Friday, April 19, 2013
Thursday, April 18, 2013
Barua zilizotumwa kwa rais Obama zagundulika kuwa na sumu aina ya ricin.
Barua
zilizokuwa zimetumwa kwa Rais Barack Obama na Seneta wa Mississippi
Senator Roger Wicker zmebainika kuwa na sumu hatari aina ya ricin.
Idara
kuu ya upelelezi ya Marekani FBI imetoa taarifa hiyo na barua
zilizotumwa kwa viongozi hao wawili zinahusiana.
Barua
hizo zote zilitumwa kutokea Memphis, Tennessee na mtu mmoja mwenye umri
wa miaka 45 amekamatwa Mississippi kuhusiana na barua hizo.
Pamoja
na barua hizo, polisi mjini Washington wanavichunguza vifurushi vitatu
wanavyovitilia mashaka vilivyogunduliwa katika ofisi za majengo ya
seneti.
Kugunduliwa
kwa vifurushi hivyo kwenye eneo kubwa la majengo ya ser
AUNTY EZEKIEL: WABUNGE BAADA YA MATUSI BUNGENI SASA WANATAKA KUVUNJA AMRI YA 6!!
DIVA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel ameinua kinywa
chake na kudai kwamba
kuna baadhi ya
wabunge wamekuwa wakimtongoza kwa nia ya kupata penzi kwake,
Akizungumza na mwandishi wa habari hii juzi jijini Dar,
Aunt alisema waheshimiwa hao
wanajua
tayari yeye ameshaolewa lakini wamekuwa wakimpa usumbufu mkubwa na
kutoa ahadi balimbali, ndogo na kubwa kitendo ambacho
anaamini kinaweza
kuhatarisha ndoa
yake.
"Mimi nawashangaa sana baadhi ya waheshimiwa, wanajua
tayari nimeolewa lakini
wananitongoza,
mimi siwezi,” alisema Aunt bila kuwataja majina wazito hao Akaongeza:
“Mume wangu akisikia napata usumbufu kutoka kwa watu
wazito, hawezi kuwa na
amani, bado
naipenda ndoa yangu na kuachana na Sunday wangu ni ndoto.”
Mwishoni mwa mwaka jana, Aunt alifunga ndoa na
mfanyabiashara Sunday Dimonte,
Dubai
na mpaka sasa wanaishi kama mke na mume
SOURCE: GPL
HALI NI MBAYA SANA BUNGENI
Wabunge watano wa Chadema
jana walitimuliwa bungeni na kuamriwa kukaa nje ya Bunge kwa siku tano
kutokana na vurugu zilizotokea jana usiku.Wabunge hao ni Lissu,
Hezekiah Wenje (Nyamagana), Highness Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi
(Mbeya Mjini) Godbless Lema (Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa
(Iringa Mjini).
Chanzo za kufukuzwa kwao ni
kuwazuia askari wa Bunge kumtoa nje Lissu ambaye alikuwa ameamriwa
kutoka nje na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kuingilia hotuba ya
Mbunge wa Iramba Mashariki,
Mwigulu Nchemba.
Kutokana na tafrani hiyo,
Nchemba hakuweza kuhitimisha hotuba yake hivyo Ndugai alilazimika
kukatisha mkutano wa Bunge.Hata hivyo wakati akiahirisha mkutano huo,
tayari wabunge hao walikuwa wameshatolewa nje baada ya askari
kuongezwa.
Mapema Mbunge wa Kigoma
Mjini (CCM), Peter Serukamba alitoa tusi zito la nguoni wakati wa
hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, licha ya Spika wa Bunge, Anne Makinda
kupiga mkwara wa kuwashughulikia wabunge watakaorusha matusi.
MAJIRANI WALAMZIMISHA LIONEL MESSI KUNUNUA NYUMBA ZAO BAADA YA KUFULIA
Mwanasoka bora wa dunia Lionel Messi,
hivi karibuni alilazimika kununua nyumba za majirani wanaoizunguka
nyumba huko Barcelona Hispania bila kupenda.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka SportsGrid
ni kwamba majirani wa Messi
walikuwa wanazifanyia marekebisho nyumba zao, lakini kwa bahati mbaya
wakaishiwa na fedha katikati ya marekebisho hayo huko mjini
Castelldefels, Spain, hivyo wakamuomba kijana tajiri Messi azinunue
nyumba hizo zilizokuwa kwenye marekebisho na kwa utaratibu Messi
akakataa.
Baada ya ombi lao kukataliwa majirani
wakaamua kuanza kufanya vitimbi ili Messi aone kero na kuamua kununua
nyumba zao, walizikodisha nyumba zao na wapangaji wao wakawa watu wa
fujo wenye makelele muda wote na hatimaye vitimbi hivyo vikazidi kuwa
kero kwa Baba Thiago na familia yake. Mara ya kwanza Messi alienda
kuongea nao waache tabia hizo lakini hali haikubadilika hivyo akaamua
kujenga ukuta mrefu wa kuitenganisha nyumba take na majirani - lakini
jaribio hilo likawa linaenda kinyume na baadhi ya sheria za Spain kuhusu
ujenzi na majirani wakatumia nafasi hiyo kutishia kumshtaki Messi.
Hivyo ili kuepeukana na skendo ya
kupelekwa mahakamani Messi akaamua kuwait a wanasheria wake na kuwaambia
wafanye taratibu za kisheria kufanya manunuzi ya nyumba zote za
majirani waliokuwa wakitaka kuziuza. Hatimaye mpango wa majirani
ukafanikiwa na Messi akanunua nyumba zote za majirani wake hivyo
kumfanya kuwa mmoja ya watu wanaomiliki maeneo makubwa kwenye sehemu
ya Castelldefels, Spain.
HUKUMU YA PONDA NA WENZAKE LEO
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini iliwaona wana kesi ya kujibu katika
mashtaka yote matano yanayowakabili. Katika moja ya mashtaka hayo,
Sheikh Ponda na wenzake anadaiwa kula njama na wizi wa mali yenye
thamani ya Sh59.6 milioni.
Awali, Hakimu Mkazi,
Victoria Nongwa alitoa uamuzi kuwa kina Sheikh Ponda wana kesi ya
kujibu baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 17 wa upande
wa mashtaka, ikaonekana shauri hilo limetokana na kipande cha ardhi.
Kesi hiyo iliposikilizwa mara ya mwisho, Hakimu Nongwa alisema kuwa baada ya Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) kubadilisha ardhi ya ekari nne iliyopo Chang’ombe Markazi na ekari 40 za Kampuni ya Agritanza Ltd zilizopo Kisarawe, kuna baadhi ya Waislamu hawakuridhika.
Mbali na mashtaka hayo, Ponda na mshitakiwa mwingine Sheikh Mukadam Abdallah Swalehe wanakabiliwa na shtaka la uchochezi wakidaiwa kuwa kati ya Oktoba 12 na 16, mwaka jana katika eneo la Chang’ombe Markazi, wakiwa viongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, waliwashawishi wafuasi wao kutenda makosa hayo.
Pia inadaiwa kuwa kati ya Oktoba 21 na 16, mwaka jana katika eneo hilohilo, washtakiwa hao pasipo uhalali wowote, walijimilikisha ardhi ambayo ni mali inayomilikiwa kihalali na Kampuni ya Agritanza Ltd na kusababisha uvunjifu wa amani.
Kati ya Oktoba 12 na 16, mwaka jana, huko Chang’ombe Markazi, washtakiwa hao wanadaiwa kuiba vifaa na malighafi mbalimbali za ujenzi, yakiwamo matofali 1,500, tani 36 za kokoto na nondo vyote vikiwa na thamani ya Sh59,650,000 mali ya Kampuni ya Agritanza Ltd.
Wednesday, April 17, 2013
HISTORIA YA BI. KIDUDE KWA UFUPI
Mwanamuziki mkongwe katika
Taarab Fatuma Binti Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude amefariki
dunia leo mchana huko Bububu Zanzibar, sehemu alikokuwa anaugulia kwa
kipindi sasa.Mwili wake utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa
kesho.
Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha
Mfagimaringo..Alikuwa binti... wa mchuuzi wa nazi na hakuna anayejua
haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa
alikwishafikisha miaka 102.
Katika
mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya
sanaa kule kwao...mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar
es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule .....
Mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa
amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.
Bi
Kidude pia aliwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na
katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba
katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni
Mungu
Amlaze Pema Peponi Bibi yetu. Amen.
NDOA YA UWOYA NA NDIKU SASA YAFIKA MWISHO RASMI! KISA NI DIAMOND
Mapenzi bwana! Ukiambiwa yanaweza kuua usibishe kabisa, kwani
ukiondoa mifano mingine ya kufikirika, kitu ‘live’ ni kwamba mwanasoka
raia wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’, alianguka na kuzimia, baada ya
kupata taarifa mbaya kuhusu mkewe.Ndikumana, alianguka na kuzimia,
asubuhi ya Aprili 8, mwaka huu, baada ya kusoma Gazeti la Ijumaa
Wikienda, lililoandika habari ya usaliti wa mkewe, Irene Uwoya,
aliponaswa hotelini na mwamuziki, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
Habari za kuzimia kwa Ndiku, zimewekwa kweupe na Uwoya mwenyewe,
aliyesema: “Maskini Ndikumana wangu, baada tu ya kusoma habari ya mimi
na Diamond alianguka na kuzimia.”
Kwa tafsiri, Uwoya anamsikitikia mume wake
kuanguka na kuzimia, upande wa pili anajuta kumfahamu Diamond, kwani
ndiye aliyemsababishia majanga yote.
MIRATHI YA KANUMBA, BADO NI UTATA.
Ngoma inaonekana kuwa bado ni nzito
kuhusiana na mirathi ya marehemu Steven Kanumba kwani taarifa
zilizopatikana hivi karibuni zinaeleza kuwa, hakuna kitu kilichofanyika
mpaka sasa kutokana na mvutano uliokuwepo ndani ya familia.
Akizungumza na Risasi Jumatano hivi karibuni, mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa alisema yeye aliamua kukaa pembeni na kumuachia baba wa marehemu, mzee Charles Kusekwa afuatilie suala hilo lakini anashangaa mwaka umepita hakuna kilichofanyika.
Akasema, alisikia mzee huyo alituma wawakilishi wake walishughulikie suala hilo lakini wakachemsha kutokana na kukosa viambatanisho muhimu.
“Mimi niliamua kusubiri upande wa baba Kanumba wafungue mirathi kwa sababu Kanumba hakuwa na mtoto kusema nina ulazima wa kuharakisha ili apate haki zake, cha ajabu hakuna kilichofanyika mpaka sasa,” alisema mama Kanumba.
Akasema, kutokana na kwamba ametoa muda mrefu kwa mzee Kusekwa kushughulikia suala hilo bila mafanikio, ameamua kuingia ‘front’ mwenyewe ili kuhakikisha haki za mwanaye zinapatikana.
Credit:Global Pubishers.
Akizungumza na Risasi Jumatano hivi karibuni, mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa alisema yeye aliamua kukaa pembeni na kumuachia baba wa marehemu, mzee Charles Kusekwa afuatilie suala hilo lakini anashangaa mwaka umepita hakuna kilichofanyika.
Akasema, alisikia mzee huyo alituma wawakilishi wake walishughulikie suala hilo lakini wakachemsha kutokana na kukosa viambatanisho muhimu.
“Mimi niliamua kusubiri upande wa baba Kanumba wafungue mirathi kwa sababu Kanumba hakuwa na mtoto kusema nina ulazima wa kuharakisha ili apate haki zake, cha ajabu hakuna kilichofanyika mpaka sasa,” alisema mama Kanumba.
Akasema, kutokana na kwamba ametoa muda mrefu kwa mzee Kusekwa kushughulikia suala hilo bila mafanikio, ameamua kuingia ‘front’ mwenyewe ili kuhakikisha haki za mwanaye zinapatikana.
Credit:Global Pubishers.
BI KIDUDE AFARIKI DUNIA
MSANII
WA MUZIKI WA TAARABU NCHINI TANZANIA KUTOKA VISIWANI ZANZIBAR FATUMA
BINT BARAKA MAARUFU KAMA BIBI KIDUDE AMEFARIKI DUNIA LEO HUKO VISIWANI
ZANZIBAR.
BI. KIDUDE AMEFIKWA NA MATUTI HAYO
LEO KUTOKANA NA MARADHI YALIYOKUWA YAKIMSUMBUA KWA MUDA MREFU.
BI. KIDUDE AMESHAWAHI
KUFANYA KAZI NYINGI IKIWEMO MHONGO WA JANG'OMBE, KIJITI, ALAMINADURA,
YA LAITI, AHMADA NA NYINGINE NYINGI.
Mwana Mziki wa Tanzania AY awa Verified on Twitter
Account ya mtandao wa kijamii ya Twitter ya
mwanamuziki maarufu Afrika kutoka Tanzania, Ambwene Yesaya (AY)
yatambulika rasmi na kuwa mwanamuziki wa kwanza hapa Bongo account yake
kutambulika yaani (Verified Account) .
Twitter ambayo hufanya hivyo kwa kukuwekea alama ya tick ya blue mbele ya jina lako ili kukutambulisha kwa marafiki, ndugu, jamaa, mashabiki wako wanaokufuata [followers] kuwa wewe ni mtumiaji halisi wa account hiyo walifanya hivyo kwenye account ya Ambwene ndani ya masaa kadhaa yaliyopita.
Twitter pia hufanya hivi ili kukutofautisha na watumiaji wengine wanaoweza kutumia jina lako katika mtandao huo na wamekuwa wakifanya hivyo kwa watu maarufu katika nyanja mbalimbali.
AY amekuwa mmoja kati ya watanzania wachache ambao account zao zimekuwa hivyo akiwemo mcheza kikapu wa Oklahoma City Thunder(OKC) Hasheem Thabeet [@hasheemthedream], Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete [@jmkikwete] Flaviana Matata [@FlavianaMatata] na Waziri January Makamba
Twitter ambayo hufanya hivyo kwa kukuwekea alama ya tick ya blue mbele ya jina lako ili kukutambulisha kwa marafiki, ndugu, jamaa, mashabiki wako wanaokufuata [followers] kuwa wewe ni mtumiaji halisi wa account hiyo walifanya hivyo kwenye account ya Ambwene ndani ya masaa kadhaa yaliyopita.
Twitter pia hufanya hivi ili kukutofautisha na watumiaji wengine wanaoweza kutumia jina lako katika mtandao huo na wamekuwa wakifanya hivyo kwa watu maarufu katika nyanja mbalimbali.
AY amekuwa mmoja kati ya watanzania wachache ambao account zao zimekuwa hivyo akiwemo mcheza kikapu wa Oklahoma City Thunder(OKC) Hasheem Thabeet [@hasheemthedream], Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete [@jmkikwete] Flaviana Matata [@FlavianaMatata] na Waziri January Makamba
VIGOGO WIZARA YA ARDHI KORTINI KWA UBADHIRIFU
Simoni Lazaro (kushoto) akiwa na mtuhumiwa mwenzake,
Gerald Mango.
Charles Kijuba akikwepa kamera mahakamani.
MAOFISA watatu
waandamizi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi leo wameburuzwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za ufujaji wa pesa
za serikali zaidi ya milioni 200. Watuhumiwa hao ni Simon Lazaro ambaye
alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Sera, Gerald Mango, Mkuu wa
Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi , na Charles Kijuba, Kaimu Mhasibu
Mkuu.Watuhumiwa hao wamekana mashitaka na mahakama hiyo imesema kuwa dhamana iko wazi
Subscribe to:
Posts (Atom)