Friday, January 03, 2014
Thursday, January 02, 2014
MWANAJESHI AUA VIJANA WAWILI KWA BASTOLA
Mwanajeshi
wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ), ambaye jina lake limehifadhiwa
anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kuwaua kwa kuwapiga risasi
vijana wawili na kisha kuwajeruhi vibaya wengine wawili walipokuwa
katika shamrashamra za kuukaribisha mwaka mpya. Tukio hilo lilitokea
majira ya saa sita na robo usiku wa kuamkia jana, katika eneo la Pugu
Kinyamwezi, Ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na Mwandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha
Minangi (pichani) alisema tukio hilo lilitokea baada kundi la vijana
waliokuwa wakisherehekea mwaka mpya kuzingira gari la mwanajeshi huyo
aliyekuwa akielekea nyumbani kwake Pugu Kinyamwezi, akitokea katikati ya
Jiji kwa shughuli zake.
Alisema
mwanajeshi huyo alikuwa na gari aina ya Toyota Rava 4 na baada ya kufika
katika eneo hilo alizingirwa na kundi la vijana hao waliokuwa
wakisherehekea mwaka mpya na ndipo aliamua kutoa bastola yake na
kufyatua risasi ambapo iliwapata vijana hao na kufa papo hapo na
kujeruhi wengine.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
RAY C AFUNGUKA KUHUSU JACK CLIF... ASEMA WACHA AFE TU TENA ANYONGWE KABISA...!!!
Kutokana
na maswahibu makubwa yaliyompata Ray C juu ya madawa ya kulevya,
ameshindwa kujizuia kutokusema ya moyoni mwake juu ya mwanadada Jack Cliff aliyekamatwa na madawa ya kulevya nchini China. Kafunguka maneno
mengi sana na alionyesha ni jinsi gani alivyokuwa hamuonei huruma
mwanadada Jack mpaka kuamua kutamka bora anyongwe tu.
Soma alichokisema hapa
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
LOWASAA ATANGAZA KUANZA RASMI SAFARI YA NDOTO ZAKE...!!!
Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametangaza kuanza rasmi kwa safari
aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo amesema itatimiza ndoto za
Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.
Akizungumza
katika ibada ya shukrani na kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika ya Monduli Mjini, Lowassa
bila ya kutaja safari hiyo ni ipi, aliwashukuru watu wote kutoka maeneo
mbalimbali nchini, ambao walimsindikiza katika ibada hiyo.
Lowassa alisema anaamini watu hao waliofika, wana uhakika wa ushindi katika safari hiyo kwa kumtegemea Mungu.
"Nimefarijika
sana leo kuwaona hapa marafiki zangu wengi. Ninapowatazama hadi machozi
yananitoka na kwa uwezo wa Mungu tutashinda kwani nyote mnajua nia na
ndoto yangu,'' alisema Lowassa na kupokelewa na sauti za shangwe
kanisani.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
HII NDIO HISTORIA NZITO NA FUPI YA MAREHEMU DK. MGIMWA...!!!
Kuzaliwa: Januari 20, 1950 Kalenga Iringa.
Elimu:
1961 -1965 Shule ya Msingi Wasa
1966 - 1967 Shule ya Msingi Tosa
1968 - 1969 Tosamaganga Sekondari
1970-1971 Seminari ya Mafinga
1975 - 1984 Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) - Postgraduate in Finance
1989 - 1991 IDM Mzumbe (MBA - Finance)
Ajira
1981 - 2000 - NBC Ltd (Mhasibu, Mhadhiri, Mkurugenzi, Mkurugenzi Mkuu)
2000 - 2010 - Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania Mwanza (Mkuu wa Chuo)
2010 - 2013 - Mbunge, Kalenga (CCM)
Waziri wa Fedha,Dkt. William Mgimwa (pichani) alifariki Dunia Januari 1, 2014 katika Hospitali ya Mediclinic Kloff,alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Wednesday, January 01, 2014
KHERI YA MWAKA MPYA 2014...!!!
Jambo Tz Blog inapenda kuwatakia Watu wote husani wadau wa blog hii popote pale
walipo HERI YA MWAKA MPYA 2014. Nakutakia furaha, Baraka, Mafanikio, Afya tele,
Amani na Upendo.
Kwa namna ya kipekee kabisa. Pia endelea kuwa nasi mwaka 2014 kwani tumejipanga vilivyo kukuletea habari.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
AJALI MBAYA IMETOKEA ENEO LA CCM MBEYA USIKU WA MWAKA MPYA NA KUUA MTU MMOJA
Boda boda Mbili zikiwa zimegongana
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Tuesday, December 31, 2013
JAMAA APANDA JUU YA MNARA WA SIMU UBUNGO JIJINI DAR LEO NA KUGOMA KUSHUKA MPAKA AONANE NA RAISI KIKWETE
Askari
wa Kikosi cha Zima moto na Uokoaji Wakiwa wamepanda juu ya Mnara wa
Simu Uliopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam Muda mfupi uliopita kwaajili ya
kumuokoa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Hassan Ambaye
alipanda juu ya mnara huo kwa lengo la kufikisha Ujumbe wa kutaka
kuonana na Raisi Kikwete ili aweze kumwelezea kwa kile anachodai kuwa
jeshi la polisi lilimbambikia kesi na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha
Miaka 6 kwenda jela.
MAAJABU YA MWAKA: MUME AUZA KABURI LA MKEWE...!!!
Hii ndiyo
kali ya kufungia mwaka katika zote zilizotokea mwaka 2013! Mwanaume
aliyetajwa kwa jina moja la Abrahaman, mkazi wa Kimara-Kilungule, Dar,
anadaiwa kuuza kiwanja ambacho ndani yake kuna kaburi marehemu mkewe,
Aisha Abdul aliyefariki Julai 21, 2004.
MALALAMIKO MEZANI
Wakizungumza na Uwazi kwa nyakati tofauti, watoto wa marehemu ambao
wanapingana na tukio hilo la baba yao kuuza eneo hilo ambalo ni mali ya
marehemu mama yao, walidai kuwa wamefedheshwa na kitendo hicho.
“Kiukweli alichokifanya baba siyo sawa. Haiwezekani auze eneo ambalo
lipo kaburi la mama yetu. Mbaya zaidi hadi sisi watoto wa kutuzaa yeye
mwenyewe anatutishia maisha.
RAIS KIKWETE AMWAPISHA IGP MPYA PAMOJA NA NAIBU WAKE
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP)
mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam
jioni hii
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha
Naibu Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki
katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
Monday, December 30, 2013
BONGO MOVIE KAMA KAWADA YAO SAFARI HII WAMFANYIA WASTARA, MWEEEEEEE...!!!
DUA maalum ya kumbukumbu na kumuombea aliyekuwa msanii wa filamu Bongo,
Marehemu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ imezua minong’ono mingi kufuatia
wasanii wengi wanaounda Kundi la Bongo Movie kudaiwa kumfanyia mbaya
mkewe, Wastara Juma kwa kutohudhuria.
Dua hiyo ya ilifanyika Jumamosi iliyopita nyumbani kwa marehemu Tabata-Bima, Dar na kumalizikia kaburini kwake Kisutu.
Katika tukio hilo, wadau mbalimbali wa filamu na burudani,
walionekana kushangazwa na kitendo cha wasanii wengi wa Bongo Movie
kutokuwepo licha ya marehemu Sajuki kushirikiana nao kwa karibu enzi za
uhai wake.
Aidha, wengine walifika mbali kwa kuhoji kulikoni wafanye hivyo,
maswali ambayo yalimuongezea uchungu mkubwa Wastara aliyekuwa
akibubujikwa machozi mara kwa mara.
Kwa upande wake, Wastara alisema anamshukuru Mungu kwa kufanikisha
shughuli hiyo na kuwaombea kwa Mungu wote waliojitokeza kumuunga mkono
kwenye dua hiyo.
“Nawashukuru wote waliojitokeza, wamenifariji sana,” alisema Wastara kwa simanzi.
Wasanii wa filamu waliohudhuria dua hiyo, ni pamoja na Denis Sweya ‘Dino’, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Flora Mvungi, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ na Suleiman Bin Sinan ‘Bond’.
Wasanii wa filamu waliohudhuria dua hiyo, ni pamoja na Denis Sweya ‘Dino’, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Flora Mvungi, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ na Suleiman Bin Sinan ‘Bond’.
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’ alipotafutwa, simu iliita bila kupokelewa.
Sajuki alifariki dunia Januari 2, 2012 na katika kutimiza mwaka mmoja kaburini misa nyingine itafanyika nyumbani kwa wazazi wake mkoani Songea Januari 2, 2014. Na GPL
Sajuki alifariki dunia Januari 2, 2012 na katika kutimiza mwaka mmoja kaburini misa nyingine itafanyika nyumbani kwa wazazi wake mkoani Songea Januari 2, 2014. Na GPL
Tafadhari Like page yetu ya facebook kwa ku-click Jambo Tz
Subscribe to:
Posts (Atom)