Thursday, January 22, 2015
WHATSAPP YAWABANA WATUMIAJI
Mtandao
wa kijamii wa WhatsApp unawabana watu wanaotumia huduma hiyo kupitia
programu bandia na ambayo haijaidhinishwa ya Android kwa muda wa saa 24.
WhatsApp
ambayo inamilikiwa na Facebook, ilisema kuwa imechukua hatua dhidi ya
watumiaji wa huduma ya WhatsApp Plus kwa sababu ya wasiwasi kwamba
programu hiiyo huenda iksababisha kuvuja kwa taarifa za siri za
watumiaji wa WhatsApp.
Programu hio bandia na isio rasmi ya Android inawezesha watumiaji wa WhatsApp Plus kupamba mawasiliano yao wanavyotaka.
Wataalamu
wanasema kwamba watumiaji wa Android wanapaswa kuwa makini na
kutahadhari kuhusu wanavyodownload programu flani au 'Apps'. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
WATOTO WA HOSNI MUBARAK KUACHIWA
Mahakama
nchini Misri imeamrisha kuachiliwa kwa watoto wa kiume wa rais wa
zamani Hosni mubarak wakati wanaposubiri kesi yao pamoja na baba yao
inayohusu ufisadi.
Wakili wa Alaa na Gamal Mubarak anasema kwa anatarajia wawili hao kuachiliwa leo.
Hasira
kutokana na kile kilichoonekana kama jitihada za kumuandaa Gamal
Mubarak kuweza kumrithi babake kama rais ni moja ya sababu
zilizosababisha maandamano makubwa yaliyomundoa madarakani rais Hosni
Mubarak. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na BBC
UJUMBE WA UTURUKI SOMALIA WASHAMBULIWA
Kumekuwa
na shambulizi la mlipuaji wa kujitolea muhanga katika hoteli moja mjini
Mogadishu nchini Somali ambapo maafisa wa Uturuki walikuwa wakijiandaa
kumlaki rais Recep Teyyip Erdogan.
Takriban raia watatu wa Somali
waliuawa wawili kati yao wakiwa maafisa wa usalama wakati gari lililojaa
vilipuzi lilipogonga lango la hoteli.
Uturuki hatahivyo imesema
kuwa hakuna mjumbe wake aliyejeruhiwa na kwamba ziara ya rais Erdogan
itaendelea kama ilivyopangwa siku ya ijumaa.
Kundi la wapiganaji wa Alshabaa limesema kuwa lilitekeleza shambulizi hilo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
TUNISIA KUTOANA JASHO NA ZAMBIA
Zambia
italazimika kuimarisha safu ya kati katika mechi didi ya Tunisia
kufuatia jeraha la mchezaji Nathan Sinkala ambalo limemuweka nje ya
michuano yote ya mataifa ya Afrika.
Hatahivyo kikosi hicho cha Chipolopolo hakina tatizo kubwa juu wachezaji wake.
Mkufunzi wa Tunisia ana wachezaji wa kutosha wa kujumuisha katika timu yake,ijapokuwa wamekuwa na tatizo katika hoteli yao.
Kunako
mwendo wa saa nane leo alfajiri ,kulikuwa na maji chungu nzima katika
vyumba vya hoteli wanaolala wachezaji wa kikosi hicho.
Inadaiwa kuwa wachezaji hao walilazimika kubadili vyumba huku wachezaji wengine wakilazimika kulala wanne katika chumba kimoja. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Wednesday, January 21, 2015
KANISA KATOLIKI LAUNGA MKONO MAANDAMANO DRC
Mkuu wa kanisa katoliki nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo ameunga
mkono maandamano ya kupinga mabadiliko katika ya sheria ya uchaguzi
ambayo imezua siku tatu za maandamano.
Kadinali laurent Monsengwo ameitaka mamlaka kwa maneno yake mwenyewe kusitisha mauaji ya raia wake. Amewataka waandamanaji kuweka amani.
Makundi ya haki za kibinaadamu yamesema kuwa zaidi ya watu 40 wamefariki katika ghasia hizo.
Vyama
vya upinzani vinasema kuwa sheria hiyo iliyopendekezwa ililenga
kuchelewesha uchaguzi ili rais Joseph Kabila aendelee kuwa mamlakani
baada ya kipindi chake cha utawala kuisha mwaka ujao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
MWANAJESHI WA UK HATIANI KWA KUMBAKA MTOTO
Mwanajeshi mwingereza ameshtakiwa kwa kosa la kumbaka na kumdhalilisha mtoto mwenye umri wa miaka 6 nchini Austria.
Viongozi
wa mashitaka wanasema kuwa mwanajeshi huyo ambaye hajatajwa alikamatwa
mwezi Novemba katika eneo la Tyrol ambako alikuwa anafanya mazoezi yake
ya kijeshi.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 10 mwezi Machi.
Msemaji
wa kiongozi wa mashtaka alisema kua wendeshja mashtaka wanaamini kwamba
mwanajeshi huyo aliingia nyumbani kwa familia ya msichana huyo akiwa
mlevi nyakati za asubuhi na kufanya kitendo hicho.
Mwanajeshi huyo alipatikana katika chumba cha mtoto huyo baada ya babake kusikia kelele.
Alikamatwa mjini Neustift na ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miaka 10.
Msemaji wa kiongozi wa mashtaka aliambia BBC kuwa mtoto huyo alihojiwa na kiongozi wa mashitaka. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na BBC
TAZAMA PICHA ZA SAMATTA KATIKA MAJARIBIO CSKA MOSCOW
Hatimaye nyota ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe Mbwana Samatta imeanza kung’ara katika anga ya kimataifa ya soka.
Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba mshambuliaji huyo yupo kwenye
majaribio katika klabu ya CSKA Moscow – moja ya klabu kubwa kabisa
nchini Urusi ambayo kwa miaka kadhaa imekuwa ikitawala soka la nchi hiyo
na kucheza katika michuano ya mabingwa wa ulaya.
Samatta alipewa nafasi ya kufanya majaribio ya siku 3 na klabu hiyo
kwenye kambi yao ya mazoezi iliyopo Spain, lakini sasa ameongezewa wiki
moja ya ziada ili maofisa ya jopo ya ufundi la timu hiyo wapate muda wa
kumuangalia vizuri.
Pamoja na CSKA Moscow – timu nyingine ambazo zinatajwa kumtaka
mshambuliaji huyo ni Inter Milan na Udinese za Italia, Atletico Madrid
ya Spain, FC Basel ya Uswis na Kaiserslauten ya Ujerumani. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
TAMBWE ASIMULIA ANAVYOTESWA, YANGA YASHITAKI
Klabu ya Yanga imepanga leo kuwasilisha malalamiko yao juu ya tukio
la kunyanyaswa kwa mshambuliaji wake Amissi Tambwe kwa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) lakini pia mchezaji husika amefafanua kwa kina juu
ya manyanyaso anayoyapata.
Akizungumza mchana wa leo katika makao makuu wa klabu hiyo Mkuu wa
Kitengo cha Habari Jerry Muro amesema uongozi wao unakusudia kuwasilisha
malalamiko yao hayo ambayo mengi yametokana na vitendo alivyofanyiwa
Tambwe wikiendi iliyopita katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambapo
wanataka mapendekezo yao manne yafanyiwe kazi.
Muro amesema kwanza Yanga ingwetaka kuona TFF inawachukulia hatua
kali wahusika wote waliomdhalilisha Tambwe huku pili wakilitaka
shirikisho hilo kutoa hadharani taarifa ya tathimini ya waamuzi wa
mchezo huo lengo likiwa ni kujua umakini wa waamuzi hao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
“Tatu tungewaomba wenzetu wa TFF kwa kuwa wao wapo kimya pia
kuwachukulia hatua wahusika wote waliosimamia mchezo huo kwa kushindwa
kubaini haya ambayo vyombo vya habari imeyafichua lakini ikiwezekana
wafungiwe na Yanga hatuwataki kuwaona wanachezesha mechi zetu vinginevyo
tutagoma na hata Ruvu nao tungependa kuona wanapewa adhabu kwa viongozi
wao kushabikia maovu haya.
Aidha Tambwe mwenyewe amechukizwa na matukio hayo akisema
ameshangazwa kuona anafanyiwa vitendo vya kinyama ambapo mengine hawezi
kuyaweka hadharani.
“Mpira ni starehe mimi sikatai mchezaji anikabe lakini ni jinsi gani
unanikaba hapo ndiyo tatizo, naambiwa mimi mkimbizi hivi hawa wenzangu
wanajua maana na haya maneno yapo mengi ambayo nimedhalilishwa nayo
kiungwana siwezi kuyaweka wazi hapa lakini viongozi nitawaeleza,”alisema
Tambwe. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
KLABU KUJIGHARAMIA HOTELI MICHUANO YA CAF
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) limefanyia marekebisho kanuni zake za michuano ya ngazi ya
klabu kwa upande wa malazi ambapo sasa timu zitachagua na kujilipia
zenyewe hoteli zinapokuwa kwenye mechi za ugenini.
Kabla ya marekebisho ya kanuni hiyo, timu ngeni ilikuwa ikilipiwa
hoteli na timu mwenyeji kwa msafara usiozidi watu 25. CAF ilikuwa
imepitisha hoteli maalumu katika kila nchi ambapo mwenyeji alitakiwa
kuziweka timu ngeni.
Kwa marekebisho hayo, Chama cha Mpira wa Miguu cha nchi mwenyeji
kitakuwa na wajibu wa kuitafutia hoteli timu ngeni iwapo tu kitaombwa
kufanya hivyo, lakini jukumu la kulipia malazi litakuwa la timu yenyewe.
Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na timu mbili za Azam na Yanga
katika michuano ya CAF. Azam inacheza Ligi ya Mabingwa (CL) ambapo
itaanzia nyumbani Februari 15 mwaka huu kwa kuikaribisha El Merreikh ya
Sudan kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Nayo Yanga itacheza michuano ya Kombe la Shirikisho (CC), na
imepangiwa kucheza mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya BDF IX ya Botswana.
Mechi hiyo itafanyika Februari 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
GERVINHO AOMBA MSAMAHA KWA KADI NYEKUNDU
Mchezaji
wa Ivory Coast Gervinho ameomba msamaha baada ya kupewa kadi nyekundu
kwa kumpiga mlinzi wa timu ya Guinea Naby Keita katika mechi ya timu
hizo mbili ilioisha 1-1.
''Nataka kuomba msamaha kwa taifa la
Ivory Coast,wachezaji wenzangu na waandalizi wa michuano ya mataifa ya
Afrika kwa kitendo hiki cha hasira'',aliandika katika mtandao wake wa
Twitter.
''Haikuwa mimi na vitendo kama hivyo havina nafasi katika viwanja vya soka'',,aliongezea.
Kulingana
na sheria za FIFA, mchezaji hukosa mechi moja anapopewa kadi nyekundu
,lakini shirikisho la Soka barani Afrika huenda likaongeza adhabu hiyo.
Kawaida
mtu hupewa marufuku ya mechi mbili katika michuano ya Afrika,lakini
adhabu hiyo inaweza kuongezwa na kufikia mechi nne iwapo kamati ya
nidhamu itahisi mchezaji huyo anahitaji kupewa adhabu kali. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
BUKINA FASO YAAPA KUWASHINDA WENYEJI
Nahodha
wa timu ya taifa ya Burkina Fasso Charles Kabore amesisitiza kuwa
wataimarisha mchezo wao baada ya kushindwa na Gabon katika mechi yao ya
kwanza.
''Mashindano haya hayajakamilika kwetu sisi.''Iwapo
tutashinda dhidi ya wenyeji wa maandalizi haya basi kila kitu kitakuwa
shwari''.
Mkufunzi wa timu ya Equitorial Guinea Esteban Becker
anajua kwamba timu yake ni sharti ishinde mchuano huo dhidi ya Burkina
Fasso ilio na washambuliaji mahiri.
Hatahivyo Equitorial Guinea ni
sharti iimarishe safu yake ya Ulinzi,baada ya kushindwa kuweka rekodi
ya kutofungwa katika mechi zake nne katika michuano hiyo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
ARSENAL YAMSAJILI KRYSTIAN BIELIK
Arsenal imekamilisha usajili wa
kiungo wa kati Krystian Bielik mwenye umri wa miaka 17 kutoka kilabu ya
Legia warsaw kwa kitita kisichojulikana.
Bielik aliichezea timu kubwa ya kilabu hiyo ya Poland mnamo mwezi Agosti akiwa na umri wa miaka 16.
Pia
alishiriki katika mechi tano ya kilabu hiyo na mara moja katika ligi ya
yuropa.Mchezaji huyo anayesifiwa na wengi anaweza kucheza katika safu
ya kati na ile ya Ulinzi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Sunday, January 18, 2015
MATOKEO YA MECHI ZA EPL LEO JUMAPILI HAYA HAPA
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
England – Premier LeagueJanuary 18 | ||||
---|---|---|---|---|
FT | West Ham United | 3 – 0 | Hull City | |
FT | Manchester City | 0 – 2 | Arsenal |
UPINZANI DRC: KATIBA IMEPINDULIWA
Wabunge wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wamekubali mswada ambao
wadadisi wanasema unakusudiwa kumpa Rais Joseph Kabila idhini ya kubaki
madarakani, baada muhula wake wa pili kumalizika.
Mswada huo
unapendekeza kufanywe sensa ya taifa kabla ya uchaguzi ambayo serikali
inasema inaweza kuchukua miaka kadha kukamilisha.
Rais Kabila anamaliza muhula wa pili mwaka ujao.
Katiba ya nchi haimruhusu kugombea muhula wa tatu.
Mwandishi
wa BBC mjini Kinshasa anasema wabunge wengi wa upinzani walisusia kura
hiyo ya bunge, na kuielezea kuwa mapinduzi ya katiba. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Subscribe to:
Posts (Atom)