Mzee
Nelson Mandela ameandika wosia kwenye karatasi moja ya ukubwa wa A4
ambamo ameagiza azikwe katika milima iliyojitenga nyumbani kwa mababu
zake huko Qunu, imebainika.
Rais
huyo wa zamani wa Afrika Kusini, mwenye miaka 94, bado yuko mahututi
lakini lakini hali yake inaimarika hospitalini mjini Pretoria ambako
amekuwa huko kwa siku 21 zilizopita akitibiwa maambukizi kwenye mapafu.
Mnamo
Januari 1996, wakati akiwa bado Rais, Mzee Mandela aliripotiwa kuandika
wosia ambao aliagiza kufanyiwa maziko ya kawaida karibu na kijiji
ambako alikulia kwenye rasi ya Mashariki.
Alisema
kwamba wakati akifurahia kumbukumbu ya kulitumikia taifa hilo mjini
Pretoria angetaka kuzikwa katika eneo la familia hiyo na kuwekewa jiwe
la kawaida kama alama ya lilipo kaburi lake.
Gazeti
la South African Mail na Guardian yaliripoti yakimnukuu rafiki wa siku
nyingi wa familia akisema: "Hakuwahi kukifanya kifo kuwa jambo kubwa la
kufikiriwa, lakini hakuwahi kutaka chochote cha ufahari".
Licha
ya ukweli kwamba mauzo ya kitabu cha Mandela cha Long Walk To Freedom,
na michoro yenye jina lake, kumpatia mamilioni ya pesa kwa hadhi wosia
wake uliripotiwa kutosha kwenye karatasi moja ya ukubwa wa A4.