Tukio la kutupwa bomu katika Kanisa Katoliki la Joseph Mfanyakazi, Arusha limetua katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) baada ya kuwasilishwa na Balozi wa Vatican UN, Askofu Mkuu Frances Chullikatt.
Askofu Chullikatt anakuwa kiongozi wa kwanza wa Vatican kutoa tamko kuhusiana na shambulizi hilo ambalo mmoja wa viongozi wake alikuwapo.
Bomu hilo lilirushwa katika kanisa hilo wakati likizinduliwa na Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Francisco Padilla Mei 5, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu watatu na
kujeruhi zaidi ya 50.
kujeruhi zaidi ya 50.
Wakati wa shambulizi hilo, Askofu Padilla na Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha, Josephat Lebulu walionusurika.