Hii ndiyo
kali ya kufungia mwaka katika zote zilizotokea mwaka 2013! Mwanaume
aliyetajwa kwa jina moja la Abrahaman, mkazi wa Kimara-Kilungule, Dar,
anadaiwa kuuza kiwanja ambacho ndani yake kuna kaburi marehemu mkewe,
Aisha Abdul aliyefariki Julai 21, 2004.
MALALAMIKO MEZANI
Wakizungumza na Uwazi kwa nyakati tofauti, watoto wa marehemu ambao
wanapingana na tukio hilo la baba yao kuuza eneo hilo ambalo ni mali ya
marehemu mama yao, walidai kuwa wamefedheshwa na kitendo hicho.
Watoto hao walidai kuwa baba yao anauza mali huku akijua kabisa mama
yao aliacha wosia juu ya nani mrithi wa mali hizo (kopi ya wosia
tunayo).
“Hatujui nini kimemkumba baba maana amekuwa mkatili asiyekuwa na huruma
ya aina yoyote kwetu hadi na kwa majirani,” walisema watoto hao.
USHUHUDA
Gazeti hili lilifika eneo la tukio na kulishuhudia kaburi hilo huku
watoto hao wakipiga nalo picha kwa woga wasikute na aliyeuziwa.
Pia majirani walithibisha ukali wa baba huyo katika siku za hivi karibuni.
Katika hali ya kushangaza, wakati watoto hao wakitoa malalamiko hayo
walianza kugawanyika kifamilia ambapo mmoja wa mwisho wa kiume alikuwa
upande wa baba akiunga mkoni kile alichokifanya mzazi wake huyo.
Baada ya kusikia malalamiko hayo na kuoneshwa vielelezo, ilibidi kumtafuta mume huyo wa marehemu ili kuthibitisha madai hayo.
Alipopatikana alipelekewa tuhuma zake juu ya sakata ambapo bila hata
kusikia kwa makini alichokuwa akielezwa alianza kutukana huku
akilichimba mkwara Uwazi kufuatilia habari zake.
“Endeleeni kunifuatilia lakini mtakachokiona nisilaumiwe,” alisema baba huyo aliyeonekana kuwa na umri mkubwa.
Katika hitimisho, watoto hao walishauriwa kwenda kwenye vyombo au mamlaka za kisheria ili kupata haki zao
No comments:
Post a Comment