Friday, May 10, 2013
Prezzo kuhusu penzi la Diva: Bado mahari tu ipo njiani kutoka Mwanza
Apparently watangazaji wa kike wa Clouds FM humchanganya sana Rapcellency, Prezzo. Kama unakumbuka aliwahi kudai kuwa hasemi wala haongei kwa uzuri wa Dj Fetty.
Na sasa word on the street ni kwamba jicho la rapper huyo mwenye asili ya Kenya na Tanzania limetua kwa mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho, Loveness Diva. Wiki iliyopita, Diva alimwalika Prezzo kwenye show yake na huenda ukaribu huo uliongezeka zaidi siku hiyo.
Kwa mujibu wa You Heard ya Clouds FM, Diva na Prezzo ni item.
“Diva siwezi kumwachia bwana, nimwachie nichekwe,” alisema Prezzo.
“Bado mahari tu mshkaji wangu inatoka kutoka Mwanza. Only time can tell, nikikuambia sasa hivi ukweli wangu ntamaliza uhondo. Inaitwa yaani love at first sight, Diva mwenyewe umeshamwona, she is classy yaani she is beautiful,” alisisitiza Prezzo ambaye jina lake ni Jackson Makini.
Hata hivyo Diva amekanusha kwa kudai kuwa yeye na Prezzo ni marafiki tu.
KOCHA WA EVERTON DAVID MOYES ATANGAZWA KURITHI MIKOBA YA SIR ALEX FERGUSON MAN U
Kocha wa Klbau ya Everton, David Moyes, leo mchana ametangazwa rasmi kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson, aliyetangaza kujiuzulu jana, ambapo sasa kocha huyo atakua na kibarua cha mkataba wa miaka 6, ya kuinoa timu hiyo ya Mashetani wekundu.
Moyes, amesaini kataba wa miaka sita leo mchana na kutangazwa rasmi kukabidhiwa mikoba hiyo, ya Ferguson, aliyeitumikia Klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 27 na kuipa mataji 20.
Akizungumza wakati wa mahojiano na waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba huo, Moyes, alisema kuwa anatarajia kujiunga na wekundu hao mara tu utakapomalizika rasmi msimu huu wa Ligi ya England.
Wakati hayo yakijiri, Kuna habari zilizochini ya Kapeti hadi sasa kuwa huenda, katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya England, Timu hito ya Man U, ikamkosa mshambuliaji wake, Wyne Rooney anayetarajia kutimka katika Kikosi hicho na badala yake sasa anayetarajia kujiunga kwa mara ya pili na kikosi hicho ni aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, ambaye kwa sasa anakipiga na Klabu ya Real Madri, Christiano Ronaldo.
Thursday, May 09, 2013
UWOYA AJISAFISHA KUPITIA JINA LA RAISI, SOMA ALICHOKISEMA HAPA
Irene Uwoya.
STAA wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya haachi vituko, safari hii ameibuka na kujisafisha kupitia Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza akidai kuwa yeye na tasnia nzima ya sinema za Kibongo hawana tabia za hovyo bali Magazeti Pendwa ndiyo yanasababisha waonekana hivyo.
Pamoja na skendo nyingine, Uwoya hivi karibuni alinaswa kwenye mtego baada ya kuingia kwenye kumi na nane za kamera za mapaparazi wa Global Publishers akiwa na kinda la muziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul ‘Diamond’ wakiingia katika hoteli moja jijini Dar usiku mnene na kutoka mchana wa siku iliyofuata. Akizungumza hivi karibuni kupitia runinga moja jijini Dar es Salaam, Uwoya alijitetea kwamba sanaa ya filamu za Kibongo ni safi na kwamba magazeti ndiyo yanayowaharibia sifa.
“Mfano mimi, kama ningekuwa mchafu ningeitwa na rais wa Burundi kwenda ikulu? Ameniona mimi ni msafi ndiyo maana aliniita mwaka 2011 kupitia sanaa yangu. Tungekuwa wachafu tusingekubalika hadi na viongozi wakubwa wa nchi, tatizo ni magazeti,” alisema Uwoya akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho, aliyetaka kujua kuhusu madai ya wasanii kuwa na tabia chafu.
Uwoya ni kama alikuwa akikwepa hoja ya msingi na kuyatupia lawama Magazeti Pendwa kwa kuegemea mgongo wa Rais Nkurunzinza, kwa sababu rekodi za skendo zake zipo na yeye mwenyewe anazijua – Mhariri
BAHATI BUKUKU APATA MCHUMBA
Mwimbaji wa Muziki wa Injili Bahati Lusako Bukuku.
MWIMBAJI wa Muziki wa Injili mwenye muonekano wa ‘mama mwenye ndoa’, Bahati Lusako Bukuku amefunguka kuwa amepata mchumba lakini tatizo linabaki kuwa mume wake wa zamani, Daniel Basila ambaye anasuasua kumpa talaka yake, Amani lina mkoba mkononi.
Akizungumza na ‘balozi’ wetu jijini Dar juzikati, staa huyo anayetamba na wimbo wake wa Dunia
Akizungumza na ‘balozi’ wetu jijini Dar juzikati, staa huyo anayetamba na wimbo wake wa Dunia
Haina Huruma aliweka ‘pleini’ kwamba hivi karibuni Mungu amemjalia kupata mchumba ambaye anahofia kumwanika kwa kuwa anabanwa na kifungo cha ndoa yake ya kwanza aliyofunga na Basila.
Bahati alisema kuwa kifuatacho inabidi adai talaka yake kwa nguvu zote hata ikiwezekana kufikishana polisi ili aondokane na kifungo cha ndoa hiyo na aanze mipango ya ndoa kwa kuwa hataki kumtendea Mungu dhambi.
Alisema kuwa, mara nyingi amekuwa akimkumbusha mumewe huyo wa zamani kuhusu talaka lakini amekuwa akimwambia asikonde talaka yake ipo hivyo avute subira.
Bukuku aliolewa na Daniel na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye alifariki dunia mwaka 2006 kabla staa huyo kutengana na mumewe.
Bukuku aliolewa na Daniel na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye alifariki dunia mwaka 2006 kabla staa huyo kutengana na mumewe.
CHANZO CHA HABARI NI MTANDAO WA GLOBAL PUBLISHERS
KIOJA CHA MWAKA 2013...MWANAUME KWA MWANAUME WAFUMWA LAIVU GEST..Angalia PICHA
Aibu hiyo ya mwaka ambayo ilionekana pia kama kituko ilijiri Mei 3, mwaka huu ndani ya gesti moja maarufu iliyopo Devi’s Corner –Tandika, jijini Dar es Salaam.
Breaking Newzzzzzzzz......!!! SHEIKH PONDA AHUKUMIWA MWAKA MMOJA
Hukumu ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda imetolewa leo katika mahakama ya kisutu jijini dar es salaam ampapo kahukumiwa kifungo cha nje mwaka mmoja.
HUYU NDIE KIJANA ALIYEMKAMATA MLIPUA BOMU KANISANI ANENA MAZITO, SOMA ALICHOKISEMA HAPA
Kijana aliyemkimbiza hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha akiwaelezea wananchi ilivyokuwa.
ALIYEMKIMBIZA hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha Jumapili iliyopita na kuua watu 3 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ameibuka.
Kijana huyo ambaye wakati akizungumza na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari jijini Arusha juzi alisahau kutaja jina lake, alisema kuwa shughuli ya kumnasa mtuhumiwa huyo haikuwa lelemama hata kidogo.Alisema siku ya tukio baada ya bomu hilo kulipuliwa kanisani hapo, yeye alimwona mlipuaji huyo hivyo akaungana na watu wengine kumkimbiza.
“Mtuhumiwa alikuwa akikimbia ujue, sisi tulimkimbiza bila kuogopa kama ana mabomu mengine kwenye mfuko. Alipoona hatukati tamaa, alifika kwenye shamba la miwa akajilaza, lakini mbwa waliokuwa na sisi walitusaidia sana,” alisema shujaa huyo.
Aliendelea kusema kuwa walipomdaka mtuhumiwa huyo walimkuta na mfuko wa rambo, walipochungulia ndani yake walishtuka, kumbe alikuwa na mabomu yaliyosalia!
Hata hivyo, alisema yeye na mabomu yake hawakumwachia na dakika chache wananchi wenye hasira kali walifika eneo hilo wakiwa na silaha za jadi wakitaka kumuua ndipo polisi walipofika eneo hilo na kumchukua mtuhumiwa huyo kwenda naye kituoni.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kijana huyo amekuwa staa ghafla, hivyo wakaitaka serikali kumfikiria kwani ameonesha kitendo cha kishujaa.
“Huyu kijana amekuwa staa ghafla aisee, kitendo alichokifanya ni cha kishujaa, si rahisi, serikali ingemfikiria kwa lolote,” alisema mtu mmoja aliyejiita Massawe na kuungwa mkono na wenzake.
DIAMOND ALIWA DENDA KILAZIMA JUKWAANI..........!!!
EEHH!!! jamani kina dada mbona mnajidhalilisha kiasi hicho!! ni pombe ulilewa au kitu gani!?? au ndio mambo ya NATAKA KULEWA hayo ukaamua ummwagie radhi mtoto wa mwenzio kilazima, au huna habari KAMA MCHUMBA WA MTU HUYO DADA!!?? mmmh!! WATOTO WA UK MMETISHA!!!
ALAFU nimesikia kuna mdada kaenda kulala na dancer wa DIAMOND akizani ni DIAMOND MWENYEWE biatchhh! yereeeuwiiiiiiii!!!!!!
tunaendelea kuifatilia kwa ukaribu tutawaletea picha kamili sooooon!!!
HUYU NDIYE ANAYETARAJIWA KUWA MRITHI WA MIKOBA YA SIR ALEX FERGUSON PALE OLD TRAFFORD
NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA KWA MWAKA 2012/2013
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, alitangaza nafasi za ajira kwa Wataalam wa Kada za Afya kwa mwaka 2012/2013 ambapo tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi hayo ilikuwa tarehe 10 Mei, 2013. Kwa tangazo hili Wananchi wanajulishwa kuwa muda wa kuwasilisha maombi hayo umeongezwa hadi tarehe 20 Mei, 2013. Aidha inasisitizwa kuwa hata wahitimu wa mwaka 2012 wanapaswa kutuma maombi yao kwa sababu hakutakuwa na utaratibu wa wahitimu kupangiwa vituo vya kazi moja kwa moja.Maombi hayo yaendelee kuwasilishwa kwa njia ya Posta kwa kutumia anuani iliyopo chini ya tangazohili.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
KAIMU KATIBU MKUU,
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII,
S.L.P. 9083,
DAR ES SALAAM.
HakiElimu YAKATAA KUFUTA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE.
SERIKALI imetakiwa kuacha kukurupuka kufuta matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 kutokana na sababu za msingi za kufeli kwa wanafunzi hao zinafahamika.
Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam na muungano wa asasi tano za kiraia uliowakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Elizabeth Missokia.
Kwa niaba ya mitandao hiyo mkurugenzi huyo alisema hakukuwa na haja ya kufuta matokeo hayo na kufanya maboresho kwa kuwa sababu zilizosababisha kufeli kwa wanafunzi zinajulikana na si kama serikali inavyodai kwa sasa.
Missokia alisema kabla ya serikali kutoa uamuzi huo ilitakiwa kuweka wazi mapendekezo ya Tume ya Waziri Mkuu iliyoundwa kuchunguza matokeo hayo ili wadau wa elimu wapate fursa ya kuona sababu zilizochangia kushuka kwa ufaulu katika mitihani hiyo.
“Kwa kufuta matokeo hayo bila wadau kujua sababu na kutoa mchango wao inawaaminisha Watanzania kwamba sababu nyingine hata kama zipo ziliathiri kwa kiwango kidogo matokeo hayo na suala la upangaji wa madaraja kuonekana ni sababu kubwa zaidi kuliko nyingine,” alisema Missokia.
RATIBA YA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA HII HAPA.
KLABU ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambayo inajivunia washambuliaji wawili wa Kitanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu itamenyana na Liga Maculmana ya Msumbiji kuwania tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Hiyo inafuatia upangwaji wa droo ya hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo, inayodhaminiwa na Orange mjini Cairo, Misri leo. Katika droo hiyo, AS FAR Rabat ya Morocco iliyoitoa Azam FC katika Kombe la Shirikisho imepangwa kukutana na wapinzani wao, FUS Rabat. Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani aliongoza droo hiyo kwa pamoja na wawakilishi wa baadhi ya klabu zinazoshiriki michuano hiyo.
Klabu nane zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa, St George, CA Bizerte, TP Mazembe, Enugu Rangers, JSM Bejaia, FUS Rabat, Stade Malien na Entente Setif zimeingia kwenye mbio za kuwania kurithi taji la AC Leopards ya Kongo, mabingwa wa Kombe la Shirikisho na mechi za kwanza zitachezwa kati ya Mei 17, 18 na 19 mwaka huu wakati marudiano yatakuwa kati ya Mei 31 , Juni 1 na 2. Mazembe ambao ni mabingwa mara nne Afrika, walitolewa na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika Raundi ya Tatu ya Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 3-2, wakifungwa 3-1 Afrika Kusini na kushinda 1-0 nyumbani.
DROO KAMILI YA 16 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO:
Stade Malien (Mali) vs Lydia (Burundi)
Enugu Rangers ( Nigeria) vs C.S.S (Tunisia)
FUS Rabat ( Morocco) vs ASFAR (Morocco)
CAB (Tunisia) vs Ismailia (Misri)
E.S Setif ( Algeria) vs US Bitam (Gabon)
JSM Bejaia ( Algeria) vs E.S.S (Tunisia)
TP Mazembe (DRC) vs Liga Maculmana (Msumbiji)
St George (Ethiopia) vs ENPPI (Misri)
DROO KAMILI YA 16 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO:
Stade Malien (Mali) vs Lydia (Burundi)
Enugu Rangers ( Nigeria) vs C.S.S (Tunisia)
FUS Rabat ( Morocco) vs ASFAR (Morocco)
CAB (Tunisia) vs Ismailia (Misri)
E.S Setif ( Algeria) vs US Bitam (Gabon)
JSM Bejaia ( Algeria) vs E.S.S (Tunisia)
TP Mazembe (DRC) vs Liga Maculmana (Msumbiji)
St George (Ethiopia) vs ENPPI (Misri)
Subscribe to:
Posts (Atom)