Mkali wa miondoko ya bongo fleva anatamba na ngoma yake kali
aliyomshirikisha OMMY DIMPOZI chukua tyme SUMA MNAZALETI ameyasema
maneno hayo leo kwa njia ya masseji Alisema'' ebana nadhani unajua nini
kinaendelea kuhusu lady jaydee! nachukua nafasi hii we kaka yangu ambaye
umenisaidia sana kwa mda mrefu kukujulisha kuwa mdogo wako,Nitakuwa
msanii miongoni mwa wasanii wanao support maneno ya lady jay dee
Nakwambia haya kwasababu najua umenisaidia sana,but kama baada ya haya
utaamua kuona sifai sio tatizo pia! no interview 4 NOW Nilikuwa nakupa
habari kama ndugu yangu wa karibu. lakini kama hili unaliunga mkono
sio mbaya ukinijulisha kwamba hakuna tatizo na unaendelea kusaport kazi
zangu. alimaliza kwakuandika jina lake suma mnazaleti.
Monday, May 06, 2013
CUF: SPIKA MAKINDA HAIFAI.
WADAI ANA
UWEZO MDOGO WA KUONGOZA.
Mwenyekiti wa TAIFA wa
Chama Cha Wananchi –CUF Profesa Ibrahim Lipumba.
Spika wa Bunge,Anne
Makinda.
Profesa Lipumba amemtaka Makinda atafakari na apime uwezo wake wa kiuongozi katika Bunge na afanye maamuzi magumu ya kubadilika kifikra kwa kuacha upendeleo anaoufanya kwa sasa.
Kauli hiyo aliitoa juzi jijini Mwanza alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima, muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa kujadili na kuchangia mawazo juu ya maendeleo kwa wote mkoa wa Mwanza, uliofanyika katika Hoteli ya JB Belmont.
Alisema Spika amejionyesha uwezo wake mdogo wa kuongoza Bunge na akubali kushau
riwa au kubadilika kifikra ili alinusuru Bunge lisiendelee kudharaulika ndani na nje ya nchi.
JACQUILINE WOLPER ATUPIWA VIRAGO VYAKE NJE BAADA YA KUSHINDWA KULIPA KODI YA NYUMBA.....!!
STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper
Massawe anadaiwa kutupiwa nje na baadaye kuzuiliwa vyombo vyake kwenye
ile nyumba ya kifahari ya kupanga aliyokuwa akiishi Mbezi Beach, Dar es
salaam.
Madai hayo yalitua kwenye dawati la Ijumaa Wikienda hivi karibuni ambapo ilielezwa kuwa ishu hiyo ilijiri maeneo hayo baada ya bishosti huyo kudaiwa kuwa alishindwa kulipa kodi ya pango ya mwezi mmoja ambayo ni Dola 1,500 (zaidi ya Sh. milioni 2.4 za madafu).
Kwa mujibu wa ‘sosi’ wetu aliyekuwepo eneo la tukio, Wolper aliwatuma ndugu zake kwenda kuchukua vyombo hivyo lakini walipofika mama mwenye nyumba (jina tunalo), aliwazuia na kumpigia simu staa huyo akimwambia kuwa anatakiwa kulipa fedha kabla ya kuchukua vitu vyake.

“Wolper alipopigiwa simu
alikuja juu na kumwambia mama mwenye nyumba kuwa kama anamfuatilia eti
atamfunga kama mume wa mama huyo alivyofungwa na kumwambia kuwa
atampelekea polisi wakamkamate,” alidai mtu huyo.
Sosi huyo aliendelea kudai kuwa baada ya kuona soo limekuwa la kutishana, mama huyo alikwenda kumfuata mjumbe wa nyumba kumi aliyefahamika kwa jina moja la Musa na kumueleza kisha kumuomba asimamie zoezi hilo.
Baada ya kujazwa data hizo, Ijumaa Wikienda lilifanya jitihada za kumsaka Wolper na alipopatikana alisema kuwa hajawahi kudaiwa na huyo mama na anayesema hivyo huenda alimuona wakati anahamisha vitu vyake kwani kwa sasa amehama kwenye nyumba hiyo.
Mwandishi wetu hakuishia hapo, alimtafuta shemeji wa mama mwenye nyumba aliyetajwa kwa jina moja la Jamal ambaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo na kwamba suala hilo lilimalizika ambapo vyombo vya Wolper vilitolewa kwa ajili ya kufanya usafi kwani kuna mtu mwingine alikuwa akihamia.
Mjumbe wa Nyumba Kumi, Musa alipotafutwa kwenye simu yake ya kiganjani ili kuzungumzia sakata hilo alikiri kufikishiwa malalamiko ya Wolper.
Alisema kuwa msanii huyo alikuwa hajamaliza kulipa fedha, akawatuma ndugu zake wakachukue vitu vyake lakini kabla hawajavichukua mama mwenye nyumba aliwazuia mpaka alipwe chake na alipotimiza hilo ndipo akaachiwa vitu vyake.

BIFU LA JAYDEE NA CLOUDS SASA LAFIKIA PABAYA, RUGE AAMURU CLOUDS KUTOPIGWA NYIMBO YOYOTE YA BONGOFLEVA.......
Akizungumza kupitia kipindi cha Power
Breakfast, Meneja wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ameelezea
yafuatayo kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na msanii Judith Wambura
‘Lady Jaydee’ wiki iliyopita:
Asema vita ya Lady Jaydee ameielekeza sehemu isiyo sahii kama tatizo ni Bendi ya SkyLight basi apambane kuipiku bendi hiyo na si kugombana na watu wengine.
Awaasa wasanii kukubali kupokezana vijiti na kujiandaa kwa maisha yajayo
Aelezea Clouds ilipomtoa Jaydee mpaka sasa alipo. Aaamua siku ya leo kutopigwa muziki wa Bongo Flava
Asema kuwa Clouds ni chombo binafsi kina maamuzi ya kufanya chochote pasipo kuvunja sheria
Asema siyo vizuri watu kuchafuana katika mitandao ya kijamii, kama kuna tatizo ni vyema kuonana na muhusika ili kumaliza tatizo
Awaasa wasanii kukabiliana na changamoto na si kuziona kuwa ni tatizo

ANGALIA PICHA ZA TUKIO ZIMA LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI HUKO ARUSHA
Hali ya eneo mlipuko ulipotokea
Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea
Ulinzi umeimarishwa
Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio
Sunday, May 05, 2013
RPC ARUSHA ATHIBITISHA KUWA KILICHOLIPUA KANISA NI BOMU....WATU 3 WANAHALI MBAYA, 50 WAMEJERUHIWA...!!
Mkuu wa Mkoa
Mulongo naye amefika eneo la tukio na kuwafariji wahanga wa
tukio la bomu....
RPC wa mkoa wa Arusha naye aliambatana na mkuu wa
mkoa na muda huu alikuwa anatoa nasaha zake kwa wananchi....
RPC amesema tukio hili ni la kigaidi. Amesema kuwa
aliyehusika alijitokeza nyuma ya jengo kwa kujificha na kurusha bomu.
...
Amesema kuwa Polisi
wanawasaka waliohusika na unyama huu na ameomba yeyote mwenye
taarifa yoyote aisaide polisi. ..
Waliojeruhiwa
ni 50 .Hao wana majeraha ya kawaida na 3 wako mahututi
Mpaka sasa mtu mmoja anashikiliwa na polisi kwa mahojiano
zaidi
"WAZIRI WA ELIMU AKAMATWE NA ASHITAKIWE"... MBATIA
Baada ya
Serikali kutoa kauli kuhusu mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka
jana, Mbunge James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ametaka Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, awajibike na ikiwezekana
akamatwe na kushitakiwa.
Kauli hiyo aliitoa jana kwa waandishi wa
habari akisema kuvurugika kwa utaratibu kutokana na kuanzisha utaratibu
mpya wa usahihishaji na kutoa alama bila kushirikisha wadau, unamgusa
Waziri ambaye ndiye mwenye dhamana.
Alisema watu wa Baraza la Taifa la Mitihani
(NECTA) hawawezi kufanya uamuzi bila kujulikana na watu wengine wa juu
akiwamo Waziri na kusababisha wanafunzi wengi kufeli mitihani ya
kidato cha nne mwaka jana.
Aidha, Mbatia alisema kwa mantiki na falsafa
ya utendaji haiwezekani utaratibu huo ukakosa baraka za Waziri wa
Elimu.“Si kujiuzulu tu kuna watu wanatakiwa wakamatwe na kushitakiwa
kwa kosa hili, kwa kuwa limefanyika kwa makusudi…limetengenezwa,
halikutokea kwa bahati mbaya,” alisema.
Mbatia ambaye alifuatana na Mbunge wa Kasulu
Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), alisema Dk Kawambwa alitakiwa kwa
ripoti ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, asionekane hadharani kwa
sababu ni aibu kwake.
MFANYA BIASHARA ALIYEJIRUSHA TOKA GOROFA YA TISA AFARIKI DUNIA
TAARIFA
za awali zina arifu kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima anaedaiwa
kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo
Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa alikuwa asafiri na ndege ya saa 10
jioni kuelekea China kufuata bidhaa za maduka yake.
Shirima
(47), ambaye amefikwa na umauti muda mfupi baada ya kudondoka chini ni
mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina mama yaliyopo jirani na Hoteli hiyo ya Concord.
Aidha
taarifa hizo za awali kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye alidai
kuwa si msemaji wa familia ya Shirima ya Mwika Moshi mkoani Kilimanjaro,
nikuwa Marehemu mara kwamara alikuwa akipendelea kula katika hoteli
hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa anapanda juu ya
Hoteli hiyo kupunga upepo baada ya kuhisi hewa nzito mahali alipokuwa.
Inadaiwa
kuwa baada ya kupanda huko juu ghafla alianguka chini na kudondokea
gari dogo aina ya Toyota Corola linalofanya biashara ya Taxi na kupoteza
maisha yake na gari hilo kuharibika vibaya kutokana na kishindo hicho.
Marehemu
Shirima mbali na kuwa Mfanya Biashara wa muda mrefu Kariakoo pia
alikuwa akiendelea na Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya Kariakoo.
Marehemu ameacha Mjane na watoto 5.
Uchunguzi wa Kipolisi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na taarifa kamili zitatolewa pindi zitakapo kamilika
Mfanya
biashara huyu mkazi wa Dar es salaam mzaliwa wa Moshi kilimanjaro
alikutwa na mauti hayo baada ya kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya
hoteli hiyo ambayo alienda kwa lengo la kuuona ukumbi wa tukio hilo
ambao uko gorofa ya tisa ya hoteli hiyo.
Chanzo Cha Mfanyabiashara huyu kujirusha bado hakijafahamika mpaka sasa.
Taratibu za Mazishi ya Marehemu Zinapangwa jijini dar es salaam na tukizipata tutakuhabarisha mapema.
Ndugu Costa shirima ameacha mke na watoto.
Mungu ailaze roho ya marehemu Mahali Pema Peponi
Amina
LINA NA BARNABA WAIKACHA SHOW YA MIAKA 13 YA LADY JAY DEE.
Linah
na Barnaba wameiambia Bongo5 kuwa hawatakuwepo kwenye show ya miaka 13
ya muziki ya Lady Jaydee itakayofanyika May 31, kwa kile walichodai ni
kutoafikiana kwenye malipo.
Wamesema licha ya kuendelea kuwepo kwa majina yao kwenye poster ya show hiyo, hawatotumbuiza siku hiyo.
“Dada
yetu alituita, akatuambia kwamba ana kazi yake ya kutumiza miaka 13
kwahiyo akawa anasema anahitaji wasanii ambao watamsupport kwaajili ya
kufanya show,” amesema Linah. “Sisi tulifuata protocol zote
kwasababu kama wasanii tuna viongozi, tukafuata protocol zote kuweza
kukubaliana naye mpaka tukafikia hatua kwenye masuala ya biashara,
yaani malipo. Kwenye upande huo kidogo tukawa tumepishana, kwenye
upande wa masuala ya maslahi. Lakini sasa tunashangaa yeye kuanza
kuweka posters.”
Kwa
upande wake Barnaba amesema hawajashindwana na Lady Jaydee lakini wao
kama wasanii wana menejementi na matakwa ya ofisi zao na hivyo muafaka
ulishindwa kufikiwa na pia walikuwa na booking zingine.
Hata
hivyo Barnaba amesema hakuna ugomvi wowote baina yao na Lady Jaydee.
“Tuko safi tu na dada, mbona tuliafikiana vizuri tu na tuko kwenye
maongezi mazuri tu, tulishaongea na hili suala liko vizuri,” amesema
Barnaba.
source-zeddylicious
PENZI LA WEMA LAMTESA PREZZO..........!!!
Wema akiwa kwenye pozi la kimahaba na msanii wa Kenya PrezoDar es Salaam, Tanzania
BAADA
ya uvumi kwamba msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Kenya Prezo kuzama
kwenye mahaba mazito na msanii wa filamu nchini Tanzania Wema Sepetu,
Msanii huyo ameshikwa na kigugumizi na kushindwa kukanusha tuhuma hizo.
Prezo ambaye alifiwa na mchumba wake ambaye pia alikuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Nigeria marehemu Goldie Harvey, aliyefariki dunia February mwaka huu, juzi alishindwa kudhibitisha tuhuma hizo baada ya kuulizwa swali na kushindwa kulijibu.
Prezo ambaye yuko nchini kwa ziara ya muziki alionekana katika picha za mahaba akiwa na Wema Sepetu, hata hivyo Wema aliwahi kukanusha picha hizo na kudai kwamba walipiga wakati walipokuwa wakirekodi filamu mpya ya Wema na kwamba hana mahusiano yoyote ya mapenzi na msanii huyo.
Akiwa
katika mahojiano maalum kwenye kipindi cha mapenzi kilichorushwa usiku
na Redio Clouds FM Prezo alishikwa na kwi kwi cha gafla baada ya
kutakiwa kudhibitisha juu ya uvumi kwamba amenasa kwenye mahaba mazito
na mrembo huyo mwenye skendo za kubadilisha wanaume kila kukicha.
MWANAUME AKIKOSA MTOTO HUPATA HUZUNI ZAIDI KULIKO MWANAMKE
Tofauti na mazoea na mtazamo wa wengi kwamba mwanamke ndiye anayeumia zaidi akikosa mtoto, wataalamu wamegundua kuwa anayeumia zaidi kwa kukosa mtoto ni mwanamume.
Utafiti huo umeonyesha kuwa wanaume wanahitaji mtoto sawa sawa na wanavyohitaji wanawake, lakini wao wanaumia zaidi wanapokosa bahati ya kupata mtoto.
Wataalamu
hao wamebaini kuwa sababu kubwa zinazowafanya wanaume wajisikie vibaya
zaidi wanapokosa watoto ni tamaduni za toka enzi kuwa wao wanaweza kila
kitu na msukumo wa familia.
Tofauti
na wanawake, ambao wanahitaji mtoto kwa ajili yao binafsi kwa asili ya
kuumbwa kwao, hali ambayo kitaalamu inajulikana kama ‘biological urge’.
Taarifa
za utafiti huo ulioongozwa na Robin Hadley, wa Chuo Kikuu cha Keele,
ukishirikisha wanaume 27 na wanawake 81, ambao hawajapata mtoto,
uliwasilishwa mbele ya Wanasaikolojia wa Taasisi ya British Sociological
Association, ya Uingereza.
Saturday, May 04, 2013
SAKATA LA PADRI ALIYENASWA NA MKE WA MTU..... MAPYA YAIBUKA BAADA YA MUME KULIPONDA KANISA KATOLIKI....!!
LILE saga la madai ya fumanizi la Padri Urbanus Ngowi aliyekuwa akihudumu katika Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishiwa Makomu, Marangu limeibua mtikisiko mkubwa kwa Kanisa Katoliki nchini, .
KWANI ILIKUWAJE?
Katika habari iliyofichuliwa , Aprili 29 hadi Mei 5, mwaka huu, ilidaiwa kuwa Father Ngowi alinaswa chumbani akiwa na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la kijamii la Mama P.
Katika habari iliyofichuliwa , Aprili 29 hadi Mei 5, mwaka huu, ilidaiwa kuwa Father Ngowi alinaswa chumbani akiwa na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la kijamii la Mama P.
Mara baada ya ‘mzigo’ huo kuingia mitaani nchi nzima, mhariri wa gazeti hilo (jina linahifadhiwa) alianza kupokea simu na ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kutoka kona mbalimbali kwa watu waliojitambulisha kuwa ni waumini wa kanisa hilo wakidai kushtushwa na tukio hilo.
VIKAO VIZITO
Habari za ndani kutoka Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi zilieleza kuwa baada ya ishu kuwa ‘hoti’, viongozi wa jimboni hapo, Jumatatu iliyopita walikaa vikao vizito kulijadili suala hilo na kulitolea uamuzi.
Ilidaiwa kuwa uongozi ulikubaliana kumwita mume wa Mama P ambaye wakati tukio hilo likitokea alikuwa jijini Dar es Salaam kwa shughuli zake binafsi.
Ilisemekana kuwa waliwasiliana na mwanaume huyo ambaye alitakiwa kuondoka Dar, Alhamisi iliyopita kwenda Moshi kukutana na viongozi hao kwa lengo la kuweka mambo sawa.
Ilidaiwa kuwa jamaa huyo ambaye amezaa na Mama P watoto wawili, alikubali kukutana na viongozi hao kwa shingo upande huku akitishia kulipeleka suala hilo mbele zaidi kwa kuwa alishalalamika muda mrefu kwamba Father Ngowi ana ukaribu wenye maswali mengi na mkewe.Tulitonywa kuwa baada ya mwenye mke huyo kulalama sana, Father Ngowi aliitwa na uongozi wa jimbo hilo kisha akaonywa lakini hakuna kilichobadilika.

Subscribe to:
Posts (Atom)