelezewa hali halisi. Serikali ya Obama ilitangaza kisasi hicho siku ya Alhamisi.

Sunday, December 25, 2016

JAMBO TZ INAWATAKIA KHERI YA CHRISTMAS WATU WOTE DUNIANI

 
Jambo Tz inawatakia heri ya Christmas🎄 wakristu na watu wote duniani. Tusherehekee kwa amani na utulivu.
Like page yetu ya facebook/jambotz

Thursday, December 22, 2016

UWEZO WA WANAWAKE KUPATA MIMBA WASHUKA TANZANIA

Viwango vya wanawake kuweza kupata mimba nchini Tanzania vimepungua hadi 5.2 kwa kila mwanamke nchini Tanzania mwaka 2015/2016 kutoka 6.2 kwa kila mwanamke miaka ya 1991/92, kulingana na utafiti wa afya nchini humo

Kulingana na gazeti la The Citizen la nchini Tanzania, utafiti huo uliofanywa na kutolewa na Afisi ya kitaifa ya Takwimu nchini humo NBS wiki iliopita unaonyesha kushuka kwa viwango vya uwezo wa kushika mimba miongoni mwa wanawake .

Kwa mfano mwaka 1996 ripoti hiyo inaonyesha watoto 5.8, mwaka 2004/05} ni watoto 5.7 mwaka 2010 ni watoto 5.4.

WAJUMBE WAIDHINISHA USHINDI WA TRUMP

Wajumbe wa jopo la wateule wanaoamua ushindi wa rais wa Marekani, wamemwidhinisha Donald Trump kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba 8, mwaka huu.

Hatua hiyo imezima juhudi za dakika za mwisho za kutaka kumzuia Trump kuingia ikulu ya White House Januari 20.

Baada ya ushindi huo, Trump ameahidi ‘kufanya kazi kuunganisha nchi yake na kuwa rais wa Wamarekani wote’.

RAIS WA GAMBIA ASEMA HANG'ATUKI MADARAKANI NG'OO............!!!

Rais wa Gambia Yahya Jammeh ameonya kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi wa kieneo kumlazimisha kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi na mfanyibiashara Adama Barrow.

Akihutubia wanachama wa muungano wa Bar Afrika nchini humo Bw Jammeh alisema: ''Waje wajaribu kuniondoa.wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka mshindi''.

Amesema kuwa alikataa wito wa muungano wa viongozi wa mataifa ya Magharibi ECOWAS akiwemo rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia kuondoka nchini Gambia.

Saturday, December 10, 2016

RAIS DR. MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA DANGOTE IKULU DAR ES SALAAM

Rais Magufuli alivyokutana na Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao cha pamoja na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kumaliza kwa kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza kikao chake na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo  Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.

Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

Tuesday, November 01, 2016

WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE KUANZA MITIHANI LEO, WAZIRI AONYA UDANGANYIFU

 
Wanafunzi wa kidato cha nne wakimsikiliza naibu waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo mara baada ya kukagua maandalizi ya mtihani wa kidato cha nne unaofanyika Leo. 
 

Naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiagana na wanafunzi wa  shule ya sekondari Msalato mara baada ya kuzungumza nao.

Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, amefanya ziara kwenye shule mbalimbali mjini Dodoma kuangalia maandalizi kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne unaoanza Leo nchini.

Katika ziara yake kwenye Shule ya sekondari Jamhuri, Kiwanja cha ndege na Msalato, Jafo amewaonya walimu na wanafunzi hao nchini kuepukana na vitendo vya udanganyifu.

Akizungumza na walimu na wanafunzi katika shule hizo, Jafo amesema katika mtihani huo hawatarajii kuwepo na udanganyifu kwa kuwa wamejifunza kupitia mtihani wa darasa la saba ambapo kumekuwepo na tabia ya walimu kujificha chooni ili kuwasaidia wanafunzi.
Amesema shule zitakazofanya fanya hivyo zitakuwa zimepoteza thamani yake. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

WANAWAKE WANAOFANYA NGONO BILA KINGA WANAUWEZEKANO MKUBWA WA KUPATA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI

Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala akiwa anazungumza na waandishi wa habari wanawake kuhusu tatizo la Saratani ya shingo ya Kizazi, katika Ukumbi wa Olasiti Lodge Jijini Arusha, aliyepo kushoto kwake ni Dkt. Mathew Kasumuni kutoka hospital ya Mountmeru iliyopo jijini Arusha.
Waandishi wa habari wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala, Aliyepo kushoto kwake ni Dkt. Mwanahamis Ghembe kutoka Mountmeru Hospital.

Naibu waziri wa Afya Hamisi Kigwangala amesema kuwa wanawake wanaoshiriki tendo la ndoa bila kinga wapo hatarini kupata virusi vinavyoitwa HPV vinavyosababisha   Saratani ya mlango wa kizazi.

Kigwangala amesema wanawake wanaofanya ngono bila kinga wanaweza kupata saratani ya mlango wa kizazi, ambapo husababishwa kwa kufanya ngono bila kinga,huambukizwa  kwa kujaamiana. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 1, 2016 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

20161101_041402

20161101_041409

20161101_041420

Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

Thursday, October 27, 2016

SERIKALI YATANGAZA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2016

Serikali imetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la 7 kwa mwaka 2016 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.52 na shule iliyoongoza kitaifa ni shule ya Msingi Kwema ya mkoani Shinyanga. 

Mtihani huu ulifanyika tarehe 7 na 8 mwezi Septemba mwaka huu. Kutazama matokeo hayo bofya hapa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...