Mashoga hao wakifungishwa ndoa kwenye ofisi ya msajili nchini Uingereza.
Wanawake wawili raia wa Pakistan wameweka historia kama Waislamu wa kwanza wa jinsia moja kufunga ndoa nchini Uingereza.
Rehana
Kausar, miaka 34, na Sobia Kamar, miaka 29,wameweka historia pale
walipofunga pingu za maisha katika sherehe iliyofanyika kwenye ofisi ya
msajili, kisha haraka wakaomba hifadhi ya kisiasa baada ya kuwa
wamefunga ndoa, wakidai kwamba maisha yao yatakuwa hatarini kama
wakirejea kwenye nchi yao ya asili.
Wakishuhudiwa
na wasimamizi wao na marafiki wawili, wanandoa hao walivalia mavazi
meupe asilia ya ndoa pale walipofunga ndoa mjini Leeds, West Yorkshire.
Wawili
hao, kutoka mikoa ya Lahore na Mirpur ya Pakistan, walisema walipokea
vitisho vya kuuawa kutoka kwa wapinzani nchini Pakistan - ambako
mahusiano ya jinsia moja ni kinyume cha sheria na kuchukuliwa ni
kusaliti Uislamu.
Na
tangu habari za ndoa yao mapema mwezi huu kuzagaa, wanandoa hao walidai
kupokea vitisho vya kuuawa hata kutoka nchini Uingereza
Kabla
ya zoezi hilo, hata msajili aliwashauri wawili hao kufikiria kwa makini
kuhusu uamuzi wao wa kufunga ndoa sababu ya mtazamo wa baadhi ya
Waislamu kuhusu mahusiano ya jinsia moja.