Mutharika, ambaye ni mwanasheria, aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi Mkoa wa Kati.
Akikaririwa na gazeti la Nyasa Times, Mutharika alisema Tanzania haina cha kuambulia kwa Ziwa Malawi.
Kiongozi huyo ambaye hakuwapo katika
mkutano wa Rais Joyce Banda na wapinzani kuzungumzia mustakabali wa
ziwa, aliwahakikishia Wamalawi kuwa wasiwe na wasiwasi wa mvutano huo.
Tuesday, August 06, 2013
MGOMBEA ALITUMIA ZIWA NYASA KUJIPIGIA DEBE MALAWI
Mgombea Urais wa Democratic Progressive Party (DPP) nchini Malawi, Peter Mutharika, amesema hakuna sababu za kufanya majadiliano kuhusu Ziwa Malawi ambalo Tanzania wanaliita Ziwa Nyasa. (HM)
TAARIFA YA SIKU KUU YA EID KUTOKA JESHI LA POLISI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani ya Simu “ MKUUPOLISI” Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734 Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556 S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dar Es Salaam Agosti 06, 2013.
Ndugu Wanahabari,
Jeshi la Polisi Nchini linatoa shukrani kwa wananchi wote wakiwemo waandishi wa habari, viongozi wa dini, wanasiasa, makampuni binafsi ya ulinzi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa njia mbalimbali katika kuhakikisha kwamba nchi yetu ya Tanzania inakuwa salama na raia wote wanaishi kwa amani na utulivu bila hofu ya uhalifu na wahalifu.
Katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki na za haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo wanamoishi na sehemu mbalimbali zikiwemo maeneo ya biashara.
Ikumbukwe kuwa, wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe. Uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu. Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha kwamba, wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu, pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
Monday, August 05, 2013
KESI YA UGAIDI TABORA YAFUTWA, MUME WA JOYCE KIRIA NA WENZAKE WABAKI NA SHITAKA MOJA...!!!
Katibu
Wa Chadema mkoa wa kinondoni na Kanda maalum ya Dar es salaam, mjumbe
wa mkutano mkuu Henry Kilewo(Kulia) na Wenzake Wanne Wameachiwa. Wamefutiwa mashitaka yote ya Ugaidi, sasa wamebakia na shitaka moja la
kudhuru mwili, dhamana itatolewa na mahakama ya wilaya Igunga. Habari zaidi Baadae
WEMA SEPETU NA IRENE UWOYA WAPIMANA UWEZO, ALIANZA WEMA, UWOYA AJIBU MASHAMBULIZI
“Mashabiki wa Clouds TV watapata kuona vita ya kibiashara, Uwoya atakuwa akionekana katika kipindi hicho ambacho kitakuwa kinahusu upakaji rangi katika nyumba za watu mbalimbali huku Wema naye akikimbiza katika In My Shoes,” alisema Ruge.
ARSENAL 1 VS 2 GALATASARAY: DROGBA AKUMBUKIA ENZI ZAKE, AWAFUMUA ARSENAL MAWILI NA KUTWAA KOMBE LA EMIRATES
Kama kawaida rafiki wa nyavu: Drogba alifumania nyavu mara mbili na kutwaa taji la kombe la Emirates
Drogba akimpeleka sokoni kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny
Mnanikumbuka? Drogba akishangilia baada ya kipenga cha mwisho cha mwamuzi
Ufunguzi wa karamu ya mabao: Walcott akiandika bao la kuongoza kwa klabu yake ya Arsenal
DR. SLAA AWAUNGA MKONO WAASI WA KONGO NA KUMKINGIA KIFUA KAGAME...!!!
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli yake ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake ...
Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo.
Slaa aliyasema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani na hajachukua hatua dhidi ya wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi...
"Alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda na badala yake amempandisha cheo,” alisema Slaa.
MTOTO MDOGO WA KIKE AUAWA KINYAMA MKOANI MBEYA...!!!
MTOTO mmoja
wa kike ameuawa kinyama kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kisha kunyofolewa
macho na ubongo wake.
Tukio hilo
la kikatili, limetokea mwishoni mwa wiki eneo la Idiwili kata ya Isuto wilaya
ya Mbeya vijijini mkoani hapa.
Mtoto huyo
wa kike, asiye na hatia, mwenye umri wa miaka miwili, aliyejulikana kwa jina la
Lilian Nex Kasonso, alikatishwa uhai wake kwa makusudi kisha mwili wake
kutelekezwa chini ya mti.
Baadhi ya
wananchi wa eneo hilo waliozungumza mwandishi wa habari hii wamesema kuwa, Mama wa mtoto huyo, alimwacha
mwanae akiwa salama mikononi mwa bibi yake kisha yeye kwenda kutafuta kuni.
Punde, Bibi
yake Lilian, naye alienda kuchota maji mtoni huku akimwacha mjukuu wake akiwa
na furaha tele, ndipo majitu hayo makatili, kwa makusudi walimteka mtoto huyo
kisha kutokomea naye pasipo mtu kuwaona ama kuwashitukia.
PEPSI WAIPA YANGA KIBURI...!!!
Habari za uhakika ambazo Mwananchi limezipata zinadai kuwa, Yanga wamepata kiburi cha kugomea udhamini wa Azam baada ya kuwa na ofa mbili mkononi ya Pepsi na ile ya Zuku.
“Pepsi wanatoa kinywaji chao kipya Pepsi Cola na wametupa ofa ya Sh600 milioni, Azam walifuatwa na kuelezwa juu ya ofa hiyo wakakataa Pepsi wasiingie kwa vile ni wapinzani wao kwa Azam Cola,” kilisema chanzo cha habari.
Chanzo hicho kilisema kuwa, Yanga waliwapa sharti Azam la kuongeza dau kutoka Sh100 milioni na kama isingewezekana basi waingie mkataba na Kampuni ya Pepsi.
Sunday, August 04, 2013
TAMBUA SABABU ZA WATOTO WACHANGA KULIA, HIZI NDIZO SABABU ZAKE !!!!.
Sababu za Watoto Wachanga Kulia Mara kwa Mara na Namna ya Kuwabembeleza
Kwa nini watoto wachanga wanalia .?
Ni
kawaida kwa watoto kulia. Hata watoto wanaozaliwa na afya njema kabisa
wanaweza kulia kwa jumla ya wastani wa kati ya saa moja mpaka matatu kwa
siku. Kwa vile watoto hawawezi kujifanyia chochote wao wenyewe zaidi ya
kutegemea wazazi, walezi ama watu wengine wanaowazunguka katika
kuwapatia chakula, joto, na faraja, kilio ni njia ya mtoto ya
kuwasilisha moja ya mahitaji hayo.
Kama
mzazi mpya, wakati mwingine inakuwa vigumu kutambua mtoto wako
anahitaji nini anapolia. Mzazi anaweza kuwa na maswali kadhaa kichwani
mwake, je, mtoto ana njaa, anasikia baridi, ana kiu, anaumwa ama
amechoka ? Katika siku za mwanzo, hali ya namna hii inawawia vigumu
wazazi wengi, wasijue nini la kufanya.
Hata hivyo, kwa kadiri siku
zinavyopita mzazi mpya ataweza kutambua kuwa kilio cha mtoto wake
kinamaanisha anahitaji nini kutokana na mfumo wake wa kulia.
SERIKALI: WALIOOANA NA WAHAMIAJI HARAMU WAVUNJE NDOA HIZO.....!!!
Mkuu wa mkoa wa Geita, Said Magalula
******
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa mkoa wa Geita, Said Magalula, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya ulinzi na usalama wa mkoa huo.
Agizo hilo limekuja siku chache, tangu Rais Jakaya Kikwete kutoa siku 14 kwa wahamiaji wote haramu kutokana nje ya nchi kuondoka kwa hiari yao kabla ya kuwasaka na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
JK AKUTANA NA BINGWA WA DUNIA WA KURUKA KAMBA HAMISI MOHAMED NA WENZAKE
Rais
Jakaya Kikwete akimpongeza kijana wa Kitanzania Hamisi Mohamed mwenye
umri wa miaka 14 aliyeipatia sifa Tanzania kwa kunyakua ubingwa wa
Dunia wa mchezo wa kuruka kamba kwenye michuano iliyofanyika huko
Orlando, Marekani, mwezi uliopita. Kijana huyo, ambaye awali
alilelewa katika kituo cha watoto yatima cha Dogo Dogo Dar es Salaam,
alianza kupata mafunzo ya mchezo huo ambapo alishiriki mashindano ya
Afrika Mashiriki yaliyofanyika Mombasa na kunyakua Medali ya Dhahabu.
Kulia ni mfadhili wa kijana huyo, Amy Canady, na kushoto kwa Rais
Kikwete ni Sister Jean Pruitt, mwanzilishi wa kituo cha kule yatima cha
Dogodogo Centre |
Rais
Kikwete akiwa na bingwa wa dunia Hamisi Mohamed pamoja na wachezaji
wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya
dunia
RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BILL CLINTON ATUA BONGO KIAINA.....!!!
Rais Jakaya Kikwete akimpokea mgeni wake Rais mtaafu wa Marekeni Bill Clinton anayepanda gari (HM)
Clinton alitembelea eneo hilo akitokea moja kwa moja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam (JNIA), alipowasili akiwa katika ziara ya nchi mbalimbali za Afrika kukagua miradi inayoendeshwa na mfuko wake.
Katika eneo hilo rais huyo mstaafu alipokewa kwa shamrashamra mbalimbali ikiwamo ngoma za kiasili huku baadhi ya wananchi wakipigwa butwaa na kutoamini macho yao kwa kiongozi huyo kutembelea makazi yao.
Subscribe to:
Posts (Atom)