Paroko
wa Parokia ya Roho Mtakatifu Cheju Zanzibar, akisaidiwa na Frateri,
Richard Haki kupumzika kitandani baada ya kuzungumza na waandishi katika
katika Wodi ya Kibasila iliyopo katika Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH) jijni Dar es Salaam jana.Picha Salim Shao
…………….
Dar es Salaam/Zanzibar.
Padri wa Parokia ya Mpendae ya
Kanisa Katoliki Zanzibar, Anselmo Mwang’amba amesema kuwa alimwona mtu
aliyemwagia tindikali na kumsababishia majeraha na kueleza kuwa
anashangaa kuona polisi hawajamkamata hadi sasa.
Akizungumza jana katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kwenye Wodi namba 16, Kibasila
alipolazwa, Padri Mwang’amba alisema baada ya kumwagiwa tindikali,
alimwona mtu huyo akikimbia kuelekea katika nyumba moja jirani.
“Kwa kuwa mimi nilikuwa na
taharuki na maumivu, sikuweza kuendelea kumfuatilia, ila dereva
aliyenikimbilia kunipa msaada aliniambia kwamba alimwona mhusika
akikatiza kwenye uchochoro hadi alipoingia kujificha kwenye nyumba
iliyopo jirani na eneo hilo,” alisema.
Alisema majeraha aliyoyapata
wakati akitokea katika duka la huduma za mawasiliano ya mtandao la Shine
Shine saa 10.15 jioni, ambayo yanamsababishia maumivu makali, hayawezi
kumfanya aikimbie Zanzibar, kwa kuwa hata Yesu Kristo wakati alipokuwa
katika kazi za utumishi duniani alipata mateso makali kuliko yake.