Sunday, August 11, 2013

WAINGEREZA WALIOMWAGIWA TINDIKALI WAITESA SERIKALI

071 c44b8

Siku tano baada ya raia wawili wa Uingereza kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar, Serikali kupitia vyombo vyake vya uchunguzi imeibuka na kueleza kuwa bila wananchi kutoa taarifa za ushahidi wa uhalifu wa aina mbalimbali, ni vigumu kuwabaini wahusika. (HM)

Kauli hiyo ilitolewa kwa pamoja jana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) Eliezer Feleshi, katika mkutano wao na waandishi wa habari, uliolenga kueleza mikakati ya kupambana na matumizi yasiyo sahihi ya tindikali nchini.

Katika ufafanuzi wao walisema, "Kutoa taarifa ya uhalifu wa jambo lolote siyo hiari, ni jukumu la kisheria na kikatiba," huku Feleshi akitolea mfano jinsi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk Steven Ulimboka alivyoshindwa kutoa ushahidi wa tukio lililomkuta la kutekwa, kupigwa na kisha kutupwa katika Msitu wa Mabwepande, hivyo kufanya uchunguzi kuwa mgumu.

Saturday, August 10, 2013

NDEGE YA KIJESHI YALIPUKA NA KUTEKETEA KWA MOTO WAKATI IKITUA KWA DHARURA.

Ndege hiyo ilikuwa ya jeshi la Ethiopia.MOJA YA NDEGE ZA NCHI YA SOMALIA.Ndege ya kivita MaliPICHA YA NDEGE ZA JESHI YA MAKTABA SIO YA SOMALIA.
NDEGE ya kijeshi imelipuka na kuteketea nchini Somalia baada ya kutua kwa dharura katika uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Mogadishu.
Kikosi cha muungano wa Afrika nchini Somalia ambacho kina kambi yake katika uwanja huo wa ndege kimesema kuwa wanajeshi wake kadhaa wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa.

Inasemekana kuwa ndege hiyo ilikuwa ya jeshi la Ethiopia.
Kuna ripoti kuwa ndege ilikuwa imebeba zana za kivita.
Wafanyakazi katika uwanja huo wa ndege waliel
ezea kusikia milipuko kadhaa huku moto ukienea kwa ndege hiyo.

JESHI LA POLISI LATANGAZA DAU LA MILIONI 10 KWA MTU ATAKAYEWATAJA WATU WALIOWAMWAGIA TINDIKALI WAZUNGU

Zanzibar, Tanzania — Kamanda wa Polisi, Kamishna Musa Ali Musa amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kutoa Shilingi milioni 10/= kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa watu waliowashambulia mabinti wawili kutoka Londona, Uingereza, Kirstie Trup na Katie Gee.

Mabinti hao walishambuliwa kwa tindikali usoni, kifuani na mikononi siku ya Jumatano walipokuwa njiani kuelekea kwenye chakula cha jioni.

Friday, August 09, 2013

JAJI MUTUNGI AANZA KUTUMA SALAMU ZA UTENDAJI KAZI WAKE ....!!!



Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman akimpongeza Francis Mutungi baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Jaji wa Mahakama Kuu katika hafla iliyofanyika Ikulu, Juni 19,2012. Jaji Mutungi jana aliteuliwa kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa. Picha na Maktaba. 
********
Dodoma. Msajili mteule wa Vyama vya Siasa nchini,  Jaji Francis Mutungi amewataka Watanzania kutulia na kusubiri utendaji wake atakapokabidhiwa rasmi jukumu hilo jipya alilopewa na Rais Jakaya Kikwete.
Mutungi aliteuliwa kushika wadhifa wa msajili wa vyama vya siasa kuchukua nafasi ya John Tendwa ambaye amestaafu. Tendwa aliiongoza taasisi hiyo kwa miaka 13.
Mutungi alisema: “Ninafahamu nina majukumu mazito mbele yangu, lakini siwezi kusema chochote kwa kuwa sijakabidhiwa rasmi ofisi. Ninachotaka kusema ni kwamba nitakuwa mtumishi wa kila mmoja.”

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI SWALA YA SIKUKUU YA IDDI KITAIFA MKOANI TABORA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa salamu maalum za Sikukuu ya Iddi baada ya Swala iliyofanyika Kitaifa Mkoani Tabora katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi leo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa sita kutoka kulia), akishiriki na waumini wa dini ya Kiislamu katika Swala ya Sikukuu ya Iddi, iliyoswaliwa Kitaifa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora leo.

SIMBA KUADHIMISHA SIMBA DAY KESHO TEREHE 10.

KESHO, Jumamosi tarehe 10 Agosti mwaka 2013, klabu ya soka ya Simba itaadhimisha kile kinachoitwa Siku ya Simba (SIMBA DAY) katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 
Utaratibu wa kuwa na Simba Day ulianzishwa na klabu kwa lengo la kuwa na siku ambapo wapenzi, wanachama, viongozi, wachezaji wa zamani na wa sasa pamoja na watu wengine mashuhuri, hukutana kwa pamoja na kusherehekea klabu ambayo imewafanya wawe wamoja pamoja na tofauti nyingi walizonazo.
 
Mwaka huu, shughuli hiyo itafanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, Simba SC inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na klabu ya soka ya Sports Club Villa kutoka nchini Uganda.
Katika kusherehesha tukio hilo, wasanii maarufu kama vile Juma Nature, Tunda Man na Snura maarufu kwa jina la ‘Mama Majanga’ watatumbuiza uwanjani hapo.

MUME WA JOYCE KIRIA, HENRY KILEWO AWALIZA WATU KWENYE MKUTANO MABIBO SAHARA

Leo akiwa anawahutubia wakazi wa mabibo-Sahara kwa mara ya kwanza toka atoke jela huko gereza la uyui- Tabora ktk mkutano ambao mgeni rasmi alikua John Mnyika, aliwaliza baadhi ya wananchi waliofika katika mkutano huo. Hii kutokana na kuguswa na hotuba ya kamanda Kilewo ambayo ilikua inaudhunisha kutokana na simulizi ya namna alivyokamatwa na huko jela namna ya watu waliofungwa pasipo na hatia.

kiukweli inasikitisha, lakini bado alisisitiza kwa kusema 'hakuna dhambi kubwa hapa duniani kama uoga' na ' watatupiga kwa mabomu na watatu ua kwa risasi lakini na wao watakufa kwa presha ya dhambi

WANYARWANDA 520 WATII AGIZO LA RAIS KIKWETE LA KUONDOKA NCHINI

044 2423a 
Zikiwa zimesalia saa 48 kabla ya kumalizika kwa muda uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa wahamiaji haramu kuondoka nchini au kuhalalisha ukaazi wao na wenye silaha kuzisalimisha, makundi ya wahamiaji hao, yameanza kuondoka kwa hiari.
Wastani wa wahamiaji haramu 150 wanaendelea kujiandikisha kuvuka mpaka katika Kituo cha Rusumo, Ngara mkoani Kagera kutekeleza agizo hilo.

Ofisa Uhamiaji wa Kituo cha Rusumo, Samweli Mahirane alisema mpaka sasa Wanyarwanda 520 wameshaondoka katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Ngara na kurejea makwao huku Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe akisema silaha 17 za aina mbalimbali zimesalimishwa.
Mahirane alisema wahamiaji hao wanatokea katika vijiji vya Wilaya za Ngara, Karagwe, Kyerwa, Biharamulo na Geita pamoja na Runzewe na wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo bila vibali halali. (HM)

"Kuondoka kwa hiari kwa wahamiaji haramu, kutahitimishwa Jumatatu Agosti 12 na baada ya tarehe hiyo, vyombo vya dola vitaanza kufanya kazi kama agizo la Rais Kikwete lilivyoelekeza katika Mikoa ya Kagera na Kigoma," alisema.
Aliwahakikishia wahamiaji hao usalama katika mataifa yao kwani hivi karibuni Serikali ya Rwanda ilikubali kuwapokea hata walio na mifugo kwa masharti kuwa ndani ya kipindi kifupi wataipunguza kwa kuiuza na kuboresha maisha yao.

"Rwanda wanahitaji mifugo michache, hivyo walio na mingi wanatakiwa kuipunguza kwa kuuza na kujenga makazi bora ikiwa ni pamoja na kuhifadhi ama kulinda mazingira ya nchi hiyo," alisema Mahirane. Chanzo: mwananchi

MOURINHO: HATUTAKATA TAMAA MPANGO WA KUMSAJILI ROONEY...!!!

jose 13f47
Jose Mourinho amesisitiza kwamba atapigana mpaka siku ya mwisho katika jaribio lake la kumsaini Wayne Rooney. (HM)

Chelsea tayari walishatuma ofa mbili ambazo zimekataliwa na Manchester United, ofa ya mwisho inayotajwa kuwa ni zaidi ya paundi million 25 ilitumwa jumapili. Lakini Mourinho alisema: "Hatuna kizuizi cha muda kwenye suala hili.

'Tumemuona Rooney kama ni mchezaji ambaye tungependa kuwa nae. Tumefanya kila kitu katika utaratibu unaopaswa na tutafanya hivyo mpaka siku ya mwisho ya usajili. Tunafnya kila kitu tukizingatia sheria, kutoa ofa rasmi kwa klabu moja kwa moja.
 

'Hakujawahi kuwepo kwa mawasiliano na mchezaji, hakijatokea kitu kama hicho. Tusubiri tuone kama mambo yatabadilika.'

Rooney inaaminika kwamba amemwambia kocha wake David Moyes kwamba anataka kuondoka, lakini United imekuwa ikisisitiza kwamba hauzwi. Chanzo: shaffihdauda

Thursday, August 08, 2013

WAPINZANI WACHEZEA KICHAPO KIKALI KIBONDO....!!!

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akizungumza na madiwani wa CCM wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wiki iliyopita.

Katika hali inayothibitisha ule usemi wa mwanamuziki Chameleon wa Uganda kuwa "fitina yako bahati yangu" wapinzani wamechezea kichapo cha mwaka kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kibondo baada ya CCM kushinda kwenye nafasi zote za kuongoza Halmashauri hiyo, ushindi uliowaacha midomi wazi wapinzani waliokuwa wakisubiri kufaidi kwenye ugomvi wa madiwani wa CCM wilayani hapo.

Diwani wa CCM Ndugu  Emily Msanya kuibuka Mwenyekiti wa Halmashauri baada ya kupata kura 14 kati ya 17 zilizopigwa na Makamu Mwenyekiti ni Apronary Mazinda ambaye pia alishinda kwa kura 14 kati ya 17.

Kuchaguliwa kwa madiwani hao na ushindi huo wa CCM kwenye ngome ya upinzani ambapo Mbunge wa jimbo hilo ni Ndg. Mkosamali wa NCCR-Mageuzi ni uthibitisho dhahiri kuwa CCM ina mkakati mkubwa wa kuzidhibiti ngome zote za upinzani nchini kuelekea uchaguzi wa 2014 na 2015.

MUME WA PILI WA WASTARA AIBUKA, ADAI WASTARA NI MKEWE....!!!

Na Issa Mnally
MIEZI nane baada ya kufariki dunia mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’, ...


 hatimaye mume wa pili wa staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma aitwaye Ahmed Kushi ameibuka na kudai kwamba anatambua kwamba staa huyo bado ni mkewe na anataka ampatie mwanaye aliyezaa naye.
Kwa muda mrefu kulikuwa na taarifa kuwa Wastara aliachana na mwanaume huyo kwa talaka kabla ya kuolewa na Sajuki lakini kuibuka kwake na madai kuwa bado mwanadada huyo ni mkewe kumezua mshangao mkubwa.

MADAI YA KUSHI
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Kushi alifunguka kwa mara ya kwanza kuwa yeye na Wastara walifunga ndoa ya Kiislamu mwaka 2000 na kujaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Fares.

Alisema: “Kisheria bado ni mke wangu kwa kuwa nilikuwa nimempa talaka moja tu wala hazikufika tatu,” alisema Kushi na kudai kwamba ndoa yake na staa huyo ilidumu kwa mwaka mmoja na nusu na kuvunjika kutokana na kutawaliwa na migororo.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 08, 2013

DSC 0002 ffed9
DSC 0003 490e8

HII NDIO HOTEL ILIYOKUWA INAUZA NYAMA ZA WATU ILIYOBOMOLEWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI...!!!

hotel human heads in onitsha
HAPA WANANCHI WAKIIVUNJA HOTELI HIYO
Polisi walifanikiwa kuvikamata vichwa hivyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema wanaoishi karibu na hoteli hiyo ambapo mbali na vichwa hivyo viwili lakini pia walikamata bunduki mbili aina ya  AK47,kofia mbili za jeshi pamoja na simu nyingi.

Watu saba wanashikiliwa na jeshi la polisi nchini Nigeria katika hoteli moja iliyopo karibu na soko moja maarufu sana nchini humo linalofahamika kwa jina la Ose-Okwodu katika mji wa Anambra baada ya kukamatwa kwa vichwa viwili vya binadamu vikiwa bado vibichi lakini jina la hoteli hiyo linahifadhiwakutokana na sababu za kiusalama

"MAUAJI YA SOWETO YALIPANGWA NA KUTEKELEZWA NA POLISI" LEMA

Mbunge wa Arusha, Godbless Lema, ameendelea kushikilia madai yake kuwa polisi wanahusika na tukio la bomu lililolipuka katika mkutano wa kampeni ya chama hicho Viwanja vya Soweto Arusha na kusababisha vifo vya watu wanne.

Lema alitoa madai hayo juzi alipohutubia mkutano wahadhara Viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro.


Alidai Rais Jakaya Kikwete amegoma kuunda tume huru ya kimahakama kuchunguza tukio hilo, ili kunusuru polisi na aibu ya kushiriki uhalifu na mauaji ya raia wasio na hatia.


“Mauaji ya Soweto yalipangwa na kutekelezwa na polisi, RPC (Kamanda wa Polisi) wa Arusha anajua mpango mzima ndiyo maana Rais hataki kuunda tume kama Chadema tulivyomuomba, ili tuwasilishe ushahidi wa video kuonyesha jinsi walivyohusika,” alisema Lema

MTUHUMIWA WA WIZI WA FEDHA KWENYE ATM ANASWA JANA JIJINI DAR



Dar es Salaam. Msako wa wezi wa kwenye Mashine za Kutolea Fedha (ATM), umeanza kuzaa matunda baada ya raia wa Bulgaria kukamatwa akiiba kwenye ATM ya Bank of Africa (BOA), Tawi la Afrikana, Kinondoni, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za benki, mtuhumiwa huyo ambaye
hakutajwa jina lake alikamatwa baada ya kamera maalumu zilizowekwa kwenye ATM za BOA, kumtambua kuwa ni mwizi sugu wa benki hiyo anayetafutwa.

Mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo ambaye hakupenda kutajwa jina kwa kuwa si msemaji, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 12 asubuhi baada ya mtuhumiwa huyo kuwekewa mitambo maalumu ya kumnasa.

Alisema benki hiyo ilipelekewa malalamiko na baadhi ya wateja kwamba wakienda kutoa fedha kwenye ATM wanakuta akaunti zao hazina salio wakati wanaamini zilikuwa na fedha.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...