Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif
Hamad amesema Wazanzibar wanaisubiri kwa hamu Rasimu ya Katiba ya Tume
ya Mabadiliko ya Katiba ili kuona kama imezingatia masilahi na matakwa
yao katika kupata mamlaka kamili ya Zanzibar.
Msimamo huo ameutoa kwenye mkutano wa
hadhara wa CUF uliofanyika Kinyasini, Mkoa wa Kalazini Unguja na
kuhudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Maridhiano inayoongozwa na
Mwenyekiti wake, Mzee Hassan Nassor Moyo.
Aidha, katika mkutano huo, kwa mara ya
kwanza Waziri wa zamani wa SMZ na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
(NEC), Mansoor Yussuf Himid alihutubia tangu avuliwe uanachama wa CCM
kutokana na madai ya kwenda kinyume na sera, maadili na nidhamu ya chama
hicho.
Katika maelezo yake, Maalim Seif alisema wanachodai Wazanzibar
ni mamlaka kamili ni kuifanya Zanzibar ijitegemee kiuchumi, kujipangia na kujiamulia mambo yake ya ndani na nje bila ya kutegemea upande wowote.
ni mamlaka kamili ni kuifanya Zanzibar ijitegemee kiuchumi, kujipangia na kujiamulia mambo yake ya ndani na nje bila ya kutegemea upande wowote.
Alisema Zanzibar ilikuwa taifa huru
lililoungana na Tanganyika kwa ridhaa na siyo mateka wa Tanganyika,
hivyo wanayo sababu ya kujitegemea.
Tafadhari Like page yetu ya facebook kwa ku-click Jambo Tz
"Madai yetu yako wazi, hayana kificho
na siyo mageni, tunaisubiri kwa hamu rasimu ya Jaji Warioba, kama ni
supu isiyolika, hatutaila tutamrudishia mwenyewe na kuendeleza madai
yetu," alisema Maalim Seif.
Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa
Kwanza wa Rais Zanzibar, alisema Zanzibar itasimama wenyewe na
kujiendeleza kwa kufuata misingi iliyowekwa na Rais wa Kwanza wa
Zanzibar hayati Mzee Abeid Amani Karume.
"Madai yetu ni kama meli iliyobeba
watu wengi, ikizama tunazama wote, lengo letu ni kufika salama katika
bandari ya matumaini na kila mmoja aweze kunufaika na matunda ya nchi
yake," alisema Maalim Seif.
Alisema ikiwa Wazanzibari watapata
Serikali, anaamini mengine yatakuja yenyewe na kuinufaisha Zanzibar
kiuchumi na kusisitiza kuwa muundo wa Serikali mbili umepitwa na wakati.
Chanzo: mwananchi
Tafadhari Like page yetu ya facebook kwa ku-click Jambo Tz
No comments:
Post a Comment