Sunday, April 10, 2016
NDANDA KOSOVO AFARIKI DUNIA
Msanii
mkongwe kwa miondoko ya dansi nchini, ambaye aliwahi kuwa katika bendi ya FM
na baadae kuanzisha yake iliyofahamika kwa jina la Stono Musica au
jina linguine Wajela Jela, Ndanda Kosovo amefariki dunia. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz
Katika
taarifa ambayo imetufikia imeeleza kuwa marehemu amefariki jana asubuhi
katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa alipokuwa
amelazwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo. Mungu ailaze roho ya marehemu peponi, Amin.
YANGA YATOKA SARE NA AL AHLY
Mchezo
wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya 16 kati ya wawakilishi pekee wa
Tanzania katika mashindano hayo, Yanga ya Tanzania na wageni Al Ahly ya
Misri umemalizika katika uwanja wa taifa kwa timu hizo kutoka sare ya
goli moja kwa moja.
Katika
mchezo huo, Al Ahly ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa mchezaji
wake Amr Gamal na dakika chache baadae Yanga kusawazisha baada ya
mchezaji wa Al Ahly, Ahmed Hegazy kujifunga dakika ya 16 ya mchezo huo
ambapo mpaka mchezo unamalizika, Yanga 1 na Al Ahly 1
WADHAMINI WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE WAJITUPA SOKA LA BONGO
Shirikishio la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeishukuru kampuni ya
bia ya Heineken ambao ni wadhamini wakuu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa
barani Ulaya (UEFA) kwa kujitolea kufanya ukarabati wa viwanja vitatu
vya mpira wa miguu vilivyopo jijini Dar es salaam.
Katika barua ya Meneja Mkuu wa Heineken nchini Tanzania, Michael
Mbugu kwenda kwa wakurugenzi ya Manispaa wilaya za Ilala na kinondoni,
nakala yake kutumwa kwa Rais wa TFF, imeeleza mdhamini ameelekeza nguvu
zake kwenye kukarabati baadhi ya viwanja nchini ili viwe katika hali
nzuri na salama ili kukuza vipaji vya vijana kwenye mchezo wa soka.
Heineken imelenga kuboresha dhamira yake ya kushirikiana na jamii
sehemu mbalimbali kwa kuchangia ukarabati wa viwanja vya TP Manzese kata
ya Sinza, Sigara Segerea kata ya Tabata Sigara na uwanja wa Magunia
Msasani uliopo kata ya Msasani.
Kufanya ukarabati wa viwanja hivyo kutatoa nafasi kwa vijana wa
maeneo ya Ali Maua, Darajani, Sweet Corner na Kijiweni (uwanja wa TP
Manzese), Macho, Kisiwani, Msasani na Msikitini (uwanja wa Magunia),
Barakuda, Tabata, Senene, Mwembeni, Chang’ombe, Kinyerezi na Segera
(uwanja wa Sigara) kufanya mazoezi na kuendeleza vipaji vya mpira wa
miguu.
Aidha TFF inazipongeza Halmashauri za Manispaa za Ilala na Kinondoni
kwa kupata nafasi ya kufanyiwa ukarabati viwanja vyao na kampuni ya
Heineken, na kuziomba mamlaka hizo kuvitunza viwanja hivyo ili viweze
kutumiwa na vijana wa kike na kiume katika mchezo wa mpira wa miguu. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
CRISTIANO RONALDO AANDIKA REKODI MPYA LA LIGA
Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 30 ndani
ya misimu sita ya La Liga baada ya Madrid kuichapa Eibar kwa bao 4-0
kwenye mchezo wa ligi. Karim Benema ambaye anapambana na majeruhi ya goti pamoja na Gareth
Bale walipumzishwa wakati Madrid inasubiri mchezo wa marudiano siku ya
Jumanne wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Wolfsburg.
James Rodriguez alianza kuzifungua nyavu za Eibar kwa mkwaju wa mpira
wa adhabu ndogo kabla ya Lucas Vazquez hajapachika bao la pili. Hadi mapumziko tayari Madrid ilikuwa mbele kwa magoli 4-0 huku
Ronaldo akitumbukia nyavuni kupiga bao la tatu akiunganisha pasi ya Jese
ambaye naye alipiga bao na kukamisha idadi ya magoli 4-0.
Real inakumbuka kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa Wolfsburg wakati
ikijiandaa na mchezo wao wa marudiano kwenye uwanja wa Bernabeu huku
kocha wa klabu hiyo Zinedine Zidane kiweka wazi kwamba, endapo
watashindwa kufuzu kwa hatua ya nusu fainali basi msimu wao utakuwa
umemaliza.
Kikosi cha Zidane kwa sasa kipo nyuma ya vinara wa ligi hiyo (Barca)
kwa pointi nne nyuma kikisimama nafasi ya tatu nyuma ya Atletico Madrid. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
Saturday, April 02, 2016
MAKONDA ATANGAZA NEEMA KWA BODABODA
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekutana na waendesha bodaboda na kuahidi kushugulikia kero zinazowakabili ikiwemo kuondoa vikwazo vya wao kuingia katikati ya jiji.
Aidha, amewaahidi kuwapatia pikipiki kwa marejesho ya Sh25,000 kwa wiki kwa muda maalum kabla ya kuwaachia kabisa.
Kwa mantiki hiyo, Makonda amewataka kufanya usajili upya na kusajili vituo vyao ili watambulike kisheria huku akisema atawapatia mavazi maalum 'reflectors' kama utambulisho.
Awali, mmoja wa waendesha bodaboda hao, Daud Laurian alimsomea RC Makonda risala iliyoainisha matatizo yao ikiwemo zuio la ya jiji kutokana na agizo la aliyekua mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick Machi 3, 2014.
Waendesha hao wamehaokikishia Makonda kuwa raia wema katika suala zima la ulinzi iwapo Jeshi la Polisi Kanda Maalum litawachukulia kama ndugu zao na marafiki.
KONDAKTA ALIETISHIA KUMUUA MAGUFULI ASHTAKIWA
Kondakta wa daladala amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kutishia kumuua Rais John Magufuli.
Hamim Seif (42) mkazi wa Mwananyamala Ujiji, alidaiwa kutenda kosa hilo Machi 10 mwaka huu katika baa ya Soweto, maeneo ya Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Wakili wa serikali Keneth Sekwao aliambia mahakama Alhamisi kuwa mshtakiwa, akiwa katika baa hiyo, alitishia kumuua Dkt Magufuli kwa maneno kwa njia ya kujitoa mhanga.
“Kwa haya mambo anayoyafanya Rais Magufuli, mimi nimo tayari kujilipua kwa kujitoa mhanga ili kumuangamiza,” alinukuliwa na Wakili Sekwao. Mshtakiwa alikana shtaka hilo
Hakimu Mkazi, Hellen Liwa aliweka wazi dhamana ya mshtakiwa huyo na kumtaka kutafuta wadhamini wawili, kutoka taasisi ya Serikali inayotambulika, ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni.
Alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na akawekwa rumande hadi 14 Aprili kesi ikatapotajwa tena.
BOKO HARAM WAAPA KUTOSALIMU AMRI
Abubakar Shekau kiongozi wa Boko Haram
Wapiganaji wa kundi la Boko Haram wametoa kanda mpya ya video wakiapa kuendeleza vita vya kutaka uongozi wa sheria za kiislamu.
'Lazima mujue kwamba hakuna ukweli, hakuna majadiliano,hakuna kusalimu amri'', alisema mtu mmoja aliyejifunika uso na kuzungumza kwa lugha ya hausa.
Ujumbe huo unajiri baada ya kanda ya video isiojulikana mwezi uliopita kumuonyesha kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau akionekana dhaifu swala linaloongeza uvumi kwamba mda wake katika uongozi wa kundi hilo unaelekea ukingoni.
Katika kanda hiyo ya video kuna watu wamesimama na bunduki za AK-47 mbele ya magari.
Sunday, March 27, 2016
Friday, March 25, 2016
Tuesday, March 22, 2016
MWALIMU ANAEHITAJI KUBADILISHANA KITUO
TANGAZO: Mimi ni mwalimu wa secondary nipo halmashauri ya Tandahimba nahitaji mwalimu wa kubadilishana nae Mbeya kutoka Iringa, Morogoro, Pwani au tuwasiliane kwa no. 0655591881.
Monday, March 21, 2016
SHEIN ASHINDA URAIS KWA ASILIMIA 91.4
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha amemtangaza Rasmi Mgombea urais wa CCM Dr. Ali Mohammed Shein kuwa mshindi wa kiti cha urais wa Zanzibar akiwa na kura 299.982 sawa na asilimia 91.4.
Sunday, March 13, 2016
Friday, March 11, 2016
HATIMAE MAGUFULI AWAPA SAFARI YA NJE MAWAZIRI WAWILI
Tangu Novemba 5 wakati Dk John Magufuli alipoapishwa, ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustine Mahiga pekee waliotoka nje ya nchi, lakini jana Rais aliwaruhusu mawaziri wengine wawili kusafiri nje.
Rais Magufuli alizuia safari za nje siku chache baada ya kuapishwa akisema watumishi wa umma watakaokuwa wakitaka kwenda nje watalazimika kuomba kibali kutoka Ikulu, ikiwa ni mkakati wake wa kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali.
Tangu wakati huo, safari za nje kwa watumishi wa umma zimekuwa za nadra na mawaziri wamekuwa wakifanya ziara za kwenda mikoani kufuatilia utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
Subscribe to:
Posts (Atom)