Monday, January 20, 2014

AJALI YATOKEA MBALIZI MBEYA, MAGARI ZAIDI YA MATANO YAGONGWA

 Magari yakiwa yamegongwa Mbalizi Mbeya

MWANAJESHI FEKI AKAMATWA TANGA AKIMTAPELI DC

'Koplo' feki wa JWTZ akiwa ofisini kwa mkuu wa wilya.


 'Koplo' feki akijiandaa kupanda  kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi

SOMA SABABU YA MAWAZIRI MIZIGO KUACHWA KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI...!!!


RAIS JAKAYA KIKWETE.

SERIKALI imetoa kauli kuhusu tuhuma zilizokuwa zikiwakabili baadhi ya mawaziri, waliobatizwa jina la ‘Mawaziri Mizigo’, na hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa kukabiliana na kero zilizosababisha wapewe jina hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Ikulu Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Safue, alisema mawaziri hao walituhumiwa kutokana na changamoto zilizopo katika wizara zao; na si upungufu wao binafsi kama viongozi.

Mawaziri hao saba walitajwa katika ziara ya mikoani ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na baadae walihojiwa katika kikao cha Kamati Kuu cha chama hicho.

Baada ya kuhojiwa, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema Kamati Kuu ilimuachia Rais Kikwete jukumu la kuamua kuwafukuza kazi, kuwahamisha au kuwataka kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Miongoni mwa mawaziri waliohojiwa ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, ambaye sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.

HII NDIO THAMANI YA JINO MOJA LA NDOVU NA JINSI BIASHARA INAVYOFANYWA

  2013-04-28-TimphotobyCarlSafina.JPG
Yafuatayo ni kuhusu biashara ya meno ya tembo

Kwanza: Matumizi yake; meno ya tembo hutumika kutengeneza vitu vya urembo kama vile hereni , mikufu, mapambo kama vile sanamu na hata keys za keyboards za vinanda.
Vifaa vilivyotengenezwa kwa meno ya tembo hutumika nchini China kama sehemu ya kuonyesha ufahari, kwa mujibu wa Wikipedia.


Pili: Bei ya meno ya tembo

Bei inategemea na soko , hata hivyo kwa mujibu wa answers.com , jino moja la tembo huweza kuuzwa kwa dola za kimarekani mia saba (700).

Tuesday, January 14, 2014

MHUDUMU WA MOCHWARI 'AMCHIMBA MKWARA' WAZIRI...!!!


Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid. PICHA|MAKTABA 
*******
Mfanyakazi wa Kitengo cha Kuhifadhi Maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Eugene Vurugu amemtisha Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid kuwa ikitokea amefariki dunia akiwa mkoani Mbeya, basi maiti yake italazwa kwenye sakafu hospitalini hapo.
Akizungumza kwenye mkutano wa wafanyakazi na naibu waziri huyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Vurugu alisema kitengo hicho kimezidiwa na wingi wa maiti zinazopelekwa hospitalini hapo.
Alisema kitengo hicho cha kina majokofu sita tu na hulazimika kuhifadhi miili kwa zamu ili angalau maiti zisiharibike.
“Hata wewe Waziri ukifa leo, hakuna pa kukuweka.
Utawekwa sakafuni kusubiri maiti nyingine zipoe halafu utaingizwa ndani kwa kuingizwa maiti mbili kwenye eneo la mtu mmoja,’’ alisema Vurugu.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

JAMBO TZ BLOG INAWATAKIA WAISLAM WOTE DUNIANI KHERI YA SIKUKUU YA MAULID

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 14, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC03476

DSC03460
DSC03463
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

CHRISTIANO RONALDO ATWAA TUZO YA FIFA BALLON D'OR 2013

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ameuvunja utawala wa miaka minne wa Lionel Messi wa Argentina anayechezea klabu pinzani ya Barcelona baada ya kunyakua tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa Fifa usiku wa kuamkia leo.
Ronaldo amemshinda pia Franck Rivery, Mfaransa anayechezea Bayern Munich.
Sherehe za tuzo hizo zilifanyika Zurich, Uswisi.
Nadine Angerer
Kwa upande wa wanawake, kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani, Nadine Angerer ameibuka kinara mbele ya Marta (Brazil) na Abby Wambach (Marekani). Mdada huyo aliisaidia Ujerumani kutwaa taji ya Euro 2013 kwa wanawake akiokoa penati katika mechi yao ya fainali dhidi ya Norway waliyoshinda 1-0.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Monday, January 13, 2014

HODI TENA...!!! OPERESHENI TOKOMEZA YA PILI KUANZA KARIBUNI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
WAKATI hatua zaidi zikisubiriwa kuchukuliwa kwa watendaji waliohusika na ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa Operesheni Tokomeza, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kutangaza kuanza kwa awamu ya pili ya Operesheni hiyo wakati wowote kuanzia sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema wakati wowote Rais Kikwete atatangaza kuanza kwa Awamu ya Pili ya Operesheni Tokomeza na itazingatia haki zote ikiwemo haki za binadamu.
Nyalandu alisema ingawa awamu ya kwanza kulikuwa na kasoro zilizojitokeza, awamu hii ya pili kasoro hizo zitafanyiwa kazi ili kuhakikisha rasilimali za Taifa zinalindwa.
Kusitishwa kwa operesheni hiyo kulikosababisha uteuzi wa mawaziri watatu kutenguliwa na waziri mmoja, kujiuzulu kwa mujibu wa Nyalandu, kulisababisha pia tembo 60 kuuliwa.
Mawaziri ambao uteuzi wao ulitenguliwa na Rais Kikwete mwishoni mwa mwaka jana ni Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Dk David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo) huku Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), akijiuzulu.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

TAARIFA YA CHADEMA KWA UMMA KUHUSU TUHUMA DHIDI YA M/KITI, FREEMAN MBOWE

TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU TUHUMA DHIDI YA MWENYEKITI WA TAIFA, FREEMAN MBOWE
Kama mojawapo ya mikakati ya baadhi ya watu wanaotaka kuhamisha mjadala wa makosa yanayowaandama ya utovu wa maadili na usaliti dhidi ya chama, hivi karibuni, Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe amezushiwa tuhuma zisizokuwa na ukweli wowote zikilenga kumchafua kwa nafasi yake ya uongozi na kuipaka matope taasisi anayoiongoza;

Tuhuma hizo ni pamoja na;

1.     Kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa mwaka 2005 eti alichukua fedha kutoka kwa Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kiasi cha sh.Milioni 40 ili Mwenyekiti Mbowe asifanye kampeni katika jimbo hilo.

2.     Mwaka 2008, eti Mbunge Mkono alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa, sh. Milioni 20 kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa
Tarime, kisha akazitoa kwenye chama kama mkopo na akalipwa.

3.    Mwaka 2010, wakati wa uchaguzi mkuu Mbunge Mkono eti alimpatia Mwenyekiti wa Chama Taifa sh. Milioni 200 kwa ajili ya kampeni za mgombea urais.

4.     Mwaka huo huo wakati wa uchaguzi mkuu, eti Mwenyekiti wa Chama Taifa, alipokea sh. Milioni 100 kutoka kwa Rostam Aziz kwa ajili ya kampeni.

Idara ya Habari ya CHADEMA, inapenda kusema yafuatayo;

1.    Hakuna ukweli hata mmoja katika tuhuma hizo. Ni uongo na uzushi uliopangiliwa kama moja ya mikakati ya watu wenye malengo ya kutaka kuilaghai jamii kwamba viongozi wa CHADEMA hawana tofauti na wale wa CCM na kwamba chama hiki kikuu cha upinzani kinachobeba matumaini ya Watanzania katika kupigania haki zao na kupinga kila aina ya ufisadi, kionekane hakina tofauti na chama kilichoko madarakani, ambacho kimepoteza ushawishi kwa wananchi.

2.     Matokeo ya uongo huo ni kutaka kuisaidia CCM na kugeuza mjadala.

3.    Idara ya Habari ya CHADEMA inapenda kuuambia umma wa Watanzania wote, hususan wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko nchini kwamba,Mwenyekiti wa Chama Taifa, ameshawasiliana na mawakili walifanyie kazi suala hili kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria.

4.     Kwa uhakika tunapenda kuiambia jamii ya Watanzania wote, hususan wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na wapenda mabadiliko wote nchini, kwamba; Chama wala Mwenyekiti wa Chama Taifa, mahali popote na wakati wowote, hajawahi kupokea msaada wa fedha hizo kutoka kwa waliotajwa kwa malengo yaliyosemwa.

5.     Tungependa kuwaambia waliozusha tuhuma hizo, ni vyema kama wanapenda kutunza heshima kidogo waliyobakiza katika jamii kutokana na kuelemewa na mzigo wa tuhuma za utovu wa maadili na usaliti dhidi ya CHADEMA, badala ya kugeuka kuwa mabingwa wa kupika uongo, wajibu masuala ya msingi yanayowaandamana kuhusu mikakati yao ya kuhujumu CHADEMA na viongozi wake, ambayo iwapo chama kisingeibaini na kuchukua hatua za kinidhamu, ingesababisha kuua ndoto na matumaini ya Watanzania kufanya mabadiliko ya kimfumo na kiutawala, kwa kuiondoa CCM madarakani.

6.     Taarifa kuhusu baadhi ya tuhuma katika mkakati huo ambazo zimemlenga Mwenyekiti wa Chama Taifa, kwa kuhusisha shughuli zake binafsi za uwekezaji, zitajibiwa kupitia taasisi husika.

Imetolewa leo Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA

MALINZI AZINDUA KAMPENI YA ISHI HURU

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akizungumza kwenye uzinduzi wa programu ya Ishi Huru jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amezindua programu ya kutoa elimu ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana iitwayo Ishi Huru.
Programu hiyo iliyozimduliwa tarehe 10 Januari mwaka huu jijini Dar es Salaam iko chini ya taasisi ya Africa Inside Out inayoongozwa na Rebecca Young wakati washirika (partners) ni TFF na kampuni ya Rhino Resources ya Marekani.
Rais Malinzi amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamekuwa yakiongezeka, hivyo kuwa kikwazo kwa maendeleo ya vijana ambapo ameipongeza Africa Inside Out kwa programu hiyo kwa vile itazuia vijana wengi kujiingiza katika matumizi ya dawa hizo.
"Moja athari kubwa za matumizi ya dawa za kulevya ni kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutokana na kuchangia sindano za kujidunga dawa hizo.
"TFF tutatoa ushirikiano wa kutosha katika programu hii. Lakini pia tutaingiza Ishi Huru katika programu zetu za mpira wa miguu kwa vijana. Tutahamasisha jamii katika kupambana na dawa za kulevya," amesema.
Katika uzinduzi huo, pia Rais Malinzi alizundua semina ya waelimishaji na kuwaeleza kuwa wamepata fursa hiyo kwa vile ni vijana wanaojituma, hivyo watafikisha vizuri ujumbe wa Ishi Huru katika shule na vituo vya vijana nchini.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MBUNGE WA CHADEMA MH. NDESAMBURO AMKINGIA KIFUA LOWASSA ASEMA ASISAKAMWE

Philemon Ndesamburo na Edward Lowassa 
WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikionekana kutikiswa na ushawishi wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, wa kutaka kutimiza safari yake ya kuwapatia Watanzania elimu bure, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (CHADEMA), amejitokeza kumkingia kifua na kutaka asisakamwe.

Kauli ya Ndesamburo inakuja siku chache wakati kukiwa na harakati za wazi wazi kuwapinga wanaotajwa kutaka kuwania urais, zikishika kasi ndani ya CCM na kuonekana kuzigonganisha vichwa jumuiya zake.  
Akitoa salamu zake za mwaka mpya jana, pamoja na kuzungumzia hali ya kisiasa nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani, Ndesamburo alisema Lowassa hapaswi kushambuliwa kwa kigezo cha kutangaza safari yake.  
“Wanaotangaza nia mbona wako wengi sana huko CCM na wala siyo Lowassa peke yake? Kwenye urais na hata huku chini kwenye ubunge na hata udiwani wako wengi tu wanafanya hivyo. Ina maana hao wanaomnyooshea kidole Lowassa hawa wengine hawawaoni?
“Hata huku kwenye vyama vyetu CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi wapo wanaotuvuruga, lakini sasa hivi habari ya mjini ni Lowassa, Lowassa… kama kweli hatupendezwi na hali hiyo tuwanyooshee wote basi, kama hatuwezi wamwache aendeleze ndoto yake. The best way to predict the future is to invent it,” aliongeza Ndesamburo.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

CHELSEA YATOA PAUNI MILIONI 25 KUMSAJILI NEMANJA

Kiungo wa Benfica, Nemanja Matic (kulia) anahusishwa na kurejea Chelsea kwa Pauni Milioni 25
Toughness: Jose Mourinho sees Matic as the man to fill Chelsea's need in the holding role
Jose Mourinho anaona Matic ndiye anayefaa katika nafasi ya kiungo mkabaji Chelsea
KLABU ya Chelsea imetoa ofa ya Pauni Milioni 25 kumsajili kiungo wa Benfica ya Ureno, Nemanja Matic arejee Stamford Bridge.
Kiungo huyo hodari alijiunga na Chelsea mwaka 2009, lakini akacheza mechi mbili tu kabla ya kutimkia Ureno mwaka kama sehemu ya dili ya David Luiz kutua Stamford Bridge.
Pamoja nayo, kocha Jose Mourinho sasa anaona Matic kama mtu anayefaa katika nafasi ya kiungo mkabaji wa timu yake.
Chanzo:BIN ZUBEIRY

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...