JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 18 Februari, 2014
TAARIFA KWA UMMA: VIPINDI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA.
Taarifa Na. 201402-03
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 8:30 Mchana
Daraja la Taarifa:- Tahadhari
Kuanzia: Tarehe 19 Februari, 2014
Mpaka: Tarehe 21 Februari, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa ni vipindi vya mvua kubwa (zaidi ya mm 50 ndani ya saa 24) kwa siku.
Kiwango cha uhakika:- Wastani (60%)
Maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni Kanda
ya kati (mikoa ya Singida na Dodoma), nyanda za juu kusini magharibi
(mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe) na maeneo ya kusini (Mikoa ya Ruvuma na Morogoro).
Maelezo:-
Hali hii inatokana na kuimarika kwa mfumo wa mgandamizo mdogo
wa hewa katika rasi ya Msumbiji. Mfumo huu unatarajiwa kuvuta
upepo kutoka misitu ya Congo kupitia maeneo tajwa hapo juu.
Angalizo:-
Idara zinazohusika na hali ya tahadhari pamoja na wakazi wa maeneo
hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Maelezo ya Ziada:-
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa
mrejeo kila itakapobidi.
Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Monica Mutoni
Public Relation Office
Tanzania Meteorological Agency