Tuesday, August 06, 2013

TAARIFA YA SIKU KUU YA EID KUTOKA JESHI LA POLISI


3 c9818
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA



Anuani ya Simu “ MKUUPOLISI”                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                   Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734                                                                                    Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556                                                                                                         S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:                                                                                    DAR ES SALAAM.



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Dar Es Salaam Agosti 06, 2013.

Ndugu Wanahabari,


Jeshi la Polisi Nchini linatoa shukrani kwa wananchi wote wakiwemo waandishi wa habari, viongozi wa dini, wanasiasa, makampuni binafsi ya ulinzi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa njia mbalimbali katika kuhakikisha kwamba nchi yetu ya Tanzania inakuwa salama na raia wote wanaishi kwa amani na utulivu bila hofu ya uhalifu na wahalifu.


Katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki na za haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo wanamoishi na sehemu mbalimbali zikiwemo maeneo ya biashara.


Ikumbukwe kuwa, wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe. Uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu. Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha kwamba, wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu, pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.

Monday, August 05, 2013

KESI YA UGAIDI TABORA YAFUTWA, MUME WA JOYCE KIRIA NA WENZAKE WABAKI NA SHITAKA MOJA...!!!

 
Katibu Wa Chadema mkoa wa kinondoni na Kanda maalum ya Dar es salaam, mjumbe wa mkutano mkuu Henry Kilewo(Kulia) na Wenzake Wanne Wameachiwa. Wamefutiwa mashitaka yote ya Ugaidi, sasa wamebakia na shitaka moja la kudhuru mwili, dhamana itatolewa na mahakama ya wilaya Igunga. Habari zaidi Baadae

WEMA SEPETU NA IRENE UWOYA WAPIMANA UWEZO, ALIANZA WEMA, UWOYA AJIBU MASHAMBULIZI


VITA mpya imeibuka ikiwahusisha warembo wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Irene Pancras Uwoya kufuatia kuanzisha vipindi vya runinga kwa mpigo.
Irene Pancras Uwoya.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, katika harakati za vipindi hivyo, alianza Wema kwa kuanzisha ‘aidia’ ya kipindi kipya kiitwacho In My Shoes ambacho kitaanza kuoneshwa kuanzia Alhamisi hii, saa tatu na nusu usiku kupitia Clouds TV.Alisema baada ya Wema kutengeneza kipindi hicho na kupata maoni mengi, Uwoya akajibu mapigo kwa kuanzisha cha kwake kinachoitwa Paradise ambacho kitakwenda hewani Jumanne hii (kesho).
“Mashabiki wa Clouds TV watapata kuona vita ya kibiashara, Uwoya atakuwa akionekana katika kipindi hicho ambacho kitakuwa kinahusu upakaji rangi katika nyumba za watu mbalimbali huku Wema naye akikimbiza katika In My Shoes,” alisema Ruge.
Na Erick Evarist

ARSENAL 1 VS 2 GALATASARAY: DROGBA AKUMBUKIA ENZI ZAKE, AWAFUMUA ARSENAL MAWILI NA KUTWAA KOMBE LA EMIRATES

On target: Drogba scored a late double to clinch the Emirates CupKama kawaida rafiki wa nyavu: Drogba alifumania nyavu mara mbili na kutwaa taji la kombe la Emirates  

Spot on: Drogba sends Wojciech Szczesny the wrong way Drogba akimpeleka sokoni kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny 

Remember me? Drogba celebrates after the final whistleMnanikumbuka? Drogba akishangilia baada ya kipenga cha mwisho cha mwamuzi

Opener: Walcott watched his cross-come-shot give Arsenal the leadUfunguzi wa karamu ya mabao: Walcott akiandika bao la kuongoza kwa klabu yake ya Arsenal

DR. SLAA AWAUNGA MKONO WAASI WA KONGO NA KUMKINGIA KIFUA KAGAME...!!!


Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli  yake ya  kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake ...

Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo.

Slaa  aliyasema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani  na hajachukua hatua dhidi ya wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi...

"Alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda  na  badala  yake amempandisha cheo,” alisema Slaa.

MTOTO MDOGO WA KIKE AUAWA KINYAMA MKOANI MBEYA...!!!


MTOTO mmoja wa kike ameuawa kinyama kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kisha kunyofolewa macho na ubongo wake.


Tukio hilo la kikatili, limetokea mwishoni mwa wiki eneo la Idiwili kata ya Isuto wilaya ya Mbeya vijijini mkoani hapa.


Mtoto huyo wa kike, asiye na hatia, mwenye umri wa miaka miwili, aliyejulikana kwa jina la Lilian Nex Kasonso, alikatishwa uhai wake kwa makusudi kisha mwili wake kutelekezwa chini ya mti.


Baadhi ya wananchi wa eneo hilo waliozungumza mwandishi wa habari hii wamesema kuwa, Mama wa mtoto huyo, alimwacha mwanae akiwa salama mikononi mwa bibi yake kisha yeye kwenda kutafuta kuni.


Punde, Bibi yake Lilian, naye alienda kuchota maji mtoni huku akimwacha mjukuu wake akiwa na furaha tele, ndipo majitu hayo makatili, kwa makusudi walimteka mtoto huyo kisha kutokomea naye pasipo mtu kuwaona ama kuwashitukia.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 5, 2013

DSC 6296 cdb25
DSC 6297 a4a94

PEPSI WAIPA YANGA KIBURI...!!!



056 8dc84
Sakata la Yanga kugomea udhamini wa Azam Tv limechukua sura mpya baada ya klabu hiyo kutaka kupewa kitita cha Sh600 milioni ili kukubali kudhaminiwa na Azam. (HM)


Habari za uhakika ambazo Mwananchi limezipata zinadai kuwa, Yanga wamepata kiburi cha kugomea udhamini wa Azam baada ya kuwa na ofa mbili mkononi ya Pepsi na ile ya Zuku.
 

“Pepsi wanatoa kinywaji chao kipya Pepsi Cola na wametupa ofa ya Sh600 milioni, Azam walifuatwa na kuelezwa juu ya ofa hiyo wakakataa Pepsi wasiingie kwa vile ni wapinzani wao kwa Azam Cola,” kilisema chanzo cha habari.

Chanzo hicho kilisema kuwa, Yanga waliwapa sharti Azam la kuongeza dau kutoka Sh100 milioni na kama isingewezekana basi waingie mkataba na Kampuni ya Pepsi.

Sunday, August 04, 2013

TAMBUA SABABU ZA WATOTO WACHANGA KULIA, HIZI NDIZO SABABU ZAKE !!!!.

Sababu za Watoto Wachanga Kulia Mara kwa Mara na Namna ya Kuwabembeleza




Kwa nini watoto wachanga wanalia .?




Ni kawaida kwa watoto kulia. Hata watoto wanaozaliwa na afya njema kabisa wanaweza kulia kwa jumla ya wastani wa kati ya saa moja mpaka matatu kwa siku. Kwa vile watoto hawawezi kujifanyia chochote wao wenyewe zaidi ya kutegemea wazazi, walezi ama watu wengine wanaowazunguka katika kuwapatia chakula, joto, na faraja, kilio ni njia ya mtoto ya kuwasilisha moja ya mahitaji hayo.





Kama mzazi mpya, wakati mwingine inakuwa vigumu kutambua mtoto wako anahitaji nini anapolia. Mzazi anaweza kuwa na maswali kadhaa kichwani mwake, je, mtoto ana njaa, anasikia baridi, ana kiu, anaumwa ama amechoka ? Katika siku za mwanzo, hali ya namna hii inawawia vigumu wazazi wengi, wasijue nini la kufanya. 

 

Hata hivyo, kwa kadiri siku zinavyopita mzazi mpya ataweza kutambua kuwa kilio cha mtoto wake kinamaanisha anahitaji nini kutokana na mfumo wake wa kulia.

SERIKALI: WALIOOANA NA WAHAMIAJI HARAMU WAVUNJE NDOA HIZO.....!!!

Mkuu wa mkoa wa Geita, Said Magalula

******
Serikali mkoani Geita imetoa siku saba kwa wananchi wenye ndoa na wahamiaji haramu kuvunja ndoa hizo mara moja na kurejea makwao kwa hiari.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa mkoa wa Geita, Said Magalula, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya ulinzi na usalama wa mkoa huo.

Agizo hilo limekuja siku chache, tangu Rais Jakaya Kikwete kutoa siku 14 kwa wahamiaji wote haramu kutokana nje ya nchi kuondoka kwa hiari yao kabla ya kuwasaka na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

JK AKUTANA NA BINGWA WA DUNIA WA KURUKA KAMBA HAMISI MOHAMED NA WENZAKE


Rais Jakaya  Kikwete akimpongeza kijana wa Kitanzania Hamisi Mohamed mwenye umri wa miaka 14 aliyeipatia sifa Tanzania kwa  kunyakua ubingwa wa Dunia wa mchezo wa kuruka kamba kwenye michuano iliyofanyika huko Orlando, Marekani, mwezi uliopita. Kijana huyo, ambaye  awali alilelewa katika kituo cha watoto yatima cha Dogo Dogo  Dar es Salaam, alianza kupata mafunzo ya mchezo huo ambapo alishiriki mashindano ya Afrika Mashiriki yaliyofanyika Mombasa na kunyakua Medali ya Dhahabu. Kulia ni mfadhili wa kijana huyo, Amy Canady, na kushoto kwa Rais Kikwete ni Sister Jean Pruitt, mwanzilishi wa kituo cha kule yatima cha Dogodogo Centre
 Rais Kikwete akiwa na bingwa wa dunia Hamisi Mohamed pamoja na wachezaji wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya dunia

RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BILL CLINTON ATUA BONGO KIAINA.....!!!

055 2b82a
Rais Jakaya Kikwete akimpokea mgeni wake Rais mtaafu wa Marekeni Bill Clinton anayepanda gari (HM)


Rais wa Mstaafu wa Marekani, Bill Clinton jana alifanya ziara katika makazi ya watu duni eneo la Vingunguti, wilayani Ilala Dar es Salaam, ambapo alikagua miradi midogomidogo ya wananchi inayofadhiliwa na mfuko wake (Bill Clinton Foundation).

Clinton alitembelea eneo hilo akitokea moja kwa moja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam (JNIA), alipowasili akiwa katika ziara ya nchi mbalimbali za Afrika kukagua miradi inayoendeshwa na mfuko wake.

Katika eneo hilo rais huyo mstaafu alipokewa kwa shamrashamra mbalimbali ikiwamo ngoma za kiasili huku baadhi ya wananchi wakipigwa butwaa na kutoamini macho yao kwa kiongozi huyo kutembelea makazi yao.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI AGOSTI 4, 2013


DSC 6293 e4361
DSC 6294 115fb
DSC 6295 01075

AUA MKE WAKIBISHANA KIPI KITANGULIE KUPIKWA KATI YA MAINI NA NYAMA ....!!!

 Photo: Aua mke wakibishana nini kianze kupikwa maini au nyama

Mkazi wa kijiji cha Minyughe, wilayani Ikungi, Bonphace Misanga (70) anashikiliwa na polisi mkoani Singida, kwa tuhuma za kumpiga mkewe Amina Kunyonga (67) hadi kufariki dunia baada ya kuzuka mabishano ya nini kianze kupikwa kati ya nyama na maini.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea Jumanne wiki hii.

Alisema siku hiyo wanandoa hao walikwenda kwenye mnada kijijini hapo na baada ya kunywa kiasi kingi cha pombe ya kienyeji walikubaliana wanunue nusu kilo ya maini na nusu ingine ya nyama mchanganyiko ya ng'ombe, huku wakiwa tayari wamekwisha lewa.

Kamanda Kamwela alisema baada ya kufika nyumbani mume alimwagiza mkewe aanze kupika nyama ya maini lakini mkewe akadai anataka aanze na nyama mchanganyiko.

"Baada ya kufika nyumbani, baba mwenye nyumba alimtaka mke aanze kupika maini halafu baadaye amalizie na nyama ya ng'ombe mchanganyiko, lakini badala yake mkewe alikataa akamwambia mtuhumiwa kuwa ataanza kwanza kupika nyama ya ng'ombe kwa madai kuwa huchukua muda mrefu kuiva,"alifafanua Kamwela.

Alisema baada ya mvutano huo uliochukua muda mrefu, ndipo mtuhumiwa alianza kumpiga mateke na ngumi mkewe sehemu mbalimbali za mwili akidai hataki kufuata maagizo yake.
Kamanda Kamwela alisema kutokana na kipigo hicho, mkewe alianguka chini hali iliyomuogopesha mumewe na kutoka nje kuwaita majirani ambao walipofika walimkuta Amina akiwa amefariki dunia.

Alisema taarifa ya daktari inaonyesha kifo cha marehemu kimechangiwa na kipigo kilichosababisha bandama kupasuka na kuvuja damu pia kunyongwa shingo na kwamba baada ya upelelezi mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya mauaji hayo.
Mkazi wa kijiji cha Minyughe, wilayani Ikungi, Bonphace Misanga (70) anashikiliwa na polisi mkoani Singida, kwa tuhuma za kumpiga mkewe Amina Kunyonga (67) hadi kufariki dunia baada ya
kuzuka mabishano ya nini kianze kupikwa kati ya nyama na maini.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea Jumanne wiki hii.

Alisema siku hiyo wanandoa hao walikwenda kwenye mnada kijijini hapo na baada ya kunywa kiasi kingi cha pombe ya kienyeji walikubaliana wanunue nusu kilo ya maini na nusu ingine ya nyama mchanganyiko ya ng'ombe, huku wakiwa tayari wamekwisha lewa.

TANESCO WAANZA KUTUMIA TRANSFORMA ZISIZOTUMIA MAFUTA KUDHIBITI WIZI

Photo: Tanesco waanza kutumia transforma zisizotumia mafuta kudhibiti wizi

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limelazimika kufunga transfoma zisizotumia mafuta kutokana na tatizo kubwa la wizi wa mafuta ya transfoma kwa maeneo mengi nchini.

Meneja mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud amesema, shirika hilo limelazimika kufunga transfoma zijulikanazo kama ‘Dry type Transfoma’ambazo hazitumii mafuta ili kupambana na changamoto za wizi wa mafuta unasababisha baadhi ya maeneo kukosa umeme.

“Tatizo la wizi wa mafuta ya Transfoma ni kubwa, limesababisha shirika kununua transfoma zisizotumia mafuta ambazo zinapatikana kwa gharama kubwa ukilinganisha na transfoma zitumiazo mafuta ili kuepusha kutokukatika kwa umeme kwa maeneo husika,” alisema Badra

Aliyataja baadhi ya maeneo ambayo yamefungwa transfoma zisizotumia mafuta kutokana na kukithiri kwa tatizo la wizi huo kuwa ni pamoja na Mbezi Beach na maeneo mengi katika Wilaya ya Temeke.

Aliongeza, Tanesco kupitia walinzi wake wanaozungukia maeneo ya transfoma, wamekamata baadhi ya watu na kuwafikisha katika mikono ya sheria ambapo wengi wao wamefungwa, pia wameomba msaada toka ulinzi shirikishi ili kuzidi kuwakamata vishoka hao ambao wanasababisha wananchi kukosa umeme na shirika kukosa mapato.

Pia alionya wezi wa nyaya za umeme hususan za copper, pamoja na wapandaji miti chini ya nguzo kama moja ya watu wanaodidimiza shirika kwa kusababisha hasara za kila siku zinazoweza kuepukika.

Badra alisema, “ili shirika liendelee ni lazima jamii itupe ushirikiano kwa kulinda miundombinu ya Tanesco, pia iwataje wahusika wanaoharibu pamoja na kuiba’’.
Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limelazimika kufunga transfoma zisizotumia mafuta kutokana na tatizo kubwa la wizi wa mafuta ya transfoma kwa maeneo men
gi nchini.

Meneja mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud amesema, shirika hilo limelazimika kufunga transfoma zijulikanazo kama ‘Dry type Transfoma’ambazo hazitumii mafuta ili kupambana na changamoto za wizi wa mafuta unasababisha baadhi ya maeneo kukosa umeme.


“Tatizo la wizi wa mafuta ya Transfoma ni kubwa, limesababisha shirika kununua transfoma zisizotumia mafuta ambazo zinapatikana kwa gharama kubwa ukilinganisha na transfoma zitumiazo mafuta ili kuepusha kutokukatika kwa umeme kwa maeneo husika,” alisema Badra

Aliyataja baadhi ya maeneo ambayo yamefungwa transfoma zisizotumia mafuta kutokana na kukithiri kwa tatizo la wizi huo kuwa ni pamoja na Mbezi Beach na maeneo mengi katika Wilaya ya Temeke.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...