Monday, July 15, 2013
CHADEMA YAIBUKA KIDEDEA KATIKA MATOKEO YA UDIWANI KWA KUZOA KATA NNE, JIJINI ARUSHA
HOFU YAKIMBIZA
WAPIGA KURA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeibuka na ushindi mnono katika uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata nne za jijini Arusha.
Katika Kata ya Elerai, mgombea wa CHADEMA
Injinia Jeremia Mpinga alimbwaga Emanueli Laizer wa CCM kwa kura 1,715, dhidi ya
1,239.
Kata hiyo ilikuwa na wapiga kura 23,797
waliojiandikisha na vituo 55 vya kupigia kura, lakini idadi kubwa ya wananchi
hawakujitokeza.
Matokeo ya kura yalitangazwa chini ya ulinzi
mkali wa askari polisi zaidi ya 40 wenye silaha, na kupokelewa kwa shangwe kubwa
na wafuasi na mashabiki wa CHADEMA.
Katika Kata ya Kaloleni, mgombea wa CHADEMA,
Kessy Emmanuel Miliare alimshinda kwa mbali mgombea wa CCM kwa kura 1,470 dhidi
ya 530, wakati mgombea wa CUF ameambulia kura 275. waliojiandikisha 12,674
waliopiga kura 2,292. Kura halali ni 2,277 na zilizoharibika 15.
Akitangaza matokeo katika Kata ya Themi,
Msimamizi wa Uchaguzi, Editha Mboye alimtangaza mgombea udiwani wa CHADEMA,
Mallance Kinabo kuwa mshindi kwa kupata kura 678, akimwacha mbali mgombea wa CCM
Victor Mkolwe aliyepata kura 326, huku yule wa CUF, Lebora Ndervai akipata kura
313.
Kata ya Kimandolu, CHADEMA pia wameibuka na
ushindi mkubwa na kuiacha vibaya CCM.
Mgombea wa CHADEMA, Elishadai Ngowi amemshinda
mgombea wa CCM, Edina Sauli kwa kura 2,265, dhidi ya 1,169 za mpinzani
wake.
TAMKO LA RAIS NA AMIRI JESHI MKUU KUHUSU TUKIO LA KUUAWA KWA WANAJESHI 7 DARFUR|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa sana na tukio la kushambuliwa na kuuawa kwa
vijana saba hodari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania waliokuwa wanalinda amani
katika eneo la Darfur, Sudan.
Kwa hakika, Rais amesikitishwa sana
na kitendo hicho ambako wanajeshi wengine 14 wa Tanzania wamejeruhiwa na waasi
wa Sudan na ametuma salamu za rambirambi za moyoni mwake kwa Jeshi la Wananchi
wa Tanzania na kwa familia za wafiwa wote.
Aidha, Rais Kikwete anaungana na
Watanzania wote na hasa maofisa na wapiganaji wa JWTZ na familia za wafiwa
kuomboleza vifo vya vijana hao hodari wa Tanzania. Rais pia anaungana na
Watanzania wote kuwaombea wale walioumia katika tukio hilo waweze kupona haraka
na kuendelea na majukumu yao ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.
Katika salamu zake za rambirambi kwa
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis
Adolf Mwamunynge na familia za
wafiwa, Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu amesema:
“Sina maneno ya kutosha ya kuelezea
mshtuko, huzuni na masikitiko yangu makubwa kufuatia vifo vya vijana wetu hao
ambao wamepoteza maisha yao katika shughuli muhimu sana ya utekelezaji wa
majukumu ya Umoja wa Mataifa ya kulinda na kuleta amani katika eneo la dunia
ambako maelfu kwa maelfu ya watu wamepoteza maisha yao kwa kushambuliwa na
waassi.”
Rais Kikwete ameongeza kumwambia
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na familia za wafiwa ”Napenda kwa niaba ya Watanzania
wenzangu niwahakikishieni kwamba hakuna shaka kuwa vijana wetu hao tokea
walipokwenda Darfur Februari mwaka huu, na kwa hakika tokea Tanzania
ilipoanza kuchangia walinzi katika eneo hilo mwaka 2007, wamefanya kazi nzuri
sana, kazi iliyoongozwa na weledi wa hali ya juu na kazi ambayo imeiletea nchi
yetu heshima kubwa. Tutaendelea kuwaenzi kwa kujivunia kazi yao.”
Amesisitiza Mheshimiwa Rais Kikwete:
“Nakutumia wewe Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi salamu za rambirambi za dhati ya moyo
wangu kuomboleza vijana wetu hawa. Kupitia kwao, natuma salamu za rambirambi
kwa maofisa wakuu na maofisa wadogo pamoja na wapigaji wote wa Jeshi letu kwa
kupotelewa na wenzao. “
“Aidha, kupitia kwako, nawatuma
salamu zangu kwa wanafamilia za waliopotelewa na wapenzi wao na ndugu zao
katika tukio hilo. Wajulishe kuwa naungana nao katika kuomboleza. Wajue kuwa
uchungu wao ni uchungu wangu pia na wa Watanzania wote na kuwa kwa pamoja
tunamwomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki
kigumu. Vile vile kwa pamoja tunamwomba Mwenyezi Mungu azilaze peponi roho za
marehemu. Amina.’
Kwa walioumia, Rais Kikwete
amemwambia Jenerali Mwamunyange: “Naungana pia na Watanzania wenzangu katika
kuwapa pole nyingi walioumia katika tukio hilo tukiwaombea kwa Mwenyezi Mungu
wapone haraka na kuendelea na shughuli zao za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa
Mataifa.”
Vijana hao waliopoteza maisha yao na
walioumia, walikuwa sehemu ya askari 37 na ofisa mmoja ambao walikuwa
wanasindikiza msafara wa waangalizi wa kijeshi katika Darfur kutoka eneo la
Khorabeche kwenda Nyara waliposhambuliwa na waasi kiasi cha kilomita 20 kutoka
Khorabeche saa tatu asubuhi jana, Jumamosi, Julai 13, 2013.
MH MBATIA AITOLEA UVIVU RED BRIGADE YA CHADEMA
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR- Mageuzi James Mbatia, amekikosoa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kitendo cha kutangaza
kujihami kwa kuboresha kikosi chao cha ulinzi na usalama cha Red
Brigade, kwamba kufanya hivyo ni kushindana na serikali.
Wakati Mbatia akisema hayo siku chache zilizopita Rais Jakaya Kikwete alitoa kauli yenye mwelekeo wa kukiponda chama hicho juu ya mpango wake huo akisema kuwa mpenda amani haundi kikosi cha mgambo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, katika kikao cha Halmashauri Kuu
(NEC) ya chama hicho, Mbatia alisema ushindani wa kisiasa unatokana na
hoja za msingi na si kushindana kwa vitendo.
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR- Mageuzi James Mbatia, amekikosoa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kitendo cha kutangaza
kujihami kwa kuboresha kikosi chao cha ulinzi na usalama cha Red
Brigade, kwamba kufanya hivyo ni kushindana na serikali.
Wakati Mbatia akisema hayo siku chache zilizopita Rais Jakaya Kikwete alitoa kauli yenye mwelekeo wa kukiponda chama hicho juu ya mpango wake huo akisema kuwa mpenda amani haundi kikosi cha mgambo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, katika kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, Mbatia alisema ushindani wa kisiasa unatokana na hoja za msingi na si kushindana kwa vitendo.
Wakati Mbatia akisema hayo siku chache zilizopita Rais Jakaya Kikwete alitoa kauli yenye mwelekeo wa kukiponda chama hicho juu ya mpango wake huo akisema kuwa mpenda amani haundi kikosi cha mgambo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, katika kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, Mbatia alisema ushindani wa kisiasa unatokana na hoja za msingi na si kushindana kwa vitendo.
Sunday, July 14, 2013
BUS LA KAMPUNI YA NAJMA LIMEPATA AJALI RUFIJI...!!!
Bus la kampuni ya Najma linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Nachingwea, limepata ajali kwenye daraja la Mkapa, Ikwiriri baada ya kugonga pikipiki na kusababisha vifo vya watu wawili papohapo.
Chanzo
cha ajali hiyo ni moshi mkali uliotanda kwenye eneo la ajali kutokana
na moto uliokuwa unaunguza majani yaliyopo pembezoni mwa barabara ya
kusini mara baada ya kumaliza daraja la Mkapa. Basi hilo lilikuwa
linatokea Nachingwea kwenda Dar es Salaam.
Watu
waliofariki ni wale waliokuwa kwenye pikipiki. Ajali hiyo imetokea
majira ya saa 6:40 mchana. Hata hivyo gari hilo halikupinduka isipokuwa
imeharibika vibaya sehemu ya mbele.
Baada ya ajali hiyo, dereva alisogeza gari kwenye kituo cha polisi cha Ikwiriri na baada ya kutoa maelezo, polisi wameenda eneo la tukio kuchukua maiti.
Baada ya ajali hiyo, dereva alisogeza gari kwenye kituo cha polisi cha Ikwiriri na baada ya kutoa maelezo, polisi wameenda eneo la tukio kuchukua maiti.
Mtoa habari hii ni miongoni mwa watu waliokuwa abiria kwenye basi hilo. Namba ya gari ni T 599 CBL aina ya YUTONG.
HABARI KUTOKA ARUSHA SHEIKH MKUU AMWAGIWA TINDIKALI NYUMBANI KWAKE...!!!
Said Juma Makamba akiwa hospitalini baada ya shambulio hilo juzi. |
Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma
Makamba amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa tindikali na
watu wasiojulikana juzi usiku akiwa nyumbani kwake jijini
Arusha.
Shekhe Makamba, ambaye amelazwa katika Wodi ya Majeruhi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, amejeruhiwa vibaya maeneo ya usoni, kifuani na mgongoni huku akiendelea na matibabu.
Akizungumza kwa tabu, shekhe huyo alisema tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake kwa Mromboo Arusha, wakati akijiandaa kulala baada ya kutoka kuswali Swala ya Tarawei.
MBOWE AVAMIWA USIKU WA MANANE!! ..... !!!
Askari hao wanaokisiwa kufikia saba, wakiwa na silaha nzito katika gari la wazi waliwasili nyumbani kwa Mbowe majira ya saa saba na nusu usiku na kuwaamuru askari wanaolinda nyumbani kwake kumtoa Mbowe nje ili waonane naye.
Walinzi wa Mbowe walihoji uhalali wa ukamataji huo na kuwataka polisi wawaoneshe hati ya kumkamata, lakini hawakuweza kuionesha, hali iliyozusha wasiwasi kwa walinzi wa kiongozi huyo.
Hata hivyo walinzi hao waliwaambia polisi hao kuwa Mbowe ambaye pia ni kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni alikuwa safarini, jibu ambalo lilipokewa kwa shingo upande na askari hao.
Polisi hao baada ya kuona wameshindwa kukamilisha kazi hiyo, waliwaachia walinzi hao namba ya simu 0754-085600 ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Ernest Kimola, wakiwaagiza kuhakikisha wanamwambia Mbowe awasiliane na kamanda huyo.
RCO amsukumia RPC, akana
Hata hivyo, alipohojiwa na Tanzania Daima Jumapili kwa njia ya simu, Mkuu wa Upelelezi Kimola aligoma kuzunguzia suala hilo na kumtaka mwandishi kuwasiliana na mkuu wake wa kazi, ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamilius Wambura, akidai ndiye mwenye haki ya kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.
“Unajua mimi si msemaji wa polisi, wasiliana na kamanda wa mkoa, maana ndiye mwenye uwezo wa kutoa maelezo,” alisema Kimola na kukata simu. Lakini alipopigiwa simu Kamanda Wambura aliruka kimanga, kwa mshangao, akidai kutojua lolote kuhusiana na polisi kuvamia nyumbani kwa Mbowe.
Saturday, July 13, 2013
MSHIRIKI WA TANZANIA (NANDO) AAMBUKIZWA GONJWA LA ZINAA NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER...!!!
In a hushed conversation between Nando and Bimp, Nando narrated how he got infected with an STD after his liason with Selly!
For the past days we have been seeing Nando and Selly who were once an
item getting distant and avoiding each other but not knowing what
happened between them. Thank God that nothing can be kept secret forever
and so we had to know the cause why the two fell out.
Nando disclosed that Selly gave him chlamydia a Sexually Transmitted
Disease, but we can’t tell how true this is. However, if we are to go by
the Tanzanian’s revelations, it explains why the two are no longer
getting along well as it was the case at the beginning.
MWANGALIE RAY C, AZIDI KUPENDEZA MUNGU MKUBWA...!!!
Mwanamuziki
staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye amepotea katika
anga la muziki kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo ya matumizi ya
madawa ya kulevya, amejitokeza akiwa amefutuka. Hivi karibuni, Ray C
ameibuka na kuanza kutundika picha na vipande vya video zake katika
kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni sehemu ya kujiweka
karibu na mashabiki wake.
Kufuatia
ishu hiyo, kumeibuka mshtuko mkubwa kwa baadhi ya watu kutokana na
picha hizo kumuonesha ‘bidada’ akiwa amenenepeana ghafla tofauti na
alivyozoeleka.
UNENE UNATOKANA NA DOZI?
Baadhi ya mashabiki wake katika mtandao wa Instagram walidai kuwa inawezekana unene huo unatokana na dozi ya kuacha ‘unga’.
Hata
hivyo, wengine walimshukuru Mungu kwa kuwa sasa afya ya mwanadada huyo
inaonekana kurudi katika hali yake ya kawaida tofauti na miezi kadhaa
aliporipotiwa na gazeti hili akiwa amezimika kutokana na matumizi ya
unga.
HUYU NDIYE KIJANA ALIYETOKA MBEYA HADI DSM KWA MIGUU...!!!
Kijana Wiseman Luvanda(23) akikamilisha safari yake ya kutoka Mbeya hadi Dar es salaam kwa miguu.
Kauli mbiu yake "Tanzania nchi yangu,Taifa Stars Timu yangu, Amka wakati wa Uzalendo ni Sasa". Tumefanya nini kuienzi nchi
WATIWA MBARONI KWA KUSAMBAZA UJUMBE WA CHUKI KWAMBA RAIS KIKWETE KAMUUZIA NCHI OBAMA
Jeshi la polisi Geita linawashikilia watu wawili kwa kosa la kusambaza ujumbe kwa njia ya simu usemao, UMEPOKEA SHILINGI 50,000.KUTOKA KWA RAIS KIKWETE KAMA SEHEMU YA MGAO WAKO BAADA YA KIKWETE KUMUUZIA OBAMA NCHI!!
Kamanda
wa polisi mkoani hapo alisema kwamba watu hao walikamatwa baada ya
kukutwa msg hizo ktk simu zao za mikononi huku wakiwa wanasambaza kwa
watu wengine.
Aliendelea
kudai kua jeshi la polisi linatoa onyo kwa wale wote wanaowachafua
viongozi wa kitaifa kwa njia za ujumbe kwa simu na kwamba watawachukulia
hatua kali.
Source; Radio Free Afrika Matukio!
MCHUMBA WA NAY WA MITEGO APOTEZA KICHANGA CHAKE BAADA YA KUANGUKA...!!!
Rapper Nay wa Mitego leo anasherehekea siku ya kuzaliwa ya mchumba wake
aliyekuwa mjamzito kwa huzuni kubwa baada ya mchumba wake huyo
kukipoteza kichanga chao kufuatia kuanguka jana usiku.
“Jana usiku mke wangu alianguka,
alifikia tumbo kwahiyo akawa anasikia kizunguzungu nilipompeleka
hospitali daktari akasema mtoto amekufa,” alisema.
Awali, Nay wa Mitego ameweka picha ya mchumba wake kwenye Instagram akiwa hospitali na kuandika:
Happy bday my lv, Mungu akupe maisha marefu na yenye mafanikio tele.
Japo imekukuta uko vibaya tumempoteza kijacho bt ni mipango ya mungu,
nakupenda sana mke..!! happy bday 2u ma.”
Subscribe to:
Posts (Atom)