Rais Peter Mutharika wa Malawi na naibu wake wameakhirisha kujipa nyongeza ya mishahara baada ya kuzuka malalamiko.
Nyongeza
kutoka mshahara wa dola 3,000 na kufikia dola 5,000 kila mwezi,
imezusha malalamiko nchini Malawi ambako pato la nusu ya wananchi
halitimii dola moja kwa siku.Bwana Mutharika na makamo wake, Saulos Chilima wamesema hawatojipa nyongeza ya mishahara hadi uchumi wa nchi utengenee.
Kabla ya viongozi hao kushika madaraka wafadhili walisimamisha msaada wa dola 150-milioni kwa sababu ya wasiwasi kuhusu rushwa.
Mishahara ya wabunge itazidishwa asili-mia-mia-tatu (300%) Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment