GARI YA AINA YA COSTA T 399 AUD ILIYOGONGWA KWA NYUMA NA KISHA KUPINDUKA ENEO LA KANYEGELE UWANJA WA NDEGE WILAYANI RUNGWE |
Tuesday, May 14, 2013
AJALI YA COASTER NA LORI YAUA ABIRIA MMOJA AFARIKI DUNIA WENGINE 17 WAKIJERUHIWA WILAYA RUNGWE MKOANI MBEYA.
MSANII WA BONGO MOVIE ATAFUTA MUME WA KUMZALISHA
Baada ya kuadimika kwa muda mrefu, mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aisha Bui ameibuka na kusema kuwa anatafuta mwanaume ambaye atamzalia mtoto na hatimaye waoane ila akadai wa kumuoa kwa sasa hamuoni
Akizungumza na mwandishi wetu, Aisha amefunguka kuwa alikuwa kimya kwa sababu kuna mambo alikuwa akifanya.
Alisema kwa kuwa ameyakamilisha, sasa ana nafasi ya kusaka mtoto iwapo atampata mwanaume sahihi.
Aisha amevitaja vigezo vya mwanaume wa kumzalia kuwa amjengee nyumba ya kuishi yeye na mtoto wake kisha awe na uwezo wa kumlea na kumpatia elimu bora.
Monday, May 13, 2013
WHO yasema coronavirus yaambukiza.
Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema inaelekea sana kuwa aina mpya ya virusi vinavouwa, vya coronavirus, vinaweza kuambukizwa baina ya watu walio karibu sana.
Virusi hivyo ni sawa na vile vya homa ya SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome) na vinamfanya mgonjwa kuwa na shida sana ya kuvuta pumzi.
Nchini Ufaransa mwanamume mwengine hivi sasa ni mahtuti baada ya kuambukizwa na mgonjwa wa mwanzo nchini humo, ambaye walilazwa chumba kimoja hospitali.
Hadi sasa watu 34 wanajulikana kupata ugonjwa huo duniani tangu mwaka wa 2012, 18 kati yao walikufa Saudi Arabia.
WHO inasema ni muhimu kujulisha watu kuhusu virusi hivyo kwa sababu kuna wasi-wasi mkubwa kuwa vinaweza kusambaa.
Chanzo ni BBC Swahili.
MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE KUTANGZWA WIKI HII
Matokeo mapya ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012 yanatarajia kutangazwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi siku yeyote wiki hii.
Kutangazwa upya kwa matokeo hayo kunafuatia uamuzi uliochukuliwa na serikali hivi karibuni kufuta wa matokeo hayo ili yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011.
Habari ambazo NIPASHE imezipata jana na kuthibitishwa na
viongozi wandamizi wa wizara hiyo, kazi ya kufanya marekebisho ya matokeo hayo imeshakamilika na yatatangazwa wiki hii.
“Kazi ya kuandaa matokeo imekwishakamilika sababu ni kazi inayofanywa na watu watatu kwa kutumia kompyuta,” alisema ofisa mmoja ambaye alisema taarifa rasmi zitatolewa na Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.
AFANDE SELE AMSHUKURU MH. ZITTO KABWE KWA KUGHARAMIA VIDEO YAKE, HIKI NDO ALICHOKISEMA
Mapema asubuhi hii Mfalme wa Rhymes Afande Sele ametoa ya moyoni na kuelezea lengo lake la kutunga wimbo wa DINI TUMELETEWA kumrudisha Muafrika kwenye Uafrika na msingi wake wa UMOJA, USHIRIKIANO na UPENDO. Pia hakuwa nyuma kutoa shukrani zake kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe kwa kumuwezesha kugharamia Video ya wimbo wake huo mpya ambao unafanya vizuri sana kwa sasa.
Nanukuu "Lengo la hii kazi yangu mpya DINI TUMELETEWA ni kumrudisha mwafrika kwenye uafrika wake ambao msingi wake ni UMOJA, USHIRIKIANO NA UPENDO. Ambao kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia ukitoweka. Tumeona mapigano/mauaji ya itikadi za kidini wenyewe kwa wenyewe, pia kuelezea uhuru wa kuabudu kwa imani yoyote bila kuvunja sheria za Taifa letu. Kwa mtu yoyote makini mwenye mapenzi mema kwa Taifa letu na AFRIKA hawezi kupingana na hilo, kwa kutambua hilo MH; ZITTO ZUBERI KABWE(ZZK) kajitolea kugharamia gharama zote kwa ajili ya kufanikisha vidio bora kabisa ya wimbo huu, hii ni kazi yetu wote mimi na wewe, tunasema asante sana kwa Mh; Zitto. AMANI NA UPENDO KWANZA"
KIFAA CHA CHANJO YA UKIMWI CHAGUNDULIKA
'Ugunduzi huu ni ukombozi katika kuharakisha kupatikana kwa chanjo ya ugonjwa wa Ukimwi' Dk Seif Rashid
Dar es Salaam. Wanasayansi nchini Marekani wamebaini kifaa kipya kitakachoharakisha upatikanaji wa chanjo ya virusi vya Ukimwi (VVU).
Taarifa kwa Mwananchi Jumapili iliyotolewa Alhamisi wiki hii na Taasisi ya Tafiti Kukabiliana na Magonjwa ya Mzio na Kuambukiza (NIAID) ya nchini Marekani ilieleza kuwa mfumo wa kifaa hicho siyo tu utasaidia kurahisisha chanjo kukabiliana na VVU, bali hata kwa magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi kama mafua na yale yanayosababisha uvimbe wa ini.
“Ni mfumo wa hali ya juu wenye uwezo wa haraka wa kuchambua chembechembe kinga zenye uwezo wa kuangamiza aina mbalimbali za VVU zinazopatikana duniani,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliyoambatanisha majina ya wanasayansi nguli wa NIAID ambao wamethibitisha kifaa hicho chenye mfumo mpya katika teknolojia ya kuchambua VVU, umeweka wazi kuwa matatizo waliyokuwa wakipata wanasayansi katika kudhibiti virusi sasa imepata ufumbuzi.
Uzuri wa kifaa hicho unaelezwa kwamba ni kuweza kuchambua na kutofautisha chembe kinga za aina mbalimbali, hata kujua idadi na uwezo wake katika kushambulia adui katika mwili wa binadamu.
MSICHANA WA MIAKA 16 APIGWA RISASI BAADA YA KUKUTWA AKIVUNJA AMRI YA SITA NDANI YA GARI NA MWANAUME JIJINI DAR ES SAALAM
JESHI la polisi limekumbwa na kashfa nyingine baada ya askari wake kudaiwa kumpiga risasi msichana wa miaka 16 baada ya kumkuta akivunja amri ya sita ndani ya gari.
(Jina tunalihifadhi) alikumbana na mkasa huo Jumatano usiku eneo la Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam, ambapo alipigwa risasi sehemu ya makalio wakati akijaribu kuwakimbia polisi kwa kutumia gari la mpenzi wake.Mpenzi huyo (jina linahifadhiwa), alikamatwa na kuwekwa mahabusu na kufunguliwa kesi ya ubakaji.
Akizungumza na NIPASHE Jumapili jana katika wodi ya Hospitali ya Temeke alikolazwa, msichana huyo alisema siku ya tukio alikutana na kijana huyo majira ya saa 8:00 usiku katika baa moja inayoitwa Kindau na kukubaliana kwenda kushiriki tendo la ndoa kwa malipo ya Sh 20,000.
DHAMANA YA LWAKATARE LEO
Jopo la mawakili wanaomtetea Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare leo linaanza harakati za kumtoa mahabusu kwa dhamana.
Hatua hiyo inatokana na uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kumfutia Lwakatare mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yakimkabili yeye na mwenzake Joseph Ludovick Rwezaura, ambayo hayana dhamana na kubaki na shtaka moja la kula njama ambalo linadhaminika.
Kesi hiyo namba 6 ya mwaka 2013, inayosikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inatajwa leo, lakini mawakili wa Lwakatare wamejipanga kumwombea dhamana Lwakatare.
Mmoja wa mawakili wa Lwakatare, Peter Kibatala aliliambia Mwananchi jana kuwa kwa kuwa kosa lililobaki linadhaminika, basi jambo moja watakalolifanya leo ni kuwasilisha maombi ya dhamana.
Sunday, May 12, 2013
SCHOLES NAE ATANGAZA KUSTAAFU KUICHEZEA MAN UNITED
Wiki hii imeendelea kuwa mbaya kwa mashabiki wa Manchester United, siku chache baada ya Sir Alex Ferguson kutangaza kustaafu, leo hii kiungo wa timu hiyo Paul Scholes nae ameamua kumfuata kocha wake kwa kutundika daluga kuitumikia klabu yake pekee katika soka la kulipwa.
Gwiji huyo wa Manchester United mwanzoni alistaafu wakati wa mwisho mwa msimu wa 2010/2011, lakini akaamua kubadili maamuzi na kurejea kwenye timu mwezi January mwaka jana.
Katika taarifa yake Scholes, 38, alisema:Hatimaye ninatundika daluga zangu kabisa!
"Kucheza soka ndio ilikuwa kila kitu kwangu, na kuwa na na mafanikio kwa muda mrefu kwenye soka ndani ya Manchester United, chini ya meneja bora kabisa wa muda wote, ni heshima kubwa.
“Timu ipo kwenye hali nzuri na itaendelea kufanikiwa chini ya uongozi wa David Moyes.”
Scholes amecheza zaidi ya mechi 700 akiwa na jezi ya United na kesho atakusanya medali yake ya 11 ya kombe la premier league watakapocheza dhidi ya Swansea.
SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WACHOCHEZI WA KIDINI- WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
“Tunajua nia yao ni kufanya nchi isitawalike lakini sisi tumesema hatukubali. Tumekubaliana na Waziri wa Mambo ya Ndani, ulinzi uimarishwe kila mahali, mshingae kuona watu wanawahoji lakini nia njema, ya kurudisha amani yetu,” alisema Waziri Mkuu.
Ametoa kauli hiyo juzi mchana (Ijumaa, Mei 10, 2013) wakati akiwasilisha salamu za rambirambi kwa niaba ya Serikali wakati wa ibada ya mazishi ya waumini watatu wa Kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha waliofariki dunia kutokana na mlipuko wa mabomu uliotokea Jumapili iliyopita, Mei 5, mwaka huu kanisani hapo.
Waziri Mkuu amewaomba wanachi kutoka ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kutoa taarifa zozote zitakazosaidia kwenye upelelezi wa tukio hilo.
DIAMOND PLATNUM AFANYA JAMBO KUBWA UINGEREZA ,NA KUWA MSANII WA KWANZA BONGO KUUZA WIMBO UINGEREZA
WAKATI baadhi ya wasanii wakijitoa katika mikataba ya kuuza miito ya nyimbo zao kwenye Makampuni ya Simu, Msanii maafuru ndani na nje ya nchi Naseeb Abdul Diamond amekuwa msanii wa kwanza kupata mkataba wa kuuza nyimbo zake kwenye miito ya simu nchini Uingereza.
Diamond ambaye ndiye msanii pekee wa bongo fleva anaelipwa pesa nyingi nchini kutokana na mauzo ya nyimbo zake katika miito ya simu( caller tune), amesema kwamba miito hiyo ya simu itaongeza mauzo ya kazi zake na kwamba watanzania wanaoishi nchini humo pia watapata fulsa ya kusikiliza nyimbo zake kila wakati.
Mwanamuziki huyo wa Bongo Fleva amepata dili hilo kubwa la kuuza miito hiyo ya simu na kuwa msanii wa kwanza nchini kujipatia kitita kikubwa cha fedha kupitia nyimbo zake(caller tune) Nchini Uingereza.
Dili hilo limeonyesha kumfurahisha sana Diamond kwani tayari anaamini kuwa kazi anayoifanya ni nzuri na inaweza kusikilizwa na watanzania waishio Uingereza na Waingereza pia kwa kununua miito ya simu wakiwa nnchini humo.
Msanii huyo anajivunia suala hilo kwa sababu itawezesha watanzania waishio nchini Uingereza kupata nyimbo zake kwa wakati unaotakiwa tofauti na ilivyo sasa.
Diamond Platinum ambaye hivi karibuni alikumbwa na kashfa ya kudanganya umma kuwa mpenzi wake wa sasa ambaye ni mtangazaji wa Runinga katika kituo cha DTV Peniel Mungilwa 'Penny' ni mjamzito wa miezi mitatu alikuwa nchini humo kwa ziara ya kisanaa.
Hata hivyo mwana dada huyo alikanusha taarifa hizo na kudai kwamba hana ujauzito wa msanii huyo na kwamba hajawai kubeba ujauzito wake.
YANGA YATENGA MIL 50 KUMUUA MNYAMA MEI 18
Yanga
YANGA imeweka fungu la Sh.150 milioni mezani kuwapa motisha wachezaji wake iwapo wataifunga Simba Mei 18 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mgawo huo kila mchezaji atalamba shilingi milioni tano taslimu.
Hiyo ni kama advansi. Uongozi pia umetenga fungu jingine la Sh.100 milioni kwa ajili ya sherehe za Jangwani baada ya mechi ya Simba, kwenda Bungeni, Dodoma pamoja na Zanzibar.
Awali Yanga walikuwa wamewaahidi wachezaji wake zawadi ya Sh.100 milioni lakini jana Ijumaa Ibrahim Akilimali ambaye ni Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga alitamka kwamba wameongeza Sh. 50 milioni na kufanya ziwe Sh.150 milioni kwa timu tu.
Hiyo inamaanisha kwamba katika wachezaji 30 kwenye mgawo huo kila mmoja anakunja shilingi milioni tano na chenji chenji.
Akilimali alisisitiza kuwa fungu hilo litahusisha zawadi ya Sh. 70 milioni ya bingwa wa Bara.
Katika hatua nyingine, Yanga imeondoka jana Ijumaa kwa mafungu matatu kuelekea Pemba, Zanzibar kuweka kambi ya mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba ambao Kocha Ernest Brandts amesisitiza kuwa anataka mvua ya mabao.
Fungu la kwanza la wachezaji liliondoka asubuhi, la pili likaondoka jioni na la tatu litaondoka leo Jumamosi alfajiri. Kutoka Dar es Salaam mpaka Pemba kwa ndege ni mwendo usiozidi dakika 45. Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz
Awali Yanga walikuwa wamewaahidi wachezaji wake zawadi ya Sh.100 milioni lakini jana Ijumaa Ibrahim Akilimali ambaye ni Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga alitamka kwamba wameongeza Sh. 50 milioni na kufanya ziwe Sh.150 milioni kwa timu tu.
Hiyo inamaanisha kwamba katika wachezaji 30 kwenye mgawo huo kila mmoja anakunja shilingi milioni tano na chenji chenji.
Akilimali alisisitiza kuwa fungu hilo litahusisha zawadi ya Sh. 70 milioni ya bingwa wa Bara.
Katika hatua nyingine, Yanga imeondoka jana Ijumaa kwa mafungu matatu kuelekea Pemba, Zanzibar kuweka kambi ya mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba ambao Kocha Ernest Brandts amesisitiza kuwa anataka mvua ya mabao.
Fungu la kwanza la wachezaji liliondoka asubuhi, la pili likaondoka jioni na la tatu litaondoka leo Jumamosi alfajiri. Kutoka Dar es Salaam mpaka Pemba kwa ndege ni mwendo usiozidi dakika 45. Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz
Subscribe to:
Posts (Atom)