Friday, June 28, 2013

BAADA YA MIAKA KUPITA LADY JAY DEE NA Q CHIEF WAINGIA STUDIO TENA

 
Wakali wa bongo fleva wenye vocal zenye ladha na nguvu ya aina yake Lady JayDee ‘Anaconda’ na Q-Chillah, wamekutana tena studio kurekodi wimbo mpya ikiwa ni miaka kadhaa imepita walipotisha na wimbo wao ‘Zamani’. 
Lady JayDee alipost picha kupitia akaunti yake ya Twitter ikimuonesha yeye na Q-chilla wakiwa ndani ya studio za Combination sound na Man Walter, na kuisindikiza na maelezo. 
"Mtu 3 ndani ya studio. Mwaikumbuka Zamani - Q Chief feat Jide?? Nikilala naotaa, naota km unaniita. Sasa yaja mpya."Alitweet Jide June 26.

Hakuchelewa kutaja jina la wimbo huo “Sukari” na kuonesha kuikubali sana, hii inatoa picha kuwa kitu kikubwa kinakuja.
“Sukari - Qchillah & Jide another hit ??? ☺ #Justasking.” Aliongeza.

Tuisubiri hiyo sukari tuonje ladha yake kwa masikio.

WAGANGA WA JADI AFRIKA KUSINI WAMFANYIA TAMBIKO MZEE MANDELA

Sasa ni dhahiri kuwa maisha ya kiongozi wa zamani wa nchi hii, Nelson Mandela yamo hatarini kutokana na kwamba anaishi kwa msaada wa mashine, imethibitishwa na mmoja wa wazee wa ukoo wa kiongozi huyo.

Binti yake mkubwa Makaziwe naye amethibitisha hilo, akisema hali ni mbaya na chochote chaweza kutokea.
"Naweza kusisitiza hilo, kwamba Tata (baba) hali yake ni mbaya sana, chochote chaweza kutokea, lakini nataka nisisitize tena, kwamba ni Mungu tu ndiye anajua muda wa kuondoka,” alikiambia kituo cha utangazaji cha SAFM jana.
Hali hiyo inayotia mashaka imesababisha hata Rais Jacob Zuma afute safari yake ya Msumbiji ambako alipanga kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
“Ndiyo, anatumia mashine kupumua,” Mzee Napilisi Mandela aliiambia AFP muda mfupi baada ya kumtembelea Mandela hospitalini juzi. “Hali ni mbaya, lakini tutafanyaje.” 
Zuma alifuta safari yake iliyokuwa ifanyike jana baada ya “kubaini, kwamba kiongozi huyo wa zamani hali yake bado ni mbaya,” taarifa kutoka Ofisi ya Rais ilisema.
Wakati huo huo, kiongozi wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu Ban Ki-moon alisema juzi kwamba dunia yote inamwombea Mandela wakati huu ambapo anapigania maisha yake.

BINTI AJIFUNGUA BARABARANI AKIKIMBIZWA HOSPITALI KWA BODABODA

Josephine Michael akiwa barabarani baada ya kujifungua.
Na Dustan Shekidele, Morogoro
BINTI mmoja aitwaye Josephine Michael mkazi wa Kijiji cha Kiegea nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, Jumatano iliyopita alijifungua barabarani wakati akikimbizwa hospitalini kwa kutumia usafiri wa bodaboda.


Tukio hilo lililowashtua watu wengi lilitokea asubuhi kwenye Kituo cha Daladala Cha Nanenane kandokando ya Barabara Kuu iendayo Dar es Salaam.
Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kumshuhudia askari wa kike wa kikosi cha usalama barabarani ‘trafiki’ (jina lake halikupatikana) akiacha kazi ya kuongoza magari na kugeuka mkunga kwa muda ili kumsaidia binti huyo akiwa sambamba na wanawake wengine na kufanikisha kupatikana kwa mtoto wa kiume ‘dume la nguvu’.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 28, 2013

.
.

Thursday, June 27, 2013

MELI YA MAGUFULI YAZAMA BAHARINI.


 
PICHA ya maktaba ikionyesha meli ikizama baharini.

ILE meli maarufu kwa jina la ‘Meli ya Magufuli’ ambayo serikali iliinasa katika eneo lake la bahari ya Hindi ikivua samaki bila ya kibali, imezama baharini, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Habari ambazo gazeti hili limezipata, meli hiyo ambayo ina uwezo wa kuvua samaki kwenye kina kirefu baharini, imezama  baada ya wajanja wachache kukata vyuma vyake na kuuza kama chuma chakavu.

Kwa mujibu wa habari hizo, wajanja wamekuwa wakiingia na kukata vyuma vya meli hiyo baada ya serikali kuitelekeza kwa muda mrefu bila uangalizi tangu ilipoitaifisha.

Vyanzo vyetu vya habari vilipasha kuwa vyuma chakavu vya meli hiyo vimekuwa vikiuzwa kwa kampuni zinazonunua na kuvisafirisha nje ya nchi na kujiingizia mabilioni ya fedha.

Sehemu kubwa ya vyuma chakavu kutoka kwenye meli hiyo, vimeuzwa kwa kampuni moja inayomilikiwa na mmoja wa wabunge wa Jamhuri ya Muungano.

Inaelezwa kuwa sehemu kubwa ya meli hiyo imetengenezwa kwa malighafi aina ya Brass ambayo kilo moja kwa sasa inauzwa kwa sh 5,200.

Malighafi nyingine zilizotumika na bei yake kwa kilo kwenye mabano vikuzwa kama chuma chakavu ni Cast Aluminum (sh 1,700), Stainless (sh 1,500) na Soft (sh 2,000).


CCM WANG'ANG'ANIA SERIKALI MBILI KATIKA KATIBA MPYA.

 

Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kimemalizika mjini Dodoma huku kukiwa na taarifa kuwa chama hicho kimeweka msimamo wa kutaka kuwepo kwa mfumo wa Serikali mbili katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mchakato wa Katiba Mpya ya Tanzania upo katika hatua ya rasimu na watu mbalimbali kupitia Mabaraza ya Katiba, wamekuwa wakitoa maoni yao.Tayari Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa chama hicho kitakuwa moja ya mabaraza ya katiba na kupata nafasi ya kuichambua, kuijadili na kutoa maoni kuhusu rasimu ilitolewa hivi karibuni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya mwenyekiti wake Jaji mstaafu Joseph Warioba.
Habari za ndani zilisema kuwa kikao hicho kilichoongozwa na Rais Kikwete kilijadili mchakato wa Katiba Mpya, masuala ya maadili ndani ya chama na kuyatolea uamuzi.


Hata hivyo mmoja wa watendaji ndani ya chama hicho alisema kikao kilikuwa cha kawaida na kwamba kilikuwa kinapitia majukumu na kwamba hakuna kubwa lililojadiliwa. Habari zaidi zinadai kuwa mbali ya kuunga mkono mfumo wa Serikali mbili, CCM imetoa adhabu kwa wanachama wake wawili ambazo zitatangazwa katika siku iliyopangwa.

WATU 10, 799 WANASWA NA DAWA ZA KULEVYA TANZANIA

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Mizengo Pinda

WATU 10,799 wamenaswa wakijihusisha na dawa za kulevya katika kipindi cha miaka mitano pekee na kuonyesha namna gani biashara ya dawa hizo lilivyo tatizo nchini.
Kwa mujibu wa hutuba ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Urasimu na Bunge) William Lukuvi katika Siku ya Kupiga vita Dawa za Kulevya Duniani ni kwamba biashara ya dawa za kulevya ni tatizo nchini.
Pinda alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.

WATU WA MIKOANI WASHAURIWA KUTOENDA DAR WAKATI WA ZIARA YA RAIS OBAMA HADI ATAKAPO MALIZA ZIARA YAKE.

 

Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe(PICHANI) amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.

Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.

 

“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.

Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 27, 2013





KUMEKUCHA BIG BROTHER, MWAKILISHI WA BB TANZANIA FEZA KESSY NDANI YA PENZI ZITO NA O"NEAL WA BOTSWANA

 
FEZA KESSY (TANZANIA)
  
O"NEAL (BOTSWANA) 
Feza akilana denda na O'neal kitandani.

HAKI ZA BINADAMU WAMTAKA WAZIRI MKUU PINDA AOMBE RADHI WATANZANIA, AKIKATA AWAJIBISHWE KWA MUJIBU WA SHERIA....!!!

Akizungumza na waandishi wa habari janaMkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba amesema kitendo cha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuruhusu matumizi ya nguvu kwa polisi dhidi ya raia ni cha kulaaniwa na wapenda haki wote na amemtaka waziri mkuu kuwaomba radhi watanzania.


KUPINGA KAULI YA WAZIRI MKUU "Wapigwe tu" ALIYOITOA BUNGENI TAREHE 20/06/2013

Taarifa hii ni matokeo ya ufuatiliaji wa utendaji wa shughuli za Serikali kama zinavyowasilishwa bungeni na kauli ya Waziri Mkuu (Mtendaji Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni) aliyoitoa, Alhamisi ya tarehe 20 Juni 2013, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo. Waziri Mkuu Pinda, alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama, hususan Jeshi la Polisi kuwapiga wananchi watakao kaidi na kupinga amri halali ya jeshi hilo. Katika tamko hilo, Pinda alisema Serikali imechoshwa na vurugu na kwamba hakuna namna nyingine ya kupambana na wananchi wanaodharau vyombo vya dola zaidi ya kipigo.

Waziri Mkuu Pinda alitoa msimamo huo Bungeni, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM), aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kufuatia kuwa na matukio ya vurugu ya mara kwa mara nchini, hususan huko Mtwara na Arusha.
Katika majibu yake, Mh. Pinda, pamoja na mambo mengine alisema kuwa; “Mheshimiwa Mangungu hapa ameanza vizuri, lakini mwisho hapa naona anasema vyombo vya dola vinapiga watu, ukifanya fujo au umeambiwa usifanye hiki ukaamua kukaidi utapigwa tu. Akaendelea kusema kuwa, “Lazima wote tukubaliane kuwa nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya sheria na kama wewe umekaidi, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi, watakupiga tu.

CHADEMA WAKATAZWA KUVAA KOMBAT BUNGENI...!!

Kombati za CHADEMA mzozo
Siku moja baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na wabunge wenzake watatu kuzuiwa kuingia bungeni juzi, uongozi wa Bunge umesisitiza kuwa kombati zao zinakiuka kanuni.

Mbowe na wabunge wenzake wa CHADEMA, Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini) na Ezekiel Wenje (Nyamagana) walizuiwa na askari kwa madai kuwa wamevalia sare za chama ambazo kikanuni haziruhusiwi.

 

Uamuzi huo uliibua hali ya sintofahamu kwa wabunge wa CHADEMA kutokana na Mbowe kuvalia vazi hilo mara nyingi tangu aingie bungeni mwaka 2010.

Licha ya kanuni za Bunge kuruhusu vazi la ‘safari suti’ kwa wanaume lenye mshono kama kombati zinazovaliwa na baadhi ya wabunge wa CHADEMA, Tanzania Daima Jumatano limebaini kuwa uamuzi huo unaacha maswali mengi yanayohitaji majibu.

Akizungumzia uamuzi huo jana, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema suti hizo za wabunge wa CHADEMA zilikiuka kanuni ya 149 (3) (b) (i).

Kipengele hicho cha kanuni kinasomeka kuwa inaruhusiwa suti ya Kiafrika au safari ya mikono mirefu au mifupi yenye ukosi au shingo ya mviringo na yenye fulana au bila fulana ndani, ya rangi moja, isiyokuwa na nakshi, pamoja au bila baragashia.

Joel alifafanua kuwa yawezekana huko nyuma wamekuwa wakifanya makosa kwa kuwaruhusu wabunge hao kuingia na suti hizo, lakini sasa kuanzia juzi wameamua kuanza
 kuchukua hatua ya kuwazuia.

“Zile wanasema sio sare ya chama, lakini wote tunawaona kwenye mikutano na shughuli za chama ndizo zinavaliwa na isitoshe tuliwahi kuwatahadharisha kuwa ziko kinyume na kanuni wasizivalie bungeni ila wamekuwa wakiendelea kuzivaa,” alisema.

SAFARI YA RONALDO KUREJEA MAN U YAIVA

ronaldo2 b06e8
CRISTIANO Ronaldo anaweza kurejea Manchester United baada ya kugundulika atakuwa na mkutano na viongozi wa klabu hiyo ya Old Trafford ndani ya siku tatu zijazo. 
Nyota huyo wa Real Madrid amekuwa akihusishwa na kurejea England baada ya kupitia msimu wa bila furaha Bernabeu, lakini ilitarajiwa kuwasili kwa kocha mpya, Carlo Ancelotti kungemfanya abaki Hispania. 
Na gazeti la Hispania, El Pais limeripoti kwamba nahodha huyo wa Ureno atakutana na viongozi wa Man u kabla hajaenda kuanza msimu mpya Madrid.

Kwa kuwa FIFA inazuia klabu kufanya mazungumzo na wachezaji walio ndani ya Mikataba na klabu zao, pande zote zimejipanga kukana kufanya mazungumzo, ambayo itamsaidia sana kocha mpya, David Moyes kuelekea msimu ujao.

Lakini Ancelotti amesema wakati akitambulishwa kuwa kocha mpya wa Madrid leo kwamba: "Cristiano ni mchezaji mkubwa na ninajivunia kufanya naye kazi. 

"Nimewakochi Zidane, Ronaldo na Ronaldinho, na ninajivunia kumuongeza na yeye.' 


Alipoulizwa kuhusu Radamel Falcao, mchezaji aliyekuwa anawaniwa na Madrid ambaye amesaini Monaco, Ancelotti alisema: "Ni mchezaji mzuri, lakini kuna Ronaldo, Higuain na Benzema,"alisema. Chanzo: binzubeiry

Wednesday, June 26, 2013

TANGAZO: NAFASI ZA MASOMO



|             ST. THOMAS INSTITUTE OF TECHNOLOGY & MANAGEMENT
                 
                              P.O. BOX 6089, Morogoro. CEL: 0713 530261, 0717-707025, 0767 530261, 0655 758980
                                                  Email: magkit2005@yahoo.com
Chuo kipo Morogoro mjini, Kilakala. Chuo Kipo katika mazingira mazuri ya kujifunzia. Studio za kisasa kwa wanafunzi wa Uandishi wa habari na Utangazaji.
LIST OF COURSES
S/N
COURSE
DURATION
1
CERTIFICATE IN BUSINESS ADMINISTRATION
1YEAR
2
 CERTIFICATE IN HOTEL MANAGEMENT
6MONTHS
3
CERTIFICATE IN HUMAN RESOURCE MANAGEMENT.
1YEAR
4
CERTIFICATE IN INFORMATION TECHNOLOGY (IT).
1YEAR
5
CERTIFICATE IN COMPUTER SCIENCE.
1YEAR
6
CERTIFICATE IN RECORD MANAGEMENT
1YEAR
7
  CERTIFICATE IN PROCUREMENT AND SUPPLY
1YEAR
8
CERTIFICATE IN NURSERY TEACHING AND KIDERGATEN
6MONTHS
9
CERTIFICATE IN ACCOUNTANCY.
1YEAR
10
CERTIFICATE IN COMMUNITY DEVELOPMENT.
1YEAR
11
CERTIFICATE IN JOURNALISM&MASS COMMUNICATION

1 YEAR
12
BASIC CERTIFICATE IN BUSINESS ADMINISTRATION
6MONTHS
13
BASIC CERTIFICATE IN HUMAN RESOURCE MANAGEMENT.
6MONTHS
14
BASIC CERTIFICATE IN INFORMATION TECHNOLOGY (IT).
6MONTHS
15
BASIC CERTIFICATE IN COMPUTER SCIENCE.
6MONTHS
16
BASIC CERTIFICATE IN RECORD MANAGEMENT
6MONTHS
17
  BASIC CERTIFICATE IN PROCUREMENT AND SUPPLY
6MONTHS
18
BASIC CERTIFICATE IN ACCOUNTANCY.
6MONTHS
19
BASIC CERTIFICATE IN COMMUNITY DEVELOPMENT.
6MONTHS

Kwa wanachuo wa Uandishi wa Habari na Utangazaji Muhula mpya utaanza Rasmi tarehe July 8 mwaka huu..

MZEE MANDELA AFANYIWA MAOMBI MAALUM


 ASKOFU mkuu wa kanisa la kianglikana mjini Cape Town, Afrika Kusini, Thabo Makgoba, amejitolea kufanya maombi kwa niaba ya rais mstaafu Nelson Mandela ambaye anaugua sana hospitalini.
Kasisi huyo anamuombea Mandela aweze kupata nafuu na amewataka wananchi kumshukuru kwa yote aliyowafanyia.
Jamaa za Nelson Mandela wamekutana nyumbani kwake huko Kunu, huku hali yake ya afya ikizidi kudorora hospitalini, Pretoria.
Afya ya Bwana Mandela ilikuwa mbaya zaidi Jumapili.
Maombi hayo yalitolewa baada ya Askofuu huyo kumtembelea Mandela hospitalini ambako kiongozi huiyo wa zamani amekuwa akilazwa kwa wiki mbili na nusu zilizopita baada ya kuugua mapafu.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa wajukuu wa rais huyo wa zamani wa Afrika kusini wanakutana nyumbani kwake kijijini katika mkoa wa Eastern Cape province, ambako viongozi wa kitamaduni wamealikwa.
Halikopta ya jeshi kadhalika zilionekana zikipaa karibu nyumbani kwa mandela. Afisi ya Rais jacob Zuma ilitangaza jumapili kuwa hali ya mzee Mandela ya afya ilikuwa mbaya sana. Chanzo: bbcswahili

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...