Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif
Hamad amesema Wazanzibar wanaisubiri kwa hamu Rasimu ya Katiba ya Tume
ya Mabadiliko ya Katiba ili kuona kama imezingatia masilahi na matakwa
yao katika kupata mamlaka kamili ya Zanzibar.
Msimamo huo ameutoa kwenye mkutano wa
hadhara wa CUF uliofanyika Kinyasini, Mkoa wa Kalazini Unguja na
kuhudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Maridhiano inayoongozwa na
Mwenyekiti wake, Mzee Hassan Nassor Moyo.
Aidha, katika mkutano huo, kwa mara ya
kwanza Waziri wa zamani wa SMZ na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
(NEC), Mansoor Yussuf Himid alihutubia tangu avuliwe uanachama wa CCM
kutokana na madai ya kwenda kinyume na sera, maadili na nidhamu ya chama
hicho.
Katika maelezo yake, Maalim Seif alisema wanachodai Wazanzibar
ni mamlaka kamili ni kuifanya Zanzibar ijitegemee kiuchumi, kujipangia na kujiamulia mambo yake ya ndani na nje bila ya kutegemea upande wowote.
ni mamlaka kamili ni kuifanya Zanzibar ijitegemee kiuchumi, kujipangia na kujiamulia mambo yake ya ndani na nje bila ya kutegemea upande wowote.
Alisema Zanzibar ilikuwa taifa huru
lililoungana na Tanganyika kwa ridhaa na siyo mateka wa Tanganyika,
hivyo wanayo sababu ya kujitegemea.
Tafadhari Like page yetu ya facebook kwa ku-click Jambo Tz