Siku za furaha: Mario Balotelli akiwa mwenye furaha wakati wa mazoezi ya Italia Uwanja wa Craven Cottage jana
'KACHAA' Mario Balotelli alikuwa
mwenye furaha aliporejea England wakati mshambuliaji huyo wa AC Milan
alipokuwa akifanya mazoezi na kikosi cha Italia Magharibi mwa London.
Balotelli aliichezea Manchester City
kabla ya kutibuana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Roberto Mancini na
wachezaji wenzake kadhaa hivyo kuondoka, lakini nyota huyo mwenye umri
wa miaka 23, aliyeondoka Etihad miezi 10 iliyopita, alikuwa mtulivu
jana.
Kikosi cha The Azurri kinaendelea na
maandalizi ya Fainali za Kobe la Dunia mwakani nchini Brazil na leo
usiku kitacheza mechi ya kirafiki na Nigeria, kwenye Uwanja wa Fulham,
Craven Cottage.