Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk. Norman Sigalla |
Saturday, March 23, 2013
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MBEYA IMEPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YALIYOPANGWA NA CHADEMA TAREHE 25 MACHI MWAKA HUU
Friday, March 22, 2013
JK aziponda Simba, Yanga
RAIS
Jakaya Kikwete
amezipiga ‘kijembe’ klabu kongwe hapa nchini, Simba na Yanga, kutokuwa
na maendeleo kisoka na kuiacha Azam FC, ikiwapiga kumbo kila idara huku
wao wakiendekeza ushirikina mbele na migogoro.
Kikwete aliyasema hayo jana,
wakati akiweka jiwe la msingi la klabu ya Azam iliyoko Chamazi nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Rais
aliipongeza Azam kwa hatua ambayo imefikia, licha ya kuwa na uchanga
katika soka na kuzipita klabu za Simba na Yanga.
Alisema endapo Azam inataka kupiga hatua na
kuifikisha nchi mbali kwa kulitangaza jina la Tanzania, ifanye mambo
yake bila kuzifuata timu kongwe na kudai kuwa itafika mbali kitaifa na
kimataifa pia.
“Naamini mna uwezo wa kufika mbali katika
ulimwengu
wa soka, ila msiwe karibu na hizi timu, mtajikuta mnaishia hapahapa;
wao mechi mechi moja wanatolewa,” alisema Kikwete na kuwafanya watu
walioshuhudia hafla hiyo kuvunjika mbavu.
Aidha Kikwete alisema
kutokana na mafanikio ambayo Azam wameyapata hadi sasa, ikiwemo uwanja
na mambo mengine, imeonekana kama wao ndio vigogo na kusababisha
kuogopwa na jamaa ambao wanajifanya wakubwa.
Alikwenda mbali zaidi na kuwataka Azam, kuacha
kufuata vivuli vya hizo timu na kujisimamia wenyewe, kwa kuwa timu
mbili kongwe zina wanachama wanaopiga kura kwa kuhongwa, sambamba na
kutumia muda mwingi kulumbana, wakati hawana kitu wanachoingiza katika
timu.
Alisema
timu kubwa
zikiambiwa kutumia Uwanja wa Chamazi, zinaanza kuleta maneno ya ajabu
na kuongeza kuwa ushirikina haufai katika soka, cha muhimu ni kucheza
mpira na sio kazi ya kuandaa kamati za ufundi na kushindwa kutazama
benchi la ufundi ili kujenga timu.
“Ingekuwa mpira ni
ushirikina, basi Afrika tungekuwa mabingwa kila mwaka, kama timu inaona
uchawi dili, basi ikusanye wachawi wote dunia nzima ikae nao klabuni
kwao tuone!” aliongeza Kikwete.
Aliwataka
Azam endapo watakuwa na shida yoyote, wasisite kumjulisha na kudai
kuwa ombi lao la kupunguziwa VAT katika bidhaa zao za kisoka,
atawasiliana na wahusika ili aweze kulipatia ufumbuzi.
Naye Mkurugenzi wa Azam,
Yusuph Bakhressa, alishukuru sana kupata nafasi ya Rais kuzindua mradi
wao maalumu, ambao lengo lake ni kukuza na kuendeleza mpira wa miguu
nchini.
Alisema hadi sasa wametumia sh bilioni 3 katika mradi huo.
Katika hafla hiyo, Rais
aliambatana na mkewe Mama Salma Kikwete, Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, Mkuu wa Mkoa Dar es
Salaam, Mecky Saidi Sadick, na viongozi mbalimbali.
‘Love and Power’ ya Kanumba kuzinduliwa Leaders Aprili 7
from IRENE MWAMFUPE JAMII
by IRENE
MWAMFUPE
FILAMU
ya aliyekuwa nguli wa tasnia hiyo hapa nchini, marehemu Steven Kanumba,
inayokwenda kwa jina la ‘Love and Power’ inatarajiwa kuzinduliwa rasmi
Aprili 7, mwaka huu.
Filamu hiyo, ambayo wengi wanasema marehemu Kanumba
alijitabiria kifo chake, itazinduliwa kwenye viwanja vya Leaders,
Kinondoni jijini Dar es Salaam, huku ikienda sambamba na kumbukumbu ya
mwaka mmoja tangu kufariki dunia kwake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mdogo wa
marehemu Kanumba, ambaye pia ni kiongozi wa ofisi yake ya ‘Kanumba The
Great’ iliyopo Sinza, Seth Bosco, alisema zaidi ya waigizaji 10 kutoka
Ghana wanatarajiwa kuwepo siku hiyo.
Alisema mbali na waigizaji
hao wa Ghana, pia rafiki wa marehemu, ambaye ni muigizaji maarufu
barani Afrika, Mnigeria Ramsey Noah, pia anatarajiwa kuwepo siku hiyo
ya uzinduzi.
“Ramsey tulimpigia simu na tukamtaarifu na akasema kuhusu uwepo
wake siku hiyo, atatujulisha kabla kama anakuja au la, kutokana na kuwa
na majukumu mengi ya kikazi,” alisema Bosco.
Akizungumzia
ratiba ya siku hiyo, alisema itaanzia nyumbani kwa marehemu, baada
ya hapo wataelekea makaburini na baadaye Leaders kwa ajili ya uzinduzi
huo.
Alisema wapenzi na mashabiki wa filamu za Kanumba wanatakiwa
kufika asubuhi nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya ibada itakayoanza saa
nne asubuhi na kwisha saa tano.
Alisema mara baada ya
ibada hiyo, ndugu, jamaa, marafiki, waigizaji pamoja na mashabiki wake
watakula chakula cha pamoja kisha kuelekea makaburini.
Aliongeza kuwa bendi ya
muziki wa dansi ya Twanga Pepeta, ndiyo itahusika siku hiyo kwa upande
wa burudani, kisha uzinduzi rasmi utafanyika huku nakala za filamu hiyo
zikiuzwa papo hapo.
Marehemu
Kanumba alifikwa na mauti Aprili 7, mwaka jana nyumbani kwake Sinza
Vatican, huku kifo chake kikihusishwa na msanii wa filamu, Elizabeth
Michael ‘Lulu’.
Pinda akutana na Papa Francis 1, Vatican City.
Waziri
Mkuu,Mizengo Pinda akisalimiana na Kiongozi wa Kanisa
Katoliki Duniani, Papa Francis 1 , Vatican City, Machi 21, 2013.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakisalimiana na Kiongozi wa Kanisa
Katoliki Duniani, Papa Francis 1 ,Vatican City Machi 21, 2013. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
CHINUA ACHEBE AFARIKI DUNIA
Mwanafasihi mahiri duniani pamoja na
mwandishi wa Novel wa Naijeria, Profesa Chinua Achebe amefariki usiku wa
leo hospitalini huko Boston Massachusetts, USA akiwa na umri wa miaka
82.
Taarifa kutoka kwa moja ya chanzo karibu na
familia wa Chinua Achebe huyu amesema kuwa kwa kipindi sasa Chinua
Achebe amekuwa akisumbuliwa na maradhi na amekuwa akitibiwa katika
hospitali moja ambayo hakuitaja jina huko Boston.
Taarifa rasmi juu ya kifo hiki kutoka
katika familia ya mwanazuoni huyu ambaye alikuwa mwalimu wa chuo kikuu
huko Marekani ambapo amekuwa akiishi kwa miaka mingi sasa, itatolewa
wakati wowote kuanzia sasa.
Kibongo bongo tunamfahamu sana chinua achebe kwa vitabu
vyake maarufu ambavyo vimetumika katika kufundishia shule mbalimbali,
kama vile Things Fall Apart alichokichapisha mwaka 1958, Kitabu ambacho
kimeandikwa kwa lugha tofauti zaidi ya 50 duniani na kuuza nakala zaidi
ya milioni 12, na vitabu vyake vingine maarufu ni pamoja na Arrow of
God, No Longer at Ease, Anthills of the Savannah pamoja na A man of the
People.
WAFUASI WA SHEIKH PONDA WATUPWA JELA
WAFUASI
52 wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa
Ponda, waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya maandamano haramu,
wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela kwa kila mmoja.
Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana, baada ya wafuasi hao kukutwa na hatia kwa makosa matatu kati ya manne yaliyokuwa yakiwakabili. Hata hivyo watakaa jela kwa mwaka mmoja kutokana na adhabu zote kwenda kwa pamoja.
Hata hivyo aliyekuwa mshtakiwa wa 48, Waziri Omar Toy, aliachiwa huru baada ya Mahakama kuridhika kwamba hana hatia kutokana upande wa mashtaka kushindwa kuthitibisha madai dhidi yake.
Baada ya Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo kusoma hukumu hiyo, ilizuka tafranwi miongoni mwa ndugu wa washtakiwa hao ambapo wengine waliangua vilio na wengine kuanguka na kujigaragaza chini.
Mwanamke ambaye ni ndugu wa washtakiwa hao, alionekana kama mtu “aliyepandwa mashetani” na kutaka kumvamia askari wa kike ambaye katika kujihami alimpiga ngumi, kisha watu wakafanikiwa kumdhibiti kumshika.
Hakimu Fimbo katika hukumu hiyo alisema baada ya kusikiliza ushahidi na hoja za pande zote pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo ameridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka matatu dhidi ya washtakiwa hao.
Hata hivyo, Hakimu Fimbo alisema kuwa katika shtaka la uchochezi lililokuwa likiwakabili washtakiwa wanne, upande wa mashtaka umeshindwa kulithibitisha.
“Mahakama imeridhika na ushahidi uliwasilishwa na upande wa mashtaka kuwa umethibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa wote isipokuwa mshtakiwa wa 48,” alisema Hakimu Fimbo na kuongeza:
“Hivyo Mahakama imewatia hatiani washtakiwa wote isipokuwa mshtakiwa wa 48, katika shtaka la kwanza, la pili na la tatu na katika shtaka la nne, Mahakama imeona kuwa washtakiwa hawana hatia.”
Washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama za kutenda makosa, kufanya maandamano yaliyozuiwa na Polisi na kwa pamoja kufanya mikusanyiko haramu na kusababisha uvunjifu wa amani.
Akitoa adhabu kwa washtakiwa hao baada ya kuwatia hatiani, Hakimu Fimbo alisema: “Nimezingatia kuwa karibu kila mshtakiwa ana majukumu ya kifamilia na kwa kuzingatia `nature’ (asili) ya mashtaka.”
Aliongeza: “Katika kosa la kwanza ninawahukumu kifungo cha mwaka mmoja jela na kosa la pili pia mwaka mmoja jela na tatu mwaka mmoja jela. Adhabu zote zinakwenda kwa pamoja.”Kauli za Mawakili
Kabla ya adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Ladislaus Komanya aliyekuwa akisaidiana na Wakili Joseph Maugo, aliieleza Mahakama kuwa hawana kumbukumbu za makosa ya jinai kwa washtakiwa hao na akaiomba Mahakama iwape adhabu kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake, Wakili wa washtakiwa hao, Mohamed Tibanyendela aliiomba Mahakama iwaonee huruma kwa kuwaachia huru washtakiwa hao au kwa kuwapa adhabu ndogo sana.
Wakili Tibanyendelea alidai kuwa washtakiwa hao ni mara yao ya kwanza kutenda makosa hayo na kwamba wana familia ambazo zinahitaji huduma kutoka kwao huku akidai kuwa wengine tangu walipokamatwa, familia zao hazijui waliko.
Pia Wakili Tibanyendelea alidai kuwa washtakiwa wengine wanaumwa kisukari na shinikizo la damu, huku akitoa mfano wa mshtakiwa wa 21, Kassim Mohamed Chogo, aliyefutiwa mashtaka kuwa alikuwa mgonjwa na ameshafariki dunia.
Ponda ajitetea
Wakati hukumu hiyo ikitolewa, Sheikh Ponda (55) amemaliza utetezi wake akiieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa yeye hana nyaraka za umiliki wa kiwanja cha Malkazi Chang’ombe bali historia ya eneo hilo inawafanya wao kuwa wamiliki.
Mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa, Sheikh Ponda alitoa utetezi wake dhidi ya mashtaka matano yanayomkabili yeye na wenzake 49 likiwamo la uchochezi na wizi wa mali yenye thamani ya Sh 59.6 milioni.
Ponda alidai kuwa awali kiwanja hicho kilikuwa kinamilikiwa na Taasisi ya Jumuiya ya Kiislamu ya East African Muslim Welfare Society(EAMWS) ambayo ilivunjwa na Serikali mwaka 1958 na Serikali kuunda Bakwata.
Akiongozwa na wakili wake kutoa utetezi, Juma Nassoro, Sheikh Ponda alidai; “Bakwata iliundwa ili kusimamia shughuli zilizokuwa zikiendeshwa na Taasisi ya Jumuiya ya Kiislamu ya East African Muslim Welfare Society na siyo mali kama majengo, viwanja na hata shule.
“Tulitumia njia ya mazungumzo ya Kidiplomasia kurejesha kiwanja cha Malkazi Chang’ombe kwa kuzingatia kuwa itatatua mgogoro huo katika njia nyepesi,” alidai Sheikh Ponda.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka alimuuliza Sheikh Ponda ni kwa nini hawakuwahi kwenda kuonana na mmiliki wa shule ya Yemeni, ambao nao walinunua eneo hilo la Chang’ombe Malkazi wakaenda kwenye Kampuni ya Agritanza Ltd.
Aliendelea kuhoji kuwa ni kwa nini, pia walikubali kutafutiwa eneo lingine na Kampuni ya Agritanza Ltd kama nyinyi ni wamiliki halali wa lile eneo?
Akijibu hoja hizo, Sheikh Ponda alidai kuwa ; “Tulitumia njia ya kumshawishi mtu ili aweze kuliona tatizo kwa sababu alikuwa na umiliki, ndiyo sababu tulikubali kutafutiwa eneo lingine.
“Wakili Kweka Sheikh Ponda nafikiri unajua taratibu za kisheria, kwa nini ulipoona huo ni mgogoro wa ardhi hukwenda kwenye Mahakama ya Ardhi?”
Sheikh Ponda akijibu, alimwambia wakili huyo kuwa hakuna mahali katika ushahidi wake aliomwambia kuwa mazungumzo yalishindikana bali alisema yalikuwa yanakwenda vizuri ndiyo sababu hakufanya hivyo.
Wakili wa Serikali aliuliza;”Utakubaliana na mimi kuwa mali za Kampuni ya Agritanza Ltd ambazo zinadaiwa kuibwa mlizitumia katika ujenzi wenu wa msikiti wa muda?”
Sheikh Ponda alidai kuwa hilo ni gumu kulijibu, bali wanachotakiwa ni kwenda eneo la tukio ili wathibitishiwe ni kipi kilitumika na kipi hakijatumika.
Baada ya kujibu hilo, Wakili wa Serikali alisisitiza swali hilo ambapo Ponda alimwambia; “Mimi mwenzio nafanya mijadala na Jeshi la Polisi toka enzi za Nyerere sasa tusilete mijadala isiyokuwepo.”
Hata hivyo, Sheikh Ponda alikubali kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliohusika kutoa taarifa kwa maimamu wa misikiti mbalimbali kuwaeleza waumini wao kushiriki kujitolea katika ujenzi wa msikiti wa muda uliojengwa katika eneo la Malkazi Chang’ombe, Oktoba 11 na kukamilika Oktoba 14, mwaka jana.
Alidai kuwa walijenga msikiti huo baada ya kufanya makubaliano na mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Agritanza Ltd, Hafidhi na kukubaliana kuweka alama ambayo kila mwislamu akiiona ataiheshimu na kutofanya shughuli zake binafsi katika eneo hilo na kupendekeza kujenga msikiti huo wa muda.
Kuhusu kukamatwa kwake
Sheikh Ponda alidai kuwa yeye alikamatwa Oktoba 16, 2012, nyakati za saa 4 kasoro robo usiku alipokuwa akijiandaa kuingia katika msikiti wa Tungi Temeke, akipanda ngazi alitokea mtu mmoja aliyekuwa kwenye gari nyeusi aina ya Toyota Harrier akimtaka amfuate.
Anadai alimpuuza na akaamua kuingia ndani ya msikiti huo, lakini alisikia kishindo cha gari na alipogeuka nyumba aliona gari tatu zilizojaa askari wa FFU wakiwa wamebeba silaha.
Aliendelea kudai kuwa, baada ya kuona hivyo aliendelea kuingia ndani lakini alipofika katikati ya msikiti alivamiwa na askari hao ambao walikuwa wamevalia sare zao na viatu na kumbeba kama mtu aliyetekwa nyara kwa kumshika mguu na mkono na kuondoka naye kwa kasi hadi Kituo cha Polisi
Chang’ombe na baadaye Kituo cha Polisi Kati.
Alidai kuwa alipofika huko alielezwa kuwa anatuhumiwa kuwa yeye siyo raia wa Tanzania, ni Mrundi na pia alidhalilishwa kwa lugha ya matusi.
Lakini baadaye alielezwa na askari mmoja kuwa anakabiliwa na tuhuma za kuingia kwa kosa la jinai katika kiwanja cha Chang’ombe Malkazi.
CHANZO CHA HABARI NI MWANANCHI
J MARTINS AFANYA COLLABO NA OMMY DIMPOZ, MWANA FA NA AY
Kuanzia
kushoto ni Mwana FA, AY (katikati), Ommy Dimpoz, J Martins na Marco
Chali wakiwa kwenye studio za MJ Records
Mwanamuziki na producer mahiri wa
nchini Nigeria, Martins Okey Justice aka J Martins yupo nchini na
amefanya collabo na Mwana FA, AY na Ommy Dimpoz.
Inavyoonekana staa huyo
amewashirikisha AY na Mwana FA kwenye wimbo mmoja uliotayarishwa na
Marco Chali kwenye studio za MJ Records.
“Confirmed now @Realjmartins ft on
@AyTanzania and @MwanaFA New Single coming out soon,” imesomeka tweet moja.
Pia Ommy Dimpoz amemshirikisha staa huyo
kwenye wimbo wake.“Finally
@ommydimpoz did the Song with @Realjmartins (J.Martins) pic after the
session,” imesomeka tweet nyingine ikiwa pamoja na
picha.
Ommy Dimpoz akiwa ana J Martins
Mwana FA na J Martins
“Just left stu got an exclusive pre listening sesh of
new @RealJMartins and @AyTanzania – INSAAAAANE #EastMeetsWest,” ametweet Vanessa Mdee.
KESI YA LWAKATARE: TUNDU LISU AMLAUMU "ISSA MICHUZI" NA " MWIGULU NCHEMBA
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu akiongea na
wanahabari (hawapo pichani).
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu leo amefanya mkutano
wa wanahabari. Katika mkutano huo, Lissu ameongea yafuatayo:
1. Atafungua kesi Mahakama kuu kuiomba iiamuru Mahakama ya Kisutu kuendelea kusikiliza kesi ya awali iliyofutwa na DPP katika kesi inayomhusu Lwakatare kwani DPP amevuka mipaka yake inayomruhusu kufuta kesi na isitoshe kesi aliyofungua ni ile ile hivyo Mahakama iamuru shauri la awali liendelee.
2. Kuhusu video iliyoonyeshwa kwenye mitandao Lissu anasema kuna mashaka makubwa sana kuhusiana na video ile na kisheria kesi hiyo ikifika mahakamani haitachukua hata nusu saa ataibuka mshindi.
1. Atafungua kesi Mahakama kuu kuiomba iiamuru Mahakama ya Kisutu kuendelea kusikiliza kesi ya awali iliyofutwa na DPP katika kesi inayomhusu Lwakatare kwani DPP amevuka mipaka yake inayomruhusu kufuta kesi na isitoshe kesi aliyofungua ni ile ile hivyo Mahakama iamuru shauri la awali liendelee.
2. Kuhusu video iliyoonyeshwa kwenye mitandao Lissu anasema kuna mashaka makubwa sana kuhusiana na video ile na kisheria kesi hiyo ikifika mahakamani haitachukua hata nusu saa ataibuka mshindi.
Lissu
anasema
- Hakuna mtu anayepanga mauaji katika hadhara mahali ambapo watu wanapitapita kama inavyoonekana kwenye video ile.
-Lwakatare kama alirekodiwa basi lazima ielezwe je ilikuwa ni kwa hiari yake kama si hivyo ni makosa
-Issa Michuzi Mpiga picha wa Rais alikuwa akipongezana na watu wa Ikulu wenzake kuwa TISS (Usalama wa Taifa) wamefanya kazi nzuri kwa kurekodi ile video. Kisheria usalama wa taifa hawatakiwi wala hawaruhusiwi kurekodi au kuvifanyia ushushu vyama vya siasa kwa maslahi ya Chama tawala.
-Ludovick baada ya kukutana na Lwakatale tarehe 28 Desemba mwaka jana saa 5 muda mfupi baadaye yaani saa 5:59 alimpigia simuMwigulu Nchemba kwa kutumia namba ya simu ya Mwigulu ambayo ameiandikisha kwenye kumbukumbu na vitabu vya Bunge Lissu anadai wana rekodi ya mazungumzo yao.
-Siku iliyofuata tarehe 29 Desemba mwaka jana akiwa kwenye kipindi cha Tuongee asubuhi cha Star TV alidai ana mkanda wa video unaowaonyesha CHADEMA wakipanga mauaji.
-Pia amedai itabidi waambiwe video hiyo imerekodiwa studio gani, maneno gani yameondolewa na yapi yameongezwa.
Anamalizia kwa kusema walianza kwa kusema CHADEMA ni chama cha familia wakashindwa, wakasema ni chama cha wachaga wakashindwa, wakesema ni chama cha wakatoliki wakashindwa, wakasema ni chama cha wakristo wakashindwa, wakasema ni chama cha ukanda wakashindwa leo wanasema ni chama cha kigaidi WATASHINDWA.
(Picha / Habari na Kurugenzi Ya Habari Chadema)
- Hakuna mtu anayepanga mauaji katika hadhara mahali ambapo watu wanapitapita kama inavyoonekana kwenye video ile.
-Lwakatare kama alirekodiwa basi lazima ielezwe je ilikuwa ni kwa hiari yake kama si hivyo ni makosa
-Issa Michuzi Mpiga picha wa Rais alikuwa akipongezana na watu wa Ikulu wenzake kuwa TISS (Usalama wa Taifa) wamefanya kazi nzuri kwa kurekodi ile video. Kisheria usalama wa taifa hawatakiwi wala hawaruhusiwi kurekodi au kuvifanyia ushushu vyama vya siasa kwa maslahi ya Chama tawala.
-Ludovick baada ya kukutana na Lwakatale tarehe 28 Desemba mwaka jana saa 5 muda mfupi baadaye yaani saa 5:59 alimpigia simuMwigulu Nchemba kwa kutumia namba ya simu ya Mwigulu ambayo ameiandikisha kwenye kumbukumbu na vitabu vya Bunge Lissu anadai wana rekodi ya mazungumzo yao.
-Siku iliyofuata tarehe 29 Desemba mwaka jana akiwa kwenye kipindi cha Tuongee asubuhi cha Star TV alidai ana mkanda wa video unaowaonyesha CHADEMA wakipanga mauaji.
-Pia amedai itabidi waambiwe video hiyo imerekodiwa studio gani, maneno gani yameondolewa na yapi yameongezwa.
Anamalizia kwa kusema walianza kwa kusema CHADEMA ni chama cha familia wakashindwa, wakasema ni chama cha wachaga wakashindwa, wakesema ni chama cha wakatoliki wakashindwa, wakasema ni chama cha wakristo wakashindwa, wakasema ni chama cha ukanda wakashindwa leo wanasema ni chama cha kigaidi WATASHINDWA.
(Picha / Habari na Kurugenzi Ya Habari Chadema)
Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala yakutana na Ofisi ya Bunge
Kamati ya Bunge ya Katiba,
Sheria na Utawala leo imekutana na Ofisi ya Bunge kwa lengo la kupata
taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo ikiwa ni utekelezaji wa
shughuli za kamati. kama anavyoonekana Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba
Sheria na Utawala Mhe. Pinda Chana akizungumza jambo katika kikao na
watendaji wa Ofisi ya Bunge wakati kamati hiyo ilipokutana na watendaji
wa Ofisi ya Bunge kufuatilia utekelezaji wa majuku ya Ofisi
hiyo.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. William Ngeleja
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas
Kashililah akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa kamati ya katiba, Sheria
na Utawala wakati wa kikao na kamati hiyo iliyokutana na watendaji wa
Ofisi ya Bunge kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya
Ofisi hiyo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali watu Bi.
Kitolina Kippa.
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas
Kashililah akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa kamati ya katiba, Sheria
na Utawala wakati wa kikao na kamati hiyo iliyokutana na watendaji wa
Ofisi ya Bunge kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya
Ofisi hiyo.
MTOTO WA MIAKA 12 APATA MTOTO.....ALIKUWA DARASA LA SABA
Mtoto Sean Stewart wa nchini Uingereza, amekuwa baba mdogo
pengine kuliko wote duniani baada ya mpenzi wake kujifungua wiki hii
mtoto wa kiume mwenye afya.
Sean aliyetimiza miaka 12 mwezi
uliopita, aliruhusiwa kutoenda shule ili kuwa pembeni ya mpenzi wake
mwenye miaka 16, Emma Webster, wazazi wake Ray na Shirley, na mama yake
Sean, Theresa. Alikuwa na miaka 11 na Emma miaka 15 alipopata ujauzito
huo.
Sean
akimnywesha mwanae maziwa
Baba na mwana
Yupo darasa la saba katika shule ya
Margaret Beaufort.
Mwaka jana Sean alisema kuwa atakuwa
bega kwa bega na Emma na mtoto wake pia. “I was shocked at first when I
was told Emma was pregnant but I am all right about it now,” alisema
Sean.
JK: Mzee Kingunge Ngombale Mwiru Hospitali ya Taifa Muhimbili
Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mzee Kingunge
Ngombale Mwiru aliyepumzishwa katika chumba cha Dharura katika hospitali
ya Taifa ya Muhimbili leo.Mzee Kingunge alikimbizwa Hospitalini Hapo
Baada ya Kujisikia Vibaya.jopo la Madaktari Bingwa linamfanyia uchunguzi
Mzee Kingunga ili kubaini ugonjwa unaomsumbua.Aliyesimama Nyuma ya Rais
ni mke wa Mzee Kingunge na kushoto ni Mtoto wa Mzee Kingunge Bwana
Kinjekitile(picha na freddy Maro)
Rais Kikwete awataka vijana wawe wazalendo, wasifurahie nchi inaposemwa vibaya
Rais wa JK amewataka
vijana kuacha kushabikia watu wanaoisema nchi vibaya, amesema enzi zao
watu waliokuwa wakiisema nchi vibaya walikuwa wanawachukia tofauti na
saizi vijana wanashabikia!
Akizidi kuongea,
kuwa endapo nchi itasemwa vibaya basi wao huchukia!
Kauli hiyo ameitoaJana jijini
D'Salaam
WAZIRI SITTA ACHONGEWA KWA LOWASSA
Edward Lowassa
KWA UFUPI
Historia ya kisiasa baina ya vio ngozi hao inakifanya kikao cha
leo kuwa mvuto wa aina yake kwani kitendo cha wabunge kuichongea Wizara
ya Sitta kwa Kamati ya Lowassa kitatoa mwanya wa mpambano kati ya
wanasiasa hao wawili.
Wakati hayo yanatokea, kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake,
Edward Lowassa itakutana na Wizara hiyo inayoongozwa na Waziri Samuel
Sitta kujadili mambo mbalimbali yakiwamo sera ya Tanzania katika jumuiya
hiyo.
Lowassa, alijiuzulu Uwaziri Mkuu 2008 wakati Sitta akiwa Spika
na inasadikiwa kwamba tukio hilo lilijenga ufa kati ya wanasiasa hao
wawili, ambao tayari wanatajwa katika kinyang’anyiro cha Urais 2015.
Wakizungumza mbele ya kamati hiyo, wabunge wa EAC walisema
wizara hiyo haijawapa mwongozo wa kutetea maslahi ya Tanzania ndani ya
jumuiya, jambo ambalo linawafanya washindwe kuchangia hoja zenye uzito.
“Tunatengwa na wizara, jambo ambalo linatufanya tutoe hoja
tunazozijua wenyewe, kutokana na hali hiyo wanapaswa kubadilika,”alisema
Shyrose Bhanji.
Aliongeza kuwa kila wanapojaribu kuwasiliana na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, wamekuwa waki pigwa kalenda, jambo ambalo linawafanya
kupata taarifa nyingine kupitia vyombo vya habari.
“Tulitarajia tungeelezwa msimamo wa nchi, lakini mpaka sasa
hatujaelezwa chochote na kwamba kila mmoja anachangia kutokana na upeo
wake,” aliongeza. Mbunge mwingine, Abdallah Mwinyi alisema mpaka sasa
Tanzania haina sera ya mtangamano ambao utawaweka pamoja wabunge hao
katika kujadili mambo ya jumuiya.
“Nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki zina sera ya
mtangamano ambazo zinawaweka pamoja wabunge kujadili mambo mbalimbali
yanayohusu maslahi ya nchi zao, lakini sisi hatuna, wakati Rwanda
imejiunga juzi tu tayari wameandaa sera inayowapa mwongozo wabunge wao,”
alisema Mwinyi.
Sitta akana
Alipoulizwa juu ya malalamiko, Sitta, ambaye jana jioni alikuwa
anahudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu, alijibu
kwa ujumbe mfupi wa maandishi;”Si kweli...niko kwenye kikao nitakupigia
baadaye.”
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Stargomena Tax
amewashangaa wabunge hao kwa kulalamika kukosa ushirikiano na kwamba
madai hayo si ya kweli.
“Hivi wabunge hawa wanataka tuwape ushirikiano wa aina gani?
Mbona tumekuwa tukikutana nao mara kwa mara na kuwapa misimamo ya nchi?
“Tulishakaa na Bunge la Jamhuri ya Muungano na tuliwapa hadidu
za rejea ili wawape wabunge wa Afrika Mashariki,” alieleza Dk Tax.
Dk Tax pia alisema wamechapisha kijitabu cha kuwapa mwongoza wa
maeneo ya kuzingatia wakati wanapokwenda kwenye vikao vya Bunge la
Afrika Mashariki.
Miss Utalii Tanzania 2012/13 watembelea Ukumbi wa Kimataifa na kisasa wa Makumbusho ya Taifa.
Washiriki
wa Fainali za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2012/13,jana
wametembelea Ukumbi wa kwanza na wa Kisasa na wa aina yake Tanzania
ambao unamilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia kurugenzi ya
mambo ya kale na makumbusho ya Taifa uliopo ndani ya Makumbusho ya Taifa
jirani na Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) karibu na maeneo ya Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Wakiwa
katika Ukumbi huo wenye uwezo wa kuchukua watu 470 kwa wakati mmoja,
walishuhudia Viti,Mitambo na vifaa vingine vya kisasa vyenye uwezo wa
kuendesha Matamasha na mashindano ya Urembo kwa kiwango cha hadhi ya
nyota tano.
Wengi
wa washiriki hao walionyesha hamasa na kujaribu kuwashawishi viongozi
na wakuu wa msafara wao ili kufanya Fainali hizo katika Ukumbi huo ambao
umekuwa ni kivutio kikubwa, jambo ambalo Viongozi na kamati iliokuwa na
jopo la msafara huo lilionekana kukubaliana na mawazo ya nia ya warembo
hao ya kuomba Fainali hizo zifanyike ndani ya Ukumbi huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Rais wa Mashindano hayo
nchini na Barani Afrika Erasto G., Chipungahelo,kuhusu uwezekano wa
kuandaa Fainali hizo katika Ukumbi huo wa kimataifa wa NATIONAL MUSIUM
THEATRE, alisema kuwa kila jambo ni mipango, hivyo na kwa kuwa lengo na
nia ya Mashindano ya Miss Utalii ni kutangaza Vivutio vya Taifa kuna
uwezekano pia Fainali hizo zikafanyika hapo ikiwa pia ni kuwapa heshima
Wizara ya Maliasili na Utalii ambao ndiyo walezi wakuu wa mashindano ya
Miss Utalii Tanzania kwa kuwa wao ndiyo wamiliki wa Ukumbi huo ambao kwa
sasa unaonekana kuwa ni kati ya kumbi pekee zilizojengwa kisasa na
hadhi ya kimataifa hapa nchini Tanzania.
ziara
hiyo ya kutembelea Ukumbi huo kwa washiriki wa Miss Utalii Tanzania
2012/2013 iliandaliwa na Washiriki wenyewe baada ya kuusikia sifa zake
kutoka kwa watu mbalimbali na Mitandao ya Kijamii.
Aidha
Chipungahelo amesema kwamba warembo hao wanatarajia kupanda katika
jukwaani baada ya kutoka kwenye ziara ya kutembelea hifadhi za Taifa
ambazo ni pamoja na Saadan, Mikumi, Udzungwa, Mkomanzi, Arusha na Mlima
Kilimanjaro watakaokuwa wameambatana na waandishi wa habari.
Akizungumzia
hali ya Ukumbi huo Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo
amesema kwamba ni heshima kubwa kwa Taifa na sekta nzima ya Utalii kuona
Warembo ambao wanatangaza Utalii wa Nchi yetu wakivutiwa na ukumbi huo
hata kufikia kupeleka maombi ya kutaka wao kuwa Warembo wa kwanza
kupanda katika jukwaa hilo la Ukumbi wa kisasa na wa kimataifa wa
NATIONAL MUSIUM THEATRE ulipo ndani ya Makumbusho ya Taifa ambao ni
kivutio kikubwa kwa sasa katika anga za Burudani na sanaa.
“Ukumbi
ni mzuri kama ambavyo wenyewe wandishi mlivyoona na kutazama, hakika ni
jambo la kujivunia na kusifiwa kwa Wizara yetu, maana unaonekana ni
jambo la kujipanga hadi kuweza kutengeneza kwa ubora huo unaoonekana
sasa, bila shaka nyie wenyewe mtaona ni kwa kiasi gani Umeandaliwa,
lakini hata hivyo ni changamoto kwa Wizara zingine katika kubuni na
kuweka rasilimali kama hizi kwa manufaa ya Taifa, kama ambavyo mnaona
wenyewe, kwani hata Washiriki wamefurahi na hata kusifia sana hivyo pia
nachukua fulsa hii kuishukuru Wizara kwa kuwekeza Ukumbi wa Kisasa ambao
ni faida kwa Taifa” alisema Chipungahelo.
Pia
aliendelea kusisitiza na kuomba wadau na wapenzi mbalimbali wa
mashindano haya kujitokeza kuunga mkono kudhamini na kununua tiketi siku
ya shindano..
Washiriki
wa Miss Utalii Tanzania wakiwa wanatembelea Ukumbi wa Kimataifa wa
Makumbusho ya Taifa(NATIONAL MUSEUM THEATRE).
Mahakama ya Zimbabwe yaweka ngumu kumuachia mwanasheria Mtetwa kwa dhamana.
Mahakama nchini Zimbabwe imekataa kumuachia
kwa dhamana mwanasheria anayetetea haki za binadamu Beatrice Mtetwa na
wasaidizi wanne wa Waziri Mkuu Bw. Morgan Tsvangirai.
Mwanasheria huyo Mtetwa alikamatwa Jumapili
iliyopita akishutumiwa kuzuia mkondo wa sheria kufanya kazi yake na
atabakia kizuizini hadi tarehe 3 mwezi Aprili mwaka huu.
Wasaidizi wane wa Bw. Morgan Tsvangirai
wanashikiliwa kwa kutuhumiwa kujifanya maaafisa wa polisi, lakini
wamekana tuhuma hizo.-DW.
Subscribe to:
Posts (Atom)