Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiaga waandishi wa
habari baada ya kuwatangazia kujivua wadhifa huo katika mkutano
alioufanya Dar es Salaam jana.
Hakuna neno jingine linalofaa
kuelezea hali ilivyo ndani ya Ukawa zaidi ya “mtikisiko” baada ya
Profesa Ibrahim Lipumba kuamua kujivua uenyekiti wa Chama cha Wananchi
(CUF) wakati mkakati wa vyama vya upinzani kushirikiana kutaka kushika
dola ukiwa umeshika kasi.
Uamuzi wa Profesa Lipumba,
mmoja wa waasisi wanne wa Ukawa-Umoja wa Katiba ya Wananchi unaoundwa na
vyama vinne vya Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na NLD-,unamaanisha
anapoteza wadhifa wake wa mwenyekiti mwenza wa umoja huo ambao umeamua
kushirikiana kwenye Uchaguzi Mkuu kwa kusimamisha mgombea mmoja kuanzia
ngazi ya urais hadi udiwani atakayeungwa mkono na vyama hivyo.
Wengine
walioongoza harakati za kuasisi Ukawa ni Freeman Mbowe, ambaye ni
mwenyekiti wa Chadema, James Mbatia wa NCCR-Mageuzi na Emmanuel Makaidi
wa NLD. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.