Tuesday, July 02, 2013
JINSI CIA NA FBI WALIVYOMLINDA RAIS OBAMA KWA ULINZI MKALI AJABU
Helikopta ya Polisi ikiwa katika doria ya hapa na pale, hata hivyo eneo lote la uwanja wa Ndege ulidhibitiwa na Wamarekani wenyewe ikiwemo na kazi ya kuongoza ndege.
Ulinzi kila
kona
Ulinzi
ulimarishwa.
Bendera ya
Tanzania ikiwekwa katika gari lililombeba Rais wa Marekani, Barack
Obama.
Gari
alilopanda Rais Obama
(Picha na Habari Mseto Blog)
KIKAPTURA KIFUPI CHA MTOTO WA KIKE WA RAIS OBAMA CHAZUA GUMZO KUBWA
amevaa kikaptura kifupi (short shorts, al maarufu kama daisy dukes.) Mapaparazzi walimpiga picha binti huyo akiwa mitaani na raha zake na kuuliza mitandaoni kama ni sahihi kwa binti wa miaka 12, kuvaa kaptura fupi hivyo. Kama kawaida za mitandaoni, kilichozuka ni ubishi mkali kati ya wanaoona si sahihi, hasa kwa binti ya rais, na wale wanaoona ni poa tu. Wewe upo kwenye camp ipi? Unaweza ruhusu binti yako avae kaptura kama hii?
Monday, July 01, 2013
HUU NDIO UJUMBE MZITO TOKA KWA ZITTO KABWE KWENDA KWA OBAMA
Obama: Tunataka Uwazi wa Mikataba. Omba radhi Kwa mauaji ya Lumumba
Hatimaye Barack Obama, Rais wa Marekani anatembelea tena bara la Afrika. Hii itakuwa ni mara ya pili Obama kutembelea Bara hili alikotoka baba yake baada ya ziara yake ya kwanza mwaka 2009. Mwaka huo alitembelea Ghana na Misri ilhali mwaka huu anatembelea Senegali, Afrika Kusini na Tanzania. Ziara hiyo itakayoanza tarehe 26 mwezi Juni, itamfikisha Tanzania tarehe 1 Julai na kuondoka siku ya pili yake.
Uchaguzi wa Obama kuwa Rais wa Marekani ulipokolewa kwa shangwe Afrika nzima. Wakati Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria alilia kwa furaha, nchi ya Kenya ilitangaza siku ya mapumziko na Rais wa zamani wa Afrika Kusini ndugu Nelson ‘Madiba’ Mandela alisema ‘ushindi wa Obama unawafanya Waafrika wathubutu kuota ndoto (Jarida la The Economist). Hapa Tanzania kulikuwa kuna shamra shamra za kila namna na magazeti yaliweka vichwa vya habari kana kwamba ni Rais wa Tanzania aliyechaguliwa.
Waafrika walikuwa na matumaini makubwa sana na bwana Obama. Yamefikiwa?
Ni vema ifahamike kuwa Barack Obama ni Rais wa Marekani na siku zote atalinda maslahi ya Marekani tu. Kuwa na matumaini makubwa kwamba labda yeye angeliweza kuiweka Afrika mbele sana ilikuwa ni kujifurahisha tu nafsi. Maslahi ya Marekani ni ya kipaumbele kuliko kitu kingine chochote kwa Rais Obama. Kwa wengi Obama amekuwa kama amewavunja moyo.

WATANZANIA 60 WAKAMATWA ZIARA YA OBAMA....!!!
Watanzania
60 wamekamatwa Afrika Kusini kutokana na maandalizi yaliofanyika nchini
humo ya kumpokea Rais Barack Obama wa Marekani.
Rais Obama amewasili Afrika Kusini juzi kwa ziara ya siku tatu akitokea Senegal.
Watu hao wamekamatwa baada ya kudaiwa kuishi kinyume cha sheria Afrika Kusini. Baada ya Watanzania hao kutiwa mbaroni na vyombo vya usalama wamehifadhiwa hapa nchini kusubiri hatua za kisheria zaidi.
Ofisa mmoja wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Sadiki Msele amesema Watanzania hao walirejeshwa nchini jana na kwamba hivi sasa wanasubiri sheria kuchukua mkondo wake.
“Safisha safisha kama iliofanyika jijini Dar es Salaam, pia imefanyika Afrika Kusini na kuwaathiri wafanyabiashara na watu wengine,” amesema ofisa huyo.
Hivi sasa Rais Obama yupo Afrika Kusini akiwa ameongoza na mkewe Michelle Obama na watoto wao wawili; Malia na Sasha.
Leo Rais Obama na ujumbe wake anatarajiwa kutua Tanzania kwa ziara ya siku mbili na Jumanne ataondoka kurejea Marekani.

WAPENZI WADONDOKA NA KUFA WAKATI WAKIFANYA MAPENZI DIRISHANI...!!!
Wapenzi wameanguka na kufa baada ya dirisha walipokuwa wakifanyia mapenzi kufunguka ghafla nchini China.
Wawili
hao wanasemekana kudondoka kutoka kwenye dirisha la jengo moja la
makazi kwenye jiji la Wuhan nchini humo pale dirisha hilo walilokuwa
wameegemea kufunguka.
Mashuhuda
walivieleza vyombo vya habari vya China kwamba wapenzi hao
walikumbatiana wakati wakianguka kwenye njia ya waenda kwa miguu nje.
Kwa
mujibu wa The Sun, chanzo kimoja cha habari kilisema: "Huku wawili hao
wakiwa wameshikamana vilivyo, walianguka nje ya jengo hilo."
Picha za kuogofya zimefichuliwa kwenye tovuti za nchini humo zikionesha wapenzi hao wakiwa wamefunikwa kwa mashuka na polisi.
Damu ilitapakaa kwenye njia ya waenda kwa miguu karibu na wapelelezi wanaonekana wakichunguza eneo la tukio.
Miili
ya wapenzi hao ilipigwa picha karibu na baiskeli ambayo ilikuwa
imelazwa chini, lakini hakukuwa na ripoti zozote kwamba yeyote chini
alikuwa amejeruhiwa katika ajali hiyo.
Ripoti zinasema kwamba madirisha hayo kwenye jengo hilo la makazi yalikuwa hayana ubora unaotakiwa.
Inafikiriwa
kwamba mwanaume huyo na mwanamke wanawezekana walikuwa wakijaribu
kujipooza kando ya dirisha hilo ndipo tukio hilo likatokea.
Haikufahamika ni umbali gani kutoka juu wawili hao walikuwa wakati wakianguka.
Wuhan ni jiji maarufu zaidi lililopo katikati ya China.
Ukiwa na historia ya miaka 3,500 ni moja kati ya miji mikongwe na iliyostaarabika katika China.
HUYU NDIYE MWANAMKE ALIYEMKATA UUME MUMEWE AFUNGWA MAISHA GEREZANI...!!!
Mwanamke mmoja wa California ambaye alituhumiwa kukata uume wa mumewe kabla ya kuutupa kwenye mashine ya kusagia taka amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
Catherine
Kieu, mwenye miaka 50, alipatikana na hatia ya mashitaka ya kutesa na
kosa la kuharibu viungo vya mwili katika shambulio la Julai 11, 2011 na
kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, lakini anaweza kufikiriwa kupewa
msamaha baada ya kutumikia miaka saba.
Alitiwa hatiani Aprili kwa kila kosa moja la kutesa na kuharibu viungo vya mwili.
Muathirika, anayefahamika kama Glen wakati wote wa kesi, alikuwa mahakamani kwa ajili ya hukumu ya jana.
"Natumaini
hii itakuwa mara ya mwisho kabisa ninayoweza kumwona," alisema Glen.
"Najihisi nafuu kiasi fulani, na ilikuwa siku ya huzuni kubwa kwangu."
Muathirika huyo alikimbizwa hospitali, lakini upasuaji kurejesha uume wake haukufanikiwa.
Wakati
wa kesi hiyo, muathirika huyo mwenye umri wa miaka 60 alitoa ushahidi
kwamba uume wake hauwezi tena kuunganishwa mahali pake na kwamba anahisi
kama ameuawa.
Kieu
alikuwa na wivu na hasira kuhusu mipango ya mumewe kumpa talaka sababu
alimwona rafiki yake wa zamani wa kike, upande wa mashitaka ulisema.
Sunday, June 30, 2013
LOWASSA AMTAKA OBAMA ASIZUNGUMIE MAMBO YA USHOGA NA NDOA ZA JINSIA MOJA AKIWA TANZANIA
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa, amemtahadhalisha kujiepusha na kauli za kuunga mkono ushoga.
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Alisema jana kuwa ushoga na hai za ndoa kwa watu wa jinsia moja vinaweza `kuiharibu’ ziara yake hapa nchini.
Mapema wiki hii, Rais Obama alikaririwa akizungumzia masuala hayo yanayotajwa kuwa ni moja ya haki za msingi za binadamu, alipokuwa Senegal, lakini akapingwa.
“Watanzania hawatalikubali na wataendelea kushikilia uhuru na heshima walizojengewa tangu awali, kwamba ushoga na ndoa za jinsia moja havikubaliki,” alisema.
Akiwa Senegal, Rais Obama alitaka serikali za Afrika kutoa haki kwa mashoga kama inavyotoa kwa raia wengine.
"Ninachotegemea, I pray and hope (ninasali na kutegemea) kwamba kuhusu mashoga na ndoa za jinsia moja, Rais Obama hatarudia kauli aliyoitoa kule Senegal,” alisema.
Aliongeza, "ninasema hivi kwa sababu Tanzania hatuamini katika ushoga, na endapo utawalazimisha Watanzania, watakukatalia na kushikilia uhuru na heshima waliyojengewa toka awali."
JK AMGEUKA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA JAJI JOSEPH WARIOBA
RAIS
Jakaya Kikwete amemgeuka Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Jaji Joseph Warioba, kwa kuridhia azimio la Chama Cha Mapinduzi (CCM),
kutaka uwepo muundo wa serikali mbili.
Rais
Kikwete ambaye juzi aliongoza kikao cha Kamati Kuu (CC), mjini Dodoma,
aliridhia azimio hilo, huku akijua fika kuwa ndiye aliyemruhusu Jaji
Warioba kuingiza kipengele hicho kwenye rasimu wakati alipoifikisha
mbele yake kabla ya kuitoa hadharani.
Kutoka
na hali hiyo, Kamati Kuu imewataka wanachama wao wote kupitia mabaraza
ya CCM kuhakikisha wanakubaliana na msimamo wa chama wa kupinga muundo
wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa na tume ya Jaji Warioba.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho kutoka Zanzibar, waliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa Kamati Kuu
imepitisha azimio la kutaka mabaraza ya Katiba ya chama hicho yajadili na kuridhia msimamo wa kuwa na serikali mbili.
Kamati
Kuu ya CCM imekuja na mapendekezo ya namna ya kurekebisha kasoro kubwa
za Muungano ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikilalamikiwa na
Wazanzibari.
BEYONCE ATINGA VAZI LA KANGA, ILIYOTENGENEZWA NA MTANZANIA
Christina (katikati)
Utajiskiaje
kuona Beyonce akiwa amevaa vazi lililotengenezwa kwa kanga yenye
maneno ya Kiswahili? ‘Wawili Ninyi Yawahusu….’ yanasomekana maandishi
kwenye vazi alilolivaa mwanamuziki wa Marekani,
Beyonce Knowles.
Vazi
hili alilolivaa Beyonce kwenye moja ya show zake za tour ya Mrs
Carter, limetengenezwa na mwanamitindo wa Tanzania aishie jijini London
Uingereza, Christine Mhando mwenye brand ya Chichia London.
Chichia London ndio brand iliyo maarufu sana nchini Uingereza kwa
kutengeneza nguo za Kitanzania kwa kutumia Kanga na material mengine
Kiafrika.
Hizi ni baadhi ya nguo alizotengeneza.
LOWASSA AWATEKA WAENDESHA BODABODA ARUSHA...!!!
Wafanyabiashara
maarufu jijini Arusha wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu na
Diwani wa Mererani, Mathias Manga, ndiyo waliyobuni wazo hilo la
kuwaanzishia mfuko vijana wa bodaboda.
Katika harambee hiyo, sh milioni 84 zilipatikana huku Lowassa pamoja na marafiki zake wakichangia sh milioni 10 na pikipiki 1WAZIRI
Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amesema usafiri wa pikipiki maarufu
kama bodaboda ni sera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kusaidia
kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
Akizungumza
katika haraambee na uzinduzi wa mfuko wa waendesha pikipiki maarufu
mkoani Arusha, Lowassa alisema sera hiyo ni ya kuwakomboa vijana.
Alisema kuwa kitendo cha wafanyabishara wa Arusha kujipanga kusaidia bodaboda ni mfano kwa wafanyabishara wengine nchini.
“CCM
ni chama kinachotetea wanyonge, na nyinyi ni wanyonge mnaohitaji
kunyanyuliwa kimaisha, kitendo hiki cha wafanyabisharaa wa Arusha ni cha
kuunga mkono sera ya CCM,” alisema.
Lowassa
alisema tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka na kwamba
wasipowasaidia vijana kuondokana na tatizo hilo amani itatoweka.
“Ndiyo
maana CCM katika ilani yake ya uchaguzi imeliweka hilo na pia
kulisisitiza katika vikao vyake vya juu vya Mkutano Mkuu pamoja na
Halmashauri Kuu,” alisema.
HUU NDIO WOSIA WA MZEE MANDELA NA MAHALI ANAPOPENDA KUZIKWA
Mzee
Nelson Mandela ameandika wosia kwenye karatasi moja ya ukubwa wa A4
ambamo ameagiza azikwe katika milima iliyojitenga nyumbani kwa mababu
zake huko Qunu, imebainika.
Rais
huyo wa zamani wa Afrika Kusini, mwenye miaka 94, bado yuko mahututi
lakini lakini hali yake inaimarika hospitalini mjini Pretoria ambako
amekuwa huko kwa siku 21 zilizopita akitibiwa maambukizi kwenye mapafu.
Mnamo
Januari 1996, wakati akiwa bado Rais, Mzee Mandela aliripotiwa kuandika
wosia ambao aliagiza kufanyiwa maziko ya kawaida karibu na kijiji
ambako alikulia kwenye rasi ya Mashariki.
Alisema
kwamba wakati akifurahia kumbukumbu ya kulitumikia taifa hilo mjini
Pretoria angetaka kuzikwa katika eneo la familia hiyo na kuwekewa jiwe
la kawaida kama alama ya lilipo kaburi lake.
Gazeti
la South African Mail na Guardian yaliripoti yakimnukuu rafiki wa siku
nyingi wa familia akisema: "Hakuwahi kukifanya kifo kuwa jambo kubwa la
kufikiriwa, lakini hakuwahi kutaka chochote cha ufahari".
Licha
ya ukweli kwamba mauzo ya kitabu cha Mandela cha Long Walk To Freedom,
na michoro yenye jina lake, kumpatia mamilioni ya pesa kwa hadhi wosia
wake uliripotiwa kutosha kwenye karatasi moja ya ukubwa wa A4.
OBAMA ATOA SABABU YA KUTOFANYA ZIARA KENYA...!!!
Rais Barack Obama. |
Wakati
Rais wa Marekani, Barack Obama amesema asingeweza kufanya ziara Kenya
kutokana na Rais wake, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Rutto
kukabiliwa na mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa
Kivita (ICC), pia amehadharisha Afrika kuhakikisha kuwa kampuni za
kigeni zinaajiri wafanyakazi wazalendo ili wawekeze nchini mwao.
Alitoa
kauli hizo mbili kwa nyakati tofauti, alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari na baadaye alipozungumza na viongozi vijana wa
Afrika akiwa katika ziara yake nchini Afrika Kusini.
Akizungumza jioni jana na vijana katika eneo la Soweto jijini Johannesburg, Obama alisema ataangalia uwezekano wa kwenda Kenya akiwa bado madarakani kwani bado ana miaka mitatu na miezi saba ya uongozi wake.

Subscribe to:
Posts (Atom)