Sunday, September 13, 2015

MATOKEO YA MECHI ZA UFUNGUZI WA LIGI KUU TANZANIA BARA (VPL) HAYA HAPA


Pazia la ligi kuu Tanzania bara limefunguliwa rasmi jana ambapo michezo saba zimechezwa kwenye viwanja tofauti wakati jumla ya timu 14 zilikuwa viwanjani zikiwania pointi tatu muhimu, matokeo ya mechi zote zilizochezwa siku ya Jumamosi ni kama ifuatavyo; 

Azam FC 2-1 Tanzania Prisons (Azam Complex, Chamazi) 

African Sports 0-1 Simba (Mkwakwani, Tanga) 

Ndanda FC 1-1 Mgambo JKT (Nangwanda Sijaona, Mtwara)

Toto Africans 1-0 Mwadui FC (CCM Kirumba, Mwanza) 

Stand United 0-1 Mtibwa Sugar (Kambarage, Shinyanga)

Majimaji FC 1-0 JKT Ruvu (Majimaji, Songea) 

Mbeya City FC 0-1 Kagera Sugar 

Leo utachezwa mchezo mmoja wa ligi kuu Tanzania bara kwa kuzikutanisha Yanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA EPL ZILIZOPIGWA JUMAMOSI NDIO HAYA HAPA

Jana kulipigwa michezo saba kwenye ligi kuu nchini England (VPL) ambapo mbali na mchezo wa Manchester United dhidi ya Liverpool, kulikuwa na michezo mingine ambayo huenda hukupata muda wa kuitazama yote kwa pamoja. hapa chini kuna matokeo ya mechi zote saba zilizochezwa Jumamosi.

Friday, September 11, 2015

MBUNGE WA CCM ATOA 'SALARY SLIP' KWENYE MKUTANO WA ACT


Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), aliyemaliza muda wake, Ally Keissy. PICHA|MAKTABA 

Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), aliyemaliza muda wake, Ally Keissy jana aliibuka kwenye mkutano wa kampeni wa chama cha ACT-Wazalendo na kupinga maelezo kwamba mshahara wake wa ubunge ni zaidi ya Sh10 milioni.

Keissy aliwasili kwenye mkutano huo uliokuwa wa mgombea urais wa ACT-Wazalendo, Anna Mghwira na mgombea mwenza wake, Hamad Yusuph Mussa uliofanyika Kijiji cha Namanyere, akiwa kwenye gari lake aina ya Toyota Land Cruiser. 

Mgombea mwenza, Mussa alipopanda jukwaani, alianza kuhutubia kwa kuwaeleza wananchi kwamba mbunge wao, Keissy anayemaliza muda wake ameshindwa kuwaletea maendeleo, hivyo mwaka huu wasimpe kura zao.

ABUBAKAR ZUBERI ACHAGULIWA KUWA MUFTI MPYA WA TANZANIA


Mufti mpya, Sheikh Abubakari Zuberi (aliyeketi katikati) ambaye amechaguliwa leo na wajumbe wa BAKWATA mkoani Dodoma kuwa Mufti wa Tanzania akichukua nafasi ya hayati Sheikh Issa Bin Simba 

ALIYEKUWA Kaimu Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zuberi amechaguliwa kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Sheik Zuberi amewashinda wagombea wengine watatu waliokuwa wakiwania nafasi hiyo ya juu ya kuwaongoza waislamu katika Mkutano mkuu wa Bakwata ulioshirikisha wajumbe zaidi ya 550 ambapowajumbe 310 wa Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata) walipiga kura na kumchagua.

Mashehe wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo ni pamoja na Ally Muhidin Mkoyogole, Khamis Abbas Mtupa na Hassan Ibrahim Kiburwa. 

Mufti Zuberi anakuwa ni Mufti wa tatu kuchaguliwa kushika wadhifa huo akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Marehemu Muftu Issa Shaaban Bin Simba aliyefariki Juni 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Mufti wa kwanza alikuwa Mufti Hemed Bin Jumaa bin Hemed. 

Kabla ya kuchaguliwa , Sheikh Abubakar Zuberi alikuwa Naibu Mufiti wa Sheikh Mkuu wa Tanzania na pia Mjumbe wa Baraza Kuu la Ulamaa nchini.

MAN U YAMRUDIA TENA DE GEA

David De Gea

Manchester United imeanza mazungumzo ya mkataba mpya na mlinda mlango wake David De Gea. 

Mkataba wa sasa na Muhispaniola huyo unafikia ukingoni mwaka 2016 na United wameonyesha matumani ya kurefusha muda wa De Gea kutumika ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi hii ikitokana na mipango ya De Gea kutimkia kunako klabu ya Real Madrid kukwama.

Manager Louis van Gaal hakumtumia mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid mpaka dirisha la usajili lilipofungwa kwa vile hakukuwa na uhakika juu ya mustakabali wake.

Bado haijajulikana kama De Gea ataanza katika mchezo wa jumamosi wa Ligi ligi dhidi ya Liverpool.

Thursday, September 10, 2015

ZIJUE REKODI ZA RONALDO NA MESSI KWENYE MICHUANO YA ULAYA

Messi vs Ronaldo
Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wote kwa pamoja wana magoli 80 katika michuano ya Ulaya–lakini je, kila mmoja amefunga kuoka eneo gani? je, kwa mguu gani (kushoto ama kulia)? ndani ya boksi au nje ya boksi? dhidi ya nani (timu gani)? Takwimu zote zipo hapa

Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

KUMBE ARSENE WENGER ALIKUA ANAKARIBIA KUJIUGA NA REAL MADRID

dadff

Kocha wa club ya Arsenal alikaribia sana kujiunga na club ya Real Madrid, rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon ametoa hiyo siri kwamba walijaribu kumpata kocha mara kadhaa lakini Arsene Wenger alisisitiza kubaki na club yake ya Arsenal.

Ramon Calderon alisema,“Nafikiria kila mtu akiwa kama kocha au mchezaji katika wakati wake kucheza soka lazima atakua na hamu ya kujiunga na club ya Real Madrid, hasa ukiwa kwenye club moja kwa miaka 15. 

Kwa kipindi kile Arsene Wenger alikua anapenda kilichokua kinaendelea kwenye club yetu. Nakumbuka aliniuliza unapanga kutengeneza Hollywood au unataka kutengeneza club ya soka. Alikua anazungumzia sera yetu ya kusajili nyota.”

“Mambo hayakwenda kama tulivyotegemea kwasababu alikua anaipenda sana Arsenal, Wenger ni mtu mwenye heshima sana. Hauwezi kumuona yupo kwenye mzozo, anaweza kuwa kwenye mzozo na marefa lakini haiwezi kuwa kama anavyofanya Mourinho.”

“Wenger ni manager mzuri na mtu safi na nina imani hiyo ndiyo sababu ya mafanikio yake.” Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Wednesday, September 09, 2015

WANNE WAJITOSA KUWANIA UMUFTI WA TANZANIA


KAIMU Mufti wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), Shekhe Abubakar Zuberi Ally ni miongoni wa mashehe wanne waliojitokeza kuwania kuchaguliwa kwenye nafasi ya Mufti kwenye uchaguzi utakaofanyika kesho jijini hapa. 

Akizungumza jana, Shehe wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajab aliwataja mashekhe wengine waliochukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo kuwa ni Ally Muhidin Mkoyogole, Khamis Abbas Mtupa na Hassan Ibrahim Kiburwa. 

Alisema maandalizi ya mkutano mkuu kwa ajili ya uchaguzi huo, yamekamilika na kwamba wajumbe zaidi ya 550 kutoka mikoa mbalimbali, wameanza kuingia. Katika mkutano huo wa uchaguzi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. 

Alisema wajumbe wa mkutano huo wa kumchagua Mufti wa kuiongoza Bakwata ni wengi, ambapo utawashirikisha mashekhe wote wa mkoa, wilaya, mwenyeviti na makatibu wa mkoa na wilaya na Baraza la Maulamaa, pia viongozi wa serikali wataalikwa.

Alisema Mufti atakayechaguliwa atakuwa wa awamu ya tatu, ambapo walitanguliwa na Mufti Hemed Bin Jumaa bin Hemed na Mufti Issa Bin Simba aliyefariki dunia Juni 22, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam.

WANAFUNZI 775,729 KUFANYA MTIHANI WA DARASA LA SABA


JUMLA ya watahiniwa 775,729 wanatarajiwa kuanza mtihani wa kumaliza elimu ya msingi utakaofanyika leo na kesho nchi mzima.

Aidha, serikali imesema hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kumzuia mtahiniwa yeyote kufanya mtihani kwa sababu yoyote ile, hata ikiwa ni kutolipa ada.

Akizungumza jana, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania, Dk Charles Msonde alisema kati ya hao, watahiniwa wavulana ni 361,502 ambao ni sawa na asilimia 46.6 na wasichana ni 414,227 sawa na asilimia 53.4.

Watahiniwa wasioona walioandikishwa kufanya mtihani ni 76, wakiwemo wavulana 49 na wasichana 27 wakati wale wenye uoni hafifu wanaohitaji maandishi makubwa ni 698, wavulana wakiwa ni 330 na wasichana 368.

Monday, August 31, 2015

MAMBO 10 YA KUZINGATIA ILI SHERIA YA MTANDAO ISIKUPITIE

1. Epuka Kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii yetu kupitia mitandao

2. Epuka Kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza kupelekea kuvuruga amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao

3. Epuka Kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadili kwa jamii kupitia mitandao mbalimbali ( Whatsapp, Facebook, YouTube, Instagram n.k)

4. Epuka Kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya kijamii

Friday, August 28, 2015

ANGALIA MAJINA YA WALIOKOSEA KUJAZA FOMU ZA MIKOPO KWENDA CHUO KIKUU 2015/2016

https://www.facebook.com/jambotz
Kuangalia majina ya waliokosea bofya hapa. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz upate habari zetu haraka zaidi.
http://jambotz8.blogspot.com/
Bofya Hapa au picha yeyote hapo juu.

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU (HESLB) YAWATAKA WAOMBAJI WAREKEBISHE TAARIFA ZAO

 
Mkurugenzi Mtendaji HESLB Bw. George Nyatega

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao fomu za maombi zimegundulika kuwa na upungufu na kuwataka kufanya marekebisho kabla au ifikapo tarehe 11 Septemba mwaka huu (2015).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi hiyo leo (Ijumaa, Agosti 28, 2015), jumla ya fomu za waombaji wa mikopo 7,788 kati ya 68,445 zilizopokelewa na kuhakikiwa zimegundulika kuwa fomu zina upungufu na kuwataka waombaji kusoma majina yao katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega, waombaji ambao fomu zao zimegundulika kuwa na upungufu wanatakiwa kurekebisha kabla au ifikapo tarehe 11 Septemba mwaka huu (2015). Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

JOKATE MSEMAJI KAMATI MPYA YA MISS TANZANIA

MSIMAMIZI wa mashindano ya Urembo Tanzania, ‘Miss Tanzania’, Hashimu Lundenga, ametambulisha kamati mpya ya muda inayoundwa na wajumbe 12 akiwemo Jokate Mwegelo aliyekuwa Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ni Juma Pinto, makamu mwenyekiti, Lucas Ritta, katibu mkuu ni Doris Mollel na Joketi Mwegelo ambaye ndiye anakuwa msemaji wa kamati hiyo. 

Wajumbe wengine ni Hoyce Temu, Mohamed Bawazir, Gladyz Shao, Magdalena Munisi, Shah Ramadhani, Hamm Hashim, Khalfan Saleh na Ojambi Masaburi.

Lundega alidai ameunda kamati hiyo ili kubadilisha mwonekano mpya wa wajumbe katika shindano hilo kwa mwaka huu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page yetu ya facebook bofya Jambo Tz sasa

WATU 9 WA FAMILIA MOJA WATEKETEA KWA MOTO, ANGALIA PICHA ZAIDI


Askari na wakazi wa Buguruni Malapa, Dar es Salaam wakitazama nyumba iliyoteketea kwa moto na kuua watu tisa wa familia moja usiku wa kuamkia jana.

Watu tisa wa familia moja wameteketea kwa moto baada ya nyumba yao kuungua usiku wa kuamkia jana jijini Dar es Salaam, huku mashuhuda wakisema walikuta miili yao ikiwa imeshikana.

Juhudi za kuwaokoa watu hao waliofariki dunia wakiwa kwenye moja ya vyumba vya nyumba hiyo namba 40 iliyoko katika Mtaa wa Ulam, Buguruni Malapa wilayani Ilala, zilishindikana na chanzo cha moto huo hakijajulikana ingawa mashuhuda wanasema mtungi wa gesi ulilipuka baada ya moto kuwaka kwa muda mrefu.

Walioteketea katika tukio hilo ni mama wa familia hiyo, Samira Juma Ibrahim (42), maarufu kwa jina la Mama Aisha na watoto wake wanne, Ahmed Masoud (15) aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Aisha Masoud (17), aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la sita, Abdillah Masoud (10) na Ashraf Masoud (5).

Wengine ni Bimdogo Masoud (72), ambaye alikuwa mgonjwa na mama wa Samira, pamoja na wadogo zake wawili wa kike, Samira Harood (17) na Wahat Saleh (27), ambaye alitokea Unguja, pamoja na Fahir Fesal mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page yetu ya facebook bofya Jambo Tz sasa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...