Sunday, June 07, 2015
Friday, June 05, 2015
IDADI YA WALIOFARIKI GHANA YAFIKIA 175
Takriban
watu 175 wamefariki kufiakia sasa kufuatia moto uliotokea katika kituo
kimoja cha mafuta katika mji mkuu wa Ghana Accra.
Moto huo
uliozuka siku ya jumatano usiku ulianza wakati wakaazi wa mji huo
walipokuwa wakikabiliana na siku mbili za mvua kubwa ambayo imewaacha
raia wengi bila makaazi pamoja na stima.
Mafuriko hayo yaliathiri juhudi za uokozi na huenda yalisababisha moto kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Darko mjini Accra. Tayari Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo hivyo.
Mlipuko huo ulitokea hapo jana
wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha
mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha. Rais wa Ghana, John Mahama amesema janga hilo halitajirudia tena.
RAHEEM STRLING KUELEKEA OLD TRAFFORD
Mshambuliaji
wa Liverpool Raheem Sterling huenda akaelekea katika kilabu ya
Manchester United ,hatahivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ana
wasiwasi kuhusu athari za uhamisho huo hususan kutokana na ushindani
mkali uliopo kati ya klabu hizo mbili.
Sterling amekataa ombi la kitita cha pauni laki moja kutoka kwa Liverpool akisema kuwa anataka kuondoka na kukichezea kilabu ambacho kina uwezo wa kushinda mataji. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.
SERENA ATINGA FAINALI FRENCH OPEN 2015
Serena
Williams amefanikiwa kutinga fainali za michuano ya tenis ya French
Open. Licha ya kujisikia kuumwa Serena aliweza kupambana vikali na
kumbwaga mpinzani wake Timea Bacsinszky kwa seti 4-6 6-3 6-0 na kufuzu
kucheza fainali za mwaka huu.
Serena nambari moja duniani kwa wanawake sasa atapambana na Lucie Safarova katika mchezo wa fainali kesho, Jumamosi. Serena amekuwa akiumwa kipindi chote cha michuano hiyo, kiasi kwamba anasema hakutarajia kushinda katika mchezo huo.
Serena anajaribu kushindi taji la tatu la michuano hiyo ya French Open na taji la ishirini la michuano mikubwa. Mapema
katika uwanja wa Philippe Chatrier, Safarova wa 13 kwa ubora alimtupa
nje MSerbia Ana Ivanovic na kuwa mwanamke wa kwanza wa Czech kufika
fainali za michuano hiyo katika uwanja wa Roland Garros katika kipindi
cha miaka 34.
Kwa upande wa Wanaume, fainali zitafanyika Jumapili hii. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.
Tuesday, June 02, 2015
AL-SHABAAB WADAIWA KUVITEKA VIJIJI KENYA
Hofu
kubwa imetanda Kaskazini mwa nchi ya Kenya,baada ya kuwepo kwa taarifa
kwamba kundi la wapiganaji wa Al shabaab Limeviteka vijiji kadhaa katika
mpaka wa Kenya na somalia.
Mamia ya wakaazi wameyatoroka makaazi yao kufuatia taarifa za kuwepo kwa wapiganaji wa Alshabaab wapatao thelathini.
Shule nne zinaripotiwa kufungwa.
Naibu
kamishna wa kaunti ya Mandera amenukuliwa akisema kwamba wamepokea
ripoti za kuwepo kwa wapiganaji hao na watawaandama na kulidhibiti eneo
hilo. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.
MLIPUKO WA BOMU WAUA WATU 20 NIGERIA
Takriban watu 20 wamefariki kutokana na mlipuko wa bomu katika mji wa kaskazini mashariki wa Maiduguri nchini Nigeria.
Mji huo ulikuwa umeshambuliwa saa za alfajiri siku ya jumanne na washukiwa wa kundi la Boko haram .
Saa
chache baadaye ,mlipuaji wa kujitolea muhanga alijilipua katika soko la
kuuza ngombe la Gamboru ndani ya mji huo kulingana na walioshuhudia.
Wakati
wa kuapishwa kwake rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema kuwa
anayahamisha makao makuu ya kijeshi katika vita dhidi ya wapiganaji hao
kutoka mji mkuu wa Abuja hadi Maiduguri. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.
Thursday, May 28, 2015
MWANASHERIA KENYA AJITOSA KUMUOA MTOTO WA OBAMA...!!!
Mwanasheria kijana nchini ametuma ombi la kumuoa mtoto wa Rais Barack Obama anayeitwa Malia.
Mwanasheria Felix Kiprono alisema jana kwamba yupo
tayari kutoa ng’ombe 50, kondoo 70 na mbuzi 30 ikiwa ni mahari ya
kumposa mtoto huyo.
Alisema kuwa analazimika kufanya hivyo ili kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kumuoa mtoto wa Rais Obama.
“Nimevutiwa kumchumbia Malia tangu mwaka 2008,” alisema Kiprono baada ya kuhojiwa na gazeti la The Nairobian. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.
ODAMA: NAOGOPA MSAADA WA MASHARTI...!!!
MWIGIZAJI mwenye mvuto katika filamu za Bongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’,
amesema anaogopa marafiki wa kiume kwa kuwa huwa na masharti magumu
pindi wanapotoa msaada.
“Wasanii wa kiume kwangu sipendi kwa kuwa huwa na masharti kuliko marafiki wa kike ambao husaidia bila masharti ya ajabu,” alisema.
Aliongeza kwamba, marafiki wa kike anakuwa huru kuwaeleza shida na matatizo yake kuliko wa kiume ndiyo maana hiyo ni sababu yake nyingine ya kutopenda marafiki wa kiume kama anavyopenda marafiki wa kike. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.
“Wasanii wa kiume kwangu sipendi kwa kuwa huwa na masharti kuliko marafiki wa kike ambao husaidia bila masharti ya ajabu,” alisema.
Aliongeza kwamba, marafiki wa kike anakuwa huru kuwaeleza shida na matatizo yake kuliko wa kiume ndiyo maana hiyo ni sababu yake nyingine ya kutopenda marafiki wa kiume kama anavyopenda marafiki wa kike. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.
"NATAKA KUWA MCHEKESHAJI" INSPEKTA HAROON
UNALIKUMBUKA kundi la Gangwe Mobb, hapo lazima utamtaja Haruna Kaena
‘Insepkta Haroun’ na Luten Kalama, wawili hao baada ya kutengana kila
mmoja akawa anafanya kazi binafsi lakini sasa Inspekta Haroun ameibuka
na kudai kwamba anataka kuwa mwigizaji wa vichekesho.
Inspekta Haroun aliyetamba na wimbo wa ‘Mtoto wa Geti Kali’ aliendelea kueleza kwamba fani anazozipenda ni muziki na kuigiza vichekesho.
“Mimi msanii hivyo natakiwa niwe mbunifu, nisibweteke na kazi, fani moja na kwa sasa napenda kuwa mwigizaji wa vichekesho kwa kuwa napenda kazi hiyo na ninaiweza,” alijinadi.
Msanii huyo aliwahi kushirikishwa katika vipengele vya uigizaji katika kipindi cha vichekesho kilichokuwa kikirushwa na televisheni ya Clouds. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.
Inspekta Haroun aliyetamba na wimbo wa ‘Mtoto wa Geti Kali’ aliendelea kueleza kwamba fani anazozipenda ni muziki na kuigiza vichekesho.
“Mimi msanii hivyo natakiwa niwe mbunifu, nisibweteke na kazi, fani moja na kwa sasa napenda kuwa mwigizaji wa vichekesho kwa kuwa napenda kazi hiyo na ninaiweza,” alijinadi.
Msanii huyo aliwahi kushirikishwa katika vipengele vya uigizaji katika kipindi cha vichekesho kilichokuwa kikirushwa na televisheni ya Clouds. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.
WABUNGE WAMKAANGA MAGUFULI
Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe Magufuli amekuwa hapati wakati mgumu anapowasilisha bajeti ya wizara hiyo, lakini hali ilikuwa tofauti jana wakati wabunge walipoungana kueleza hofu yao katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara kutokana na madeni ya makandarasi.
Wabunge hao walidiriki kueleza kuwa kuna ufisadi
katika ununuzi wa kivuko cha Bagamoyo na wengine kueleza kuwa miradi
iliyotajwa kwenye hotuba ya bajeti ilishatekelezwa miaka ya 80 na 90.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Miundombinu
kuhusu bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/2016 iliyosomwa na
Makamu Mwenyekiti, Profesa Juma Kapuya, deni linalodaiwa na makandarasi
ni kati ya Sh850 bilioni na Sh900 bilioni.
“Kamati haijaridhishwa kabisa na hali hii kwani
deni hili sasa ni kubwa kuzidi hata bajeti inayotengwa kwa ajili ya
miradi ya maendeleo ya wizara hii, jambo ambalo linafanya bajeti hii
kuonekana ni kiini macho tu,” alisema Profesa Kapuya.
Kambi ya Upinzani
Katika taarifa yake, Kambi ya Upinzani Bungeni
(KUB) ilimshutumu Waziri Magufuli kwa kuandika hotuba ndefu ili
kuwachanganya wabunge, huku hotuba hizo zikitaja hata miradi ya barabara
zilizojengwa miaka ya 80 na 90.
Friday, May 22, 2015
UCHAGUZI FIFA, WAWILI WAJITOA
Wagombea
wawili kati ya wanne waliojitokeza kuwania nafasi ya urais wa
shirikisho la vyama vya soka Duniani FIFA wamejitoka katika
kinyang'ang'anyiro hicho.
Nyota wa zamani wa soka huko Ureno ,
Luis Figo ambaye ni mmoja wa waliojitoa kuwania nafasi hiyo,amelalamikia
mfumo wa uendeshaji wa uchaguzi huo na kuiita kuwa ni wakinafiki.
Amesisitiza
kuwa kwa mtazamo wake anaona kuwa taratibu zilizowekwa zililenga
kumnufaisha mgombea mmoja tu na si kuelta usawa wa wote waliojitokeza
kuwania nafasi hiyo,ambapo inaonekana kuwa ni mpango uliowekwa kumpatia
nafasi ya ushindi Rais wa sasa Sepp Blatter ambaye anawania nafasi hiyo
kwa kipindi cha tano.
Hata hivyo Rais wa chama cha soka huko
Uholanzi , Michael van Praag , akijitoa. Huku wapinzani waliosalia ni Bw
Blatter ambaye ni Jordan Prince Ali Al Hussein ambaye ni mwanachama wa
kamati ya utendaji ya FIFA.
Mgombea mwingine aliyejitoa pia ni
Rais wa chama cha soka cha Uholanzi Michael van Praag na hivyo kuwaacha
Blatter na mtu anayedaiwa kuwa mpinzani wake wa karibu Prince Ali Al
Hussein ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Wednesday, May 20, 2015
MICHUANO YA COSAFA YAANZA AFRIKA KUSINI
Michuano ya COSAFA,nchini Afrika Kusini Michuano ya kumi na tano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu kusini mwa Afrika,COSAFA imezikutanisha timu za ukanda huo nchini Afrika Kusini. Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi Jumapili mei 17 na itakamilika mei 30 .
Timu 12 kati ya 14 kutoka nchi wanachama wa COSAFA tayari zipo nchini Afrika Kusini kuchuana katika mashindano hayo.
Angola na Comoro ambazo ni wanachama wa COSAFA hazikuweza kushiriki mwaka huu.
Nafasi zao zimechukuliwa na Ghana iliyofikia fainali za michuano ya Caf ya mwaka huu na Tanzania kutoka ukanda wa Afrika mashariki na kati ikiwa mwanachama wa CECAFA.
Monday, May 18, 2015
NKURUNZIZA AWAFUKUZA KAZI MAWAZIRI WATATU
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza .
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewafuta kazi mawaziri watatu, huku maandamano yakiendelea katika mji mkuu kufuatia jaribio la mapinduzi, juma lililopita.
Mawaziri walioachishwa kazi ni wa Ulinzi, mashauri ya nchi za kigeni na biashara.
Mapema hii leo, polisi walifyatua risasi hewani katika mji mkuu Bujumbura, kujaribu kuutawanya umati wa vijana uliokuwa ukifanya ghasia.
Subscribe to:
Posts (Atom)