Bila kutaja taasisi wala wanaohusika katika jitihada hizo za kidiplomasia, Dk Sezibera aliwaambia waandishi wa habari jijini Arusha jana kuwa jitihada hizo zinafanyika kimya kimya bila kushirikisha vyombo vya habari "Migongano na tofauti za kimtazamo miongoni mwa viongozi wakuu wa nchi wanachama wa EAC ni jambo lisilo la afya kwa Jumuiya na linastahili kushughulikiwa kidiplomasia," alisema Dk Sezibera.
Akizungumza kwa tahadhari kubwa
kukwepa kuingia kwa undani kuhusu suala hilo, Katibu Mkuu huyo alisema
inafaa kila linalowezekana lifanyike kutatua mgongano wowote unaotokea
kati ya viongozi wakuu.
Mjini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe naye alisema katika mahojiano kuwa iwapo Rwanda itaomba kukutana na Tanzania kwa ajili ya kumaliza mzozo huo Serikali itakuwa tayari kutoa ushirikiano.