Waziri wa mambo ya nje wa Kenya
Amina Mohammed amesema kuwa hakuna rais hata mmoja aliye mamlakani
amewahi kufikishwa mbele ya mahakama ya ICC. Taarifa hii bila shaka
imetafsiriwa na wengi kuwa mpango wa Kenya kutokubali Rais Uhuru
Kenyatta kuwasilishwa mbele ya mahakama ya ICC mwezi ujao.
Duru zinseama kuwa kuwa hofu kuwa huenda Kenyatta akakosa kufika mahakamani kama alivyoamrishwa na mahakama.
Waziri Amina amesema kuwa Rais
Kenyatta yuko tayari kushirikiana na mahakama ya ICC lakini kwa kuwa
yeye ni rais hali imebadilika. Kenyatta anatakikana na mahakama ya ICC
kuhusiana na uhalifu dhidi ya bindamu katika ghasia za baada ya uchaguzi
mkuu mwaka 2007/2008
Bi Abdalla aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari siku tatu kabla ya mkutano wa Muungano wa Afrika kujadili uhusiano wa Afrika na mahakama ya ICC.
Bi Abdalla aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari siku tatu kabla ya mkutano wa Muungano wa Afrika kujadili uhusiano wa Afrika na mahakama ya ICC.