Serikali imetangaza neema kwa vijiji vinavyopitiwa na bomba la gesi ambavyo vipo mkoani Mtwara na Lindi, sasa wataunganishiwa kwa Sh27,000. (HM)
Hatua hiyo ilitangazwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uzinduzi mradi wa umeme wilayani Nanyumbu na Masasi.
Profesa Muhongo alisema gharama za kuunganisha umeme kwa sasa ni Sh177,000.
Alisema zaidi ya vijiji 50 vimepewa upendeleo huo ili kuwawezesha wananchi kuwa na maisha bora.
Lengo la Serikali ni kufikia asilimia 30 ya wasasatu waliounganishwa na umeme na kwamba, hivi sasa ni asilimia 23 pekee wanaopata umeme nchini wakati Mtwara ni asilimia nne.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz