Sunday, July 07, 2013

TBS YAPIGA MARUFUKU UUZWAJI WA MAFUTA YA KUPIKIA YA 'OKI'.....WADAI YANA MADHARA KIAFYA.

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/OKI.jpg 
Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limebaini kuwa mafuta ya kula aina ya Oki na Viking yaliyoenea sokoni nchini, yamebainika kuwa hayafai kwa matumizi ya binadamu.
Kwa mujibu wa TBS, vipimo vyote vitatu vilivyotumika kuyapima kuonyesha ubora, vimefeli na vimeonyesha mafuta hayo kuharibika kwa haraka tangu yalipotengenezwa na mpaka leo.
Pamoja na Oki, mafuta mengine yenye walakini ni Asma, Vikingi, Partiner na Premier Gold ambayo huuzwa kwa dumu lenye ujazo wa lita 20 kwa bei ya kuanzia Sh 38,000 hadi 45,000, wakati bei ya mafuta ya kula yanayotengenezwa nchini kwa ujazo huo huuzwa kati ya Sh. 52,000 na Sh.55,000.

Baada ya kupimwa, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Ubora TBS, Lazaro Msasalaga, anasema ilithibitika kuwa mafuta ya Oki yanayozalishwa Malaysia na kupakiwa Singapore hayana ubora.
Alisema mafuta hayo yametengenezwa 2011 na kuonyesha mwisho wa kutumika ni Oktoba mwaka huu. Msasalaga alisema walipoyachunguza wamebaini hayana namba ya ufuatiliaji wakati suala hilo ni la muhimu kuwekwa.
Isitoshe, wawalipoyapima kutoka kipimo kimoja kwenda kingine, majibu yake yalishindwa na kuzidi kuonyesha mafuta hayo kuharibika kila walipoyapima.
Alisema kuna vipimo vya maabara ukipima vinaeleza mafuta kama yanafaa kutumika lakini kipimo hicho hakikufanikiwa.NA TALK BONGO

LUCY KOMBA NA IRENE UWOYA NDANI YA BIFU ZITO, KISA NDIKUMANA...!!!

 
MWANAFUNZI na mwalimu wake katika sanaa, Irene Uwoya na Lucy Komba wameingia katika bifu zito chanzo kikidaiwa kuwa ni mwalimu huyo kumzunguka mwanafunzi wake kwa mumewe, Hamad Ndikumana ‘Katauti’. Lucy ambaye ndiye mwalimu wa Uwoya kisanaa, imedaiwa kuwa amemzunguka Uwoya kwa mumewe, Ndiku kwa kisingizio cha kucheza naye filamu iliyofahamika kwa jina la Kwa nini Nisimuoe?
 
“Kimenuka! Lucy Komba amemhadaa Ndiku, akazuga kuigiza naye filamu moja ndipo walipozama kwenye ukaribu kwelikweli.
“Mbaya zaidi filamu yenyewe wameigiza wahusika wawili tu (Lucy na Ndiku) mwanzo mwisho kule Tegeta. Sasa wewe unafikiri kuna nini hapo kama siyo mapenzi?’’ kilihoji chanzo hicho makini.
Baada ya paparazi wetu kuyanasa madai hayo, Jumatano iliyopita alimtafuta Uwoya kwa njia ya simu ambapo alipopewa taarifa hizo, alionesha kushtuka na kuchanganyikiwa mumewe kuigiza filamu moja na Lucy, alikata simu kisha baadaye akampigia paparazi yeye.
“Kuna wakati nilikuwa namtafuta Ndiku sijui alipo kumbe alikuwa na Lucy, sawa lakini kama Lucy ameamua kunifundisha mimi na sasa amemfundisha mume wangu sawa, tupo hapa!”
Paparazi wetu alihamishia majeshi kwa kumtwangia ‘mtuhumiwa’, Lucy ambaye alitiririka kama ifuatavyo:
 
“Nilijua Uwoya akisikia itakuwa ni balaa maana siku za nyuma niliwahi kumshutumu kutoka na mzazi mwenzangu (Patrick Mbasha) lakini mimi nipo tayari kwa lolote!”
Lucy Komba ndiye aliyemuingiza Uwoya kwenye sanaa baada ya kumchezesha Filamu ya Yolanda ambayo ndiyo iliyomtambulisha vyema staa huyo kisha kuliteka soko la sinema Bongo.

SERIKALI YA AFRIKA YA KUSINI YAKANA MZEE NELSON MANDELA KUWA HANA FAHAMU

Former South Africa's President Nelson Mandela is pictured during an interview with the media at is house in Qunu, South Africa,18 July 2008. Mandela, the anti-apartheid icon spend his 90th birthday at home in Qunu with his family, and the whole village is celebrating EPA/THEMBA HADEBE

SERIKALI ya Afrika Kusini imekanusha taarifa kuwa rais wa zamani wa nchi hiyo, Nelson Mandela, hana fahamu zake tena kama inavyoelezwa katika nyaraka za mahakama zilizowasilishwa mnamo 26.06.2013. 

Kifungu kinachoelezea hali mbaya ya Mandela kilitumika katika nyaraka za mahakama zilizowasilishwa na jamaa wa familia ya Mandela, kwa mujibu wa wakili aliyenukuliwa na vyombo vya habari. Ofisi ya rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ilisema madaktari wanakana rais huyo wa zamani amepoteza kabisa fahamu na hali hiyo haitabadilika. 
Zuma alisema jana mchana baada ya kumtembelea hospitalini kuwa Madiba anapewa matibabu ya hali ya juu na timu ya madaktari bingwa waliobobea katika taaluma ya utabibu, ambao wako kando ya kitanda chake hospitalini kila wakati.
Nyaraka za mahakama zilizopatikana na shirika la habari la AFP zinaonyesha madaktari wanaomtibu Mandela walisema hana fahamu na kuishauri familia wiki moja iliyopita iruhusu mashine zinazomsaidia kuishi zizimwe ili apumzike.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 7, 2013

.



.
.

MFANYABIAS​HARA MWENYE ASILI YA KIARABU MBARONI KWA KUMBAKA TAHIRA


Na Cresensia Kapinga,Songea.
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linamshikiria mfanyabiashara mmoja Jamali Nassoro (67) mwenye asili ya kiarabu mkazi wa eneo la Making'inda katika manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia ujauzito wa mimba ya miezi 5 msichana mwenye umri wa miaka 27 ambaye anadaiwa kuwa na ugonjwa wa utindio wa ubongo(TAILA) ambaye jina lake tunalo limehifadhiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma George Chiposi alisema kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo mwenye asili ya kiarabu limetokea hivi karibuni baada ya wazazi wa msichana kubaini kuwa mtoto wao yupo tofauti kimaumbile na kuchukuwa jukumu la kwenda kumpima ambako vipimo vilionesha kuwa ni mjamzito wa miezi 5.

Chiposi alisema kuwa wazazi wa msichana huyo baada ya kubaini mtoto wao ni mjamzito walimuhoji ili kujuwa ni nani aliyemfanyia unyama huo ambapo licha ya kuwa msichana huyo ni tahira alieleza kwa shida kuwa alikamatwa kwa nguvu na kulazimishwa kutoa nguo yake ya ndani na Nassoro ambaye alimtaka ampelekee maji ya kuoga chumbani kwake.

Saturday, July 06, 2013

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA JOYCE KIRIA BAADA YA KUSHAULIWA AMWAMBIE MUMEWE AACHANE NA SIASA

My Hubby Henry Kilewo akiwa katika shughuli zake za kisiasa.


Nimeolewa na mwanasiasa, mume wangu Henry Kilewo ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Kinondoni, Ila mimi si mwanasiasa(nahudumia watu wote wenye vyama na wasio na vyama).

 
Our Wedding Day, Nikila kiapo, "KWA TABU NA RAHA"

Muda nakubali kuolewa naye nilifahamu fika kuwa yeye ni mwanasiasa, Ila nitamsupport mume wangu kwa kazi yake aliyoichagua, siwezi kumwambia AACHE SIASA, Hilo kwa kweli HALIWEZEKANI, Hata yeye hajawahi hata siku moja kuniingilia katika kazi yangu ya kutetea haki za wanawake na maendeleo ya wanawake kwa ujumla(WANAWAKELIVE) na kuniambia niiache.

DIAMOND ASABABISHA KIFO CHA MTOTO MWANANYAMALA...!!!


Vilio  na  simanzi  vilitanda Jumatano iliyopita Mwananyamala Kisiwani, jijini Dar kufuatia mtoto wa mwaka mmoja, Rahim Rajab kufariki dunia kwa kuangukiwa na watu watatu, akiwemo baba yake mzazi, Rajab Said..

Tukio la watu hao kumwangukia mtoto huyo lilitokea Jumatatu iliyopita na lilisababishwa na ugomvi mkubwa wa CD yenye nyimbo za mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ulioibuka ndani ya chumba cha kulala kati ya mama wa marehemu na mpangaji mwenzake aitwaye Aisha.

Akizungumza kwa machungu kuelezea tukio hilo, mama mzazi wa marehemu Rahim, Habiba Ally alikiri kuwa kisa cha kifo cha mwanaye ni CD tu.Akasema: 

" Kwa kweli hakuna kingine zaidi ya CD, naamini hivyo kwa kuwa mimi sikuwa na ugomvi wowote na Aisha. Tulikuwa tunaishi kawaida tu ukiacha mikwaruzo ya hapa na pale.”

MAGAZETI YA BONGOLEO TAREHE 6 JULAI, 2013

.
.
.

SOMALIA YALIKOSOA JESHI LA KENYA KISMAYO



Wanajeshi wa Kenya walisaidia Somalia kufurusha wapiganaji wa Al shabaab kutoka Mogadishu
Kufichuliwa kimakosa kwa barua ya siri ya kidiplomasia kumefichua mgawanyiko mkubwa kati ya serikali ya Somalia inayoungwa mkono na mataifa ya Magharibi na nchi za kiafrika pamoja na kikosi cha kulinda amani cha Kenya kinachohudumu Somalia.
Katika barua hiyo,iliyoonekana na BBC, Somalia inakishutumu kikosi cha Kenya kwa kushindwa kufanya kazi na kusababisha mapigano ya hivi karibuni kati ya makundi tofauti yaliyosababisha vifo vya watu 65.
Taarifa zinazohusiana
Kenya ina kikosi Kusini mwa Somalia karibu na mpaka wake kama sehemu ya kikosi cha Umoja wa Afrika cha kulinda amani.

Somalia imekuwa katika vita kwa miongo kadhaa sasa lakini matumaini yalikuwa kwamba kikosi cha Umoja wa Afrika wakiwemo wanajeshi wa Kenya wataleta tofauti kubwa katika nchi hiyo.

CHELSEA WAKAMILISHA USAJILI WA KIUNGO WA UHOLANZI, MARCO VAN GINKEL


kiungo, Marco van Ginkel kutoka Vitesse akiwa ameshika jezi ya chelsea



 





















Van Ginkel akisaini Mkataba na Katibu wa klabu, David Barnard huko Cobham


Klabu ya Chelsea imekamilisha usajili wa kiungo wa Uholanzi, Marco van Ginkel.Kinda huyo wa umri wa miaka 20 anatua akitokea klabu ya Ligi Kuu Uholanzi, iitwayo Eredivisie, Vitesse Arnhem kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 9 na amesaini Mkataba wa miaka mitano Stamford Bridge.
Van Ginkel ameibukia kwenye programu ya soka ya vijana ya Vitesse na alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akitokea benchi Uholanzi ikitoa sare na Ujerumani Novemba mwaka jana.


NDOA YA DIAMOND NA PENNY KUFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB ...!!!















Siyo siri kwamba wapenzi wasio na kificho, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Penny Mungilwa wana malengo ya kuja kuishi kama mke na mume lakini maajabu ni namna mwanamuziki huyo alivyopanga sherehe ya ndoa yao iwe siku ikifika.
Akizungumza nasi hivi karibuni, Diamond alisema kuwa yamekuwepo maneno ya chinichini kuwa ameshatoa mahari na siku si nyingi ataingia kwenye maisha ya ndoa ila ukweli ni kwamba kila kitu kinafanyika kwa umakini na mashabiki watajulishwa hatua kwa hatua.

“Suala la ndoa yangu nalifanya kwa umakini sana, watu wawe na subira tu ila wanachotakiwa kujua ni kwamba nina plani za kuifanya sherehe ya ndoa yangu kwenye Uwanja wa Leaders Club, pale Kinondoni na watu wataingia kwa kiingilio kisichopungua shilingi elfu kumi. Itakuwa ni ndoa ya Wasafi bana,” alisema Diamond

JINI KABULA .... "MWANAUME ASIYE NA PESA HAPASWI KUWA NA WIVU KWA MPENZI WAKE"

MSANII wa filamu za Bongo, Miriam Jolwa ‘Kabula’ ameonesha kukerwa na wanaume ambao hawana hela   lakini wamekuwa wakijifanya wanajua kupenda sana huku wakiwa na wivu kupitiliza.

Akiongea na  mwandishi wetu , Kabula alisema anajua kupenda ni suala la msingi lakini anawashangaa wale wanaokuwa na wivu wa kupindukia na wakati mwingine kutoa vipigo kwa wapenzi wao wakati wao ni wanaume  wasio na kitu.


“Unajua nawashangaa sana wanaume wa aina hiyo, wanakuwa na wivu kupitiliza lakini hawawasaidii chochote wapenzi wao kifedha  zaidi ya kuonesha wana wivu  na wakipishana kidogo tu kipigo kinatembea, mimi wananikera sana,” alisema Kabula.

MOYES ASEMA: ROONEY HAUZWI, ATAENDELEA KUWA MCHEZA WA UNITED - KUHUSU RONALDO ASHINDWA KUKATAA WALA KUKUBALI KUTAKA KUMSAJILI MOYES ASEMA: ROONEY HAUZWI, ATAENDELEA KUWA MCHEZA WA UNITED - KUHUSU RONALDO ASHINDWA KUKATAA WALA KUKUBALI KUTAKA KUMSAJILI

 
Kocha wa Manchester United David Moyes leo hii amethibitisha kwamba mshambuliaji wa klabu hiyo Wayne Rooney hayupo sokoni na ataendelea kuicheza klabu hiyo kwa mingi ijayo.

Akizungumza kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu ajiunge na klabu hiyo akichukua nafasi ya Sir Alex Ferguson, Moyes alisema: "Nimeongea na Wayne Rooney. Wayne yupo nyuma ya mabao 40 kumfikia Sir Bobby na Denis Law. Wayne hauzwi - ni mchezaji wa Manchester United - na ataendelea kubakia kuwa mchezaji wa Manchester United. Nimekuwa na mikutano nae kadhaa. Amerudi kwenye hali nzuri na anafanya vizuri mazoezini. Tunajaribu kufanya kila kitu kumrudisha Wayne Rooney kuwa kama alivyokuwa zamani - Wayne Rooney ambaye tunamjua.

"Vyovyote vilivyotokea kabla, tunafanya kazi pamoja sasa. Macho yake yanaonyesha ni mtu mwenye furaha, ni lazima niseme Wayne hauzwi. Kuliwahi kuwepo mkutano wa siri baina ya Rooney na Sir Alex. Mie naendelea mbele sasa, sijui nini kilizungumzwa kwenye mkutano huo. Ninachofikiria sasa ni kusonga mbele na kufanya kazi ya kumrudisha Wayne Rooney kwenye ubora wake. "
 
Alipoulizwa kuhusu Cristiano Ronaldo, Moyes alijibu: "Sitomzungumzia yeye moja kwa moja na wachezaji wengine wa vilabu vingine. Lakini hii klabu siku zote imekuwa ikivutiwa na wachezaji bora duniani."
Pia Moyes alithibitisha kwamba winga mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutoka Crystal Palace - Wilfred Zaha ambaye amekuwa akiwindwa na vilabu vingi kujiunga navyo kwa mkopo - Moyes amesema mchezaji huyo ataungana na Manchester United kwenye tour ya pre-season, kama ilivyo kwa wachezaji wengine. 
Wakati huo huo alipoulizwa kuhusu usajili wa wachezaji wapya, Moyes amesema angependa kusajili wachezaji mapema lakini mambo yamekuwa yakichelewa kutokana na makocha ambao ndio wanaothibitisha uuzwaji wa wachezaji wengi wamekuwa likizo au ndio wanaingia kwenye vilabu vyao vipya.

Chanzo: Shaffih Dauda Blog

Friday, July 05, 2013

MAHAKAMA YAELEKEZA MAZISHI YA MANDELA, YAAMURU MIILI YA WANAWE IFUKULIWE IKAZIKWE ATAKAPOZIKWA




Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela


HATIMAYE vita iliyokuwa ikipiganwa ndani ya familia ya Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, kuhusu mahali panapostahili kuwa eneo la kuzikia miili ya wanafamilia hiyo imefikia mwisho, baada ya Mahakama Kuu ya Mthatha iliyoko Jimbo la Eastern Cape, kutoa hukumu inayoelekeza yawe katika makazi ya Mandela yaliyoko kijijini Qunu.



Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Jaji Lusindiso Pakade wa Mahakama Kuu ya Eastern Cape, aliyekuwa akisikiliza shauri lililofunguliwa mahakamani hapo na mtoto mkubwa wa kike wa Mandela, Makaziwe, aliyekuwa akipinga hatua ya Mandla ambaye alichukua uamuzi wa kufukua miili ya watoto watatu wa Mandela akiwamo baba yake mzazi, kutoka katika makaburi ya familia yaliyoko Qunu na kwenda kuizika katika makazi yake ya kichifu yaliyoko Mzove.



Jaji Pakade katika hukumu yake ya juzi, alikiita kitendo cha Mandla kufukua miili hiyo kutoka kaburini na kwenda kuizika upya bila ridhaa ya wanafamilia, kuwa hakikubaliki hivyo miili hiyo ifukuliwe na kurudishwa ilipozikwa awali.

UHUSUIANO WA IRAN NA ZIMBABWE WAPONGEZWA

 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ali Akbar Salehi amekutana na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe mjini Harare ambapo wamefanya mazungumzo kuhusu njia za kustawisha uhusiano wa pande mbili. Katika mkutano huo, Salehi amemkabidhi Mugabe salamu za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran na rais-mteule Hassan Rohani. Kwa upande wake Rais Mugabe ameashiria safari zake nchini Iran na kusema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia aliwahi kutembelea Zimbabwe wakati akiwa rais. Mapema Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alikutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Zimbabwe Simbarashe Mumbengegwi ampabo wawili hao wamepongeza uhusiano baina ya nchi zao.
  Katika mkutano huo Salehi alisema Iran na Zimbabwe ziko katika mashinikizo na vikwazo haramu na hivyo nchi hizi mbili zinapaswa kuwa na ubunifu katika kukabiliana na mzingoro wa maadui. Naye Mumbengegwi alisema Iran, kama mwenyekiti wa mzunguko wa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM imeinua itibari ya harakati hiyo. Aidha amepongeza misimamo imara ya Iran na Zimbabwe pamoja na kuwepo mashinikizo ya kila aina dhidi yao.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...