Wednesday, July 03, 2013
SIFA ZA GARI YA OBAMA INAWEZA KWENDA 97KM TU KWA SAA AT MAXIMUM ..... YA JK IPO JUU KWA SPEED
Walioona msafara wa obama wataona namna msafara ulipita kwa speed ya kawaida sana tofauti na ile speed tuliyozoea anapopita JK, our president normally huwa ana cruise at an average of 120kmh.
Ile speed ikanifanya nitafute habari zaidi, niliyoyaona yamenishangaza, kumbeMaximum speed ya limo ya obama ni 60mph tu, sawasawa na kilimita kama 97 kwa saa. hii gari haina ujanja wa kwenda hata 100km kwa saa, hata boda boda inaweza kwenda speed kuliko hii gari
- ina uzito unaokadiria kukaribia tani 9
- matumizi ya mafuta ni 8mpg, kwa
lugha ingine inahitahi lita 35.31 ili kutembea kilomita 100, hii ni sawa
na lita 1 kwa kila kilomita 2.8
- vioo vyote havifunguki isipokua pale kwa dereva kwa mbele. gari iko 100% sealed
- Vioo vya dirishani vina thickness ya inchi 5 wakati milango ni nchi 8.
- kutokana na unene wa madirisha
na milango, obama hawezi kusikia chochote kinachoendelea nnje, spika
zimewekwa ili kunasa sauti za nje
- gari ina night vision kamera zinazomuwezesha dereva kuendesha usiku bila hata kuwasha taa
OBAMA AAHIDI KUJA TENA NA KUPITA MITAANI ILI WATU WAMUONE...!!!
Kana kwamba
alisikia kilio cha wakazi wa Dar es Salaam waliokuwa na shauku ya
kumwona lakini ikashindikana, Rais Barack Obama wa Marekani amewaomba
radhi kwa hali hiyo.
Akizungumza
juzi wakati wa dhifa iliyoandaliwa kwa ajili yake na ujumbe wake na
Rais Jakaya Kikwete katika Ikulu ya Dar es Salaam, Obama alisema
akirudi nchini siku zijazo, atapita mitaani akiwa katika gari la wazi.
"Niliona
wananchi walivyojitokeza kwa wingi kutupokea barabarani, nilifarijika
sana lakini hawakuweza kutuona vizuri kwani tulikuwa ndani ya gari
maalumu-The Beast.
"Miaka ya
sitini Rais John Kennedy alipokuja hapa, alipita na gari la wazi
mitaani wananchi wakamwona, naomba radhi nikija tena nitaonekana,"
alisema Obama.
Watu wengi
waliozungumza na vyombo vya habari walionesha dhahiri kiu ya kutaka
kumwona Rais huyo wa kwanza mweusi wa Marekani, lakini wakaishia kuona
gari lake ambalo hata hivyo, lilipita kwa kasi barabarani kwenda Ikulu
na kurudi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
WATUHUMIWA WA MAUAJI YA DAUD MWANGOSI WAACHIWA HURU NA MAHAKAMA...!!!
Kiongozi huyo pamoja na wenzake walikuwa wakikabiliwa na makosa matatu likiwemo la kufanya mkutano bila kibali pamoja na kuharibu mali ambazo ni kofia za pikipiki (helmenti) 2 za polisi katika tukio lililosababisha kuuawa aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daudi Mangosi katika kijiji cha Nyololo wailayani Mufindi.
Kutokana na tuhuma hizo Chadema iliweka pingamizi za kutaka kesi hiyo ifutwe kwa kuwa ilifunguliwa kinyume cha sheria.
Wakili wa Chadema Lugaziya akisaidiana na mwanasheria wa Chadema Luka Sinkala Mwenda waliweka pingamizi kuwa aliyetoa amri ya kusitisha mkutano na kusababisha kifo cha mwandishi wa habari huyo ni kamanda wa Polisi Michael Kamuhanda ambapo aliingilia kazi ya OCD wa Mufindi kwa kuwa hakupaswa kutoa amri hiyo, kwamba wakati amri ya kusitisha mkutano ilitolewa wakati hakukukuwa na vurugu na polisi walipiga mabomu wakati watu wanatawanyika.
Pingamizi zingine ni kwamba aliyetoa amri ya kutawanya mkutano hakuwa na cheo chochote.Wakati Chadema ikizuiliwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Bububu Zanzibar walikuwa na mkutano wa kampeni za uchaguzi..
STOKE CITY YAKAMILISHA DILI YA KUMSAJILI MARC MUNIESA KUTOKA BARCELONA
Marc Muniesa, Beki wa timu ya Barcelona aliyesaini mkataba wa kuichezea Stoke City Msimu ujao
Aliyekuwa
beki wa Timu ya Barcelona ya Uhispania Marc Muniesa kijana wa Miaka 29
amekamilisha Usajili wake wa kuicheza timu yake mpya ya Stoke City ya
Uingereza.
Marc
Muniesa alikuwa ni moja wa memba wa kikosi cha Hispania chini ya Miaka
21 kilichoshinda Katika ligi ya Ubingwa wa ulaya chini ya Miaka 21.
Marc
Muniesa, alisema " anafurahi kujiunga na timu ya Stoke City na
atajitahidi kadri ya uwezo wake katika kuhakikisha timu yake hiyo mpya
ya Stoke anailetea Ushindi"
Aliongezea
kwa kusema Hakuwa na uamuzi mgumu katika kuamua kujiunga na timu hiyo
ya Uingereza ya Stoke City na nimekuja uingereza jana kwaajili ya
kukutana na watu wa klabu hii ya Stoke City na kuangalia Uwanja wa
Mazoezi na kuona unavutia
MACHANGUDOA WALALAMIKIA UJUO WA OBAMA WASEMA AFADHALI UJIO WA BUSH:
Rais Barack Obama wa Marekani
Polisi wa Kimarekani waliokuwa mwiba mkali kwa ulinzi wa Obama
Machangudoa wakiwinda wazungu maeneo ya Oysterbay Karibu na Ubalozi wa Merikani
Machangudoa wakiwa kazini
Na Livingstone Mkoi
Katika hali ilisiyokuwa ya kawaida wakina dada maarufu wanaojihusisha na biashara ya kuuza miili yao
maarufu kwa majina ya machangudoa wameulalamikia ujio wa Rais Barack
Obama kwa kile kilichodaiwa haukuwa na faida yoyote kwa kukosa dili za
pesa.
Wakiongea
Xdeejayz kwenye baadhi ya sehemu wanazopatikana wakina dada hao walisema
kuwa” Tumesikitishwa sana na ujio wa Obama kwani tulikuwa tumejipanga
kupiga hela ndefu sana lakini patutu kwani watu wake tuliokuwa
tumewategemea kuwanasa walikuwa busy na usalama pia kukaa kipindi kifupi
kumechangia sisi kukosa mapato" Walisema wakina dada hao waliokutwa
maeneo ya Coco Beack
Tuesday, July 02, 2013
ANGALIA RAIS OBAMA AKIONYESHA UWEZO WAKE WA KUPIGA DANADANA....!!!
Rais Kikwete akimwangalia Obama wakati akipiga mpira danadana.
OBAMA akionyesha uwezo wa kumiliki mpira kwa kupiga kichwa bila kutua chini wakati alipotembelea mit
ambo ya kuvua umeme Ubungo jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuondoka nchini.
Hapa akipiga danadana huku akishuhudiwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
RAIS BARACK OBAMA WA MAREKANI AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI HAPA NCHINI
Rais
Barack Obama wa Marekani ameondoka nchini mchana huu kurudi nchini
Marekani,baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini
iliyoanza jana.Rais Obama na mwenyezi wake Rais Jakaka Kikwete,leo
walifanya ziara ya kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion
iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi mradi huo.
iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi mradi huo.
MAREKANI KUFUNGUA UKURASA MPYA KATIKA UWEKEZAJI NCHINI.
Rais
wa Marekani Barack Obama akiwahutubia wafanyabiashara leo(jana) jijini
Dar es salaam juu ya mpango wa Nchi yake wa kufungua milango ya
ushirikiano na uwekezaji kwa Nchi za Afrika Mashariki katika sekta
mbalimbali na hivyo kuongeza kiwango cha bidhaa ya Afrika Mashariki
zinazoingia nchini Marekani.
Rais
wa Marekani Barack Obama akiwa katika mkutano jana (leo) jijini Dar es
salaam wa kujadiliana na watendaji wakuu(CEO) wa Makampuni mbalimbali
yaliyowekeza Afrika juu ya kuimarisha fursa za ushirikiano kati ya
Marekani na Afrika katika uwekezaji kwenye sekta mbalimbali za
maendeleo.
(Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaa)
………………………………………………
Na Eleuteri Mangi—MAELEZO—Dar es salaam
Serikali
ya Marekani imeahidi kufungua ukurasa mpya kwa Nchi za Afrika Mashariki
kwa kuongeza uwekezaji katika sekta mbalimbali ili kuinua uchumi wan
chi hizo.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Dar es salaam na Rais Barack Obama kwenye
hotuba yake kwa wafanyabiashara wakati wa ziara yake ya siku mbili
nchini Tanzania.
Alisema
kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza kiwango cha bidhaa kutoka Nchi za
afrika Mashariki kuingia nchini Marekani na hivyo kuimarisha ushirikiano
wa kibiashara na kiuchumi kwa manufaa ya pande zote.
“Sasa
ni wakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwekeza nchini Marekani ili
kuongeza mauzo yake nchini Marekani hadi ifike asilimia 40,” alisema
Rais Obama.
NANDO WA TANZANIA APENDEKEZWA KUTOKA NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER...KURA YAKO INAHITAJIKA
Mchezo unazidi kuwa mgumu kadri siku zinavyozidi kwenda sababu idadi ya wanaopaswa kuendelea na mchezo ndivyo inavyohitajika kuwa ndogo mpaka siku ya 91 atakapobaki mtu mmoja wa kukabidhiwa $300,000 kama zawadi ya BBA The Chase.
Nominations za wiki hii zimewagusa baadhi ya washiriki ambao hawajawahi kabisa kupendekezwa kutoka, na wengine ambao wameshawahi kupendekezwa mara moja na zaidi lakini waliokolewa na kura za watazamaji.
Baada ya kupona kutoka wiki iliyopita na kuwa HOH , cheo kilichompa nafasi ya kujiokoa katika nomination zilizopita Nando wa Tanzania ameungana na washiriki wengine 6 katika orodha ya majina yaliyotajwa na Biggie kuingia katika kikaango cha eviction ya wiki hii.
Washiriki ambao wameingia kwa mara ya kwanza katika nominations za wiki hii ni pamoja na aliyekuwa kipenzi cha Huddah mjengoni, Angelo wa Afrika Kusini ambaye amewekwa na HOH wa wiki hii Elikem aliyejiokoa na nafasi yake kumuwekea yeye.
Fatima wa Malawi, Bimp wa Ethiopia pamoja na Cleo wa Zambia ndio washiriki wengine ambao wameingia dangerzone kwa mara ya kwanza toka mchezo umeanza.
Washiriki ambao waliwahi kupendekezwa na kuokolewa na kura za watazamaji na wameingia tena wiki hii ni pamoja na Pokello wa Zimbabwe, Hakeem wa Zimbabwe pamoja na Nando wa Tanzania.
Wiki hii Ghana na Nigeria ndio zimekalia viti vya utawala wa nyumba, Ruby ikiongozwa na Elikem na Melvin akiiongoza Diamond.
Kura yako inahitajika kumwokoa Nando ili aendelee kubaki na kuiwakilisha Tanzania katika msimu wa 8 wa BBA The Chase unaoendelea Afrika Kusini.
MAHAKAMA YAWATIA MBARONI WAPENZI WAWILI WALIOAMUA KUTALII WAKIWA UCHI....!!!
Njemba moja, Stephen Gough aliyewahi kuwa mwanajeshi amekamatwa na polisi katika Jiji la Portsmouth, Uingereza baada ya kukutwa na mpenzi wake wakidunda kutalii mitaani wakiwa uchi wa nyama.
Mwanamke Melodine Roberts aliyefuatana naye aliachiwa na polisi kwa kuwa mara baada ya kuonywa kuacha tabia hiyo, aliacha lakini mpenzi wake huyo aligoma na hii ni mara ya 14 akifanya hivyo licha ya kufungwa jela huko nyuma.
Baada ya kugoma polisi walimfunga pingu na wakampeleka mahakamani moja kwa moja ambapo Mwendesha Mashitaka, Simon Jones alisema Gough alikuwa amekiuka sheria na aliwahi kufungwa miaka sita na moja ya makosa yaliyosababisha afungwe ni kutemba uchi wa mnyama hadharani.
Baada ya maelezo hayo, jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, Sarah Munro alisema kuwa kwenda jela kwa mtu huyo ndiyo ilikuwa njia pekee kwake kwa kuwa hilo ni kosa kubwa katika jamii ya Waingereza na ni ukiukwaji wa taratibu za umma wa sehemu hiyo.
POLISI WALA KICHAPO KIKALI KUTOKA KWA POLISI WENZAO BAADA YA KUKAIDI AMRI...!!!
MAAFISA watatu wa polisi wa utawala (AP)
walijeruhiwa kwenye mapigano yaliyozuka kati yao na wenzao wa Uganda
kwenye kisiwa kinachozozaniwa cha Migingo.
Mzozo huo wa
mwishoni mwa wiki ulianza pale maafisa wa Uganda waliokuwa na sare rasmi
walipoenda katika ufuo wa karibu wa Nyandiwa kurekebisha mashua yao.
Lakini wakazi wa
Nyandiwa waliwazuia kutia nanga wakisema kwa vile walikuwa na sare na
bunduki, walihofia wangeliwahangaisha kwa kuwapokonya samaki wao.
Mmoja wa
wavuvi wa eneo hilo Bw Oloo Okello, alisema maafisa hao wa Uganda
walirejea Migindo wakuwa na hasira bila ya kurekebisha boti lao.
“Waliporejea walisema
kwamba polisi wa Utawala wa Kenya wa kitengo cha kushika doria mpakani,
Rural Border Patrol Unit (RBPU), walio kisiwani Ugingo hawatakiwi kutia
guu Migingo.
TANZANIA YAUMBULIWA....GAZETI MAARUFU LA MAREKANI LAANIKA UKATILI UNAOTENDEKA NCHINI
Tanzania imekosolewa na gazeti maarufu la
Marekani wakati Rais Obama akipokewa kwa nderemo na
vifijo.
Gazeti hilo maarufu nchini Marekani la The New York Times, limechapisha habari za kuonesha matukio ya ukatili yanayofanyika Tanzania.
Habari hiyo iliyochapishwa katika toleo lake ya Juni 30, imeleza tukio la kuteswa na kuumiza kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka.
Mwandishi wa habari hiyo amejaribu kunukuu kauli ya Dk. Ulimboka akieleza jinsi alivyotekwa na kuteswa kinyama kisha kutupwa kwenye Msitu wa Mabwepande.
Mwandishi huyo amesema kuwa Tanzania inaheshimika nje ya nchi kama kisiwa cha amani ndani ya ukanda wenye machafuko wa Afrika Mashariki.
Kwamba kutokana na sifa hizo, Tanzania imejizolea sifa na ufadhili wa fedha kutoka kwa mataifa mbalimbali yaliyoendelea, ikiwamo Marekani, ambayo mwaka jana
iliipatia zaidi ya dola milioni 480.
Alisema kuwa wakati Rais Obama akiwasili Tanzania makundi ya kutetea haki za binadamu na chama kikuu cha upinzani wanasema matukio ya vitisho na ukandamizaji wa wapinzani wa kisiasa yanashika kasi. “Kuna woga, si amani”.
Gazeti hilo maarufu nchini Marekani la The New York Times, limechapisha habari za kuonesha matukio ya ukatili yanayofanyika Tanzania.
Habari hiyo iliyochapishwa katika toleo lake ya Juni 30, imeleza tukio la kuteswa na kuumiza kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka.
Mwandishi wa habari hiyo amejaribu kunukuu kauli ya Dk. Ulimboka akieleza jinsi alivyotekwa na kuteswa kinyama kisha kutupwa kwenye Msitu wa Mabwepande.
Mwandishi huyo amesema kuwa Tanzania inaheshimika nje ya nchi kama kisiwa cha amani ndani ya ukanda wenye machafuko wa Afrika Mashariki.
Kwamba kutokana na sifa hizo, Tanzania imejizolea sifa na ufadhili wa fedha kutoka kwa mataifa mbalimbali yaliyoendelea, ikiwamo Marekani, ambayo mwaka jana
iliipatia zaidi ya dola milioni 480.
Alisema kuwa wakati Rais Obama akiwasili Tanzania makundi ya kutetea haki za binadamu na chama kikuu cha upinzani wanasema matukio ya vitisho na ukandamizaji wa wapinzani wa kisiasa yanashika kasi. “Kuna woga, si amani”.
Subscribe to:
Posts (Atom)