POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imebaini kuwa chombo
kilichodhaniwa kuwa bomu katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Usharika wa Kijitonyama hakikuwa bomu, bali ni kifaa cha
Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) cha kuchunguza anga.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleman Kova alisema hayo jana alipozungumza na waandishi
wa habari, baada ya kufanya uchunguzi kwa kushirikiana TMA.
"Baada ya kupata taarifa, polisi walifika eneo la tukio na
kukuta kifaa kilicho katika umbo la kasha kikining'inia kwenye transfoma
karibu na Kanisa kikiwa kinawaka taa.
“Katika kasha hilo kulikuwa na maandishi ya kalamu ya wino yaliyosomeka TMA na Airport," alisema Kamanda Kova.
Alisema baada ya uchunguzi wa awali, polisi walibaini kuwa
kifaa hicho si bomu na kuondoka nacho kwa uchunguzi zaidi. Mtabiri
Mwandimizi wa hali ya hewa kutoka TMA, Augustino Kanemba, alisema kifaa
hicho kinaitwa Radio Sound na hutumiwa na Mamlaka hiyo kufanya utafiti
wa hali ya anga za juu.
"Kifaa hiki hurushwa juu kuleta taarifa ya hali ya anga, kwa
kawaida hufungwa puto ili kipae angani na baada ya kufika juu, puto
hupasuka na kutua sehemu yoyote ya Dar es Salaam … hili
si bomu," alisisitiza Kanemba.
Hata hivyo, Kamanda Kova alipongeza washarika wa Kanisa
hilo, kwa kutoa taarifa Polisi na kuomba waendelee kufanya hivyo
wanapoona kitu wasichokielewa.
Akizungumzia mlipuko katika Kanisa la KKKT, Usharika wa
Segerea, Kamanda Kova alisema Polisi Kanda Maalumu Dar
es Salaam, kwa kushirikiana na wataalamu wa fani za ugaidi na matumizi
ya mabomu kutoka makao makuu ya Jeshi hilo, wanafanya upelelezi kubaini
waliohusika na tukio hilo. Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.
Katika tukio hilo la Agosti 24 mwaka huu
saa 8 usiku, waumini wapatao 20 wakiwa wanaendelea na ibada, ghafla
walitokea watu wanne na kuingia kanisani na kutupa chupa ya bia ikiwa na
utambi na mafuta yadhaniwayo kuwa ya taa eneo la madhabau na kusababisha
mlipuko.
Katika hatua nyingine, Polisi imekamata wahalifu 180
wakiwamo majambazi katika msako ulioendeshwa na Jeshi hilo ndani ya wiki
moja. Pia imekamata bastola mbili, risasi tisa, magunia mawili ya bangi
na magari mawili ya wizi.
SOURCE: HABARI LEO
Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.
Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.
No comments:
Post a Comment