Wednesday, December 17, 2014

KLABU BINGWA DUNIA MADRID YATINGA FAINALI

Raha ya goli ni shamra shamra, wanapongezana.
Wakicheza katika dimba la Stade de Marrakech. Mjini Marrakech Nchini Morocco, Mabingwa wa Ulaya Real Madrid wamepata ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya Cruz Azul na kutinga Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu.
Real Madrid walianza kupata magoli yake dakika ya kumi na 15 kupitia kwa beki Sergio Ramos mshambuliaji Karim Benzema akaongeza la pili dakika ya 36,
Kipindi cha Pili, Gareth Bale, alifunga bao la 3 na Isco, kuhitimisha kwa goli la 4 na kuipelea Madrid fainali.
Azul walikosa penati dakika ya 40 iliyopigwa na Gerardo Torrado, na kuokolewa na kipa Iker Casillas.
Real wanasubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya San Lorenzo ya Argentina na Auckland City ya New Zealand.
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

CHELSEA NUSU FAINALI CAPITAL CUP

Chelsea wakipasha
Chelsea, wakicheza katika uwanja wa iPro Stadium waliwachabanga timu ya Derby County, Bao 3-1 kwenye Kombe la Ligi maarufu kama Capital One Cup, na kutinga Nusu Fainali.
Eden Hazard, ndie alianza kuipatia Chelsea, goli la kwanza dakika ya 33 kabla ya Filipe Luis, kufunga goli la pili dakika ya 56 huku Andre Schurrle, akihitimisha ushindi kwa goli la dakika ya 82.
Bao la kufutia machozi kwa Derby lilifungwa na Craig Bryson, Dakika ya 71.
Kwenye Mechi nyingine ya Robo Fainali Sheffield United, waliwashangaza Southampton kwa kuwabanjua Bao 1-0.
Bao la ushindi la Sheffield lilifungwa na McNulty, Dakika ya 63. Southampton walibaki 10 baada ya Gardos kupewa Kadi Nyekundu.
Leo Usiku zitachezwa Robo Fainali nyingine mbili ambapo Liverpool, watakuwa Wageni wa Bournemouth.
Huku katika uwanja wa white Hart Lane Tottenham Hotspur watawakaribisha Newcastle United. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Tuesday, December 16, 2014

UKAWA MBELE KWA MBELE

Wafuasi wa CHADEMA mjini Nansio Wilaya ya Ukerewe, Mwanza wakishangilia ushindi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika juzi. 

Matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika juzi, yanaonyesha kuimarika kwa upinzani nchini baada ya kupata viti vingi vya uenyekiti wa mitaa na vijiji, pamoja na mamia ya wajumbe wa Serikali husika.
Hayo yanaonyesha kuwa vyama hivyo vimeanza kuimarika katika ngazi za chini, tofauti na ilivyokuwa mwaka 2009, katika uchaguzi ambao CCM kilipata ushindi wa kishindo wa asilimia 91.72, huku wapinzani wakigawana asilimia 8.28 zilizobaki.
Licha ya uchaguzi wa juzi kugubikwa na kasoro lukuki, upinzani umeonekana kuchomoza huku katika baadhi ya mikoa ukipata ushindi maradufu hasa katika ile ambayo una nguvu kubwa wakati katika maeneo ambayo ulikuwa na viti vichache au kutokuwa navyo kabisa, umeibuka na kuipokonya CCM baadhi ya mitaa na vijiji.

Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year

MARCIO MAXIMO ATUPIWA VIRAGO YANGA NI BAADA YA KICHAPO CHA 2-0 KUTOKA SIMBA

YANGA SC imeirejea historia yake ya kuwatimia makocha wake muda mfupi tu baada ya kula kichapo kutoka kwa watani zao Simba ambapo tayari uongozi wa Yanga umelivunja benchi la ufundi la timu hiyo lililokuwa likiongozwa na makocha Wabrazil, Marcio Maximo na Msaidizi wake, Leonardo Neiva na kuwarejesha Mholanzi, Hans Van der Pluijm na  Charles Boniface Mkwasa 'Master'.

Maximo anaondolewa baada ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa mahasimu Simba SC Jumamosi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, wakati Pluijm anawasili usiku huu na kesho atasaini Mkataba na kuanza kazi. Mkwasa tayari alisaini Mkataba wiki kadhaa zilizopita na ameridhika kufanya kazi chini ya Pluijm tena.
Maximo na Leonardo walitua Yanga SC Julai mwaka huu kurithi mikoba ya Pluijm na Mkwasa ambao walipata kazi Uarabuni. Hata hivyo baada ya muda usiozidi mwezi mmoja, Pluijm na Mkwasa waliacha kazi Uarabuni, wakidai kukerwa na kuingiliwa na viongozi wa klabu yao katika masuala ya kiufundi.
  Pluijm alirudi Ghana wakati Mkwasa alirejea nyumbani Tanzania kabla ya kuajiriwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kama Mkufunzi Mkuu. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutoa maoni kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

UTITIRI WA WACHEZAJI WA KIGENI KUTAICHIMBIA KABURI SOKA YA TANZANIA NA KUUWA TIMU YA TAIFA KAMA ILIVYO UINGEREZA

Simon Sserunkuma 
Mshambuliaji huyo raia wa Uganda alikuja nchini na timu ya Express ya nchini humo na kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Simba na Yanga na ndipo viongozi hao wa Yanga walipomwona na kumleta nchini ili kufanya naye mazungumzo lakini mambo yakawa tofauti kwani alitoroshwa kimya kimya na kupelekwa Zanzibar ambako Simba iliweka kambi kujiandaa na mechi ya Nani Mtani Jembe iliyochezwa juzi Jumamosi.
ACHANA na Yanga kufungwa mabao 2-0 na Simba katika mechi ya Nani Mtani Jembe, imebainika kuwa Simba iliifanyia Yanga umafia kwa mchezaji Simon Ssrenkuma baada ya kumtorosha kutoka mikononi mwa viongozi wa klabu hiyo na kwenda kumficha kwenye kambi ya timu hiyo visiwani Zanzibar wiki iliyopita.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutoa maoni kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 16, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC07117
DSC07114
DSC07116
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year

THIERRY HENRY ATANGAZA RASMI KUSTAAFU SOKA

Theirry-Henry-in-action-o-007 
Katika ulimwengu wa soka leo kuna habari kubwa ambayo imeenea duniani kutokana na staa mkubwa na mkongwe Thierry Henry kutangaza kustaafu soka na kujiunga na shughuli nyingine. Nyota huyo  ambaye ameng’aa kwenye mchezo huo kwa muda mrefu sana akichezea vilabu mbalimbali ikiwemo Arsenal na Barcelona.
download
Henry ametangaza rasmi kustaafu soka dakika chache zilizopita na kusema kuwa kuanzia mwakani ataanza kujishughulisha kama Balozi wa Sky Sports huku akisema kuwa anajisikia furaha kuchezea vilabu vikubwa na pia anaamini anajiunga na kituo kikubwa cha Television na matarajio yake ni kuwa mchambuzi bora wa michezo kwenye kituo hicho.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutoa maoni kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

HAYA NDIYO MAAMUZI MAGUMU YA YANGA KUHUSU MBRAZIL EMERSON

Moja ya vichwa vya habari vilivyokuwa vimepambwa na habari kumhusu Emerson.

Taarifa za usajili na kuachwa wachezaji zinazidi kuingia na safari hii inasemekana kuwa kiungo Mbrazil Emerson amekuwa mhanga wa kwanza wa kuondoka kwa kocha Mbrazil Marcio Maximo baada ya mchezaji huyo kuachwa na Yanga.
Mbrazil huyo anaondoka Yanga baada ya kucheza mechi moja pekee dhidi ya Simba ambako Yanga ilifungwa 2-0.
Emerson alishindwa kuwaridhisha mashabiki wa Yanga ambao wengi walionyesha kukerwa na uwezo mdogo wa kiungo huyo katika dakika 45 alizocheza kwenye mechi dhidi ya Simba.
Emerson alikuja nchini siku chache zilizopita ambapo alipaswa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mshambuliaji Genilson Santos Santana Jaja ambaye hakurudi baada ya kuondoka nchini kufuatia kusimama kwa ligi. 
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutoa maoni kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year

Tuesday, December 09, 2014

ANGALIA PICHA ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikitoa salamu ya heshma wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 09, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC06734
DSC06732
DSC06733
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Monday, December 08, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 08, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WAHAMIAJI 70 WAFA MAJI YEMEN

Boti iliyojaza wahamiaji haramu kuelekea Yemen 
 
Watu 70 wamekufa baada ya boti iliyokuwa imejaza wahamiaji haramu kupinduka baharini, magharibi mwa Yemen.
Maafisa nchini Yemen wamesema wengi ya watu waliokuwa katika boti hiyo ni raia wa Ethiopia.
Hali mbaya ya hewa inaelezwa kwamba ndio chanzo cha kuzama kwa boti hiyo.
Mamia kwa maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakihatarisha maisha yao kwa safari zisizo na usalama katika nchi zilizo katika pembe ya Afrika na Yemen kila mwaka.
Umoja wa Mataifa unamini kwamba kiasi cha watu watu mia mbili wamezama maji katika kipindi cha miezi kumi na mbili iliyopita. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

EBOLA YAUA DAKTARI MWINGINE S-LEONE

Wakuu wa Sierra Leone wanasema daktari mwengine amefariki kutokana na Ebola - ni daktari wa 10 kufa na ugonjwa huo.
Aiah Solomon Konoyima alifariki Jumamosi kwenye kituo cha matibabu karibu na mji mkuu, Freetown, siku moja tu baada ya wenzake wawili kufa na ugonjwa huo huo.
Mwezi wa Julai daktari maarufu kabisa kutibu wagonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone, Sheik Umar Khan, piya mwisho aliuliwa na virusi vya Ebola.
Vifo 1,600 vya Ebola vimesajiliwa nchini humo.
Sierra Leone imekuwa ikijaribu kukarabati huduma za afya baada ya vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka ya 1990s.
Na daktari kutoka Cuba ambaye alipona Ebola, ameahidi kuwa atarudi Sierra Leone kumaliza kupambana na ugonjwa huo nchini humo.
Dakta Felix Baez, ambaye alipata Ebola nchini Sierra Leone, alisema hayo aliporudi Havana baada ya kujaribiwa matibabu aina mpya nchini Uswiswi ambayo yalimponesha.
Dakta Baez alikuwa kati ya madkatari na wauguzi wa kwanza 250 walioambukizwa Ebola Afrika magharibi.
Cuba ndio nchi iliyotuma huko wafanyakazi wa utabibu wengi kabisa kwenda kupambana na Ebola.
Mchango huo wa Cuba umesifiwa kimataifa hata na Marekani, adui yake wa kisiasa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

Sunday, December 07, 2014

MUTHARIKA AJINYIMA NYONGEZA YA MSHAHARA

Rais Peter Mutharika wa Malawi na naibu wake wameakhirisha kujipa nyongeza ya mishahara baada ya kuzuka malalamiko.
Nyongeza kutoka mshahara wa dola 3,000 na kufikia dola 5,000 kila mwezi, imezusha malalamiko nchini Malawi ambako pato la nusu ya wananchi halitimii dola moja kwa siku.
Bwana Mutharika na makamo wake, Saulos Chilima wamesema hawatojipa nyongeza ya mishahara hadi uchumi wa nchi utengenee.
Kabla ya viongozi hao kushika madaraka wafadhili walisimamisha msaada wa dola 150-milioni kwa sababu ya wasiwasi kuhusu rushwa.
Mishahara ya wabunge itazidishwa asili-mia-mia-tatu (300%) Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MUGABE ATEULIWA TENA KUONGOZA ZANU-PF

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameteuliwa kwa mara nyengine kuongoza chama tawala cha ZANU PF 
 
Rais Robert Mugabe ameteuliwa tena kuongoza chama tawala nchini Zimbabwe na mke wake Grace akapewa wadhifa wa juu katika chama.
Kupandishwa cheo kwa Grace Mugabe kuongoza tawi la wanawake la Zanu-PF kunamuweka katika nafasi nzuri ya kumrithi mumewe katika siku zijazo,wanasema wachambuzi.
Mke huyo wa Rais amewashtumu wakinzani wake wa kisiasa akiwemo Makamo Rais Joyce Mujuru, katika miezi ya hivi karibuni.
Bwana Mugabe mwenye umri wa miaka 90,anatazamiwa kugombea tena urais mnamo mwaka 2018.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa Zanu-PF,Bwana Mugabe aliwashukuru maelfu ya wafuasi wake kwa kumchagua kuongoza chama . "Najua nilikotoka.. mimi si bora kushinda watu walonizaa ," alisema Mugabe, ambaye ameiongoza Zimbabwe tangu mwaka 1980.
Madai ya mauaji
Kuteuliwa kwa mke wa Mugabe kuongoza tawi la wanawake kunaonekana kama ni ishara nyigine zaidi kwa Joyce Mujuru ambae wakati mmoja alionekana kama angeweza kumrithi Mugabe sasa amepigwa pande.
Bi Mujuru alipigania pamoja na Bw.Mugabe uhuru wa Zimbabwe kutoka utawala wa wazungu wachache.
Lakini alijikuta matatani wakati Bi Mugabe mwenye umri wa miaka 49, kujitumbukiza katika siasa mnamo mwaka huu na kumshutumu makamo wa rais wa kula njama dhidi ya mumewe. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...