Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli (katikati) akipewa maelezo na Meneja wa Tanroads mkoa wa Iringa Eng. Poul Lyakurwa wakati alipokuwa akipita kukagua eneo la Kitonga katika barabara ya TANZAM mkoani Iringa. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) na Eng. Chrispianus Ako kutoka Tanroads Makao Makuu (wa kwanza Kushoto) pamoja na watendaji wengine kutoka Wizara ya Ujenzi.
Kujifunga
kwa barabara katika eneo la Kitonga katika barabara kuu ya TANZAM
kumekuwa kukisababisha adha kubwa kwa wasafiri. Eneo hilo liko mkoani
Iringa katika barabara kuu inayoanzia jijini Dar es Salaam ikiunganisha
na mikoa ya kusini magharibi mwa nchi yetu pamoja na nchi jirani za
Zambia, Congo DR na Malawi.
Barabara
katika sehemu ya Kitonga inapita katika muinuko mkali ambapo inapotokea
ajali au gari kuharibika, huwa ni vigumu kwa magari mengine kupita hadi
gari lilizoba njia liondolewe.
Hivi
karibuni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alikutana
na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Dkt. Christine Ishengoma ambapo
pamoja ya mambo mengine yaliyozungumziwa katika kikao hicho,
lilijitokeza suala la kujifunga mara kwa mara kwa barabara ya TANZAM
katika eneo la Kitonga.