Tuesday, April 02, 2013
KIJIJI CHA MISUKULE CHAGUNDULIWA NCHINI
Msukule.
Msukule.
Msukule.
Na Makongoro Oging', Bagamoyo
INATISHA
na hofu kubwa imetanda katika Kijiji cha Kimange, Wilaya ya Bagamoyo
mkoani Pwani kufuatia baadhi ya viongozi wa dini kuwatumia vijana wa
hapo kama misukule ili wapelekwe kanisani.
Uchunguzi umebaini kuwa nia ya viongozi hao wa dini kuteua kijiji
hicho na kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ni kuwalaghai waumini
kwamba wana uwezo wa kufufua watu wanaodaiwa kufa na kuchukuliwa
kimazingara.
Imebainika kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.
Imebainika kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.
AGNES MASOGANGE AWEKA PICHA INSTRAGRAM AKIWA KATIKA POZI ZA KIMAHABA
Ni
miezi michache imepita tangu video queen wa bongo Agnes Masogange
aadhirike baada ya video yake chafu kusambaa ikionesha waki**** na jamaa
yake.
Lakini
sasa inaanza kuonekana kuwa dada huyu hii ni michezo yake baada leo
kupost picha zinazomuonesha wakiwa kimahaba na mpenzi wake katika
mtandao wa instragram.JE HIVI TUKIONA VIDEO NYINGINE AKIWA NA HUYU
MCHIZI TUTASHANGAA AU TUTASEMA NDIO KAZI YAKE?
MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI ZANZIBAR ALIGOMBEA UBUNGE TIKETI YA CUF 2010
IMEELEZWA
kuwa, mtuhumiwa Omar Mussa Makame (35) anayeshikiliwa na Jeshi la
Polisi kwa madai ya kumuua Padri Evaristus Mushi ni mwanachama wa CUF
ambaye aligombea nafasi ya uwakilishi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2010 katika Jimbo la Rahaleo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF).
Kaimu
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Hamad Masoud alithibitisha jana kuwa,
mtuhumiwa huyo ni mwanachama wao na alishiriki katika mchakato wa
uchaguzi mkuu na kusimamishwa na chama katika kampeni za Uwakilishi
Jimbo la Rahaleo.
“Ni
kweli mtuhumiwa anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji
ya Padri Mushi ni mwanachama wetu na alishiriki katika mchakato wa
kuwania Uwakilishi Jimbo la Rahaleo mwaka 2010.
Hata
hivyo, Hamad alisisitiza na kusema suala la Omar kamwe lisihusishwe na
CUF na kusema suala hilo watalitolea tamko baadaye.
Kwa
mujibu wa kumbukumbu za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ripoti ya
matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Jimbo la Rahaleo, mgombea wa
CCM, Nassor Salim Ali maarufu kama Jazirra aliibuka na ushindi kwa
kupata kura 3,952 sawa na asilimia 63.10, wakati mgombea wa CUF, Omar
Mussa Makame alipata kura 2,310 sawa na asilimia 39.9 na kushika nafasi
ya pili.
RUNGWE MBEYA IMEENDELEA KUKUMBWA NA MATUKIO YA MAUAJI YA KUTISHA, TAHADHARI PICHA HIZI ZINATISHA.....!!
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI ZINAZOONEKANA ZA MTOTO AYUBU HAPA NICHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI TUKUYU
|
Rais Jakaya Kikwete Akutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Naibu Rais mteule wa Kenya MheWilliam Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akiongea na Naibu Rais mteule wa Kenya MheWilliam Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Monday, April 01, 2013
Mgodi wafukia wachimbaji Arusha; zaidi ya watu 18 wanahofiwa kufariki.. Wanajeshi wafanaya uokozi sasa na tayari mtu mmoja ameokolewa hai na wengine watatu wakiwa wameshakufa
Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akiwasili eneo la ajali mapema
Mwili
wa dereva wa lori moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na
askari jeshi, tayari kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva
huyu ametambulika kwa jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa
ndani ya gari hilo wakati vijana wengine wakiendelea kupakia moram
asubuhi ya leo
KAMANDA MPINGA MATATANI
ADAIWA KUAMURU GARI LILILOBEBA MAZAO YA MISITU LIACHIWE.
Kutokana na tukio hilo, askari mwenye namba D.9523 Koplo Azizi wa kituo kidogo cha polisi Ikungi mkoani Singida ameingia matatani baada ya kulikamata gari hilo lenye namba za usajili T 271 BTR na trela namba T 686 BTX lenye urefu wa futi 40.
SIMULIZI YA ALIYENUSURIKA KIFO KUTOKA GHOROFA YA 15.
Fundi ujenzi, Yusuph Abdallah ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi), ameeleza jinsi alivyonusurika kifo baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka Ijumaa iliyopita.
Rais Kikwete na Mkewe, Mama Salma Kikwete wakimpa pole Yusuph Abdallah katika Hospitali ya Muhimbili walipotembelea majeruhi wa ajali ya kuporomoka jengo la ghorofa 16. Picha na Muhidin Michuzi.
FUNDI ujenzi, Yusuph Abdallah ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi), ameeleza jinsi alivyonusurika kifo baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka Ijumaa iliyopita.
Yusuph aliliambia Mwananchi akiwa wodini kwamba kilichomponya ni neema za Mungu kwani kabla jengo hilo kuporomoka yeye alikuwa ghorofa ya 15 kwenye jengo hilo katika Mtaa wa Indira Gandhi akiendelea na ujenzi.
Alieleza kuwa hakuwa anafahamu kinachoendelea, bali aliona ghafla jengo linaaanza kuporomoka, na baada ya hapo hakufahamu zaidi kilichotokea hadi alipojikuta yuko hospitalini.
OBAMA AENDA KANISANI KWA MIGUU NA FAMILIA YAKE SIKU YA PASAKA, TAZAMA PICHA HAPA
Rais Barack Obama akitembea kwa miguu na Familia yake kutoka White House across Pennsylvania Ave. hadi Lafayette Park. huku akiwa amemshikili mtoto wake wa pili Sasha mkono pamoja, Mkewe Michelle Obama na binti yao mkubwa Malia kuelekea katika Kanisa la St. John’s Episcopal liliopo Washington, DC ambapo walihudhuria katika Pasaka Siku ya Jumapili Machi 31, 2013. ( Official White House Picha na Pete Souza)
Rais Barack Obama na first lady Michelle Obama walipotembea kutoka White House na binti zao Sasha Obama, wa pili kutoka kushoto, na Malia Obama, kulia, wakitembea kwa miguu kupitia Lafayette Park kwenda katika Kanisa la St. John’s Episcopal kwa ajili ya Pasaka Siku Jumapili, Machi 31, 2013, Mjini Washington. (AP)
Obama alipokua akitembea Mitaa ya Lafayette Park hadi St. John's Episcopal Church Siku ya Jumapili , March 31, 2013, ndani ya Jiji la Washington. (Picha na Carolyn Kaster)
Obamas akitembea kupitia Lafayette Park kwenda Kanisasani kwajili ya Pasaka.
Rais wa Marekani Barack Obama na familia yake walipo maliza ibada katika Kanisa la St. John’s Episcopal kwa ajili ya Pasaka Siku Jumapili, Machi 31, 2013, Mjini Washington.
HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 31 MACHI, 2013
Ndugu Wananchi;
Naomba
nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na kunipa
fursa ya kuzungumza nanyi kwa kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa kila
mwisho wa mwezi. Leo ninayo mambo matatu ninayopenda kuzungumza nanyi.
Ziara ya Rais wa China Nchini Tanzania
Ndugu wananchi;
Jambo
la kwanza ni ziara ya Mheshimiwa Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa
China aliyoifanya nchini kwetu kati ya tarehe 24 na 25 Machi, 2013.
Lengo la ziara yake ilikuwa kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo
kati ya China na Tanzania. Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru
wakazi wa Dar es Salaam kwa kumpokea vizuri mgeni wetu na ujumbe wake.
Wameondoka wakiwa na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu na watu wake.
MKAPA ASEMA:TUSITANGULIZE UDINI KWENYE KATIBA
Ujumbe
wa amani na tahadhari ya umakini kwenye utoaji maoni kwenye Katiba
ndiyo vilitawala wakati wa misa za Sikukuu ya Pasaka zilizofanyika
sehemu mbalimbali nchini jana na juzi.
Miongoni mwa waliotoa hotuba wakati wa sikukuu hiyo ni
pamoja
na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ambaye alikuwa mkoani
Mtwara; na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliyekuwa jijini Dar es
Salaam.
Mkapa akataa udini
Rais mstaafu Mkapa alitumia fursa ya kutoa salamu katika Kanisa
Katoliki mjini Masasi kuliasa taifa kujiepusha na utoaji wa maoni ya
Katiba kwa misingi ya dini.
Mkapa alisema katiba ijayo haipaswi kuwa na itikadi za kidini kwa kuwa zinaweza kuliangamiza taifa.
WANAUME BONGO MOVIE HAWANA MAPENZI YA KWELI: SNURA
MKALI
wa filamu na muziki Bongo, Snura Mushi amesema anaogopa kuingia kwenye
uhusiano wa kimapenzi na wasanii wa filamu kwani wengi wao hawana
mapenzi ya kweli.
Akipiga
domo na paparazi wetu, Snura alisema tangu aanze kucheza filamu
alijiapiza kuwa kamwe hatajiingiza kwenye mapenzi na waigizaji zaidi ya
kushirikiana nao katika kazi ya kuzalisha filamu.
“Mimi siwapendi wanaume wasanii wa filamu, sijawahi kuwa nao labda awe msanii wa Bongo Fleva,” alisema Snura.
“Mimi siwapendi wanaume wasanii wa filamu, sijawahi kuwa nao labda awe msanii wa Bongo Fleva,” alisema Snura.
MAKAHABA RAIA WA RWANDA MATATANI DODOMA
WANAWAKE watatu raia wa Rwanda wanaosadikiwa kuendesha biashara ya ukahaba mjini Dodoma wamekamatwa na
kupewa siku tatu kuondoka nchini, huku wawili kati yao wakikutwa na vidonge vya kupunguza makali ya virusi ya Ukimwi (ARVs).
Subscribe to:
Posts (Atom)